Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,216
- 113,510
Hakuna cha asili wala nini. Mambo yetu yalikuwa poa tu zamani. Hadi siku mvua ilipoanza kutunyea!
And what do you know?
Hakuna cha asili wala nini. Mambo yetu yalikuwa poa tu zamani. Hadi siku mvua ilipoanza kutunyea!
Ndugu zangu,
Hili ni jibu langu ninalolirudia mara kwa mara katika topic za namna hii, sambamba na Julius na msimamo wake wa 'miafrika ndivyo tulivyo'. Basi, mimi nasema hivi:
Hata kama tungelikuwa hatuna scientific ingenuity au kuwa ma-proponent wa tafiti za kisayansi ya hali ya juu, kama wengi ya watu wetu (haswa viongozi tuwachaguao) kwenye jamii zetu tungelikuwa si wenye tamaa, si wanafiki, si wazembe, si watu wa kuridhishwa na kilichopo bali wa kutafuta kilichozaidi kwa ajili ya manufaa ya jamii nzima, si watu wa kudharau wasionacho ndani ya jamii zetu; hakika tungelikuwa tuna maendeleo makubwa kuliko tulivyo hivi sasa. Kwa mara nyingine tena nitamalizia kwa sentensi ifuatayo:
Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi.
Steve Dii
Hakuna cha asili wala nini. Mambo yetu yalikuwa poa tu zamani. Hadi siku mvua ilipoanza kutunyea!
- Tunaweza sana ku-create haya yasiyoweza kutuendeleza, that is all!
Respect.
FMEs!
Umeshawahi kusikia nchi ya Malta?
ndicho nilichokisema; ni uongozi.
sasa na leo sisi tunazo?
swali zuri.
ni kwa sababu ya uongozi; mwanzoni tulikuwa tunapenda vya kwetu na kuvitumia kwa fahari.
Yapo magonjwa mengine yanayowapata watu weupe zaidi vile vile lakini haina maana huwezi kupata mweupe mwenye sickle cell!
sidhani kama hiyo ni hoja; wakati wa Warumi lugha iliyotawala ilikuwa ni Kilatini! Leo hii lugha kubwa ni kiingereza usije kushangaa huko tunakokwenda tukajifunza Kichina zaidi. Mambo mengine ni histojiografia inaoongoza.
Hatuwezi kutengeneza vya kwetu kwa sababu ya uongozi. Hivi unajua hata huko kwa wazungu na wenyewe walikuwa wanafanya madudu tunayoyafana sisi wakati huu?
nope. It starts and ends with leadership; bear in mind I'm not speaking of political leadership only!
Mwanakijiji, hayo yote au mengi ya uliyoyasema na kuyataja yanahusu Tanzania. Je, ina maana na kwingineko Afrika hususan kusini mwa sahara (black Africa) na kwenyewe tatizo lao ni uongozi mbovu? Kama ni hivyo ina maana uongozi mbovu ni common denominator Afrika nzima kusini mwa jangwa la sahara. Sasa kwa nini kote huko kuwe na uongozi mbovu? Ndivyo Tulivyo kuwa hatuwezi uongozi? What is it? Maana mimi siamini kabisa kuwa hizo nchi zingine za Kiafrika zimetuzidi kihivyo. Nimeshabahatika kutembela baadhi ya nchi za Kiafrika na sikuona lolote la ziada tulilozidiwa. Kama ufisadi hata Cameroun upo. Kama vya kupenda vya Ulaya basi hata Niger wanapenda vya Ulaya. Sasa nisichoelewa ni kwa nini Afrika nzima kusini mwa sahara ni sehemu iliyo ktk kundi la nchi za ulimwengu wa tatu. Sielewi kabisa hili. Inakuwa kuwaje eneo kubwa kama hili kiwango cha maendeleo kinakuwa kimefanana sana?
