Kigogo wa CCM amwaga noti balaa.

Hivi mtu kama huyu, kwenye kamati ya maadili alielezea vyanzo vyake vya mapato? Na vikilinganishwa vinaendana na kodi anayolipa, na pesa anazomwaga? Naomba kuiamsha kamati ya maadili ya viongozi.

hii kamati ni kama boksi tupu halina kitu ndani wala usiitegemee ni sisi tuchukue maamuzi mengine tu!!
 
kauli mbiu ya uchaguzi wa diwani kirumba ni KULA CCM, KULALA CHADEMA.....ongeza nyingine Lameck,,sisi ndo CHADEMA bwana
 
Ni Lameck Airo mbunge wa Rorya kupitia CCM ametoa milioni 60 kuhakikisha CCM inashinda kiti cha udiwani kata ya Kirumba jijini Mwanza.Zinatumika kwa rushwa na kununua shahada za kupigia kura.Lameck ni mfanyabiashara maarufu na anamiliki pia hoteli ya kifahari hapa Kirumba ijulikanayo kama La Kairo Hotel.

Yote hayo ni kwa ajili ya kuidhibiti CHADEMA.

Nawasilisha.

hiyo ni kawaida ya CCM kumwaga noti hata kwa vijiviti vidogo vidogo
 
kauli mbiu ya uchaguzi wa diwani kirumba ni KULA CCM, KULALA CHADEMA.....ongeza nyingine Lameck,,sisi ndo CHADEMA bwana

da nimeipenda hiyo aisee na 2015 naona tuipitishe kama mbie nyenza katika kuhakikisha mambo yanakwenda kama yalivopangwa
 
Jamani wanachadema pokeeni hizo hela mkaimarishe chama! Acheni kukawia kawia jama bahati haiji mara mbili!
 
Aisee kweli hiyo?, kesho naenda ofisi zao pale nikiwa nimevaa shati la kijani. Mwaka juzi kampeni za Masha wanafunzi wa SAUT tulipewa magodoro bure. Nilipewa magodoro matano nikauza. Wakati wa kupiga kura nipo mwenyewe na sanduku. Wakati wa neema ndo huu! Asante mkuu kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom