Elections 2010 Kigwangala akataliwa mbele ya Kikwete - Nzega

sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,285
Kigwangala akataliwa mbele ya JK Nzega

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora, Dk Khamis Kigwangala, amejikuta katika wakati mgumu baada ya wakazi wa jimbo hilo kudai kuwa hawatampa kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba mbele ya Rais Jakaya Kikwete.

Hatua ya wananchi ilikuja baada ya Rais Kikwete kuwataka wampigie kura mgombea huyo, lakini walipaza sauti juu wakisema kwamba hawatamchagua.

Rais Kikwete, aliuliza wananchi waliofurika katika Uwanja wa Samora mjini Nzega, kwamba 'mtanipa kura Oktoba 31 mwaka huu, wakajibu ndiyo na kisha kumtambulisha Dk Kigwangalla na kuuliza 'mtampa kura' wakajibu kwa 'kuguna mmmmmhhhhh'.

Jibu hilo lilionekana kumchanganya Dk Kigwangala, ambaye wakati akitambulishwa alikuwa na sura iliyojaa tabasamu kubwa na kugeuka kuwa sura iliyokuwa na hofu na mshituko.

Hata hivyo, alipokuwa akiwasili uwanjani hapo sanjari na msafara wa Rais Kikwete, mshindi wa kura ya maoni ya CCM katika Jimbo la Nzega, Hussein Bashe, alishangiliwa kwa furaha kubwa na umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo, kitendo ambacho kilimfanya Rais Kikwete kushindwa kushindwa kumuita jukwaani kwa ajili ya kumpigia debe Dk Kigwangala.

Wakati akiondoka mara baada ya mkutano kuisha vijana wengi waliohudhuria kwenye mkutano huo, walilisukuma gari la Bashe, huku wakiimba " Bashe, Bashe, Bashe, Bashe" na "hatumpi kura Kigwangala" huku wakielekea Ikulu Ndogo Mjini Nzega, ambako mgombea wa CCM alifika kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani hapo Ikulu Ndogo kulikuwa na mkutano mfupi wa dharura, ambao ulimtaka Bashe, avunje kundi lake ambalo linaoonekana kuinyima usingizi CCM na kuungana na chaguo la chama katika nafasi hiyo kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano.

Awali kabla ya tukio hilo, Rais Kikwete, aliwaahidi wakazi wa Wilaya ya Nzega kwamba akichaguliwa kuwa Rais atahakikisha kuwa ustawi wa Mji wa Nzega unaboreka kwa kusimamia miundombinu ya afya, elimu, maji na barabara.

Alisema anatambua matatizo kadhaa yanayoukabili Mji wa Nzega na kuahidi kufuatilia matatizo hayo kwa karibu ikiwa ni pamoja na kumaliza kabisa shida ya maji kwa kuwezesha uvutwaji wa maji kutoka katika Ziwa Victoria.

Alisema sambamba na kusimamia mambo hayo Rais Kikwete, aliahidi kutengeneza barabara ya Nzega hadi Tabora kwa kiwango cha lami na kuitengeneza pia barabara ya Tabora, Bukene, Itobo hadi Kahama kwa kiwango cha lami ili kuuwezesha Mkoa wa Tabora ufikike kwa urahisi.

Hata hivyo, mgombea huyo wa CCM alitoa kauli ya unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ambao wanatumia dawa za kurefu maisha kwamba wamepata maambukizi hayo kutokana na kiherehere chao kwani wangeweza kujizuia na maambukizi hayo.

Wakati Kikwete akitoa kauli hiyo dhidi ya waathirika, takwimu zinaonyesha kwamba watu 9500 katika Mkoa wa Tabora wanatumia dawa hizo kati yao 2,700 wanaishi katika Manispaa ya Tabora.
 
Bashe alivuliwa uanachama kwa kudaiwa kuwa SI RAIA! Sasa atavunja kundi gani wakati yeye si mwanachama wa CCM? Wanachama wa CCM watamsikiliza yeye kwa msingi upi?

