Kigwangala alia na serikali

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,556
7,084
Hamisi Kigwangalla ameandika haya yafuatayo katika ukurasa wake wa facebook.. Hebu pitieni na nyie muone wenyewe..

"Kwa hakika dhulma imetamalaki katika nchi hii!
Ukandamizaji umetamalaki katika nchi
hii! Nimekamatwa na polisi nikitetea
dhulma na ukandamizaji..."
 
Hamisi Kigwangalla ameandika haya yafuatayo katika ukurasa wake wa facebook.. Hebu pitieni na nyie muone wenyewe..

"Kwa hakika dhulma imetamalaki katika nchi hii!
Ukandamizaji umetamalaki katika nchi
hii! Nimekamatwa na polisi nikitetea
dhulma na ukandamizaji..."

Hadi akamatwe yeye ndo anajua kwamba nchi hii imejaa dhulma? kwanza alikuwa anawatetea wananchi gani? Wabunge wa upinzani wakikamatwa huwa wanawakebehi, sasa nao wakiguswa tu kidogo kelele nyingiiii. Bora yeye alikamatwa na kuachiwa siku hiyo hiyo, je wenzake wanaosota siku hadi wiki mbili! Magdalena Sakaya si aliwekwa lupanbgo karibia wiki mbili, mbona hakutoka kumsaidia japo dhamana na wote wanatoka tabora!??
 
Kingwangwa sijui kingwala sijui jina gani wewe ni KILAZA babkubwaa.

Sikiliza. Huwezi kuwa mpiganaji nchi hii bila ya kuwa opposite na CCM. Vinginevyo kaa kimya piga posho zako za kutosha ukimaliza tega mtego wa kuwadanganya tena. Angalia wenzio kina Mwandyosa, Membe, 6 na wengineo wanavyoishi kimungumungu roho mkononi, ijekuwa wewe dogo tu mpenda sifa!!!!?

Elewa hapo unapojidai kufanya maandamano ya kufunga mgodi ndio wakubwa wako wanapopita na kupewa bahasha za kaki na sio kwamba wakbwa zako hawajaona kuna tatizo.

Take care mkulu.
 
cheap popularity anataka tu huyo...hata mchongo wa kukamatwa ni maigizo ya ccm hayo ili ionekane hata wabunge wa ccm wanakamatwa...hivi kura za maoni si alishinda bashe???
 
Dr. Kigwa...

Wewe umekuwa wa kulia namna hii?!!!

Si ni wewe ulifanya makeke Bashe akipwa tiktak...

Sasa wewe leo dhulma gani unayoiongelea mkuu. Si ni wewe unayetumia jina la mwenzako ambaye ulimnyanyasa vya kutosha oct 2010, leo dhulma ndo umeijua.

Magamba ndo hivyo, tunawajua, wewe kiga kimya maisha yaendelee!!
 
Jiuzulu ndo tujue nchi imejaa dhulma!we unang'ang'ania ujinga,achia ngazi kama we mwanaume unayependa kusimama mwenyewe usiyependa huo uhuni wa ccm!kama hutaki basi wajitafutia sifa tu tena za kijinga!
 
Ama Kingwangalla anakunywa propofol na hivyo akili yake inakuwa nzito kufikiria au anaona watanzania ni majinga. Bila kufunga mgodi wa Resolute kama alivyokuwa amejiapiza hatoeleweka. Hii comedy anayocheza kwa kuwafuata vijisamaki vidogo angali mapapa yapo ni kuchezea watu akili.
 
Heko kigwangwala. Kama hutaishia hapo tutajua dhamira yako ya kweli. Tumia CCM as opportunity kuwasaidia wananchi wako.

Dhulma ipo, ndio chadema inayopingana nayo.
 
Sita analamika kuwa anatishiwa kuuawa! Kigwangala na bado mengi yatakufika! (Bapelage abana ccm)
 
Mbunge wa Nzega mjini kwa tiketi ya CCM, DK. Hamis Kigwangallah (pichani) amefikishwa mahakamani mjini Nzega mapema leo, akishitakiwa kwa makosa matatu ya Kufanya Mkutano isivyo halali, Kuingia Mgodini kinyume cha sheria na kula njama za kuteka kituo cha polisi.

Mbunge huyo amepewa dhamana na kesi yake itarudi tena katika Mahakama ya Wilaya ya Nzega baada ya wiki mbili.

DK. Hamis ameingia matatani na vyombo vya dola kutokana msimamo wake wa kuwatetea wachimbaji wadogo wa mgodi wa kijiji cha Mwabangu, Kata ya Nata dhidi ya wawekezaji wanaodai kumiliki eneo hilo.
 
Kigwa ha ha ha ha ha! leo ndo unajua hayo. Piga picha ya yaliyotokea Igunga jirani nawe. Kada wa CDM kuuwawa kinyama. NA wauwaji hawajulikani mpaka leo! ha ha ha! wangekunyofoa naniio!!
 
Na Kila atokaye chama cha upinzani ndo anapinga serikali. je, Kingwa naye vipi??
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom