Kigoda aingia kwa mkwara: Charles Ekerege wa TBS out!

Mtumishi Mkuu

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
259
92
Habari nilizozisikia mchana huu kutoka itv ni kwamba yule mkurugezni wa TBS, bwn Ekelege hatimae kasimamishwa kazi kutokana na kashfa zinazomkabili.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekerege amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50 ya punguzo la ada ya utawala kwa Kampuni mbili na kulisababishia shirika hilo hasara ya Dola 42,543 za Kimarekani.

Kampuni hizo ni, Jaffar Mohamed Ali Garage na Quality Motors za jijini Dar es Salaam.
Ekerege alifikishwa mahakamani hapo Jumatano mchana kimya kimya na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Ausustina Mmbando.

Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Janeth Machuya alidai kwamba kati ya Machi 28 mwaka 2008 na Agosti 7, mwaka 2009, katika ofisi za TBS iliyopo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa nia ovu Ekerege alitumia madaraka yake vibaya.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa punguzo la asilimia 50 ya ada ya utawala kwa kampuni hizo bila idhini ya baraza la utendaji la TBS kinyume cha sheria namba 2 kifungu kidogo cha (3) ya TBS ya mwaka 2005.

Ilidaiwa kuwa kitendo hicho kiliziongezea kampuni hizo faida ya Dola 42,543 za Kimarekani sawa na (kwa wakati huo) Sh. Milioni 68,068,800.
Upande huo wa Jamhuri ulidaiwa shitaka la pili, katika tarehe na mahali pa tukio la kwanza, mshtakiwa alilisababishia shirika kupata hasara ya fedha hizo.

Mshtakiwa alikana mashitaka yote mawili na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na haukuwa pingamizi la kutoa dhamana dhidi ya mshtakiwa.

Hakimu Mmbando alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi za kuaminika watakaosaini hati ya Sh. Milioni 35 kila mmoja.

Mshtakiwa alitimiza masharti hayo ya dhamana na yuko nje hadi Desemba 12, mwaka huu atakaposomewa maelezo ya awali.

Chanzo: Michuzi
 
Wanasimamishwa kama kiini macho kwa ajili ya kudanganya jamii, lakini mwisho wa siku wanawasafisha na kuwarudisha kazini.
 
Naona amecheleweshwa sana kwani amechangia sana kuanguka kwa Waziri wa Wizara husika.
 
Anapumzishwa nyumbani kwake ama Segerea,watu kama hawa wanaposubiri uchunguzi wanapaswa kuwa selo
 
Hii nchi yetu hii yaani huyu bwana bila wabunge na wananchi kukomaa atolewe pale tbs angeendelea kula nchi tuu.
 
Naona hii imetokana na picha alizozirusha kwa Michuzi juzi akiwa Japan na baadhi ya wakurungezi wa bodi ya TBS wakikagua ofisi za wakaguzi wa magari huko (JAAI). Reactions za watu zilikuwa mbaya juu yake wakisema amaeamua kwenda sehemu hiyo kama danganya toto kwa uhuni aliouonyesha kwa Singapore na Hong Kong. Ngoja tusubiri tuone mwisho wake.
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Dr Abdallah Kigoda amemsimisha Bwana Ekerege wa TBS.

What next? Hela walizokula wajanja kwa kisingizio cha kukagua magari huko nje zitarudi?
 
badala ya kumtimua wanamsimamisha? huu ni usanii uliotukuka
kwani kina Nyoni na Jairo nao si hivo hivo lkn tunasikia wanatumia magari ya serikali
na bado wanaonekana wizarani humo?
tuone mabadiliko makubwa sio usanii
 
Hata kama hazitarudi,hii itafanya pawepo na ka umakini kidogo ili kitumbua kisiingie mchanga mapema.
 
According to wanabidii Waziri wa Viwanda na Biashara Dr Abdallah Kigoda amemsimisha Bwana Ekelege wa TBS.

What next? Hela walizokula wajanja kwa kisingizio cha kukagua magari huko nje zitarudi?

The decision took too long. Has he been handed to PCCB?
 
Halafu kwenye orodha ya hayo makampuni hewa kuna moja lina jina la "Quality...." nahisi litakuwa la Manji hili. Kwahiyo suala hili linawezekana lina uhusika wa wakubwa sana serikalini na huenda ndo maana Chami alikuwa anapata kigugumizi kumsimamisha kazi Ekelege.
 
ekelege ekelege ekelege ekelege ekelege ekelege ekelege ekelege ekelege..
 
kama kigoda ana mamlaka ya kumsimamisha kazi Ekelege
Chami alishindwaje manake alisema hana mamlaka hayo.
by the way kumsimamisha haitoshi bila kuwaona wakifikishwa mahakamani na mali
zao kutaifishwa ikiwezekana auzwe yeye na familia yake kufidia deni
 
kama kigoda ana mamlaka ya kumsimamisha kazi Ekelege
Chami alishindwaje manake alisema hana mamlaka hayo.
by the way kumsimamisha haitoshi bila kuwaona wakifikishwa mahakamani na mali
zao kutaifishwa ikiwezekana auzwe yeye na familia yake kufidia deni

Sasa ateremke kwa Katibu mkuu, hapo kisiki!
 
Back
Top Bottom