Kifo kupitia mikono ya POLISI – Kosa la Marehemu?

...Pia hoja yako kuwa marehemu Daudi Mwangosi alimvaa RPC is very shaky. Mashuhuda wanasema kabisa kuwa marehemu alisema wengi wa askari waliofika mahali pale walikuwa ni wageni except RPC. Hivyo ni wazi, wakati anapigwa, 'alimwangukia' (asking for help) RPC kwa sababu kati ya sura ngeni zilizokuwa zinamzunguka alimtambua mkubwa huyo (RPC). Lakini RPC akaondoka! ..

FJM, Inaonekana Mashaka yako dhidi ya utendaji wa RPC yanaungwa mkono na baadhi ya polisi wenyewe. Uhusiano wa RPC na tukio zima unamuweka kwenye nafasi ngumu sana!! Ona taarifa za Polisi Wakorogana

Mkandara, Look like you postulated the correct concept to Zakumi,
Zakumi, ..Problem starts with the system itself not The Police force. I believe as long as Regional and District Commissioners will be voted in by people for the people with no influence to Magogoni.. It may work..
Read this ...

Polisi Wakorogana

• Anayetuhumiwa kuua mwandishi akwama kufikishwa mahakamani

na Abdallah Khamis​

WINGU jeusi limeendelea kutanda ndani ya Jeshi la Polisi mkoani Iringa baada ya baadhi ya askari mkoani humo kunyoosheana vidole kuhusu tukio la polisi kuua mwandishi, huku baadhi yao wakimlaumu Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), Michael Kamuhanda.

Askari kadhaa waliozungumza na gazeti hili kwa siri jana, walisema kama RPC angesikiliza ushauri wa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) kuhusu namna ya kukabiliana na wanachama wa CHADEMA, maafa yasingetokea.

Walisema Kamuhanda ndiye aliwaamuru askari wake kuwakamata viongozi wa CHADEMA waliokuwa kwenye mkutano wa ndani wa ufunguzi wa tawi katika Kijiji cha Nyololo, kwa maelezo kuwa hakuwaruhusu kufanya hivyo.

"Kama mnakumbuka, RCO mwanzo alizielewa hoja za CHADEMA juu ya vikao vyao vya ndani, lakini alipokuja RPC hali ikabadilika kutokana na kupewa maelezo na mkuu wetu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa," alidokeza mmoja wao.

Walisema kwamba hata katika tawi la kwanza walilofungua viongozi wa CHADEMA, RCO alifika lakini hakuwashambulia. Wakati wakifungua tawi la pili, ndipo RPC akafika, na amri zikatolewa kuwashughulikia viongozi na wanachama wa CHADEMA.

Kwa maelezo ya polisi hao, viongozi na wanachama wa CHADEMA hawakuwa wameleta fujo yoyote, na kwamba kama polisi wangelinda tu mikutano yao yaliyotokea yangeweza kuepukwa.

Askari hao walisema inasikitisha kwamba uamuzi wa mtu mmoja umelifanya jeshi zima lionekane baya mbele ya umma; na kwamba hata wao wanatii amri kwa sababu kazi yao haiwaruhusu kuhoji amri za wakubwa wao.

Baadhi yao walisema hata maneno na vitisho vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali, kwamba CHADEMA kina vurugu, ni uonevu na propaganda za kisiasa, kwani vurugu zilitokea pale CHADEMA walipoanza kutawanywa.

Habari ambazo hazijathibitishwa kutoka mkoani humo zinadai kuwa baadhi ya askari waliohusika kwenye vurugu hizo si polisi halali wa jeshi hilo, bali ni vijana wa mtaani ambao walivishwa sare kwa lengo la kuwadhibiti CHADEMA, ndiyo maana walikuwa wakibabaika katika matumizi ya silaha.

Wakati huo huo, jeshi hilo jana lilishindwa kumfikisha mahakamani askari polisi anayetuhumiwa kufyatulia bomu lililomchanachana na kumuua mwandishi wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Awali, taarifa za mtuhumiwa huyo kupandishwa kizimbani zilizagaa kila kona; gazeti hili likapiga kambi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa, lakini mtuhumiwa hakuletwa mahakamani.

Jana gazeti hili liliripoti taarifa za kukamatwa kwa siri na kuhojiwa kwa askari watano kati ya saba akiwamo yule anayetuhumiwa kumuua marehemu Mwangosi.

Tanzania Daima lilidokezwa kuwa askari wanaoshikiliwa kwa mahojiano zaidi ni wale walioonekana kwenye picha mbalimbali za magazeti na mitandao wakimpiga marehemu huyo kabla ya kumsababishia kifo.

Habari za ndani zilieleza kuwa mtuhumiwa huyo wa mauaji hakuweza kufikishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa kutokana na kuendelea kutoa maelezo mbele ya mlinzi wa amani.

Chanzo cha taarifa kilidai kuwa utaratibu huo wa kutoa maelezo ulianza juzi na huenda mtuhumiwa atafikishwa mahakamani Jumatatu.

"Suala la mauaji ni kubwa, si kama mashitaka ya mwizi wa kuku au karanga. Hivyo, juzi na jana yule bwana alikuwa anaendelea kutoa maelezo yake kwa mlinzi wa amani. Sasa suala la kukiri kuua au kutokuua litabaki katika moyo wake," kilisema chanzo hicho.

Source. http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=40285
 
Azimio JIpya,

Mkuu shukran kwa taarifa hii kidogo inatia moyo kwamba at last serikali imeamua kuchukua hatua japo hatufahamu hatma yake. Ni mwanzo mzuri na kwa hili nitamsifia Nchimbi na kamati yake..
 
1. Kumbuka haikuwepo ilani hiyo tu pekee, kwanza kabisa vyama vyote mkoani Iringa walishatangaziwa na Polisi wasifanye mikutano ya kisiasa wakati wa kampeni, wajizuie kwa wiki moja.

Ilani zilizotolewa zaidi ya hiyo ya kitambaa:

Halafu walitangaziwa siku ya tukio, licha ya hicho kitambaa cha ilani, walipewa ilani kwa njia ya vipaza sauti kuwa wasambaratike.
Kwa hiyo hili la Ilani utaona kuwa ni ukaidi ulifanywa makusudi kabisa na wanachadema wa Iringa, kwa nini? isitoshe:

Sasa wewe jiulize na ujibu, ikiwa mmepewa Ilani zote hizo na Polisi na mkakaidi na mkaingia kwenye vita na wao kwa dakika 30, halafu atokee mmoja hukohuko kwenye kundi linalipogana na Polisi aje amvae Mkuu wa kikosi, kwa nia yoyote ile, unafikiri kutakuwa na usalama kwake hapo?
2) Tukio lote lililotokea Iringa nalichukulia ni uvunjifu wa amani wa makusudi kabisa kwa "wapiganaji". Siasa sio kukaidi amri za Polisi kwa nguvu, hivi unategemea nini baada ya kuvunja amri za Polisi? Licha ya kuwawametangaziwa, hata ikitokea tu kuwa wamejikusanya kikundi cha watu ambapo polisi wanaona hapa kuna uwezekano wa amani kuvunjika basi wana haki ya kuwaambia watawanyike bila ilani yoyote ya kabla.

Sasa jiulize tena, hivi walikusudia nini hawa waliokaidi amri zote hizo na kupambana na mapolisi?

3. Ikiwa umeambiwa usifanye maandamano, ukayafanya kwa nguvu, ukatokea uvunjifu wa amani kwa polisi kuzuwia hayo maandamano, hapo unategemea nani alaumiwe?

Ikiwa unaambiwa usifanye mikutano siku fulani, wewe unaumuwa kufanya kwa nguvu wakaja polisi kuzuwia mkusanyiko huo ukakaidi na kupigana na Polisi ni nani wa kulaumiwa?

Conclusion:

Licha ya hoja zote hizo juu zinazoashiria uvunjifu wa amani wa makusudi kabisa, hata kwa bahati mbaya ukijikuta wewe ni mpita njia kwenye vurugu (riots) za namna hiyo na Polisi wameshatowa amri ya watu kutawanyika na wameshajipanga kuwafata na kuwatawanya wakitumia zana zao za kuzuwia fujo, usijaribu hata siku moja kuwafata wanapotokea na kuingia kwenye himaya yao kutokea walipo wanaotawanywa, kufanya hivyo ni:

1) amma kujitafutia kifo (suicide) kwa makusudi kabisa,

2) au kujitafutia kifo cha kujitowa mhanga (terrorism),

3) amma kujitafutia kifo kwa ujinga wa kwenda kuanzisha fujo na kutokujuwa namna ya kujihami yanapokushinda.

Chaguwa wewe ni yepi katika hayo yaliyomkuta Daudi?

Ukweli ubaki kuwa ukweli.

Zomba nashukuru kwa jibu lako, ila naomba nieleweshe nielewe vema. Hio ilani ilikuwa applicable kwa CDM peke yake na maeneo ya Iringa tu? Tukizungumzia kuzuiwa kwa hizo harakati za ki siasa kusimamishwa hatuwezi kusahau hoja ya sense ambayo ilikuwa ndio msingi wa sababu za kusitisha. Hapa kunakuwa na utata kidogo, kama walisitishwa ilikuwa vipi walipewa kibali cha kufungua tawi hapo na hali hairusiwi? Hivo vigezo vilitolekwa kila kituo cha mkoa na kigongoji peke yake hadi kukawa na clashes za utendaji?

Nikisoma hapo (asmuchas umesema nijjiulize) nakuwa na swali ambalo Napata kuwa kwanini walipewa kibali cha kufungua hilo t awi kama siku hio ilikuwa hairusiwi? Na jibu ambalo Napata linakuwa na uwalakini sana… Zaidi ni kuwa Napata maswali zaidi; Kwamba waliamua kupewa hicho kibali ili vurugu zije zotekee? AMA kuna mahusiano mabaya ya utendaji kama kufikisha ujumbe toka ngazi ya juu hadi ya chini?

Mie nakubaliana na kwamba in a way CDM wana makosa kadhaa katika matukio haya… Ila ambae anawezesha hayo makosa na mwenye kubeba msalaba mkubwa ni CCM. Kuna ule msemo kuwa tembo wakipigana ni nyasi ambazo zinaumia na hili hasa the applicability of it.

Hio conclusion uliotowa Zomba is just one side of the coin. Being as insightful as you are it would have been really great and brilliant to have heard another side of the coin from you… Free from ushabiki na full of reason and logic. Nina maswali yafuatayo…

Tokana na ukweli kuwa ukitowa tongo tongo na kuliangalia swala zima kama tu sio mwananchi na wala mshusika wa Siasa za Tanzania unaweza tambua na kuona kuwa kila kundi lina msalaba wa kubeba… Kwa kutumia hayo yaliyotokea unasemaje kuhusu Viongozi wa CCM kuendelea na shughuli za kisiasa wakati wa Sensa (hapa hapa Tanzania bara achana na Zanzibar ambako Mh. Nape kasema kuwa ndiko ziliendelea) na hali agizo lilitolewa kama ulivosisitiza na wala hawakugadhibiwa… Unadhani inatoa ujumbe/picha gani kwa vyama pinzani na wanachi ambao ni wanaharakati na wafuatiliaji?

N.B

Mifano halisi ya hizo shughuli na viongozi wa CCM wakati wa sensa ni:

  1. Mh. Muhsin Rafi Ismail aliesindikizwa na maandamano na wafuasi (kama sikosei siku mbili tu baada ya agizo) alipokuwa anawania nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya wa Chama cha CCM hicho pale Lindi.
  2. Mh. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo mh. Amos Makalla kuendelea na shughuli zake za kisiasa katika jimbo lake Mvomero.
 
AshaDii,

Majority of leaders in opposition camps are activists not executives or technocrats. They have never run and excute a budget. They have never run a payroll to pay salaries. They have never controlled security and defend forces. So there's a learning curve that isn't going to be achieve in a year or two.

The inexperience of opposition is there. So even though we want the opposition to win, we should control and manage our expectations. For example, changing the working habits of civil servants include the police officers will take time.

Now back to my friend Jasusi, he is being disingneous when he tells me that they will reform the police force when CHADEMA take power. I don't buy that. For, the only time Nyerere reformed the defend forces was when they undermined his authority. Likewise, if the security forces serve well those in power, we shouldn't expect miracles.

The underlined... It is so valid and yet have never observed from this angle. It is something to ponder on. Thanks.

The highlighted blue.. My EXACT thoughts and belief.
 
Azimio Jipya,

Tell me why do you need a benevolent dictator? Didn't you have one before? Anyway, the problem facing the country isn't the lack of benevolent dictator, but the lack of will.

Kagame hasa Great and strong will, does he not to some level qualify as a dictator? Come to think of it maybe it is the only way we Tanzanian would rise for the better :censored:
 
Hivi ni Polisi wangapi Tanzania hususan FFU ambao hata magazeti hawaruhusiwi kusoma wanaejuwa kuwa huyo Daudi alikuwa Mwandishi?

Hivi ni nani duniani zinapotokea fujo anatoka alikotoka kuja ku cross police line na kumvaa mkubwa wao akasilimika?

Tuache unazi. Kifo ni kifo zilizobaki ni sababu na hizo sababu nilizoweka juu haziepukiki kwa kifo cha huyu Daudi.

Ni nini kilichokuwa kinamtambulisha kuwa yeye ni Mwandishi wa habari lilipotokea tukio? ni nini kilichomfanya akamvae mkuu wa polisi, tusiwe biased kwenye hilo. Nasema huyo amma alikuwa amaemuwa kufa au kupona lakini hakubali mkutano wa chama chake uzuiliwe, au aliigia kujitowa Mhanga aondoke na askari wengine au hajui kujihami au kuhhami mwenzake zinapotokea fujo kama hizo. Yote hayo yanaishi kwenye suicide.

1. Kumbuka haikuwepo ilani hiyo tu pekee, kwanza kabisa vyama vyote mkoani Iringa walishatangaziwa na Polisi wasifanye mikutano ya kisiasa wakati wa kampeni, wajizuie kwa wiki moja.

Ilani zilizotolewa zaidi ya hiyo ya kitambaa:

Halafu walitangaziwa siku ya tukio, licha ya hicho kitambaa cha ilani, walipewa ilani kwa njia ya vipaza sauti kuwa wasambaratike.

Kwa hiyo hili la Ilani utaona kuwa ni ukaidi ulifanywa makusudi kabisa na wanachadema wa Iringa, kwa nini? isitoshe:

Sasa wewe jiulize na ujibu, ikiwa mmepewa Ilani zote hizo na Polisi na mkakaidi na mkaingia kwenye vita na wao kwa dakika 30, halafu atokee mmoja hukohuko kwenye kundi linalipogana na Polisi aje amvae Mkuu wa kikosi, kwa nia yoyote ile, unafikiri kutakuwa na usalama kwake hapo?

