KIgamboni Serikali Imelala: Kuanzia saa 2 Usiku nauli hupanda kuania TZS 500 hadi TZS 1000

Rich Dad

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
748
133
Habari ndio hiyo, Kigamboni haina serikali. Watu wanaendesha maisha wanavyotaka wao. Ikifika saa mbili usiku nauli za daladala zinapandishwa kwa kiwango wapendacho madereva kuanzia TZS 500 hadi TZS 1000.
Kiwango hicho hakiangalii unashuka wapi, sehemu yeyote utakayoshuka nauli ni hiyohiyo.
 
Habari ndio hiyo, Kigamboni haina serikali. Watu wanaendesha maisha wanavyotaka wao. Ikifika saa mbili usiku nauli zinapandishwa kwa kiwango wapendacho madereva kuanzia TZS 500 hadi TZS 1000.

Nauli zipi za ferry au hiace za huko?
 
Njia ya kigamboni inakera sana madereva wa daladala wanakata routes wanavyotaka nauli nazo ndo mvurugano mtupu.
 
Katika mchango kwenye bajetiya Wizara ya Uchukuzi jana niliongelea kuhusu kukatisha ruti na upandishaji wa nauli holela katika Jimbo la Kigamboni. Vile vile nimeshawasiliana na Mhe.Waziri kwa hatua zaidi.
Ninaomba kujua ruti nyingine zenye matatizo kama haya ili niweze kuzifanyia kazi. Ahsanteni.
Dkt Faustine Ndugulile
Mbunge Kigamboni
 
Mheshimiwa kumbe upo humu JF!
asilimia kubwa ya hiace za kigamboni hazina mistari ubavuni inayoonyesha inaelekea route gani lakini cha ajabu zinaendelea kutoa huduma bila kuchukuliwa hatua.
Mheshimiwa sio mbaya ukaangalia na swala la uporaji kwani ikifika saa 11 jioni kigamboni sio salama kwa watembea kwa miguu.
 
Bw Ndibalema! Nitashukuru kupata maeneo yenye tatizo la uhalifu ili niyafanyie kazi.
Mheshimiwa kumbe upo humu JF!
asilimia kubwa ya hiace za kigamboni hazina mistari ubavuni inayoonyesha inaelekea route gani lakini cha ajabu zinaendelea kutoa huduma bila kuchukuliwa hatua.
Mheshimiwa sio mbaya ukaangalia na swala la uporaji kwani ikifika saa 11 jioni kigamboni sio salama kwa watembea kwa miguu.
 
Katika mchango kwenye bajetiya Wizara ya Uchukuzi jana niliongelea kuhusu kukatisha ruti na upandishaji wa nauli holela katika Jimbo la Kigamboni. Vile vile nimeshawasiliana na Mhe.Waziri kwa hatua zaidi.
Ninaomba kujua ruti nyingine zenye matatizo kama haya ili niweze kuzifanyia kazi. Ahsanteni.
Dkt Faustine Ndugulile
Mbunge Kigamboni
karibu jf muheshimiwa pitia na jukwaa la mmu muheshimiwa mbunge... karibu sana
 
Mheshimiwa mbunge tatizo la kukata route limekua sugu hasa kwa daladala za kigamboni -kongowe cha ajabu zaidi hakuna msimamizi.
 
Mheshimiwa Mbunge nashukuru kwa jitihada zako za kusaidia kuondoa kero jimboni kwako kigamboni. Kwa kuongezea tu kwanye tatizo la usafiri, ni kukuosekana kwa vituo vya mabasi kwenye njia za kigamboni. Hii ni hatari na ni kero kwani madereva hupaki popote pale wanapojisikia ( kwenye vituo vingi visivyo rasmi).
Asante sana natumai utalifanyia kazi suala hili.
Katika mchango kwenye bajetiya Wizara ya Uchukuzi jana niliongelea kuhusu kukatisha ruti na upandishaji wa nauli holela katika Jimbo la Kigamboni. Vile vile nimeshawasiliana na Mhe.Waziri kwa hatua zaidi.
Ninaomba kujua ruti nyingine zenye matatizo kama haya ili niweze kuzifanyia kazi. Ahsanteni.
Dkt Faustine Ndugulile
Mbunge Kigamboni
 
Mheshimiwa Mbunge nashukuru kwa jitihada zako za kusaidia kuondoa kero jimboni kwako kigamboni. Kwa kuongezea tu kwanye tatizo la usafiri, ni kukuosekana kwa vituo vya mabasi kwenye njia za kigamboni. Hii ni hatari na ni kero kwani madereva hupaki popote pale wanapojisikia ( kwenye vituo vingi visivyo rasmi).
Asante sana natumai utalifanyia kazi suala hili.
Ni barabara zipi unazoongelea investa.tz?
 
