Kigoda cha Mwalimu: Prof. Shivji vs Mkapa

Arusha Mambo

Senior Member
Jan 27, 2011
174
150
LIVE:
ili kusikiliza tembelea www.arushamambo.com click ''Sikiliza Arusha Mambo FM....'' ili kusikiliza,
tutafurahi ukituunga Mkono kwa ku ''Like'' Radio yetu kwenye Tunein Page baada ya kufunguka.
Elewa kwa nini Rais Mstaafu Mh, Benjamin Mkapa alikuwa Mkali katika mjadala huo......
 
One of the best president of this country.

Yes wote hatujakamilika tunamapungufu, mabovu tunarekebisha.

Fuatilia TBC1
 
Speak for yourself. He could have been had he not turned out to be a thief and a sell out.
 
mdahalo ni mzito sana huu wacha tuone baadae ntarudi kwa more comment
 
Mbona anakuwa na asila anapoulizwa maswali jamani

Watu wanauliza maswali yale yale for 10 years, yaani kila mtu akipata fursa ya kuongea na Mkapa for the past 10 years atalalamika kuhusu ubinafsishaji.

Ameongea hapa kuwa kati ya Viwanda 300 alivyo binafsisha, 180 wamepewa wa Tanzania na vingine zaidi ya 40 serikali ya tanzania ina hisa, na vilivyobaki waliuziwa wageni.

Amekuwa akieleza haya mambo kwa miaka 10 sasa, why are we still asking the same question over and over again.

Na kati ya watu ambao tangu waulize hivyo viwanda hawajaviendeleza kwa asilimia kubwa ni wa TZ.

Ok Mkapa alikosea na kuuza viwanda, je baada ya yeye kuuza viwanda hivyo ni viwanda vingapi vipya vilivyojengwa so far? Kuna mtu ana takwimu zake hapa atueleze.

Criticism ni nzuri lakini mara nyingi huwa hazijengi, tuachane na ubinafsishaji wa wa viwanda wa Mh. Mkapa, je tumefanya nini kwa miaka kumi sasa kwenye secta ya Viwanda?
 
Nimemsikiliza Ben Mkapa kwa makini, huyu jamaa ALIKUWA GOOD PRESIDENT.
 
This guy was tough, imagine ten years to come, this current president in the same seat as Mkapa, unadhani ataongea nini? Atabaki kucheka tu.
 
Kwa mtazamo wangu baada ya kumsikiliza BWM. Alikuwa na mtazamo wa Tanzania aitakayo, tatizo yawezekana ni muda au waliopokea vijiti/kijiti hauwajui au hawakubaliani na nini alikuwa anafikiria. Maswali aliyotoa yanaonyesha kuwa bado anaamini alikuwa sahihi na hakuna aliyeweza kuonyesha kuwa hakuwa sahihi. Hivyo ni jukumu la serikali ya sasa kujibu kuwa hakuwa sahihi au umeshindwa kufanya kazi.
 
Ben Mkapa anauliza, nitajieni viwanda vipya vilivyofunguliwa tokea nitoke madarakani... Watu kimya...
Mkapa ameongea kwa vision kubwa sana, JK hata robo ya akili ya Mkapa hajafika.
 
Ben Mkapa anauliza, nitajieni viwanda vipya vilivyofunguliwa tokea nitoke madarakani... Watu kimya...
Mkapa ameongea kwa vision kubwa sana, JK hata robo ya akili ya Mkapa hajafika.

President Mkapa anadai tunamatatizo ya sukari jamaa wa kilombero sugar wameomba eneo ili waongeze kiwanda na uzalishaji lakini for over 5years ardhi hawajapewa.
 
LIVE:
ili kusikiliza tembelea www.arushamambo.com click ''Sikiliza Arusha Mambo FM....'' ili kusikiliza,
tutafurahi ukituunga Mkono kwa ku ''Like'' Radio yetu kwenye Tunein Page baada ya kufunguka.
Elewa kwa nini Rais Mstaafu Mh, Benjamin Mkapa alikuwa Mkali katika mjadala huo......

Waheshimiwa mbona mwapiga muziki tu..vp kigoda kishaisha?
 
Mkapa mwizi tu, yeye ndio chanzo cha kufuga mafisadi..amefanya kipi kizuri? Amewapigia debe mafisadi na chama chake kuendelea kula nchi na mali za uma, halafu leo anauliza serikali ya chama chake imejenga viwanda vingapi, kama sio upuuzi?
Binafsi naungana na hoja ya Nyerere.. Mkapa alipwe peshen yake na chama chake na sio serikali... MWIZIIIIII
 
kaka zangu...samaki wa dhahabu hana pa kujificha...niko safarini sijapata nafasi ya kutazama kivumbi, lkn namjua rais wa awamu ya tatu uwezo wake wa kujenga hoja...ah! anasema marehem shaaban roberts..."mbwa wa msasi mkali, ni wakali kama msasi mwenyewe"...huyu bwm.alikuwa ni mmoja wapo wa mawaziri waandamizi na tegemezi wa jkn....lkn bado pia...wanasema.." the more learned and witty, the more fit to serve the shetani" uuzwaji wa nyumba za serikali, mbona hajaulizwa? au hadhara hiyo si mahali pake?
 
