Kigamboni Bridge Contract Signed

,

Hii inaonesha kuwa MJI WA KIGAMBONI UTAKUWA NI WA KIBEPARI ZAIDI na kuwa watakaokaa maeneno hayo ni watu WENYE MAGARI TU ! au siyo ? Naomba Mr NSSf anijibu tafadhali ...haingii akilini kujenga daraja ambalo halina sehemu ya waenda kwa miguu wala baskeli , ni wazi huo ni mji mtarajiwa wa KIBEPARI ! Mr.NSSF tafadhali nijibu nina shauku!

Mkuu Mkomatembo punguza hasira kidogo,
Hilo daraja lina sehemu za waenda kwa miguu pia...kwa pande zote mbili. Dr. Magufuli amezungumzia pia kwenye hotuba yake hapo juu angalia kuanzia dakika ya 6.35.
 
Walengwa wa daraja hili la kulipia si ndio hao wanaoshindwa kulipia mia mbili? Ngoja tuone kama wataweza kulipia hapa! labda hao nssf na tanroad waweke kiwango hicho hicho cha jiti (mia)
 
Walengwa wa daraja hili la kulipia si ndio hao wanaoshindwa kulipia mia mbili? Ngoja tuone kama wataweza kulipia hapa! labda hao nssf na tanroad waweke kiwango hicho hicho cha jiti (mia)
nawashangaa sana watanzania -- yaani tunakubali eti daraja lijengwe la kulipia kweli? hilo daraja la mkapa Rufiji nani analipa? hili la salenda nani analipa? hilo la jangwani nani analipia? hilo daraja la Ruvu na kule wami nani analipia? yaani imefikia hatua madaraja na vivuko mnaanza kuvigeuza kutoka kwenye huduma za jamii sasa mnaingiza biashara kweli ni sahihi? yaani mmekosa vyanzo vya hela ila kuwatoza maskini wapitao kwenye hili daraja? miaka 50 ya uhuru tunaotambia tumethubutu tunashindwa kujenga daraja la 300b kwa hela zetu za ndani mpaka tukope kope toka mifuko ya jamii na wahisani? aisee let us be serious huu sasa utani umezidi guys!!!
 
nasangaa sana watanzania -- yaani tunakubali eti daraja lijengwe la kulipia kweli? hilo daraja la mkapa Rufiji nani analipa? hili la salenda nani analipa? hilo la jangwani nani analipia? hilo daraja la Ruvu na kule wami nani analipia? yaani imefikia hatua madaraja na vivuko mnaanza kuvigeuza kutoka kwenye huduma za jamii sasa mnaingiza biashara kweli ni sahihi? yaani mmekosa vyanzo vya hela ila kuwatoza maskini wapitao kwenye hili daraja? miaka 50 ya uhuru tunaotambia tumethubutu tunashindwa kujenga daraja la 300b kwa hela zetu za ndani mpaka tukope kope toka mifuko ya jamii na wahisani? aisee let us be serious huu sasa utani umezidi guys!!!

Mkataba umeshasainiwa mkuu, pole sana lakini hali ndio hiyo, watumiaji wa daraja lazima walipie ili NSSF warudishe pesa yao. Sasa hivi kampuni na watu binafsi wenye uwezo wanaruhusiwa kujenga barabara na madaraja ya kulipia ii kurudisha hela yao...

Ni mpango mzuri kwa sababu idadi ya barabara zitaongezeka kwa kasi na pia kupunguza misongamano isiyo na lazima...nchi nyingi zikiwemo za kiafrika zina miradi kama hiyo...

Nashangaa hujalalamika kwa nini miaka nenda rudi tumekuwa tunalipia kwenye vivuko vyote kuanzia cha zamani pale Rufiji, Kilombero, na Kigamboni ...:A S-coffee:

Btw, kwenye miradi ya namna hii waenda kwa miguu huwa hawalipii.
 
sasa bila ushaidi tutaweza kujadili nini?

Mbona TRA kumejaa madudu mengi tuu na hamlalamiki?

Kama wewe kweli ni msemaji rasmi wa nssf basi kuna kasoro flani hivi ambazo unazo na itabidi uzirekebishe au wakupeleke mafunzo zaid....kila kitu unajibu as if una uhakika wa asilimia mia moja...mfano ni pale unaposema wazi (pamoja na kuitaja) mifuko mingine haifanyi vizuri kama NSSF....ni vigezo vipi unatumia? Pili ni pale unaposema wazi kuwa TRA kumejaa madudu...sasa wewe ni msemaji wa TRA au NSSF? Na kama kweli wewe ni msemaji rasmi wa NSSF basi utakuwa umechomekwa.
 
Back
Top Bottom