Binafsi nina furaha sana kuhusu mbunge wangu kuwemo humu jamvini na kujadili matatizo ya jimbo letu letu moja kwa moja lakini tatizo kubwa linalozungumziwa hapa sidhani kama ni la kigamboni peke yake liko maeneo mengi sana nchi kwetu na linakera sana ila naomba kuchangia hoja hii kwa mtindo tofauti kidogo, kwanza ingependa mbunge alichukulie hili jambo kama hoja ya kitaifa badala ya kuangalia maeneo ya kwetu tu maana mara nyingi hawa wanakatisha safari hujadiliana na walioko kwenye daladala na kurudia mji mwema au ungindoni na wale wanaotaka kuja upande wa mjini hupata adhabu kubwa sana ila kwa kuna matatizo makubwa sana kigambo nzima kwa ujumla hasa masuala ya viwanja, maji, elimu na afya nadhani kuna matatizo ya ki utawala maana hata ukingalia utofauti wa shule za msingi mji mwema na maweni utaona tofauti kubwa wakati ni shule majirani kuna mengi ya kujadili kuhusu jimbo letu tena ya maana ni vizuri sisi tuliopata ka nafasi haka ka kujadiliana na mbunge wetu tujenge hoja za msingi na tuziwakilishe kwa mheshimiwa mbunge kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi badala ya kushambuliana humu jamvini.
 
Kwa kuwa na yeye ni sehemu ya jamii husika, lazima ayaelewe matatizo ya jamii yake. Pili, kuna njia nyingi za kuwasiliana na kuwasilisha maoni ofisini kwa mbunge hata kama sio muda wa kazi..yote haya ni kupitia humu jamvini..Hongera mheshimiwa kufanya kazi ya ziada ya kuonana na watu wa jimbo lako kwa njia hii ya mtandao.

Hii ni nzuri sana......kuna waheshimiwa wengine huwa wanapita JF kama watalii kutaka kujua wananchi wanasemaje lakini hawataki hata kusikia kama inawezekana kiongozi kuwa "The Solution Which is Looking Where the Problems Are"

Binafsi nina furaha sana kuhusu mbunge wangu kuwemo humu jamvini na kujadili matatizo ya jimbo letu letu moja kwa moja lakini tatizo kubwa linalozungumziwa hapa sidhani kama ni la kigamboni peke yake liko maeneo mengi sana nchi kwetu na linakera sana ila naomba kuchangia hoja hii kwa mtindo tofauti kidogo, kwanza ingependa mbunge alichukulie hili jambo kama hoja ya kitaifa badala ya kuangalia maeneo ya kwetu tu maana mara nyingi hawa wanakatisha safari hujadiliana na walioko kwenye daladala na kurudia mji mwema au ungindoni na wale wanaotaka kuja upande wa mjini hupata adhabu kubwa sana ila kwa kuna matatizo makubwa sana kigambo nzima kwa ujumla hasa masuala ya viwanja, maji, elimu na afya nadhani kuna matatizo ya ki utawala maana hata ukingalia utofauti wa shule za msingi mji mwema na maweni utaona tofauti kubwa wakati ni shule majirani kuna mengi ya kujadili kuhusu jimbo letu tena ya maana ni vizuri sisi tuliopata ka nafasi haka ka kujadiliana na mbunge wetu tujenge hoja za msingi na tuziwakilishe kwa mheshimiwa mbunge kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi badala ya kushambuliana humu jamvini.
 
Sorry Mheshimiwa mbunge nilipoweka post hii nilikwenda offline kwa muda. Mfano wa barabara zazongumzia ni ferry kuelekea mjimwema, kibugumo, gezaulole hadi kufika mwongozo. Kipande hiki tunashukuru kwa jitihada zako kimeongezwa kuwekwa lami siku za hivi karibuni, lakini shida ni kwamba hakuna vituo rasmi vya daladala ukiandoa gezaulole tu ( sehemu inaitwa geza juu). Sehemu yote iliyobaki hakuna vituo vya daladala, abiria wanakuwa kama mamwinyi vile kwa kuwataka madereva wawashushe sehemu yeyote wanayojisikia.
Ni barabara zipi unazoongelea investa.tz?
 
Ukweli ni kuwa jimbo la kigamboni serikali iliondoka zamani sana na kila mtu anajifanyia anyoona mema machoni pake mwenyewe, umetaja tu usafiri, hujaangalia kada zingine kama maji, barabara, nk. Najua sababu kubwa ni kwamba hakuna mkulu anayeishi huku hivyo ni vigumu kushughulikia mambo ya wananchi walalahoi...tena ukizidisha kidomodomo utashangaa majibu utakayopewa na wenye nchi. Usalama sifuri...weee acha tu
 
Back
Top Bottom