Kigoma nako kinawaka huko...

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Habari za kuaminika kutoka kigoma ni kwamba walimu wa sekondari na shule za msingi leo kuanzia saa 6 mchana waliwafungia wakuu wa idara katika manispaa ya kigoma ujiji akiwemo mkurugenzi wa manispaa hiyo kushinikiza walipwe mishahara yao ya mwezi Februari mwaka huu. Wakihojiwa na mwandishi wa habari wa RFA Richard Katunka kutoka kigoma, walimu hao walisema mpaka leo tarehe 5 Machi bado hajalipwa mishahara ya mwezi wa pili na wameapa kutorudi kazini mpaka watakapolipwa mishahara yao....mpaka saa 11 jioni walimu hao walikuwa bado wanawashikiria mateka wao na waliapa kufa na yeyote atakaenda hapo kujaribu kutumia nguvu kuwatimua walimu hao. My take: Ndio sirikali imefuli eh?! aibu ndio tunaota kuboresha elimu kwa mwendo huu!
 
Walipoambiwa nchi haitatawalika walipuuza, ngoja sasa waonyeshwe cha moto!
 
Hao walimu bora wafanye kwa makundi manake kuwa na msimamo wote nchi nzima haiwezekani!!!!!!!!!!!!!!!
 
JK huu moto ukiwaka nchini kote,utaweza kuuzima?

Embu fikiria,umepanga nyumba ya kuishi,mwenye nyumba anadai kodi yake!!!Ulimwambia mwisho wa mwezi ntalipa ukijua kuwa utakuwa umepata salary!!!Then what?mpaka leo tarehe 6 hujajua utalipwa lini!!!hii imekaaje?

Bili ya umeme,maji navyo vinakusubiria,hapo bado matumizi ya nyumbani na nauli ya kwenda kazini!!
Yako wapi maisha bora mlioahidi??
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom