kigoma ndiyo ngome kuu ya upinzani Tanzania bara

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
chanzo changu kimeniambia kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2010 majimbo yote ya mkoa wa kigoma yalidondokea upinzani.
Mchezo mchafu ulifanywa katika yale majimbo machache yaliyotangazwa kuchukuliwa na ccm.
Kama kawaida masanduku ya kura yalibadilishwa na yale yenye kura halali kutiwa kiberiti.

Muhabarishaji wangu ananiambia kuwa haikuwa rahisi kuiba kura bila kushirikisha mawakala wa vyama pinzani.

Muhabarishaji mwingine ananiambia yeye kama msimamizi wa kituo kimojawapo cha kupigia kura alijitolea fedha mfukoni mwake ili kuwanunulia maji mawakala wa upinzani.kwa upande wa ccm,mawakala wake walionekana wamewezeshwa vilivyo,huku wana chupa ya maji kule wana chupa ya soda.hii inapelekea mawakala wa upinzani wenye njaa kurubuniwa kirahisi na kutoa mwanya wa kuchakachua.
 
chanzo
changu kimeniambia kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2010 majimbo yote ya
mkoa wa kigoma yalidondokea upinzani.
Mchezo mchafu ulifanywa katika yale majimbo machache yaliyotangazwa
kuchukuliwa na ccm.
Kama kawaida masanduku ya kura yalibadilishwa na yale yenye kura halali
kutiwa kiberiti.
Muhabarishaji wangu ananiambia kuwa haikuwa rahisi kuiba kura bila
kushirikisha mawakala wa vyama pinzani.
Muhabarishaji mwingine ananiambia yeye kama msimamizi wa kituo
kimojawapo cha kupigia kura alijitolea fedha mfukoni mwake ili
kuwanunulia maji mawakala wa upinzani.kwa upande wa ccm,mawakala wake
walionekana wamewezeshwa vilivyo,huku wana chupa ya maji kule wana
chupa ya soda.hii inapelekea mawakala wa upinzani wenye njaa kurubuniwa
kirahisi na kutoa mwanya wa kuchakachua.

hii ni sababu ya kusahaulika kiuchumi.
 
Upinzani kigoma ni kutokana na hali ngumu na kuachwanyuma ki maendelea! kwa mchakato unaoendelea sasa hivi utaona upinzani kushuka au kufa kabisa maana ccm wamewekeza vilivyo kule
 
Upinzani kigoma ni kutokana na hali ngumu na kuachwanyuma ki maendelea! kwa mchakato unaoendelea sasa hivi utaona upinzani kushuka au kufa kabisa maana ccm wamewekeza vilivyo kule

Upinzani Kigoma unaongezeka wabunge wawili wa ccm waliobakia Kigoma lazima wachinjiwe baharini come 2015.
 
Mimi nadhani eneo kuwa hoi kiuchumi na kuwa na upinzani mkali havina uhusiano. Badala yake mikoa ile ambayo iko nyuma sana kiuchumi/kimaendeleo ndiyo inayoongoza kwa kuikumbatia ccm.
 
Upinzani Kigoma unaongezeka wabunge wawili wa ccm waliobakia Kigoma lazima wachinjiwe baharini come 2015.

Peter Serukamba hatafika 2015, Mark my words, mwisho wa ubunge wake 2011, Mahakama itatengua ubunge wake na by election hata akisaidiwa na pesa za EL hataweza kushinda. Juzi nilimuona mahakamani jinsi PRESSURE ilivyokuwa imempanda.
 
Mkuu siyo Kigoma peke yake matokeo yalichakachuliwa, ni nchi nzima.
Ingekuwa siyo uchakachuzi Dr. Slaa angekuwa rais leo.
chanzo changu kimeniambia kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2010 majimbo yote ya mkoa wa kigoma yalidondokea upinzani.
Mchezo mchafu ulifanywa katika yale majimbo machache yaliyotangazwa kuchukuliwa na ccm.
Kama kawaida masanduku ya kura yalibadilishwa na yale yenye kura halali kutiwa kiberiti.

Muhabarishaji wangu ananiambia kuwa haikuwa rahisi kuiba kura bila kushirikisha mawakala wa vyama pinzani.

Muhabarishaji mwingine ananiambia yeye kama msimamizi wa kituo kimojawapo cha kupigia kura alijitolea fedha mfukoni mwake ili kuwanunulia maji mawakala wa upinzani.kwa upande wa ccm,mawakala wake walionekana wamewezeshwa vilivyo,huku wana chupa ya maji kule wana chupa ya soda.hii inapelekea mawakala wa upinzani wenye njaa kurubuniwa kirahisi na kutoa mwanya wa kuchakachua.
 
Peter Serukamba hatafika 2015, Mark my words, mwisho wa ubunge wake 2011, Mahakama itatengua ubunge wake na by election hata akisaidiwa na pesa za EL hataweza kushinda. Juzi nilimuona mahakamani jinsi PRESSURE ilivyokuwa imempanda.

ifike sahemu mtu au chama kikithibitika kuiba kura kipigwe faini kulipia gharama za uchaguzi.na pia mbunge arudishe gari,posho na stahili zote alizopata alipokuwa mbunge feki.
 
Mkuu siyo Kigoma peke yake matokeo yalichakachuliwa, ni nchi nzima.
Ingekuwa siyo uchakachuzi Dr. Slaa angekuwa rais leo.

siku zinavyozidi kwenda watendaji waliohusika na wizi huo wanaendelea kufunguka.
 
mbona kusini pamechoka sana licha ya kuipenda ccm

Hili nitarudia kulisema tena na tena hata kama mamluki wa CHADEMA hawataki kulisikia jambo hili. Watu wa kusini na pwani kwa ujumla sio majuha kiasi wafikie kushabikia kiongozi ambae hawamjui na wanaishia kumsikia kwenye vyombo vya habari! Mamluki wa CHADEMA wamekuwa wakisema eti watu wa kusini na pwani kwa ujumla hawajasoma na ndio maana wanaichagua CCM! Ni kweli kabisa, kama alivyozumgumza mtoa mada; Kigoma ni ngomeya upinzani tangu siasa za vyama vingi vianze nchini! Mamluki wanazani Arusha ndio ngome ya upinzani, kumbe Arusha ni full CCM with exceptional of few areas!! Upinzani, hususani CHADEMA hawajafanya lolote la maana katika kutafuta uungwaji mkono mikoa ya kusini na pwani kwa ujumla! Baada ya uchaguzi mkuu 2010, CHADEMA walitangaza kufanya maandamano nchi nzima......nikasema hapa hapa kwamba am certain kwamba CHADEMA kusini hawataenda! Na hicho ndicho kilichotokea na bado wapuuzi wachache wanaishia kusema watu wa pwani hawajasoma na ndio maana wanaiunga mkono CCM! Waswahili wana msemo wao; heri ya shetani unayemjua kuliko malaika usiyemjua! CHADEMA kwa kusini na pwani kwa ujumla ni sawa na malaika anayesikika tu toka kwenye vyombo vya habari! Ni upuuzi kudhani wananchi wa maeneo hayo ni wajinga kiasi waanze tu kubabaika kwa kuwasikia viongozi kwenye medias! Tukirudi Kigoma; upinzani Kigoma haukuja kwa bahati mbaya.....upinzani Kigoma ulijengwa na ukajengeka! Upinzani wa Kigoma ulijengwa zaidi na Dr. Aman Kabouru ambae alikuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA! Aidha, ukaja kupata nguvu zaidi baada ya kuibuka kwa umaarufu wa Zitto Kabwe!! Hivyo basi, bado nawaambia CHADEMA kwamba katu wasitarajie kuungwa mkono kwa kupitia JF!! Huwezi kupata uungwaji mkono sehemu ambayo hata ofisi huna! hapa ndipo ninapomshangaa anayejiita Great Thinker kusema eti CHADEMA walipokwa ushindi 2010!!!! Utashinda vipi urais wakati umewekeza kwenye baadhi tu ya wilaya (sincerly, not mikoa!) At least hadi 2010, mathalani ukichukua Arusha; ukiondoa Arusha mjini kote CHADEMA haikuwapo!! Na huo ni mfano tu; with exceptional of Kigoma, mikoa mingine yote ipo sawa na Arusha!Then hapo atokee mtu unawaambia wengine kwamba eti CHADEMA walinyang'wanywa ushindi!!!
 
True, kwa wale wanaosema Arusha siyo. KG hawataki unafiki. Hata kama waki invest lazima wapigwe chini, CCM wamefanya kosa la kuruhusu warundi waanzishe vijiji visivyo rasmi maporini na kuruhusu wafugaji kutoka Rwanda na sehemu zinyingine kuvamia ardhi ya wakulima
 
siku zinavyozidi kwenda watendaji waliohusika na wizi huo wanaendelea kufunguka.

Kigoma haijawahi kutoa viongozi wenye msimamo toka mwanzo hadi mwisho. Akiona atapitia kipindi cha umashuhuri wake kufifia au kukosa kile alichotaka yuko tayari kuwa saliti wananchi. Toka enzi za Kassanga Tumbo hadi sasa, yaani enzi za vyama vya wafanyakazi kuelekea uhuru wa Tanganyika.

Haya ni matokeo ya namna vile jamii zao nyingi wanavyoishi; kiongozi hutoka katika jamii. Wenyeji wa huko wengi wao atakuwa rafiki yako ili afanikishe mradi wake. Akipata tu, anakutupa huko yeye anasonga na semanini zake.

Nimeyasema hayo ili 2015 utakaposikia majimbo yote kasoro moja yamerudi CCM pamoja na hali ngumu na mateso yote yanayosababishwa na CCM, usiache mdomo wazi.
 
Chadema mkiandaa mgombea mzuri kasulu vijijini jimbo la obama ( albert fanuel ntabaliba) mtalichukua ki-ulaini. Obama si mwanasiasa lakini ana uwezo wa kuwahonga wapiga kura masikini.
 
Back
Top Bottom