Kigogo UVCCM mbaroni; Kwa tuhuma za kumteka kwa silaha na kumbaka binti wa miaka 22

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
NA PETER KATULANDA, MWANZA
Thursday, 28 April 2011


MJUMBE wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Barnabas Mathayo, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumteka kwa silaha na kumbaka binti wa miaka 22.

Habari za kuaminika zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa Mwanza, Simon Sirro, zilisema Mathayo anadaiwa kutenda unyama huo Aprili 24, mwaka huu, kati ya saa mbili hadi nne usiku.

Ilidaiwa kuwa Mathayo ambaye pia ni mfanyabiashara mjini hapa, alimlazimisha binti huyo (jina linahifadhiwa), kufanya tendo la ndoa baada ya kumpa lifti kutoka baa ya Kembice, iliyopo mtaa wa Uhuru.

Awali, ilidaiwa kuwa alimuita binti huyo kwa shughuli za kikazi, lakini baada ya maongezi aliondoka naye kwa kutumia gari lenye namba za usajili T. 345 AWS, ambapo alimgeuzia kibao wakiwa njiani kwa kumtishia bastola.


"Alimweka chini ya ulinzi na kumtaka atii amri yake, vinginevyo atamtwanga risasi. Alipelekwa katika hoteli moja iliyopo mtaa wa Rwegasore na kufanya tendo hilo," kilisema chanzo kutoka ndani ya Jeshi la Polisi. Tayari Mathayo amefunguliwa jalada namba MW/RB/3988/2011, kwa kile kinachodaiwa matumizi mabaya ya silaha.

Kamanda Sirro alisema jana kuwa, mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni Aprili 27, mwaka huu na kuhojiwa katika Kituo cha Mjini Kati, ambapo aliachiwa huru kabla ya kukamatwa tena juzi.

"Hakuna aliye juu ya sheria, ukivunja sheria unawajibishwa, tunaendelea kumhoji Mathayo na kuchunguza tukio hilo kwa kina," alisema Kamanda Sirro.

Kwa upande wake Mathayo alipoulizwa juu ya tuhuma hizo, alidai binti huyo ni mpenzi wake na siku hiyo walipanga kupumzika faragha, lakini walitofautiana kidogo.
 
wanajuana hawa na watayamaliza kifamilia !!WTF?? mwanamke anazidi kuonewa tu/ mm nikiwa rais mtu kama huyo hadi uchunguzi unaendelea yeye atakuwa anasota rumande bila dhamana
but this is CCM
 
ndugu mpaka upelekwe hotelini huyo kaitaka mwenyewe wee acha ile kitu ukiamua kugoma ata aje na risasi kwa maelezo tu nafikiri akimu atawaambia kamalizeni huko nileteeni changu kabla ya kuwapa dhamana mchazo kwishna
 
ndugu mpaka upelekwe hotelini huyo kaitaka mwenyewe wee acha ile kitu ukiamua kugoma ata aje na risasi kwa maelezo tu nafikiri akimu atawaambia kamalizeni huko nileteeni changu kabla ya kuwapa dhamana mchazo kwishna

Kuna tofauti kati ya hotelini na Guest House
* Hotelini ni kwenda kupunzika kwa Raha na Furaha na Migle
* Guest House ni Mapenzi i.e Faragha
 
wanajuana hawa na watayamaliza kifamilia !!WTF?? mwanamke anazidi kuonewa tu/ mm nikiwa rais mtu kama huyo hadi uchunguzi unaendelea yeye atakuwa anasota rumande bila dhamana
but this is CCM

Chama cha maovu. Kila uovu hufanywa na wana ccm bila kuchukuliwa hatua kali
 
inamaana huyo dada alipotekwa na kufika guest hapakuwa na counter au mtu yeyote si angeomba msaada, aaaaaagh upuuzi mtupu
 
Ccm enzi hizo ndo kazi yao naona wanakumbushia enzi zao. Kiongozi akisafiri hata mke wa mtu ataletwa
 
wanajuana hawa na watayamaliza kifamilia !!WTF?? mwanamke anazidi kuonewa tu/ mm nikiwa rais mtu kama huyo hadi uchunguzi unaendelea yeye atakuwa anasota rumande bila dhamana
but this is CCM

Ndo madhara ya small house haya. Kwa nini asikubambikie kuwa ulimbaka kama umemkataa. Kama mimi yeye huyu jamaa namtokea nambinua tena kisawasawa. Week ijayo anaenda kufuta kesi mwenyewe! Nyambafu!
 
Huyo dada Ni mtangazaji wa star tv alijipeleka mwenyewe ktafuta umaarufu ma be dau alilopewa dogo muachieni kidume huyo aendelee na biashara zake bana
 
........................... Tayari Mathayo amefunguliwa jalada namba MW/RB/3988/2011, kwa kile kinachodaiwa matumizi mabaya ya silaha.

............
Kwa upande wake Mathayo alipoulizwa juu ya tuhuma hizo, alidai binti huyo ni mpenzi wake na siku hiyo walipanga kupumzika faragha, lakini walitofautiana kidogo.[/COLOR][/SIZE][/FONT]


Can somebody ready for me the shit in ready? i cant believe my eyes!!! Yaani ni kwa matumizi mabaya tu ya silaha?......hayo mengine hayaonekani au makusudi?

Huyu anatakiwa aongezewe mashtaka


  1. Matumizi mabaya ya silaha
  2. Kubaka
  3. Kutishia kuua
  4. Udhalilishaji wa Kijinsia
  5. Matumizi mabaya ya Cheo chake
  6. Kulazimisha tendo la ndoa
Hii biashara yaweaz kuwa kama ile ya Mzee wa Vijisenti na Kibajaji.........
 
watamalizana wenyewe kama ni kigogo atamwaga vijisent hapo kwa polisi na binti nae ataandikiwa cheki ya vijisent kadhaa na kwa njaa yake atakubali fasta mambo yataisha utasikia akikanisha kumbaka bali walikubaliana na kwa vile binti sii mwanafunzi hakuna sheria itakayombana huyu kigogo.
 
inamaana huyo dada alipotekwa na kufika guest hapakuwa na counter au mtu yeyote si angeomba msaada, aaaaaagh upuuzi mtupu

Mkuu haya mambo yanatengenezeka (simaanishi kama katengeneza)...

.hakuna linaloshindikana kama nia ipo babaakee, mchongo unafanyika unapitishiwa geti la uani huku kitu kimekukalia shingoni chabaridiiiiiiiii!!!


Alafu ukizingatia mida yenyewe ndio ile ya kagiza giza ka jioni, weeee


Halafu pia Mkuu sio kwamba alitekwa, alichukuliwa kwnye gari kistaarabu kabisa......hujasoma hiki kibwagizo nini?
Nanukuu "Awali, ilidaiwa kuwa alimuita binti huyo kwa shughuli za kikazi, lakini baada ya maongezi aliondoka naye kwa kutumia gari lenye namba za usajili T. 345 AWS, ambapo alimgeuzia kibao wakiwa njiani kwa kumtishia bastola."Mwisho wa kunukuu

 
Back
Top Bottom