Kifo kupitia mikono ya POLISI – Kosa la Marehemu?

pamoja na hoja yao kwamba CDM ilikiuka maaigizo, hawakupaswa kuua...walitakiwa wawakamate wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kuchukua jukumu la kuua au kuumiza bila sababu ni uhalifu kama uhalifu mwingine wowote ule. Naona polisi wanasahau hilo
 
Rai yangu kwa CDM na vyama vyote vya upinzani, makosa mawili hayafanyi jema moja. Tumeshaona kuchanganyikiwa kwa CCM kiasi wamefikia pahali tayari wanaua na kuwatesa wale wasiokubaliana nao kwa ajili ya kubaka madarakani; vyama vya upinzani visiwe tayari kufa kwa ajili ya kuingia madarakani. Kama tunavyoona, wanaokufa ni raia wa kawaida na sio viongozi, na hata kama wanaokufa au watakao uliwa ni viongozi, bado taifa linawahitaji. Busara itumike. CCM wameshaonja damu, hawatasita. Tusiwaridhishe kwa yale wanayoyataka. Tutafute njia mbadala ya kupambana nao bila ya kupoteza maisha ya watu wasio na hatia kwani tukifanya hivyo itakuwa hakuna tafauti baina ya mjinga na mwenye akili.

Ni kweli kabisa kila mtanzania, awe kiongozi ama raia/mwanachama wa kawaida anahitajika kuendelea kuishi na kufurahia maisha yake ndani ya nchi yake bila kujeruhiwa, kupata kilema cha maisha ama kuuwawa kwa sababu tu anaunga mkono chama cha upinzani. Na vyama vinawajibika kuhakikisha ulinzi wa maisha kwa watu wote kwani wanachokipigania ni pamoja na kuja kuwatumikia watu hawa wanaowaunga mkono na kuwapigania.

Umezungumza la Msingi... mie mtazamo wangu ni kuwa hata kama Serkali inaonekana ndio inahusika moja kwa moja kuwa kupelekea vifo na kujeruhi raia bado ukweli unabaki kuwa hata CHADEMA Inabidi watambue kwa njia moja ama nyingine wanahusika moja kwa moja; tena positively na negatively...
Hawana haja ya kuendeleza shughuli zao kwa ili mradi wananchi kwa kiasi kikubwa wanawaunga mkono, inabidi wawahakikishie usalama hao wana nchi kwa kuweza kufanya njia zozote ambazo zaweza epusha vurugu na hatimae vifo vya wananchi...

Kama nilivyojubaliana na mdau hapo juu ninakubaliana na wewe mia kwa mia juu ya vyama vya siasa, hasa katika mazingira ya sasa Chadema kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba hawawi chanzo cha vifo vya wananchi, ama majeraha kwa wananchi.

Hoja yangu kwenu wakuu AshaDii na MAMMAMIA ni moja tu;
Kwa mawazo yenu mnadhani ni kwa namna gani Chadema wanaweza kuepusha kabisa mauaji haya yanayofanywa kiholela na jeshi la polisi kwa kusukumwa na amri za wanasiasa wa ccm ambao hawako tayari kuona wakiondolewa madarakani. Na wakati wanapojitahidi kuhakikisha kwamba hawawi chanzo cha haya mauaji basi wakati huo huo waweze kufanya kazi zao za kisiasa kadri wanavyoona inafaa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.

Ningeomba muwe specific kabisa kwamba Chadema wanatakiwa kufanya nini katika mazingira haya kandamizi ambayo kila mmoja anayaona kwa macho yake, kwamba Chadema kufanya shughuli za kisiasa Iringa tarehe 02/09/2012 ni haramu lakini ccm kufanya shughuli za kisiasa Bububu siku hiyo hiyo ni halali.
 
AJ umeongea meengi kwa kina na msingi tena kwa kugusa hasa kitu gani humfafanua mwanadamu... In a way inagusia lile ambalo nimeandika katika moja ya bandiko hapo juu, kuwa wamefanya kazi yao kwa kuikumbatia na kufurahia sababu hata kama 'Amri' waliopewa ni nenda kakomeshe vurugu (Sidhani kama walisisitizwa kuwa lazima mmtese sana mtae mkamata... Hata hivo mim na wewe hatuwezi kujua)


Umegusia swala la unyama na jinsi gani inaweza kuwa vigumu kumrudisha mtu katika mstari kuwa mwanadamu wa kawaida na utu ndani yake. Naomba niseme kuwa sio kila mwanadamu kabahatika kuwa na akili yake timamu ya maamuzi kuegemea na kugubikwa na busara... Kuna watu wanaendeshwa kabisa kama mtoto mdogo hasa katika kazi ambazo watu hufanya kazi kwa makundi.

Pamoja na kusema kuwa askari katika hili wana tatizo - nadiriki kusema kama walivosema wadau wengine kama Nguruvi hapo nyumba kuwa tatizo lipo kwa uongozi wa juu na wao ni kama vidagaa. Kama IGP, RPC na Waziri wa Ulinzi wangesimamia/wangekuwa wanasimamia hili swala kwa manufaa ya wananchi hata waliopoteza maisha yao wangekuwa bado wapo miongoni mwetu. Walau thats what i think.

Ukiangalia wakuu wa Ulinzi wa Taifa hawa, Waziri wa ulinzi, IGP , RPC na hata kamanda Mkuu kutokuwa na Mtizamo wa kuturidhisha sisi wananchi juu ya tatizo hili kutapelekea KUUMIA MIOYO YA WATANZANI NA KUISONONEKA ...

... Kwa Mtizamo wangu hii ni HATARI KUBWA KWA USALAMA SIO WA NDANI WA TAIFA ILA WA MIPAKA YETU PIA.

NIJIELEZE!

KUTISHA, KUTESA hadi KUUA MTANZANIA... MBELE YA KAMERA Kwa MAMLAKA iliyokusudiwa KUMLINDA NA KUMTETEA ... Kuna muachia MTANZANIA Picha ya UCHUNGU NA MAJONZI MOYONI!

Watu wengi hasa VIONGOZI WETU WA KITAIFA inaonekana kutokutambua madhara ya Kinachojijenga ndani ya Ufahamu(MIOYONI) wa waadhrika ambao ni Wananchi wanao waongoza.

Picha ya Mateso ya Dr Ulimboka iliyobaki ndani ya fahamu za Watanzania "... Haijafa .. " yaani iko ACTIVE ikitafuta EXPRESSION kwa kila Mtanzania aliyegushwa na Tukio Lile. Kwani ni hakika kila Mtanzania aliona kwa Macho yake Dr Akitirikwa na Damu na majeraha ambayo WATANZANIA wengi wanaamini kuwa yamesababishwa na MAMLAKA iliyotegemewa KUMLINDA.

Kwa kifupi kama mamalka husika haikujisafisha mbele ya Watanzania na KUWARIDHISHA juu ya tukio lile picha hiyo itaedelea kudumu ambalo ni jambo la hatari. Ni hatari kwani kilicho moyoni kama msigano na uchungu lazima kijielelze nje hadharani, ndio maana mtindo huo wa Kutisha, Kuumiza hadi Kuua unaweza UKAANZA KUWA TAMADUNI NA MAZOEA kwenye jamii yetu kama expression ya kilichobebwa mioyoni.

Hili litafanywa bila hata mtu kufikiria mara mbili kwani ni mbegu iliyoko mioyoni kwa kila Mtanzania na Mamlaka za Ulinzi kushindwa kuwajibika Kuifuta kwa kuwaridhisha Waathirika, MTINDO huo utaanza kuwa mfumo wa kawaida wa maisha. Ndio maana Mwerevu yeyote angetegemea Tukio lile kuendelea kujirudia na kuanza kuonekana la kawaida na namana ya pekee ya jamii ya Kitanzania kijitatulia matatizo yake... "Kutisha, kuumiza hadi Kuua" ... na Ndicho kinachotokea na kitakachotokea hadi Suluhu ya haki katika misingi ya UTU NA UBINDAMU IFANYIKE wazi hadharani kupitia mamlaka hizo hizo.

Watanzania wakiendelea kuduguliwa kwa ZANA ZA KIVITA ambazo zilitegemewa kulinda MIPIKA YETU. Ina maana wote ambao wamekufa kupitia Mamlaka hizo wangetakiwa wawe ni maadui wa mipaka yetu. Lakini sivyo ilivyo ni Watanzania innocent kabisa, Picha ya Marehemu David Mwangosi ilivyoharibika inafanana na zile tulizoziona enzi hizo za MAADUI WA VITA YA KAGERA! Kwa adui aliyejaribu kuchezea mipaka yetu na kufanywa kama David alivyofanywa hiyo inaeleweka kuwa ni tabia ya VITA.

Lakini Gundua hapa kuwa Sasa ADUI amekuwa ni Mtanzania Ndani ya Nchi yake. Kinachotakiwa Kumlinda kinatumika KUMPONDAPONDA na Kumteketeza. HUU NI UDHAIFU unaoweza kutoa mwanya kwa majirani/maadui kuona kuwa sasa huu ni wakati muafaka kufanya wanachotaka maana Wanajishambulia na kujiangamiza Wenyewe!!

Hali hii ikienedelea hivi, inaweza KUWATAMANISHA MAJIRANI/MAADUI zetu Kutufanyia kile ambacho tunajifanyia sisi wenyewe lakini wao watakifanya kutokea kwao, hivyo dhidi ya mipaka yetu. Kwani ni kweli kabisa kuwa UDHAIFU WA KIULIZI UNAO ONYESHWA NA MAMLAKA ZA ULIZI ZA TANZANIA NDANI YA NCHI YAKE, KAMWE HAIWEZI KUWA UJASIRI NA UHODARI KWENYE KUILINDA MIPAKA YAKE!!
 
Hoja yangu kwenu wakuu AshaDii na MAMMAMIA ni moja tu;
Kwa mawazo yenu mnadhani ni kwa namna gani Chadema wanaweza kuepusha kabisa mauaji haya yanayofanywa kiholela na jeshi la polisi kwa kusukumwa na amri za wanasiasa wa ccm ambao hawako tayari kuona wakiondolewa madarakani.Na wakati wanapojitahidi kuhakikisha kwamba hawawi chanzo cha haya mauaji basi wakati huo huo waweze kufanya kazi zao za kisiasa kadri wanavyoona inafaa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.

Ningeomba muwe specific kabisa kwamba Chadema wanatakiwa kufanya nini katika mazingira haya kandamizi ambayo kila mmoja anayaona kwa macho yake, kwamba Chadema kufanya shughuli za kisiasa Iringa tarehe 02/09/2012 ni haramu lakini ccm kufanya shughuli za kisiasa Bububu siku hiyo hiyo ni halali.
:caked:
Nadhani imefika pahali imebidi viongozi wa CDM wao wenyewe wakae na kutafakari "TUFANYE NINI?, kwa sababu kama ulivyosema hapo juu kwenye nyekundu kwamba wanasiasa wa CCM (kuanzia hapa tuite serikali) hawataki kuondoka madarakani.

Mimi nina rai mbili tatu:

Kwanza, ukombozi wa Tanzania unaweza kuongozwa na CDM lakini hautafanywa na CDM bali utafanywa na Watanzania. Kwa hivyo, na hili nimekuwa nikilishauri mara nyingi, CDM iache kiburi ijaribu kuviunganisha/kuungana na vyama vyengine vya upinzani katika hili. Kwa kufanya hivyo, hazitakuwa juhudi za CDM tu bali sehemu ya Watanzania kutoka itikadi zote. Mimi sikubaliani na dhana kama CUF imeolewa, NCCR imekufa, TLP imepotea n.k. CDM kviunganisha vyama vya upinzani ni kuwaunganisha Watanzania. Tuliona mfano mdogo wakati wa sahihi 70 za kura ya kutokuwa na imani na WM, vyama vyengine vya upinzani (hata CCM) viliungana na CDM.

Pili, kuna sheria za vyama vya siasa - CDM ihakikishe inakuwa karibu zaidi na msajili wa vyama vya siasa pamoja na kuwa kuna imani (na ndivyo ilivyo) kuwa hata chombo hiki nacho ni serikali, lakini hadi hapo tutakapopata katiba mpya, hiki ndio tulichonacho. Kwa hivyo, CDM ifanye kazi zake kutokana na miongozo na maagizo ya chombo hiki ili kiwe na reference ya matendo yake na mapambano yake na serikali.