2) Tukio lote lililotokea Iringa nalichukulia ni uvunjifu wa amani wa makusudi kabisa kwa "wapiganaji". Siasa sio kukaidi amri za Polisi kwa nguvu, hivi unategemea nini baada ya kuvunja amri za Polisi? Licha ya kuwawametangaziwa, hata ikitokea tu kuwa wamejikusanya kikundi cha watu ambapo polisi wanaona hapa kuna uwezekano wa amani kuvunjika basi wana haki ya kuwaambia watawanyike bila ilani yoyote ya kabla.

Sasa jiulize tena, hivi walikusudia nini hawa waliokaidi amri zote hizo na kupambana na mapolisi?

3. Ikiwa umeambiwa usifanye maandamano, ukayafanya kwa nguvu, ukatokea uvunjifu wa amani kwa polisi kuzuwia hayo maandamano, hapo unategemea nani alaumiwe?

Ikiwa unaambiwa usifanye mikutano siku fulani, wewe unaumuwa kufanya kwa nguvu wakaja polisi kuzuwia mkusanyiko huo ukakaidi na kupigana na Polisi ni nani wa kulaumiwa?

Conclusion:

Licha ya hoja zote hizo juu zinazoashiria uvunjifu wa amani wa makusudi kabisa, hata kwa bahati mbaya ukijikuta wewe ni mpita njia kwenye vurugu (riots) za namna hiyo na Polisi wameshatowa amri ya watu kutawanyika na wameshajipanga kuwafata na kuwatawanya wakitumia zana zao za kuzuwia fujo, usijaribu hata siku moja kuwafata wanapotokea na kuingia kwenye himaya yao kutokea walipo wanaotawanywa, kufanya hivyo ni:

1) amma kujitafutia kifo (suicide) kwa makusudi kabisa,

2) au kujitafutia kifo cha kujitowa mhanga (terrorism),

3) amma kujitafutia kifo kwa ujinga wa kwenda kuanzisha fujo na kutokujuwa namna ya kujihami yanapokushinda.

Chaguwa wewe ni yepi katika hayo yaliyomkuta Daudi?

Ukweli ubaki kuwa ukweli.
zomba Mkuu wangu, naelewa allergy yako na CDM, lakini ninakuomba uziangalie Ukatili wa Polisi Kijijini cha Nyororo katika Picha - YouTube, angalia mpaka dakika ya 6:57 tu (kwani yanayofuatia yanawahusu CDM na wananchi wengine peke yao bila ya ushiriki wa polisi).

Kwa kujibu mlolongo wa hoja zako nimedondoa hii hapa:
"Kama mnakumbuka, RCO mwanzo alizielewa hoja za CHADEMA juu ya vikao vyao vya ndani, lakini alipokuja RPC hali ikabadilika kutokana na kupewa maelezo na mkuu wetu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa," alidokeza mmoja wao.

Walisema kwamba hata katika tawi la kwanza walilofungua viongozi wa CHADEMA, RCO alifika lakini hakuwashambulia. Wakati wakifungua tawi la pili, ndipo RPC akafika, na amri zikatolewa kuwashughulikia viongozi na wanachama wa CHADEMA.

Kwa maelezo ya polisi hao, viongozi na wanachama wa CHADEMA hawakuwa wameleta fujo yoyote, na kwamba kama polisi wangelinda tu mikutano yao yaliyotokea yangeweza kuepukwa.

Askari hao walisema inasikitisha kwamba uamuzi wa mtu mmoja umelifanya jeshi zima lionekane baya mbele ya umma; na kwamba hata wao wanatii amri kwa sababu kazi yao haiwaruhusu kuhoji amri za wakubwa wao.
Pamoja na yote uliyoeleza kutaka kuhalalisha matendo ya polisi, naomba uzingatie yafuatayo:

- Mkutano wa CDM ulikuwa wa ndani na sio wa nje wa hadhara.
- Katika ufunguzi wa tawi la kwanza hakukutokea maafa yoyote, bali katika ufunguzi wa tawi la pili ndipo purukushani zilianza.
- RPC alisema alipokea amri kutoka kwa Mkuu wa kuzuwia fuja, ambaye naye alipokea amri/agizo kutoka kwa Mwema, amabaye naye alipokea amri anakokujua mwenyewe.
- Na kama haitoshi, wakati polisi wanatekeleza agizo/amri la kuwazuwia CDM kwa kisingizio cha sensa, BUBUBU walikuwa na shughuli nzito kuliko ya kufungua tawi. Mwisho ni juzi tu, Waislamu waliandama bila kibali huku bado muda wa sensa ukiwa haujamalizika.
zomba Mkuu wangu, hapa tunajadili kwa kina kipi tufanye ili kupunguza kama sio kuzuwia kabisa maafa kama haya yasiyokuwa ya lazima, kama taifa na sio kama CDM wala CCM. Sioni tafauti kati ya maelezo yako na maelezo/hoja za kiCCM au KiCDM katika hili. For the first time ever, naomba utumie dakika chache tu, 5-10, ufikiri wewe mwenyewe kama Mtanzania, kama binadamu bila ya kuathiriwa na jazba za kichama chochote ulicho.
 
Last edited by a moderator:
Zomba nashukuru kwa jibu lako, ila naomba nieleweshe nielewe vema. Hio ilani ilikuwa applicable kwa CDM peke yake na maeneo ya Iringa tu? Tukizungumzia kuzuiwa kwa hizo harakati za ki siasa kusimamishwa hatuwezi kusahau hoja ya sense ambayo ilikuwa ndio msingi wa sababu za kusitisha. Hapa kunakuwa na utata kidogo, kama walisitishwa ilikuwa vipi walipewa kibali cha kufungua tawi hapo na hali hairusiwi? Hivo vigezo vilitolekwa kila kituo cha mkoa na kigongoji peke yake hadi kukawa na clashes za utendaji?

Nikisoma hapo (asmuchas umesema nijjiulize) nakuwa na swali ambalo Napata kuwa kwanini walipewa kibali cha kufungua hilo t awi kama siku hio ilikuwa hairusiwi? Na jibu ambalo Napata linakuwa na uwalakini sana… Zaidi ni kuwa Napata maswali zaidi; Kwamba waliamua kupewa hicho kibali ili vurugu zije zotekee? AMA kuna mahusiano mabaya ya utendaji kama kufikisha ujumbe toka ngazi ya juu hadi ya chini?

Mie nakubaliana na kwamba in a way CDM wana makosa kadhaa katika matukio haya… Ila ambae anawezesha hayo makosa na mwenye kubeba msalaba mkubwa ni CCM. Kuna ule msemo kuwa tembo wakipigana ni nyasi ambazo zinaumia na hili hasa the applicability of it.

Hio conclusion uliotowa Zomba is just one side of the coin. Being as insightful as you are it would have been really great and brilliant to have heard another side of the coin from you… Free from ushabiki na full of reason and logic. Nina maswali yafuatayo…

Tokana na ukweli kuwa ukitowa tongo tongo na kuliangalia swala zima kama tu sio mwananchi na wala mshusika wa Siasa za Tanzania unaweza tambua na kuona kuwa kila kundi lina msalaba wa kubeba… Kwa kutumia hayo yaliyotokea unasemaje kuhusu Viongozi wa CCM kuendelea na shughuli za kisiasa wakati wa Sensa (hapa hapa Tanzania bara achana na Zanzibar ambako Mh. Nape kasema kuwa ndiko ziliendelea) na hali agizo lilitolewa kama ulivosisitiza na wala hawakugadhibiwa… Unadhani inatoa ujumbe/picha gani kwa vyama pinzani na wanachi ambao ni wanaharakati na wafuatiliaji?

N.B

Mifano halisi ya hizo shughuli na viongozi wa CCM wakati wa sensa ni:

  1. Mh. Muhsin Rafi Ismail aliesindikizwa na maandamano na wafuasi (kama sikosei siku mbili tu baada ya agizo) alipokuwa anawania nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya wa Chama cha CCM hicho pale Lindi.
  2. Mh. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo mh. Amos Makalla kuendelea na shughuli zake za kisiasa katika jimbo lake Mvomero.

Sijui umeziona video za huo unaosemwa ni mkutano? tafadhali zisikilize na nyimbo zinazoimbwa halafu uwe mkweli wa nafsi yako kama si za uchokozi na si za watu ambao wanafunguwa tawi lao.

Kama umeomba kibali na ukapewa haina maana kuwa serikali inaweza kusitisha hicho kibali kwa sababu moja nyingine. Hebu funguka kidogo na usilazimishe kuonesha kuwa wenye makosa ni Serikali au Polisi iliyo chini ya Serikali.

Ukiambiwa usifanye mkutano hapa, husemi kuwa mimi naufanya kwa lazima, ukifanya hivyo unakuwa ni mvunjifu wa sheria na polisi ni lazima wa kudhibiti amma kwa hiyari au ukikaidi kwa kutumia nguvu kama ilani yao inavyosema.
 
zomba Mkuu wangu, naelewa allergy yako na CDM, lakini ninakuomba uziangalie Ukatili wa Polisi Kijijini cha Nyororo katika Picha - YouTube, angalia mpaka dakika ya 6:57 tu (kwani yanayofuatia yanawahusu CDM na wananchi wengine peke yao bila ya ushiriki wa polisi).

Kwa kujibu mlolongo wa hoja zako nimedondoa hii hapa:

Pamoja na yote uliyoeleza kutaka kuhalalisha matendo ya polisi, naomba uzingatie yafuatayo:

- Mkutano wa CDM ulikuwa wa ndani na sio wa nje wa hadhara.
- Katika ufunguzi wa tawi la kwanza hakukutokea maafa yoyote, bali katika ufunguzi wa tawi la pili ndipo purukushani zilianza.
- RPC alisema alipokea amri kutoka kwa Mkuu wa kuzuwia fuja, ambaye naye alipokea amri/agizo kutoka kwa Mwema, amabaye naye alipokea amri anakokujua mwenyewe.
- Na kama haitoshi, wakati polisi wanatekeleza agizo/amri la kuwazuwia CDM kwa kisingizio cha sensa, BUBUBU walikuwa na shughuli nzito kuliko ya kufungua tawi. Mwisho ni juzi tu, Waislamu waliandama bila kibali huku bado muda wa sensa ukiwa haujamalizika.
zomba Mkuu wangu, hapa tunajadili kwa kina kipi tufanye ili kupunguza kama sio kuzuwia kabisa maafa kama haya yasiyokuwa ya lazima, kama taifa na sio kama CDM wala CCM. Sioni tafauti kati ya maelezo yako na maelezo/hoja za kiCCM au KiCDM katika hili. For the first time ever, naomba utumie dakika chache tu, 5-10, ufikiri wewe mwenyewe kama Mtanzania, kama binadamu bila ya kuathiriwa na jazba za kichama chochote ulicho.

Nimeangalia na sioni mkutano hapo bali naona maadamano ya watu wanaoimba nyimbo ambazo hazihusiani na ufunguzi wa tawi, jee wewe umeona hilo? au umefunga macho na masikio?
 
Kwa hiyo marehemu kama mwandishi wa Habari anatakiwa kutii AMRI ipi ya serikali?.. sijui kama unaelewa kazi ya mwandishi wa Habari ktk tukio hili na wapi alivunja sheria. Kazi yake inamruhusu kuwepo pale hata kama ingekuwa kuna vita ku report matukio na sio yeye kuwa sehemu ya watu waliokatazwa. Jambo ambalo Polisi wangeweza kumwambia ni kwamba hawawezi kumhakikishia usalama wake na sio yeye kuwa ndiye target yao..

Hii ndio kazi za waandishi wa habari mkuu wangu na Uhuru wao huenda pasipo na mipaka hata ingekuwa Kenya au Marekani sheria ingesema waandishi wa habari hawaruhusiwi na still bado ingetakiwa maelezo ya kina kwa nini waandishi wa habari hawatakiwi. Amri ya serikali siku zote ni ktk kuwalinda wananchi hakuna amri au sheria inayowaswaga kama mawindoni serengeti. Polisi sio serikali, Polisi inatakiwa kuwalinda wananchi na sio wao kutoa amri ya kuvunja mikutano sijui kwenu Bongo.

Amri inatolewa na kiongozi wa serikali na Polisi wanatii amri hiyo sio Polisi wenyewe kuwa na maamuzi yanayohusiana na Sensa.. Nimeshakwambia sensa ilikuwa swala la KITAIFA wala sii la Mkoa na wala Mkoa wa Iringa hawana mamlaka juu ya sensa ile isipokuwa kuhesabu watu ktk mazingira ambayo serikali iliyaweka nchi nzima. Again marehemu alikuwa kazini hakuwa pale kujiandikisha kama mwanachama mpya wala kugawa kadi..Africa jamani hata tunavyofikiri tu inatisha - kama wanyama pori vile..

Ukiwa Mwandishi wa habari ndio inakupa ruksa ya kumvaa mkuu wa polisi?

Alikuwa kazini kama mwanachama na kiongozi wa mkoa wa chadema. Na uandishi wake haumpi tiketi ya kuwavaa mapolisi na kuhamasisha watu wavunje amri za Serikali. Amevuna alichokipanda.
 
Naomba niweke maelezo ya mwandishi wa habari aliyekuwepo kwenye eneo la tukio tarehe 2 Sept. Pengine maelezo ya shuhuda huyu yanaweza kutuasaidia kujadili jambo lililotekea ili walau kutafuta solution kitu kama hiki kisijirudie tena.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

SEPTEMBA 2, 2012, polisi waliua kikatili mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa. Alikufa mbele ya Kamanda wa Polisi mkoani humo, Michael Kamuhanda, wakati polisi hao walipovamia ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuwatawanya wasifungue tawi la chama chao katika kijiji hicho.

Mmoja wa watu walioshuhudia tukio zima, ni mwandishi wa Tanzania Daima, Abdallah Khamis. Ifuatayo ni simulizi ya kile alichokiona wakati polisi wanaondoa uhai wa Mwangosi.

SIKU hiyo asubuhi tulipata taarifa kuwa Kamanda wa Polisi mkoani humo (RPC), Michael Kamuhanda, alipanga kukutana na waandishi wa habari majira ya saa 2.30 ambapo waandishi walifika akiwemo Daudi Mwangosi. Tukiwa katika chumba cha mikutano katika jengo la polisi Mkoa wa Iringa, Kamanda wa mkoa huo, alifika akiongozana na maafisa wake wawili na kuanza kutusomea taarifa ya zuio la mikutano ya CHADEMA iliyokuwa iendelee siku hiyo baada ya kupisha zoezi la awali la sensa.