Mkapa is my role Model, in reality ameongea mabo ya msingi sana ambayo watanzania wa sasa hatuyatazami na wala hatuyafikirii.
Mkapa kasema kuwa tumebaki siku zote kulalamika tu,
1. Hakuna aliyekuja na utafiti kuonysha kwa nini ubinfsishaji umeshindwa tunapiga mayowe, wazungu husema no research no right to speak.
2. Mkapa kasema pia mamlaka iliyopewa hii sera ya ubinafsishaji hakutumia muda wake kumobolize wananchi ili waelewe dhana ya ubinafsishaji ili wananchi wajiandae kwa mitaji na elimu ili kuintergrate hii dhana kwa vitendo. akatoa mfano mobilization ya vita ya ID amin ilivyokuwa mobilized na wananchi kushiriki kwa kujitolea. Yeye kama Rais kazi yake kutoa chagizo na baadaye mamlaka husika kusimamia.
3. Pia Mkapa amezungumzia kuhusu vusion ya 2025 aliyoiacha ambayo mimi na wewe hakuna aliyeshaisoma, ambayo hii imeeleza kuwa Taifa hili mpaka muda huo linatakiwa kuwa Taifa la namna gani, na hii inahitaki uelewa kwa wananchi ili watekeleze kwa vitendo, lakini sasa tumekuwa walalamishi na wachakachuaji. Mfano alitoa kiwanda cha Nyumbu kilitengeneza powertllars ambazo hazikuwa na uwezo wa kulima au kutumika katika maeneo mengi hii ni kutikana na kufanya utafiti ambao hauendani na hali halisi ya mazingira. Poor in technology and innovation.
4. Pia kasema lazima tuwe na independence integrity, yaani baada ya miaka 50 lazima tuwe na haya
-food security tuwe na uwezo wa kuzalisha wenyewe chakula cha kutosha na siyo kwenda kuomba kwenye mashirika ya kimataifa kama OXFARM n.k
-tuwe na uwezo wa kutumia kile tunachozalisha lakini pia lazima tuwe na uwezo wa kutumia tekinohama. coz kama hatuna uwezo bado ubinafsishaji utakuwa hauna maana kwetu. mfano gas mikoa ya kusini, kama hatuna technologia hatuwezi kuchimba gas hivyo bado itatulazimu kuleta wawekezaji kutoka nje.
-lazima applicabl education na siyo elimu ya nadharia.
lazima tuwe na strategy na outline za Taifa .
Mh. Mkapa kasema mengi sana ya msingi ambayo watu waliokuwepo kwa ukweli walikuwa wakimshangilia kwa makofi kwa jinsi alivyokuwa anaelezea mambo kwa ufasaha. ki ukweli hata prof. Shivji alionyesha kumkubali.
My take what i see here ni kwamba Mh. Mkapa alikuwa na vision nzuri sana na taifa hili lakini time ndiyo ilikuwa shida na type ya mtu aliyemwachia madarka ndo shida zaidi.
Right angebaki madarakani hadi sasa real kwa jinsi tulivyokuwa tunakwenda kiuchumi tungekuwa mbali na uchumi ilikuwa unakuwa kweli.
Let don't blame our President he did alot of his best together with his weakness la haki yake tumpe. si kama Mkwe.re ambaye anazurura duniani.
Mh. Makapa kama uko humu nakwambia kuwa mimi i still love you forever for the whole of my life time i will be in this World.
Katika maisha yangu tangu nipate akili sijawahi kumwona kiongozi yeyote poa akawa na mafanikio katika uongozi kunzia primary mpaka sasa naona level ya rais. Kiongozi serious like Mkapa is the most of them wamekuwa na succesfully leadership na maendeleo.
 
watu wengi wanasema anakuwa na hasira, kwa binadamu wa kawaida kama unakuwa attacked kwa namna ile kwa kukosa uelewa nafikri hata mimi na wewe tungepandwa na hasira tu, si rahisi kusimama mbele ya watu ambao unajibzana nao hoja lakini mioyoni mwao wanakulaumu kuwa ni chanzo cha maisha magumu. pia cha kushangaza watu walikuwa wanarudia mabo yaleyale. Nimemshangaa hata mzee Makwaiya Mh. Rais alikuwa ameshalizungumzia afu yeye bado anarudia hilohilo.
Pia JF tuwe tunapost mambo ya kweli. Siku ile huu mjadala watu walisema Mkapa ametoka nje maada lakini jinsi nilivyoona na watu walivyokuwa wameandaliwa wala hakutoka nje mada. Mkapa namfahamu ni Brain yule he think before talking.
tukumbuke yale yote yalikuwa yanaotoka kichwani na hakuwa na karatasi zaidi ya ile ya kunukuu hoja wanazo mmuliza.
Sasa mleteni kilaza wenu MKWE>re ataanza kutafuta madesa mwisho wa siku anakolapse.
tusiongee kwa chuki ila pale penye ukweli tuseme ukweli.
MKAPA was the best presudent,
 
mkapa ana mapungufu yake, lkn ni mjenga hoja mzuri wa kiwango cha "kiulimwengu"..mimi huamini ccm isingeukimbia mdahalo wa wagombea urahisi wakati wa uchaguzi wa 2010 kama mgombea angekuwa mkapa(na si kiwete wala wa aina ya kikwete, maanake hao ndio waliojaa ndani ya ccm kwa sasa)..na "angewashangaza" wapinzani wake...! mungu amemjalia uwezo mkubwa wa kufanya tafakari... mjenga hoja "nyahala nyahala, na mwenye kichwa pamba"...ktk hadhara BWM itamuwia vigumu kumuelewa...
 
no one like former president mkapa!jf mtaongea sana lakini ukweli upo wazi kwamba mzee mkapa uwezo wake kiungozi ni mkubwa,wote tumeshuhudia kwenye kigoda cha mwalimu,na tbc jana wamerudia,hvi jaman katba inasemaje?hakuna uwezekano wa kumrudisha mzeee mkapa?
 
Back
Top Bottom