BIG Banned
JF-Expert Member
- May 4, 2012
- 262
- 71
Wanawatangaza wanapowasimamisha halafu wanawarudisha kimyakimya! Loh!
Ikelege anateuliwa na nan????na kwanini chami hakumtosa???ulimsikia alivyosema??
Nimeamini tatizo TBS lilikuwa ni Ekelege tu. Toka aondoke hatusikii upuuzi wa makampuni ya kitapeli tenaMfupa uliomshinda Dr. Cyril Chami Dr. Abdallah Kigoda ameuweza.
Nimeamini tatizo TBS lilikuwa ni Ekelege tu. Toka aondoke hatusikii upuuzi wa makampuni ya kitapeli tena
Tatizo mara nyingi ni wapuuzi wachache wakipewa madaraka huyatumia vibaya na matokeo yake kuchafua jina zima la bodi wanayoongoza. Ekelege aliigeuza TBS kijiwe cha kupiga dili za kipuuzi na alikuwa mjeuri sana, sijui ni kwa nini lakini Kigoda naona hakumuonea aibu kamtupilia mbali na vikampuni vyake vile vya Quality hongkong na Wtm uk hatuvisikii tena. Pia bidhaa feki zimekuwa adimu mitaani sasa at least watu tuna amani na vitu kutoka nje . Yule mzee angeachiwa aendelee pale tbs ingefikia siku tungeletewa dawa feki za malaria na ukimwi kwa sababu jamaa yeye alikuwa hajali uhai wa mtanzania. Hatukatai kila mtumikia zizini hula zizini lakini sio kula ng'ombe badala ya kunywa maziwa. Serikali sasa iangalie na wizara nyingine pia.Naelekea kukubaliana nawe maana hali inavyojionyesha tatizi zaidi si mfumo maana ni mfumo huo huo uliokuwepo tangu enzi za awamu ya kwanza, tatizo ni watu na hili nimeliona sehemu nyingi tu hata kwenye taasisi za kibenki. Bank hizo hizo zamani zilikuwa zinafanya kazi vizuri na kwa ufanisi mkubwa kwa utaratibu huo huo lakini leo utaratibu huo haujabadilika lakini mizengwe leo hii ni kupindukia.