Kigoda aingia kwa mkwara: Charles Ekerege wa TBS out!

Kumbe ilikuwa inawezekana Waziri kumsimamisha kazi Mkurugezi wa TBS, sasa Chami alishindwa nini?

Chami alikuwa hajapewa go ahead na JK. Kwani wewe hukusikia aliyoyasema JK siku anamtangaza Kigoda na wenzake kuwa mawaziri?. Soon utasikia na bandarini kumenuka!. Ni mwendawazimu pekee atakayedhani kuwa waziri ndiyo katoa maamuzi haya. Kuna mtu ambaye hapendi lawama ndiye anatoa idhini hii huku amejificha chini ya dawati asionekane. 'Leading while hidding'

images

 
Tena huyu mama si ndio yuko behind hii kampuni ya vitambulishi vya Biashara ( Barcodes)? Hembu wanajamvi mwageni details zake hapa watu waseme, Nchi hii tumechoka kwa kweli.
 
wakunyonga huyo,alakini kwakua lile dubwana liko na bekam ulaya , hakuna jipya.dawa yake iko jikoni
 
Jambo ambalo bado sijaelewa na serikali haitaki kueleza, ni kwanini Ekelege hajapelekwa mahakani? Ushahidi upo, report ya CAG inaelewa kila kitu, kamati ya bunge inao ushahidi, sasa kwa nini huyu bwana hajapelekwa mahakani? Tukumbuke kipindi hiki ambacho amekuwa suspended bado anahesabika kuwa ni mwajiriwa wa TBS na hivyo atakuwa analipwa mshahara! Huku sio kuchezea watu akili?
 
waooooo! mbona ule nani hii, ule wa ile wizara ya nishati na madini namaanisha D Nja... kimya au ndo wametoa kazini tu basi?????????
 
Waziri wa viwanda na biashara Abdalah Kigoda amewaambia bodi ya tbs kumsimamisha kazi mkurugenzi ili uchunguzi ufanyike,
naona kaanza na kaspeed
 
Ameiagiza body ya shirika la viwango kumsimamisha kazi Ekelege huku Uchunguzi ukiendelea

Source: Taarifa ya habari ITV saa mbili usiku leo.
 
Kwa nini imechukua muda mrefu hivi? mpaka watu walianza kuidharau serikali kwa ajili ya mwizi mmoja tu
 
Hata wangempeleka mahakamani hamna kitu ndg yangu, kwani akina Mramba na Yona wako wapi. Nchi hii ni usanii tu! Serikali ya kishikaji hii, hamna kitu hapo!.
 
Kwa taratibu zilezile za utumishi wa umma, kilichotokea ni kiini macho tu..!

Ni suala kama la Jairo tu...

Gear nyepesi sana kwa siasa za kisasa duniani.
 
Tatizo ni kwamba, I don't trust huyu Abdallah Kigoda! Endapo patatokea mtu akaniambia nitaje baadhi ya viongozi ninaoamini kwamba ni mafisadi basi nitakuwa mnafiki nisipomtaja huyu bwana! Napata shida sana kila nikikumbuka role yake alipokuwa kwenye wizara ambayo ilihusika moja kwa moja na uuzaji wa mashirika ya umma!
 
Nchi ya Wasanii. Mkwara mzito kumbe si lolote si chochote. Hawa jamaa si ndio wanaokwenda kuwalipa pesa za kustaafu Mawaziri waliofukuzwa kwa wizi!

Wonders in Tanzania shall never end!
 
Atahamishiwa kitengo gani baada ya kuharibu huko? Hawa wazee wanafikiri nini kuharibu uzeeni?
 
new episode baaada ya ile ya JAIRO NA BLANDINA
usanii mtupu.tuone anachukuliwa hatua kali.Chami alisema hana uwezo wa kumsimamisha au kumfukuza
Kigoda kapata wapi hayo mamlaka sasa?
 
Back
Top Bottom