Bara la Ulaya sio nchi zote zilizoendelea saana kihivyo. Hakuna uniformity ya maendeleo. Huwezi kulinganisha kwa mfano maendeleo ya Ujerumani na Uholanzi na yale ya Romania. Lakini hata hao Romania wameendelea kuliko nchi karibu zote kama sio zote kabisa za Afrika, Sasa huu uongozi mbovu ina maana upo Afrika nzima? WTF.....
nimekugongea senksi for this useful argument.Huwezi ukazungumzi mambo haya na haya yako hivi bila kusema ni kwanini yako hivyo,at least hapa JF tungeweza kuwa na standards hizo,za kujaribu kufikiria zaidi na zaidi.
Kwa mfano hukujiuliza ni kivipi impacts za Iron curtain Countries ama za Cold wars zilivyo tofauti na zile za Slavery,Colonialism na Neo Colonialism.
Hatuwezi kukaaa hapa JF na kusema eti sisi ndivyo tulivyo,ilitakiwa useme sisi bado tuko kwenye struggles za uhuru wa kweli ambao ndio utatupatia maendeleo ya kweli.
Mkuu kama utakumbuka kuna document linaitwa vision 2025, hilo ndio wanaliita dira ya maendeleo ya Tanzania. Mkiweza tafuteni mlisome. Mimi nimelipitia, ukiangalia unaweza kusema ni mwelekeo mzuri kweli, lakini utekelezaji wake ni sufiri. Nililisoma miaka kumi iliyopita lakini leo miaka 10 baadaye nikijaribu kuoanisha yale yaliyosemwa, kuhusu siasa, uchumi, mambo ya jamii na miundo mbinu naona sifuri hakuna kitu, tumerudi nyuma kuliko kupiga hatua yoyote. At least Ben Mkapa alijaribu kupiga hatua kwenye miundo mbinu.
Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza kulikuwa na clear vision, ambayo kiongozi wa wakati ule alikuwa akiipigania na kuitekeleza (leave alone uzuri au ubaya), na tulikuwa tunaona wazi kabisa.
Hili sio tatizo la JK, wala Pinda, ni la kwetu watanzania, may be ndivyo tulivyo, kazi zetu na mipango yetu ni ya mkono uende Kinywani. Tunaangalia mwaka huu tu, au mambo yanaweza kutufanya tushinde ubunge kipindi kinachofuata.
Haya kama historia ni ishu
Go back and check maendeleo ya wazungu kabla ya ukoloni na maendeleo yetu wakati huo.
Vingine ni visingizio tu.Tena nafikiri wakati mwingine wasingekuja hawa wakoloni kutuchapa viboko hadi leo tungekuwa tunavaa ngozi.
Si angalieni ambako wakoloni hawakufika Umasaini, wasandawe.
ama tuache hao wamasai na wasandawe nini tofauti kati ya taifa ambalo halikukubwa na ukoloni Ethiopia na South Afrika ambalo limekuwa chini ya wakoloni mpaka juzijuzi? the fact is very strong.
Mimi ningekuwa mshauri wa serikali, ningesema kabisa in the next say 5 yrs tuchague mikoa 5 yenye potential ya kuwa na success haraka kwenye kilimo, investment, viwanda nk na ndio serikali ipeleke asilimia kubwa ya funds na upendeleo huko ili maendeleo ya haraka yafanyike na iwe magnet ya watu kupunguza bomu la mauaji litakalofukuta Dar in the very near future.
Unaweza kupick Kilimanjaro/Arusha/Mbeya/Iringa/Ruvuma na kuanzia hapo.
Quoting the one and Only Kiranga, let me open a window of debate and slugs! If not the statement sort of quantify Nyani/Julius Ndivyo tulivyo.
Be it in Social aspect, economy, political, cultural, production, education entrepreneurship, management, leadership ot whatever, we always fail if not falling short and one has to wonder, TUNA MATATIZO GANI?
Is it psychological issues, colonial wounds, inferiority complex or just our nature?