Kigamboni Bridge Contract Signed

Fighter

JF-Expert Member
Aug 30, 2009
615
152
Wakuu,

Nipo kwenye hafla ya kutia sign ujenzi wa daraja Kigamboni.

Magufuli anaongea sasa!

UPDATE:

Hafla ilikuwa Serena na Clients ni NSSF na MoW kwa share ya 60 kwa 40.

Mkandarasi aliyeshinda zabuni ni CMBEC.

Shughuli imeisha hapa Serena hotel

VIDEO: Magufuli akiongea

[video=youtube_share;Ph1NCMpyxAg]http://youtu.be/Ph1NCMpyxAg[/video]

PICHA:


IMG_4361.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii,Dkt. Ramadhan Dau ( wa pili kushoto) akisaini vitabu vya mkataba wa mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ukandarasi ya China Railway Jiangchang Engineering,Bw. Shi Yuan (pili kulia) na Muwakilishi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Major Bridge Engineering,Bw. Zhou Yiqiao kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
IMG_4383.jpg

IMG_4411.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii,Dkt. Ramadhan Dau (kushoto) akibabadilirishana vitabu vya mkataba wa mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ukandarasi ya China Railway Jiangchang Engineering,Bw. Shi Yuan mara baada ya kusaini leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Wengine Pichani ni Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufulli,Waziri wa kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Sadick,Balozi wa Misri nnchini.
IMG_4477.jpg

Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufulli akihutubia leo wakati wa hafla ya utiliaji wa saini wa mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambao unatarajiwa kuanza siku yeyote kuanzia hivi sasa leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mkataba huo umesainiwa baina ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Wakandarasi kutoka nchini China ambao ni CHINA RAILWAY JIANGCHANG ENGINEERING CO. (T) LTD na MAJOR BRIDGE ENGINEERING CO. LTD.
IMG_4460.jpg

Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akihutubia katika hafla hiyo leo ambapo ametoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuomba kazi za ujenzi huo wa mradi wa daraja la Kigamboni.
IMG_4435.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick akihutubia katika hafla hiyo.
IMG_4274.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii,Dkt. Ramadhan Dau akifafanua jambo wakati wa kutoa hotuba yake juu ya mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ambao utagharimu kiasi cha sh. Bilioni 214.6 na utachukua muda wa miezi 36.
IMG_4295.jpg

Mtaalamu wa Ujenzi wa Madaraja kutoka nchini Misri,Eng. Shwaibu akitoa maelekezo ya namna ujenzi huo utakavyokuwa.
IMG_4291.jpg

Mtendaji Mkuu wa Tanroads,Eng. Patrick Mfugale akitoa ufafanuzi wa namna waliovyoweza kufanya utafiti wa namna mradi huo utakavyofanyika na mpaka kufikia kumalizika.

IMG_4500.jpg

Picha ya mfano wa Daraja hilo la Kigamboni.

Picha na maelezo yake kwa hisani ya Othman Michuzi
 
Magufuli anaongea sana kitu gani ?tuhabarishe anachoongea tuweze kuchangia,lakini tufahamishe nani amekuwa awaeded hiyo tender ya kujenga hilo daraja?
 
Samahani, hilo daraja tutajua tunalipia au?
Kama tutalipia ushuru wa daraja afadhali lisijengwe ila kama ni free kama la manzese poa tu
 
Samahani, hilo daraja tutajua tunalipia au?
Kama tutalipia ushuru wa daraja afadhali lisijengwe ila kama ni free kama la manzese poa tu

Hamna cha bure ndugu nakupa mfano nilipokuwa China kutoka hangzhou kuna barabara mbili ... Ya chini ambayo ni free utatumia masaa ma nne kufika shanghai na kuna ya juu hangzhou - shanghai express way masaa mawili ... Hiyo inalipiwa itakuja kuwa bure mpaka bajeti ya pesa iliyotumika irudi...
 
alichoongea maghufuli leo
[video=youtube_share;Ph1NCMpyxAg]http://youtu.be/Ph1NCMpyxAg[/video]
yalianzia huku
[video=youtube_share;Jh2jQcnWcQo]http://youtu.be/Jh2jQcnWcQo[/video]
 
Mbona dunia inajua limeshaisha na limeshafunguliwa na kuanza kutumika??
 
Wakuu,

Nipo kwenye hafla ya kutia sign ujenzi wa daraja Kigamboni.

Magufuli anaongea sasa!

UPDATE:

Hafla ilikuwa Serena na Clients ni NSSF na MoW kwa share ya 60 kwa 40.

Mkandarasi aliyeshinda zabuni ni CMBEC.

Shughuli imeisha hapa Serena hotel

Hiko ni kifupi cha nini? Chines .......or something else?
 
Kampuni ya wapi imeshinda zabuni hiyo,na time frame ya hiyo project ikoje?
 
Mkuu suala la kulipa ni lazima. Hata hapa Mozambique barabara itokayo Maputo kama mtu anaelekea Gaza provision maeneo ya Chokwe lazima kulipia barabara. Pia nimeona Korea Kusini mji wa BUSAN ukitokea town kuna daraja refu sana na linapunguza umbari endapo unakwenda airport. Magari wanalazimika kulipia hela. Hii ni nzuri kama haichakachuliwi. Kimsingi NSSF wanaweza kukomboa mtaji wao kirahisi!
Hamna cha bure ndugu nakupa mfano nilipokuwa China kutoka hangzhou kuna barabara mbili ... Ya chini ambayo ni free utatumia masaa ma nne kufika shanghai na kuna ya juu hangzhou - shanghai express way masaa mawili ... Hiyo inalipiwa itakuja kuwa bure mpaka bajeti ya pesa iliyotumika irudi...
 
Kati ya hizi kampuni sita mojawapo ndio itapewa zabuni ya kujenga daraja la Kigamboni sasa sijui itakuwa ni kampuni gani..

1. Long Jian Road and Bridge Limited - China
2. Schuan Road and Bridge Limited - China
3. China Communication and Construction Limited - China
4. China Railway Construction Engineer Group - China
5. China Major Bridge Engineer Limited - China
6. Chong Qung - China
 
Msanifu aliyechora daraja la Kigamboni ni kutoka Misri anaitwa Mohamed Shohayeb wa Arab Consulting Engineers

DSC00760.JPG
 
Back
Top Bottom