Tatu, CDM ifanye kile ambacho serikali kwa makusudi haitaki kukifanya - kutoa elimu ya uraia kwa wananchi. Kama alivyosema dada AshaDii kwenye moja ya mabandiko yake kuwa CDM hapaswi kujiamini sana kwa kuona kundi kubwa la wananchi wako pamoja nacho. Tukubali kuwa wananchi wetu wengi ni masikini wa mali na akili, kwa hivyo ni rahisi kurubuniwa. Wengi kati ya hawa wote wanaoonekana kuiunga mkono CDM leo, siku ya siku wanaweza kuja kurubuniwa kwa chupa ya bia, buku 5, kilo/kiroba cha mahindi, upande wa kitenge, hata kwa kofia na fulana ya kijani...na kumaliza ndoto za CDM kuingia madarakani. CDM ina kazi kubwa sana mbele ya kutoa elimu ya uraia kwa Watanzania na njia moja ni kama katika mbili hapo juu ni kuwaunganisha Watanzania, kuviunganisha vyama vyengine vya upinzani, japokuwa si kiitikadi, lakini katika ukombozi. CDM ikumbuke kuwa, kwa kutofanya hivyo, wakati wa kura, na pengine hata sasa, adui wake si CCM/serikali tu bali hata vyama vyengine vya upinzani.

Nne (na mwisho kwa sasa), CDM itumie busara zaidi katika maamuzi yake. Umesema na tumeona, kuwa serikali haitaki kuondoka madarakani kwa hivyo inafanya kila iwezavyo, hata kuua kwa kutumia vyomba vya dola. Sasa ikiwa serikali/CCM imesema msifanye mkutano na mkifanya tutawauweni, kama ilivyofanya juzi, je CDM iko tayari, imejitayarisha kutangaza na kuanzisha vita na serikali? Kama ikitokea hivyo, ikiwa kila CDM wanapofanya mkutano maisha ya wananchi wasio na hatia yanakatishwa, je CDM iko tayari kuona hali hiyo inaendelea?

Wazo langu, ni juu ya CDM kuilazimisha serikali pamoja na msajili wa vyama vya siasa, wakae pamoja na kufikia makubaliano ya kitaifa wa kuacha kutumia ubabe huu. Ni ngumu kwa serikali kukubali moja kwa moja, lakini angalau pale itakapokuwa imekiuka makubaliano tayari kutakuwa na nani wa kumwoneshea kidole moja kwa moja. Aidha, CDM ishirikiane na jumuiya zisizo za kiserikali, za kitaifa na kimataifa katika kutafuta kuungwa mkono na kusaidiwa katika kutafuta haki na kutoa elimu ya uraia kwa Watanzania.

Mwisho napenda kutumia kauli mbiu ya UKOMBOZI UNAENDELEA badala ya Mapambano yanaendelea.
 
Well said Mkandara

Tuna matatizo makubwa kwenye mfumo wa utawala na kubwa zaidi ni nchi kukosa falsafa inayotuongoza. Haya matukio ni dalili tu za ugonjwa tunaoumwa kama jamii na kinachosikitisha zaidi ni jitihada nyingi zimeelekezwa kwenye kujaribu kuzitibu hizi "dalili" za ugonjwa bila kuutibu ugonjwa wenyewe na bahati mbaya dalili zipo nyingi, ukiacha "UCCM na UCDM" tuna "UKRISTO na UISLAM" tuna "UKANDA",wenye vipande chungumbovu ndani yake, na nyingine zitaendelea kujitokeza kila uchao.
Mourinho,

Kuhusu swala la Nchi kukosa falsafa inayotuogoza.

Nadhani hii kuna wakati imejadiliwa hapa kama mada iliyeelta hoja na mitizamo mbalimbali!

Kuna ambao walidhani kuwa hili sio tatizo la msingi kwani kinachotakiwa ni uogozi unaotoa matokeo ya kazi iliyofanywa. Kuna wengi ambao waliunga mkono dhana hii Mimi nikiwa mmoja wao na kumbuka hara Mkandara aliona hii kama hoja.

Mkuu nadhani tusaidiane sasa! Falsafa ya Taifa iwe ni ipi? Tunaitoa wapi?
 
Last edited by a moderator:
Mourinho,

Kuhusu swala la Nchi kukosa falsafa inayotuogoza.

Nadhani hii kuna wakati imejadiliwa hapa kama mada iliyeelta hoja na mitizamo mbalimbali!

Kuna ambao walidhani kuwa hili sio tatizo la msingi kwani kinachotakiwa ni uogozi unaotoa matokeo ya kazi iliyofanywa. Kuna wengi ambao waliunga mkono dhana hii Mimi nikiwa mmoja wao na kumbuka hara Mkandara aliona hii kama hoja.