Alitusomea zuio hilo na kutuambia hata viongozi wa CHADEMA wameshataarifiwa usiku wa Septemba Mosi. Tukamuuliza mbona taarifa za sensa zinaeleza kuwa kuna mafanikio kwa asilimia 95 na waliobaki wanatakiwa waende kwa viongozi wao? Akatujibu kuwa hilo ni agizo na linapaswa litekelezwe na CHADEMA.

Waandishi hawakuchoka kumuuliza maswali RPC na moja ya maswali yaliyoonekana kumkera kamanda huyo ni lile lililotoka kwa Daudi Mwangosi kuwa mbona wakati wa mwanzo walipozuia mikutano ya CHADEMA mkoani humo mikutano mingine ya CCM ndani ya mkoa huo na sehemu nyingine nchini ilikuwa inaendelea. Swali lingine la Mwangosi lilimtaka kamanda huyo kutumia busara katika hali iliyopo kwa lengo la kuepusha maafa yanayoweza kutokea endapo angeendelea kushikilia msimamo wake kuwa hakuna mkutano wa aina yoyote utakaofanyika.

Baada ya maswali hayo, tulimuona Kamanda Kamhanda akiwa amekunja sura kama ishara ya kuchukizwa na maswali ya Mwangosi ambaye aliongeza swali lingine kwamba, "inaonekana Kamanda umechukia kutoka ndani ya moyo wako" na kamanda akajibu "ni lazima nichukie na nawachukia hawa CHADEMA kwa kuwa ninaipenda kazi yangu na pia ninakaribia kustaafu na sitaki kustaafu vibaya."

Baada ya hapo maafisa waliokuwa na RPC waliandika ujumbe kwenye karatasi na wakamfikishia mkuu wao, na baada ya muda mkutano huo ulimalizika huku kukiwa na kauli za utani wa hapa na pale kati ya waandishi wa habari na baadhi ya askari juu ya kwenda kuripoti matukio ya siku hiyo.

Tulipokuwa nje ya jengo, Mwangosi, kwa kuwa ni mwenyeji wa mkoa huo, alikuwa akitaniana na mmoja wa askari aliyevaa kiraia, ambaye alimwambia kuwa, "huko hakutakuwa na kujuana na kuna uwezekano wa watu kufa."

Mwangosi alijibu papo hapo kuwa hilo haliogopi kwa kuwa kifo ni ada ya mja yeyote na kwamba ataogopa kama mtu atamuahidi kuishi milele.

Baada ya hapo, kila mmoja alitawanyika katika eneo lake, na majira ya saa saba mchana baadhi ya waandishi walikutana ili kuanza safari katika Wilaya ya Mufindi kwa ajili ya kuripoti mkutano wa ndani wa CHADEMA na ufunguzi wa matawi.
Waandishi wa habari hao pamoja na mimi ni Godfrey Mushi (Nipashe), Olver Motto (Star Tv), Renatus Mutabuzi (ITV), Clement Sanga (Mwananchi), Joseph Senga (Tanzania Daima) na Tumaini Makene (Ofisa Habari wa CHADEMA).
Tulipofika katika mji wa Mafinga, tulipata chakula cha mchana kabla ya kwenda katika Kijiji cha Nyololo, na muda wote huo Mwangosi alikuwa hajaungana nasi.

Tuliondoka Mafinga kuelekea Nyololo huku mwenzetu Clement Sanga akiwasiliana na Mwangosi aliyesema yuko katika basi na angeungana nasi tukiwa Nyololo. Tulipofika pale tuliona askari wachache wakiwa wamesimama barabarani huku gari lao moja likiwa linajaza mafuta katika kituo cha mafuta kilichopo eneo hilo.

Tukiwa njia ya kwenda Mbeya, mita kama 100 kutoka katika mji wa Nyololo, kushoto kwetu tuliziona ofisi za CHADEMA zikiwa zimepambwa kwa bendera nyingi, na kulia kwake tuliona magari manne ya askari waliokuwa na silaha. Baada ya kupita eneo hilo, gari moja la polisi lilikuwa likitufuata, na hapo tulishauriana kugeuza gari kurudi katika eneo la mji. Tulipofanya hivyo, na gari la polisi lilisimama.

Wakati tunarudi katika eneo la mji, tuliegesha gari pembeni. Baadhi ya waandishi wa habari waliingia mitaani kwa makubaliano kuwa baada ya dakika 10 tuwe tumerejea kwa ajili shughuli iliyotuleta - kushuhudia ufunguzi wa tawi hilo jipya la CHADEMA. Muda huo ulipofika, tulirejea, lakini Mwangosi alikuwa hajaungana nasi. Baadaye tulianza kuona baadhi ya magari yakiwa na bendera ya CHADEMA yakipita moja baada ya jingine.

Kuwasili kwa Mwangosi eneo la Nyololo
Saa 10.22 Mwangosi aliwasili kwa basi ambalo sikumbuki kama ni Hood au Abood; na muda huo huo tukawaona askari wakiyatoa magari yao kutoka mafichoni na kuingia upande wa kulia wa mji wa Nyololo kwenye ofisi za kata za CHADEMA.
Wakati askari wakiwa wanapita walikuwa wakisema Dk. Slaa anatokea eneo la Wami. Waandishi wa habari wakawa wamejiandaa kwenda kwa kufuata njia hiyo.

Tuliegesha gari letu mbali. Mwangosi ambaye hakuwepo awali, akataka kuchukua pikipiki ili awahi. Kwa kuwa muda huo nilikuwa naye, nikamsihi kuwa hana haja ya kuingia gharama kwa kuwa gari la waandishi wa habari lipo. Akanielewa, na tukaingia katika gari hilo, huku akiwa amempakata Oliver Motto wa Star Tv.

Tulipoenda kama mita 50 hivi, tulikutana na msafara wa CHADEMA ukiwa unaelekea tunakotoka. Gari la waandishi wa habari na magari ya polisi yakalazimika kukaa pembeni kuyapisha, kisha wakaungana nao kuelekea katika ofisi za tawi za chama hicho.

Ofisi za tawi za CHADEMA katika mji huo wa Nyololo zipo mita zaidi ya 100 upande wa kushoto wa bararara ya kuelekea Mbeya. Awali polisi walikuwa wameegesha magari yao barabarani wakati CHADEMA wakielekea katika ofisi zao.
Hakukuwa na vurugu yoyote. Ghafla kiongozi wa polisi ambaye alikuwepo pale - tulimtambua kwa jina la Mnunka - aliwaamuru askari wake watoe ilani kwa kunyoosha bendera kubwa nyekundu juu na kuwataka CHADEMA waondoke katika ofisi zao. Tukapiga picha tukio hilo.

Wakati askari wakijiandaa kuwafuata wana CHADEMA katika ofisi zao, alitokea mtu aliyevaa shuka na kujifunga kitambaa kichwani ambaye baadaye alijitambulisha kama mkuu wa upelezi mkoa (RCO), akawaamuru wenzake waende katika ‘target' lakini wasithubutu kutumia nguvu bila amri. Hapa ndipo tulipoanza kupata wasiwasi ni nani anatoa amri kwa kuwa yule wa mwanzo, Mnunka alijiapiza kuwa wamechoka kuvumilia, na kwamba siku hiyo CHADEMA watawatambua. Hata tulipomuuliza maana ya kauli ile, hakutupa jibu la kueleweka.

Katika hali hiyo, mtu aliyejitambulisha kama ndie RCO alizungumza na viongozi wa CHADEMA, wao wakamwambia wako katika kikao cha ndani. Yeye akasema jukumu lake ni kuhakikisha usalama unakuwepo, na kwamba kama ni suala la kikao cha ndani hawawezi kuzuia.

Tulitaka kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kutoka kwa RCO ambaye alikuwa akizungumza kwa simu na mtu ambaye baadaye ilikuja kubainika kuwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), akawa anamueleza kuwa hali ni salama. Alituahidi waandishi wa habari tuvute subira "kwa kuwa mwenye mkoa amewasili."

Baada ya kuwasili kwa RPC Kamuhanda, Kamanda wa FFU, Mnunka alienda akamnong'oneza jambo. Pale pale, Kamuhanda akaonekana kukasirika. Akaagiza CHADEMA wasimamishe shughuli yao mara moja. Tulitaka kujua tafsiri ya mkutano wa ndani kwa Jeshi la Polisi ni ipi, ni kwa wahusika kukaa ndani au ni ule mkutano utakaowahusisha wanachama peke yao kama ambavyo CHADEMA walikuwa wanasema pale. RPC akatujibu kuwa hilo halielewi na yeye si mwanasiasa.
Baada ya maelezo hayo, waandishi wa habari tulimbana RPC kwa maswali hata ikafikia hatua ya kamanda huyo kuanza kuwanyooshea vidole baadhi yetu, huku alimlalamikia Mwangosi kwamba kwanini hakushiba na majibu aliyopewa tangu asubuhi.

RPC akaniambia mimi kwamba nauliza maswali yanayopingana na mtazamo wa jeshi hilo; akamwambia Mutabuzi kuwa anamfahamu. Baada ya hali hiyo, CHADEMA walimaliza mkutano wao katika ofisi za tawi na wakawa wanaelekea katika ofisi za kata. Gari lililotubeba lilikuwa nyuma ya gari la RPC ambaye baadaye dereva wake aliendesha kwa kasi kwenda mbele kutaka kuzuia msafara wa CHADEMA.

Lakini viongozi wa CHADEMA walikuwa wameshafika katika ofisi yao ya kata na tukashuka kwenda kushuhudia kinachoendelea. Hapo ndipo tulimkuta Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zanzibar, Hamad Yusuph na viongozi wengine wakisaini katika kitabu cha wageni. Ghafla, RPC akatoa amri ya kuwakamata viongozi wa CHADEMA waliokuwa katika ofisi yao. Baada ya amri hiyo, wanachama wa CHADEMA waliokuwa pale wote walikaa chini wakinyoosha mikono juu.

Balaa linaanza kwa amri ya RPC Kamuhanda
Baada ya RPC kutoa amri hiyo, polisi walioipokea walianza kurusha mabomu ya machozi kuelekea sehemu waliyokaa wanachama wa CHADEMA. Mabomu hayo yalirushwa na kuumiza wengi, wakiwamo waandishi wa habari. Mimi nilipigwa na kitu chenye kishindo, nikajeruhiwa mkono wa kushoto na sehemu ya paja la mguu wa kulia.

Jitihada za polisi kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA zilifanikiwa. Baadhi ya watu na viongozi waliwekwa chini ya ulinzi, sisi tukiwa tunaendelea kufanya kazi yetu ya kukusanya taarifa ili kuhabarisha umma juu ya kile kinachoendelea katika eneo hilo. Wakati hali hiyo ikiendelea, ofisi za kata za CHADEMA hazikuwa na mtu. Askari wakawa wanapiga mabomu kuelekea ndani ya ofisi hiyo tupu.

Tuliendelea kupiga picha tukio hilo. Ghafla askari mmoja akamgeukia mwandishi wa gazeti la Nipashe, Godfrey Mushi, akaanza kumpiga.Baada ya kuona mwandishi huyo anapigwa, Mwangosi aliwasogelea askari akitaka kujua sababu za kumshambulia mwandishi wakati yupo kazini kama ambavyo askari hao walivyokuwa wakiwajibika. Swali la Mwangosi likavuta askari wengine. Wakamzunguka na kuanza kumpiga kwa marungu, mateke na ngumi. Wakati hayo yakifanyika, RPC alikuwa pale anashuhudia.

Baada ya kuona kipigo kimekuwa kikali, Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) cha Mafinga aliingilia kati kutaka kumnusuru Mwangosi.Wakati Mwangosi akiwa anashambuliwa, mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga, naye alikuwa katika wakati mgumu baada ya askari kumdhibiti na kuanza kumpekua mifukoni, huku mwenyewe akijitahidi kujinasua mikononi mwao.

Mbali na mimi na Senga, muda huo hakukuwa na raia yeyote katika eneo lile, isipokuwa Godfrey Mushi wa Nipashe ambaye sina hakika kama alikuwa anafahamu kinachoendelea maana alikuwa amepigwa sana, yuko hoi.
Baada ya kuona kipigo kinazidi kwa Mwangosi huku Senga akiendelea kupiga picha, uzalendo ulinishinda, nikaamua kumfuata Kamanda wa Polisi mkoani humo aliyekuwa mita zisizozidi kumi ndani ya gari lake, akishuhudia tukio lile. Nikamuomba asaidie kumnusuru Mwangosi na kipigo kile.

RPC alishusha kioo cha gari lake, akaniangalia, kisha akafunga kioo, huku dereva wake akawa anapiga honi. Sikujua maana ya honi hiyo. Baada ya kuona hakuna msaada wowote kutoka kwa RPC, nilisogea karibu kwa ajili ya kuendelea kupata picha ya tukio, ili umma ujue juu ya madhila yanayowapata waandishi wa habari mikononi mwa polisi.

Wakati nikiwa naendelea kuchukua picha, nilimwona askari mmoja akinyoosha mkono juu na mwingine aliyevaa kiraia akiwa ameshika bastola yake kuelekeza juu, huku wengine wakiwa wanaendelea kumpiga Mwangosi aliyekuwa anajitahidi kuinuka kwa kumshika mmoja wa askari wale.

Katika harakati za Mwangosi kujinasua, nilimshuhudia mmoja wa wale askari akiwa kama anainama akaelekeza mtutu wa bunduki usawa wa tumbo la Mwangosi aliyekuwa katika hali ya kutaka kusimama huku akipiga kelele "msiniuee, msiniuee…"
Mara nikasikia mlipuko mkubwa pale pale walipo; baadhi ya nyama zikarushwa na kutapakaa, nyingine zikanirukia mimi na kuchafua fulana yangu.

Kumbe walikuwa wamemlipua Mwangosi! Nikapiga picha ya mwili uliosambaratika na kukatika vipande vipande. Nikaona askari wale wanambeba askari ambaye naye alijeruhiwa na mlipuko uliomuua Mwangosi. Nikakimbia kujinusuru na askari wale. Sikuona tena usalama wangu mbele ya polisi wake. Sikumwamini tena RPC kama angeweza kulinda maisha yangu. Nikatimua mbio kuelekea nisipopajua.

Nikiwa nakimbia nilichomoa kadi ya kamera kutoka katika kamera yangu ili nisipokonywe. Hapo ndipo nilipokutana na mwandishi mwingine, Francis Godwin, nikamwambia asielekee nilikokuwa natoka mimi – ambako ndiko alikuwa anataka kwenda - kwa kuwa Mwangosi ameshauawa na polisi!

Wakati naachana na Godwin, nilichukua simu yangu na kumpigia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, ambaye ndiye Mhariri Mtendaji wa gazeti hili kwa ajili ya kumpa taarifa. Bahati mbaya simu yake haikupokelewa.
Nikamfuata Makene (Tumaini, afisa habari wa CHADEMA) aliyekuwa amejikinga katika gogo, alikokuwa pamoja na Oliver Motto, nikawaambia eneo hili halitufai watatuua. Ndipo nikampigia simu Bakari Kimwanga, mwandishi wa gazeti la Mtanzania, nikamfahamisha kuwa Mwangosi ameuawa na polisi.

Tukakimbilia porini kujificha, kila mtu akiwa analia kivyake. Baada ya kukaa porini kwa muda, tuliamua kubadilisha nguo zetu ili tusitambulike kirahisi. Tukatoka mafichoni kuangalia hali ya usalama. Tukaanza kuwatafuta wenzetu ambao tulipoteana nao. Baadaye tulikodi teksi kuwafuata wenzetu ambao wakati huo walishakimbia kutoka eneo hilo la hatari.

Tukiwa katika hoteli ya MR mkoani Iringa, mwananchi mmoja alikuja kutueleza kuwa alifanikiwa kukusanya sehemu ya mwili wa marehemu Mwangosi pamoja na mabomu yaliyoachwa katika eneo la tukio na walipoangalia wakaona ni sehemu ya nyama ya utumbo iliyowekwa katika mfuko pamoja na mabomu ya machozi na kuyapanga yale mabomu juu ya meza ya hoteli hiyo na kuyapiga picha huku utumbo wa Mwangosi ukiendelea kuwa katika mfuko uliowekwa.

Hadi sasa sijajua endapo sehemu hiyo ya utumbo ilizikwa usiku ule mkoani Iringa au uliunganishwa na sehemu nyingine ya mwili wake uliotawanywa na bomu hilo kiasi cha kushindwa kujua kama ni mwili wa binadamu au ni ng'ombe aliyechinjwa tayari kwa mauzo.

Hivi ndivyo tulivyompoteza mwandishi mwenzetu, Daudi Mwangosi, akiwa mikononi mwa polisi.
 
Nimeangalia na sioni mkutano hapo bali naona maadamano ya watu wanaoimba nyimbo ambazo hazihusiani na ufunguzi wa tawi, jee wewe umeona hilo? au umefunga macho na masikio?
Mkuu wangu, inaonesha ama umeangalia tafauti na nilichokutuma hapa au tayari ulikuwa na jibu hata kabla ya kuangalia hicho nilichoweka. Hizi ni still pictures na kwenye picha watu hawasikiki wakiimba hata kama walikuwa wanafanya hivyo, hakuna maandamo wala watu hawaimbi.
 
Ukiwa Mwandishi wa habari ndio inakupa ruksa ya kumvaa mkuu wa polisi?

Alikuwa kazini kama mwanachama na kiongozi wa mkoa wa chadema. Na uandishi wake haumpi tiketi ya kuwavaa mapolisi na kuhamasisha watu wavunje amri za Serikali. Amevuna alichokipanda.

Unaweza kutoa ushahidi wowote kama Mwagosi alikuwa kiongozi wa mkoa wa Chadema? Na hata kama alikuwa hivyo au mpiga debe tu wa Chadema, alistahiki kufanyiwa aliyofanyiwa?.
zomba Mkuu wangu, kwa kauli na mawazo kama hayo hapo nyekundu, umenisikitsha sana. Sijui ubinadamu wako uko wapi. Mkuu, Mungu ni mwepesi wa kusamehe, rejea kwa muumba wako.
 
Last edited by a moderator:
Watch this Guy carefully huyu mwenye pensi, picha ya kwanza na ya pili yupo akiwa amenyoosha bastora juu. what was mission of this Guy!!??

attachment.php

attachment.php

Matola
,

Huyo Bwana Uliulizia ROLE YAKE (huyo mwenye Pensi) ... kaonekana vizuri kwenye VIDEO. Muone Dakika ya 2.10

Anasomeka hivi,

ASKARI huyu alikuwa na sila ya moto na mwanzoni alikuwa amevaa skafu ya CDM na kujifanya Mwanachama. INASADIKIWA alipanga kudhuru mtu ili baadae POLISI wasingizie ni CDM wamefanya tukio Hilo.

...........
 
Last edited by a moderator:
Ukiwa Mwandishi wa habari ndio inakupa ruksa ya kumvaa mkuu wa polisi?

Alikuwa kazini kama mwanachama na kiongozi wa mkoa wa chadema. Na uandishi wake haumpi tiketi ya kuwavaa mapolisi na kuhamasisha watu wavunje amri za Serikali. Amevuna alichokipanda.
Dah.... Haya mkuu lakini nimeipenda signature yako..
Azimio Jipya, Huyo mwenye Pensi ya kombat inaonyesha alivaa kitambulisho usoni lakini sio mwandishi wa habari.. Utetetzi mwingine jamani kichaa tupu..
 
Mkuu wangu, hizi ni nyakati nyingine kabasa Kuna utandawazi HABARI hazipoteleei mikonono mwa wachahe! Soma taarifa zote post namaba 110 Huyu muandishi... Alitoa pia taarifa hzi live ITV.

1. Utaona Huyo bwana mwenye kunyoosha bastola ni nani.

2. Utaona hicho kinchoitwa Kujirusha/Kumvaa mkuu wa polisi. Lakini Taratibu ona tukio lilivyojijenga hadi jamaa Kulipuliwa.

Balaa linaanza kwa amri ya RPC Kamuhanda

Baada ya RPC kutoa amri hiyo, polisi walioipokea walianza kurusha mabomu ya machozi kuelekea sehemu waliyokaa wanachama wa CHADEMA. Mabomu hayo yalirushwa na kuumiza wengi, wakiwamo waandishi wa habari. Mimi nilipigwa na kitu chenye kishindo, nikajeruhiwa mkono wa kushoto na sehemu ya paja la mguu wa kulia.

Jitihada za polisi kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA zilifanikiwa. Baadhi ya watu na viongozi waliwekwa chini ya ulinzi, sisi tukiwa tunaendelea kufanya kazi yetu ya kukusanya taarifa ili kuhabarisha umma juu ya kile kinachoendelea katika eneo hilo. Wakati hali hiyo ikiendelea, ofisi za kata za CHADEMA hazikuwa na mtu. Askari wakawa wanapiga mabomu kuelekea ndani ya ofisi hiyo tupu.

Tuliendelea kupiga picha tukio hilo. Ghafla askari mmoja akamgeukia mwandishi wa gazeti la Nipashe, Godfrey Mushi, akaanza kumpiga.Baada ya kuona mwandishi huyo anapigwa, Mwangosi aliwasogelea askari akitaka kujua sababu za kumshambulia mwandishi wakati yupo kazini kama ambavyo askari hao walivyokuwa wakiwajibika. Swali la Mwangosi likavuta askari wengine. Wakamzunguka na kuanza kumpiga kwa marungu, mateke na ngumi. Wakati hayo yakifanyika, RPC alikuwa pale anashuhudia.

Baada ya kuona kipigo kimekuwa kikali, Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) cha Mafinga aliingilia kati kutaka kumnusuru Mwangosi.Wakati Mwangosi akiwa anashambuliwa, mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga, naye alikuwa katika wakati mgumu baada ya askari kumdhibiti na kuanza kumpekua mifukoni, huku mwenyewe akijitahidi kujinasua mikononi mwao.

Mbali na mimi na Senga, muda huo hakukuwa na raia yeyote katika eneo lile, isipokuwa Godfrey Mushi wa Nipashe ambaye sina hakika kama alikuwa anafahamu kinachoendelea maana alikuwa amepigwa sana, yuko hoi.
Baada ya kuona kipigo kinazidi kwa Mwangosi huku Senga akiendelea kupiga picha, uzalendo ulinishinda, nikaamua kumfuata Kamanda wa Polisi mkoani humo aliyekuwa mita zisizozidi kumi ndani ya gari lake, akishuhudia tukio lile. Nikamuomba asaidie kumnusuru Mwangosi na kipigo kile.

RPC alishusha kioo cha gari lake, akaniangalia, kisha akafunga kioo, huku dereva wake akawa anapiga honi. Sikujua maana ya honi hiyo. Baada ya kuona hakuna msaada wowote kutoka kwa RPC, nilisogea karibu kwa ajili ya kuendelea kupata picha ya tukio, ili umma ujue juu ya madhila yanayowapata waandishi wa habari mikononi mwa polisi.

Wakati nikiwa naendelea kuchukua picha, nilimwona askari mmoja akinyoosha mkono juu na mwingine aliyevaa kiraia akiwa ameshika bastola yake kuelekeza juu, huku wengine wakiwa wanaendelea kumpiga Mwangosi aliyekuwa anajitahidi kuinuka kwa kumshika mmoja wa askari wale.

Katika harakati za Mwangosi kujinasua, nilimshuhudia mmoja wa wale askari akiwa kama anainama akaelekeza mtutu wa bunduki usawa wa tumbo la Mwangosi aliyekuwa katika hali ya kutaka kusimama huku akipiga kelele “msiniuee, msiniuee…”
Mara nikasikia mlipuko mkubwa pale pale walipo; baadhi ya nyama zikarushwa na kutapakaa, nyingine zikanirukia mimi na kuchafua fulana yangu.

Kumbe walikuwa wamemlipua Mwangosi! Nikapiga picha ya mwili uliosambaratika na kukatika vipande vipande. Nikaona askari wale wanambeba askari ambaye naye alijeruhiwa na mlipuko uliomuua Mwangosi. Nikakimbia kujinusuru na askari wale. Sikuona tena usalama wangu mbele ya polisi wake. Sikumwamini tena RPC kama angeweza kulinda maisha yangu. Nikatimua mbio kuelekea nisipopajua.

Nikiwa nakimbia nilichomoa kadi ya kamera kutoka katika kamera yangu ili nisipokonywe. Hapo ndipo nilipokutana na mwandishi mwingine, Francis Godwin, nikamwambia asielekee nilikokuwa natoka mimi – ambako ndiko alikuwa anataka kwenda - kwa kuwa Mwangosi ameshauawa na polisi!

Wakati naachana na Godwin, nilichukua simu yangu na kumpigia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, ambaye ndiye Mhariri Mtendaji wa gazeti hili kwa ajili ya kumpa taarifa. Bahati mbaya simu yake haikupokelewa.
Nikamfuata Makene (Tumaini, afisa habari wa CHADEMA) aliyekuwa amejikinga katika gogo, alikokuwa pamoja na Oliver Motto, nikawaambia eneo hili halitufai watatuua. Ndipo nikampigia simu Bakari Kimwanga, mwandishi wa gazeti la Mtanzania, nikamfahamisha kuwa Mwangosi ameuawa na polisi.

Tukakimbilia porini kujificha, kila mtu akiwa analia kivyake. Baada ya kukaa porini kwa muda, tuliamua kubadilisha nguo zetu ili tusitambulike kirahisi. Tukatoka mafichoni kuangalia hali ya usalama. Tukaanza kuwatafuta wenzetu ambao tulipoteana nao. Baadaye tulikodi teksi kuwafuata wenzetu ambao wakati huo walishakimbia kutoka eneo hilo la hatari.

Tukiwa katika hoteli ya MR mkoani Iringa, mwananchi mmoja alikuja kutueleza kuwa alifanikiwa kukusanya sehemu ya mwili wa marehemu Mwangosi pamoja na mabomu yaliyoachwa katika eneo la tukio na walipoangalia wakaona ni sehemu ya nyama ya utumbo iliyowekwa katika mfuko pamoja na mabomu ya machozi na kuyapanga yale mabomu juu ya meza ya hoteli hiyo na kuyapiga picha huku utumbo wa Mwangosi ukiendelea kuwa katika mfuko uliowekwa.
 
Unaweza kutoa ushahidi wowote kama Mwagosi alikuwa kiongozi wa mkoa wa Chadema? Na hata kama alikuwa hivyo au mpiga debe tu wa Chadema, alistahiki kufanyiwa aliyofanyiwa?.
zomba Mkuu wangu, kwa kauli na mawazo kama hayo hapo nyekundu, umenisikitsha sana. Sijui ubinadamu wako uko wapi. Mkuu, Mungu ni mwepesi wa kusamehe, rejea kwa muumba wako.

Nakuuliza swali, hivi binaadamu mpenda amani anakiuka amri za Serikali kwa makusudi kabisa? Huo ndio ubinaadamu au umwagaji damu?
 
mtu anayetetea mauaji haya ya polisi na serikali ni mawili, anahusika moja kwa moja au ana maslahi nayo.....
 
Nakuuliza swali, hivi binaadamu mpenda amani anakiuka amri za Serikali kwa makusudi kabisa? Huo ndio ubinaadamu au umwagaji damu?
Mkuu, mimi kama binadamu, ninaelewa mipaka ya wajibu na haki zangu kama raia. Kama raia na kama binadamu, siwezi kutii amri za serikali kama hizo ni kandamizi, kama amri hizo zinaniwekea amri ambapo wengine zinawaruhusu. zomba, tuombe Mungu mimi na wewe kuwa mfumo huu uliopo sasa ubadilike, vyenginevyo hii nchi itafika pabaya, siombi iwe hivyo lakini ikitokea uelewe sababu ni hii ya amri za upendeleao, kibaguzi na kandamizi.

Naona bado unakwepa suala la kwa nini siku hiyo hiyo CDM walipovamiwa na polisi kwa kufungua matawi, Bububu walikuwa na mkutano wa hadhara wa nje, tafauti ipo wapi? Kwa nini kila ambapo polisi hawaingilii mikutano ya CDM kunakuwa na amni lakini amani huvunjika pale wanapopigwa mabomu?

Unaweza kujibu kijazba na upofu wa moyo, lakini usidhani kama tukifikia huko mimi na wewe, watoto wetu, jamaa zetu na marafiki zetu tutasalimika na hilo. Vita havina macho, mara nyingi huathirika zaidi waliomo kuliko waliomo.

MUNGU AINUSURU TANZANIA!
 
Last edited by a moderator:
Kagame hasa Great and strong will, does he not to some level qualify as a dictator? Come to think of it maybe it is the only way we Tanzanian would rise for the better :censored:

AshaDii,

Kagame is doing a great job there. However, we should note that the circumstances that brought him to power were unusual, and I am not sure if Tanzanians are ready to embrace that. For, the cost of human life is prohibitive.

I come from the school of thoughts that believes that effective leaders are deliberately nurtured t. Take for example, Kagame , Zanawi or for that matter Museveni. The styles of their leadership are almost identical and didn’t fall from out sky. For, they spent their formative years as battlefield military commanders in civil wars fighting for something they believe in.

I am not saying that Tanzanians can’t find their own Kagame. They can, but we should stop yearning for a dictator because we can do better without one. If you can ride a Roll-Royce, why are you longing for a Suzuki Samurai.
 
Back
Top Bottom