Tusidanganyane. Mfa maji heshi kutapatapa. Jimbo laenda upinzani hilo!
 
Kuna mpinzani gani hapo aliye na mvuto! Halafu si wamtumie Selelii kwenye kampeni huenda watu wakamuelewa!
 
Kigwangala akataliwa mbele ya JK Nzega

Thursday, 30 September 2010 09:25
0diggsdigg
Mgombea ubunge wa jimbo la Nzega,mkoani Tabora,Dk Khamis Kigwangala
Victor Kinambile, Nzega
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora, Dk Khamis Kigwangala, amejikuta katika wakati mgumu baada ya wakazi wa jimbo hilo kudai kuwa hawatampa kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba mbele ya Rais Jakaya Kikwete.

Hatua ya wananchi ilikuja baada ya Rais Kikwete kuwataka wampigie kura mgombea huyo, lakini walipaza sauti juu wakisema kwamba hawatamchagua.

Rais Kikwete, aliuliza wananchi waliofurika katika Uwanja wa Samora mjini Nzega, kwamba 'mtanipa kura Oktoba 31 mwaka huu, wakajibu ndiyo na kisha kumtambulisha Dk Kigwangalla na kuuliza 'mtampa kura' wakajibu kwa 'kuguna mmmmmhhhhh'.

Jibu hilo lilionekana kumchanganya Dk Kigwangala, ambaye wakati akitambulishwa alikuwa na sura iliyojaa tabasamu kubwa na kugeuka kuwa sura iliyokuwa na hofu na mshituko.

Hata hivyo, alipokuwa akiwasili uwanjani hapo sanjari na msafara wa Rais Kikwete, mshindi wa kura ya maoni ya CCM katika Jimbo la Nzega, Hussein Bashe, alishangiliwa kwa furaha kubwa na umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo, kitendo ambacho kilimfanya Rais Kikwete kushindwa kushindwa kumuita jukwaani kwa ajili ya kumpigia debe Dk Kigwangala.

Wakati akiondoka mara baada ya mkutano kuisha vijana wengi waliohudhuria kwenye mkutano huo, walilisukuma gari la Bashe, huku wakiimba " Basha, Bashe, Bashe, Bashe" na "hatumpi kura Kigwangala" huku wakielekea Ikulu Ndogo Mjini Nzega, ambako mgombea wa CCM alifika kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani hapo Ikulu Ndogo kulikuwa na mkutano mfupi wa dharura, ambao ulimtaka Bashe, avunje kundi lake ambalo linaoonekana kuinyima usingizi CCM na kuungana na chaguo la chama katika nafasi hiyo kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano.

Awali kabla ya tukio hilo, Rais Kikwete, aliwaahidi wakazi wa Wilaya ya Nzega kwamba akichaguliwa kuwa Rais atahakikisha kuwa ustawi wa Mji wa Nzega unaboreka kwa kusimamia miundombinu ya afya, elimu, maji na barabara.

Alisema anatambua matatizo kadhaa yanayoukabili Mji wa Nzega na kuahidi kufuatilia matatizo hayo kwa karibu ikiwa ni pamoja na kumaliza kabisa shida ya maji kwa kuwezesha uvutwaji wa maji kutoka katika Ziwa Victoria.

Alisema sambamba na kusimamia mambo hayo Rais Kikwete, aliahidi kutengeneza barabara ya Nzega hadi Tabora kwa kiwango cha lami na kuitengeneza pia barabara ya Tabora, Bukene, Itobo hadi Kahama kwa kiwango cha lami ili kuuwezesha Mkoa wa Tabora ufikike kwa urahisi.

Hata hivyo, mgombea huyo wa CCM alitoa kauli ya unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ambao wanatumia dawa za kurefu maisha kwamba wamepata maambukizi hayo kutokana na kiherehere chao kwani wangeweza kujizuia na maambukizi hayo.

Wakati Kikwete akitoa kauli hiyo dhidi ya waathirika, takwimu zinaonyesha kwamba watu 9500 katika Mkoa wa Tabora wanatumia dawa hizo kati yao 2,700 wanaishi katika Manispaa ya Tabora.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

UNAWEZA KUWA UNAJIONA WE NI JUU ZAIDI YA YOTE LAKINI SIKU UKIJUA SAUTI YA WATU SAUTI YA MUNGU HUTOKAA UDHARAU WATU..KIKWEETE NA MENGI YATAKAKUKUMBA SHAME ON YOU
 
ni aibu ya aina gani raisi mzima unaaibishwa na mwanao live kisa chuki binafsi...kikwete huyo mwanai ipo siku atakuletea nyumba ndogo nyumban na kumfukuza mama salma kwa maisha unayoishi..ona sasa unaaibishwa na watoto wadogo badala ya kusukuma gari la raisi anageuka kuwa BASHE.....KAZI IPO NA NYIE MLIOSUKUMA GARI MSIISHIE HAPO WASUKUMENI NJE KABISA HILO JIDYBWASHA LA CCM WAJUE SAUTI YA WATU SAUTI YA MUNGU
 
Mhuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:decision:
 
Hawa mafisadi wa CCM ilitakiwa NEC ianze wananchi ndo wamalizie. Wewe watu wengi wanasema halafu unataka vihiyo wachache wenye chuki binafsi ndo wamalizie? Haiwezekani.
They will learn in a hard way, damn them!
 
Bado nashangaa sana; huyu Dr. Kigwangala ni nani hasa kiasi cha wazee wazima CCM kuwa radhi kujikanyagakanyaga hadharani kuhusu uraia wa Bashe ili tu kumpitisha kiwizi tena baada ya kutupa sababu muflisi za kumruka Selelii. Yaani wanakubali aibu yote hiyo kwa ajili ya mtu tu au ni zaidi ya hapo? He surely has to be some force to reckon with. :A S confused:
 
Hata hivyo, mgombea huyo wa CCM alitoa kauli ya unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ambao wanatumia dawa za kurefu maisha kwamba wamepata maambukizi hayo kutokana na kiherehere chao kwani wangeweza kujizuia na maambukizi hayo.

Wakati Kikwete akitoa kauli hiyo dhidi ya waathirika, takwimu zinaonyesha kwamba watu 9500 katika Mkoa wa Tabora wanatumia dawa hizo kati yao 2,700 wanaishi katika Manispaa ya Tabora.

SIjui tumetoa wapi huyu raisi...How the hell can someone say that eti kiherehere...very bad...Poleni ndugu zangu...
 
Ninaomba kutumia fursa hii kukumbusha kutimiza wajibu wako wa kupiga kura ifikapo Octoba 31. Ninatuma huu ujumbe wa watu 2000 nilio nao kwenye barua pepe yangu. Ninaomba sana utume ujumbe kwa angalau watu 50. Ujumbe uliopo chini ya shukrani ni muhimu sana hasa kwa wafanyakazi. Natanguliza shukrani.
Ujumbe kwa marafiki wote na watu wanaojali hatima ya Tanzania :Kisha nikasikia sauti ikisema "wafanyakazi wangu wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii na wana elimu lakini hawana maarifa" Je hawakuona mafisadi wakikamatwa bila kuhukumiwa? Hawakusikia JK akisema hahitaji kura za wafanyakazi? Je elimu yako inakusaidiaje kutambua kuwa rasilimali za nchi zinanufaisha watu wachache? Tanzania bila CCM inawezekana. Kubali na amini hili na ufikishe ujumbe na ndugu na jamaa 50. Mgomo ulitishiwa je hata kura yako ya siri? Ukifanya kosa Oct 31 usije tafuta mchawi. [/COLOR]
 
Back
Top Bottom