Kigoda aingia kwa mkwara: Charles Ekerege wa TBS out!

Anatakiwa achukuliwe hatua kuonyesha kuwa kumwondoa peke yake haitoshi, na pia iwe mfano kwa wengine.
Wasiifanye tbs kama jikoni tu.
 
suspension then transfer follows,overall system of acountability for public servants needs a major review.ni utoto watumishi kuharibu and let go free kama hakuna damage wamefanya!
 
Hata kama hazitarudi,hii itafanya pawepo na ka umakini kidogo ili kitumbua kisiingie mchanga mapema.

Mnasubiri amechota pdm na kwenda japan ndo mumfukuze? Yaani mwizi anasaidiwa kuiba? Mwalimu kwa nini ulikufa mapema? Akhgrrrrr
 
Kumbe ziara aliyofanya Japan, na Beijing hivi majuzi ilikuwa ya kuaga na kukusanya balance zake zilizokuwa zimebaki. Sheria ichukuwe mkondo wake ili hicho alichokusanya kitumike kwa dhamana.
 
Kumbe ilikuwa inawezekana Waziri kumsimamisha kazi Mkurugezi wa TBS, sasa Chami alishindwa nini?
 
What PCCB for, is mismanagement of Public funds dealt under PCCB ? that isn't bribery, who did Ekelege bribe then.

If PCCB has nothing to do with Ekerege, what then are PCCB doing with CAG report regarding Hon. Mkulo and other former ministers?
 
Watu kama hawa china siku nyingi wapo chini ya futi sita.Nashangaa wa bongo na umasikini wetu tunawalea
 
Haya sarakasi zimeanza, Ekelege alikula mno utamu ukakolea akajisahau akakuta amemshika kipofu mikono
 
Safi Dr Kigoda, that's a good start. Sasa chungulia na TANTRADE mapema kabla halijakulipukia bungeni Dodoma mwezi june. Natumaini umemuona Mhe. Filikunjombe juzi kwenye front page ya gazeti moja la kila siku akinywa ulanzi na wazee wake huko Ludewa yote ni maandalizi kwa mapambano ya kuleta uwajibikaji.
 
Mi' naona kaonewa tu, kwanza dili halikuwa la kwake, ulikuwa mchongo wa mtu mwingine kabisaaa! Na kwa kusimamishwa kwake ni kuondoa zengwe tu, lakini hasara tushapata kama kawa, manake fedha tulizohesabu hasara ndo hazirudi tena.
 
ufisadi wa kitanzania hauna jina wala formula. kila mtu anakula pale anapofikia. Ekelege hayupo peke yake.
 
My TAKE.

This is the Decision that Honourable Chami should have make long time back. It would have enabled him retain his post. The Honorable Chami; is a good guy who works hard, tatizo hapa nadhani ni kuoneana haya na ushauri mbaya. Sasa sijajua hatua itakayofuata, kwani kumuonda Chami na Ekelege peke yao sio muarobaini.

Uamuzi wa Mheshimiwa Waziri ni KUMSIMAMISHA KAZI sio kumfuta KAZI, hivyo; Ekelege bado ni mtumishi wa Serikali/TBS. Hili naamini limefanywa ili kupisha uchunguzi wa TUHUMA dhidi yake; endapo ataapatikana na masuala yanayoweza kupelekea kuwa na hatia, basi sheria itafuata Mkondo, ikiwemo kufutwa kazi na kufikishwa mahakamani. Kwa wakati huu, ni mapema mno kusema ni nani ndio atakayesimamia kikamilifu jalada lake, kwani kuna DCI na PCCB; ila naamini litaanzia kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa TBS ambao wanaweza kuunda Kamati, itakayowapa taarifa na maoendekezo.
 
Unajua hizi kesi ndiyo zinatumaliza dawa hapa ni kumfilisi, chukua mali zake zote maana siku hizi watu wanasafisha fedha zao chafu kwa develop assets so we should think of confiscating whatever they have accumulated all along ili kujenga discipline. Vinginevyo ni mchezo uleule.
 
kama kigoda ana mamlaka ya kumsimamisha kazi Ekelege
Chami alishindwaje manake alisema hana mamlaka hayo.
by the way kumsimamisha haitoshi bila kuwaona wakifikishwa mahakamani na mali
zao kutaifishwa ikiwezekana auzwe yeye na familia yake kufidia deni

yale yalikua ni maneno ya mkosaji...unafanya mchezo na kitumbua kuingia mchanga weye?
 
Kumbe ilikuwa inawezekana Waziri kumsimamisha kazi Mkurugezi wa TBS, sasa Chami alishindwa nini?

Kama na wewe unauliza, wengine watafanya nini sasa!? Kumbe mnajifanya mnayajua mambo ya cdm wakati hata namna serikali ya chama chenu inavyofanya kazi hamjui! Upuuzi mtupu!!!
 
Matatizo yapo kwenye uongozi na system kwa ujumla wake. Hata huyo kigoda hajamfukuza Ekelege bila kupata 'go ahead' kutoka kwa JK. La msingi hapa, inatupasa tutambue kuwa system ya nchi ni mbovu, inatupasa kwenye mabadiliko ya katiba tuweza kubadili mambo ya msingi, tufanye kadiri tuwezavyo hii katiba mpya iwezd kuziba hii mianya, vinginevyo tutaendelea kupiga kelele tu....
 
Back
Top Bottom