Kigogo wa UVCCM atiwa mbaroni

Averos

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
993
695

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Zainab Shaaban, ameburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kukata miti eneo la hifadhi ya misitu.

Shaaban, ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu, alifikishwa kortini Ijumaa iliyopita na kupelekwa rumande Gereza la Kiruru lililopo wilayani Mwanga baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Diwani huyo maarufu wilayani Same, ana mkataba wa kukiuzia magogo kiwanda kipya cha kuzalisha Spirits kwa matumizi ya viwandani cha Kilimanjaro Biochem, kilichopo eneo la Kifaru, wilayani Mwanga.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Mwanga, Hussein Mareng, kigogo huyo wa CCM anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 2, mwaka huu saa 12:30 jioni.

Inadaiwa kuwa, siku hiyo mshtakiwa ambaye hadi jana alikuwa akisota Gereza la Kiruru, aliingia eneo hilo la hifadhi ya misitu lililopo Kivisini, wilayani Mwanga na kukata miti hiyo.

Mshtakiwa alikanusha mashtaka hayo na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh5 milioni na mmoja wa wadhamini hao lazima awe mtumishi wa Serikali.

Diwani huyo na Mwenyekiti wa UVCCM Same, alishindwa kutimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni mtumishi wa Serikali na hadi jana viongozi wa CCM walikuwa wakihaha kutimiza sharti hilo.
Source: Mwananchi
 
hivi mwenyekiti wa wilaya (uvccm) naye ni kigogo?

Namimi nimeshangaa!! Ila kwa vitisho wanavyofanyaga hawa viongozi wetu, ndo hali iliyojengeka. Anaiba, anawanywesha pombe wanamuogopa, na kuanza kumuita kigogo. Haya ni baadhi ya majina kwenye sehemu za burudani kama Bar.
 
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Zainab Shaaban, ameburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kukata miti eneo la hifadhi ya misitu.

Shaaban, ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu, alifikishwa kortini Ijumaa iliyopita na kupelekwa rumande Gereza la Kiruru lililopo wilayani Mwanga baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Diwani huyo maarufu wilayani Same, ana mkataba wa kukiuzia magogo kiwanda kipya cha kuzalisha Spirits kwa matumizi ya viwandani cha Kilimanjaro Biochem, kilichopo eneo la Kifaru, wilayani Mwanga.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Mwanga, Hussein Mareng, kigogo huyo wa CCM anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 2, mwaka huu saa 12:30 jioni.

Inadaiwa kuwa, siku hiyo mshtakiwa ambaye hadi jana alikuwa akisota Gereza la Kiruru, aliingia eneo hilo la hifadhi ya misitu lililopo Kivisini, wilayani Mwanga na kukata miti hiyo.

Mshtakiwa alikanusha mashtaka hayo na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh5 milioni na mmoja wa wadhamini hao lazima awe mtumishi wa Serikali.

Diwani huyo na Mwenyekiti wa UVCCM Same, alishindwa kutimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni mtumishi wa Serikali na hadi jana viongozi wa CCM walikuwa wakihaha kutimiza sharti hilo.
Source: Mwananchi

hiyo ni kawaida ya ccm kwahiyo sioni cha ajabu. wizi wao, ufisadi wao, ubabe wao.
 
Ingawa tumeaambiwa hakuna aliye juu ya sheria, kuna wengine wana nguvu kuliko sheria hizo
 
wacha nao wajichukulie pale penye mamlaka napo kama wengine juu wanafanya hayo kwanini isiwe wao?
 
Back
Top Bottom