Kigogo ahusishwa wizi mamilioni kwa mtandao

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
TCRA nao watachunguza nini hapa? Hawana uwezo hata mdogo wa kuweza kuwagundua hao Wanigeria!
Kigogo ahusishwa wizi mamilioni kwa mtandao
Sunday, 12 July 2009 17:01 *Adaiwa kuvamiwa hotelini Uingereza
*Taarifa kuomba msaada zasambazwa
*TCRA yachunguza kubaini wahusika

Peter Masangwa na Salum Pazzy

WIZI mpya wa kutumia mtandao wa komyuta umeingia nchini na tayari ofisa mmoja wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi amehusishwa akidaiwa kuomba msaada mamilioni ya pesa kwa jamaa na marafiki baada ya kuvamiwa na kuporwa kila katika hoteli moja aliyofikia mjini London, Uingereza.

Uchunguzi uliofanywa na Majira umebaini kuwa matapeli hao wamekuwa wakitumia mbinu za kitaalam kufungua anwani za barua pepe za watu mbalimbali wakiwemo vigogo na kusambaza ujumbe kwa watu anaowasiliana nao, kuomba msaada wa haraka wa pesa.

Akizungumza na Majira mmoja wa vigogo wa Wizara ambaye jina lake limetumiwa vibaya na matapeli hao hivi karibuni,alieleza kusikitishwa kwake na mchezo huo mchafu na kuwataka ndugu, marafiki na jamaa zake kujihadhari kutapeliwa na watu hao wasiojulikana.

"Nilishangaa kupigiwa simu na watu ninaowafahamu kutoka nchi mbalimbali wakinipa pole na kutaka ufafanuzi namna ya kunisadia baada ya kupata ujumbe feki wa barua pepe kutoka kwangu kuomba msaada wa mamilioni ya pesa haraka,"alisema, Bi. Grace Kibaya, Ofisa Habari Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.


Bi. Kibaya alisema taarifa hizo zilimsikitisha na kufuatilia kujua kulikoni mtu anayesambaza ujumbe huo wa kumdhalilisha mbali ya malengo ya utapeli.


Alisema baadaye alibaini mtandao wake kuvamia na matapeli wa kimataifa wanaoendesha wizi kwa kutumia mitandao ya kompyuta ambao walifungua anuani ya barua pepe yake na kusambaza taarifa hizo.

Ujumbe uliosambazwa, ulidai kuwa Bi. Kibaya yuko nchini Uingereza na amevamiwa na kunyang'anywa kila kitu na majambazi hotelini hivyo anaomba msaada haraka wa pauni 1,500 (zaidi ya sh. milioni 1.5)

"Pole sana ndugu yangu, mimi ni mzima wala siko Uingereza. Nimepokea simu kutoka India, Algeria nao wakieleza kuwa wamepokea ujumbe wangu wa e-mail(barua pepe) nikiomba msaada, si kweli hata kidogo," gazeti hili lilimkariri Bi. Kibaya akimjibu mmoja wa watu waliompigia simu kumpa pole na kutaka ufafanuzi.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy alipoombwa kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, alisema wanalifanyia utafiti ili kubaini matapeli hao.


Aliongeza kuwa TCRA inafuatilia kujua idadi ya watu waliotumiwa ujumbe huo na namna matapeli hao walivyofanikiwa kupata anwani zao za barua pepe.


"Hatuwezi kutoa taarifa zozote kwa sasa lakini tumepokea tatizo hilo na tunalifanyia kazi, tutakapomaliza, tutawajulisha ikiwa pamoja na kuwafikisha watuhumiwa katika vyombo husika," alisema Bw. Mungy.

Katika siku za karibuni, imezuka tabia ya matumizi mabaya ya mitandao ya kompyuta hali inayotishia usalama na kupunguza ustaarabu wa teknolojia hiyo.

Hivi karibuni Serikali ililazimika kutangaza msako mkali dhidi ya wamiliki wa mtandao wa Ze Utamu ambao umekuwa ukidhalilisha watu mbalimbali wakiwemo viongozi.
 
TCRA nao watachunguza nini hapa? Hawana uwezo hata mdogo wa kuweza kuwagundua hao Wanigeria!

Acha DHARAU WEWE, ni lini umefanya utafiti na kujua uwezo wa TCRA *tanzania **ngine bwana **metekwa kifikra na wazungu kiasi cha kujidharau **nyewe....
SHAME ON YOU.
 
Back
Top Bottom