Mkuu nadhani tusaidiane sasa! Falsafa ya Taifa iwe ni ipi? Tunaitoa wapi?

Zao kubwa, bora zaidi na la mwisho kabisa la TAFAKARI ni MANTIKI...(Reasoning destination=LOGIC-the Climax of Reasoning). Na hakuna MANTIKI kuu ya maisha ya binadamu kama UTU! UTU ndio msingi mkuu wa maisha yetu, UTU ndio sheria asilia, kanuni, ustaarabu na taratibu asilia zipasazo kumfunga binadamu kulinda ubinadamu wake ili asiwe mnyama! UTU ndio MANTIKI iliyo kubwa kabisa!

Tukae chini, tuzame katika tafakari nzito, tufikie kilele cha juu kabisa cha tafakari, tutafikia MANTIKI ya maisha yetu, mimi napenda kuiita UTU!

Falsafa yetu ili iwe na tija kwetu, ni lazima ifungwe na MANTIKI HII = UTU! Falsafa zenye UTU, zitahitaji mfumo mahususi kuzisimamia, mfumo huo utazaa sera sahihi kuusimamia, sera hizo zitahitaji sheria mahususi kuzisimamia, sheria hizo zitahitaji imani, mila, desturi, itikadi, matendo, mitazamo, n.k. mahususi kuzifanya hai! Tunaweza kuanza mfumo hadi Falsafa, vilevile Falsafa hadi mfumo ni sahihi zaidi!

TUKAE CHINI! Nirudie tena, sishangazwi na chochote kitokeacho kwa sasa, kwani HULKA ZA BINADAMU ZINAPOFIKIA UKAMILIFU WAKE ZINAWEZA KUFANYA CHOCHOTE na matokeo yake siku zote huwa HASI, hali kadhalika MANTIKI INAPOFIKIA UKAMILIFU WAKE NAZO ZINAWEZA KUFANYA CHOCHOTE na matokeo yake huwa CHANYA!

Maisha ni Furaha kama haipo ni UPUMBAVU na UPUUZI MKUBWA, na hakuna furaha ya mtu ila watu!

Mungu wetu anaita sasa!
 
Mourinho,

Kuhusu swala la Nchi kukosa falsafa inayotuogoza.

Nadhani hii kuna wakati imejadiliwa hapa kama mada iliyeelta hoja na mitizamo mbalimbali!

Kuna ambao walidhani kuwa hili sio tatizo la msingi kwani kinachotakiwa ni uogozi unaotoa matokeo ya kazi iliyofanywa. Kuna wengi ambao waliunga mkono dhana hii Mimi nikiwa mmoja wao na kumbuka hara Mkandara aliona hii kama hoja.

Mkuu nadhani tusaidiane sasa! Falsafa ya Taifa iwe ni ipi? Tunaitoa wapi?

Azimio Jipya,

Falsafa has got nothing to do with what's going on. In 70s when the country was fully of philosophical cliches, but the police force behaved the same way. Do you remember mauhaji Shinyinga? Do you remember mauhaji Kilombero?

In old days we didn't have instant communication or for that matter freedom to speak.
 
Well. It depends on what it means when they say public security and protecting life. Ukiangalia kiundani unaweza kuona kuwa sasa hivi polisi wetu ni source ya insecurity...unajua polisi wetu wanaua, wanapiga, wanatesa, wanatishia, wanadai rushwa kwa nguvu wakati mwingine kwa kutumia silaha....these do not show that the force is for public security as it claims.


Mie nina hakika kuwa polisi walikuwa wakitesa na kuua toka kitambo. Miaka ya 90 jamaa ambaye nilikuwa namfahamu kwa ukaribu kabisa, aliteswa hadi kuuwawa na hakuna lilofanywa ila maiti ilikabidhiwa na kuzikwa pia. Ila walau kulikuwa na 'catch' katika hilo; inasemekana alikuwa ni jambazi sugu wa kuvuka mipaka ya Kenya, Malawi, Zambia, Botswana na South Africa. Hata hivo yalikuwa yakifanywa kwa siri na that hilo lilipotokea hata watu kujua kateswa na police inakuwa kazi kujua... Ila sasa they seem confident enough to do it publicly...
 
AshaDii,

Today the Journalist has been killed. I am pretty sure some sympatheziers of the ruling party will continue to support police's actions no matter what you tell them.

The truth is the police force still uses the colonial manuals to train its personnel. So the tradition is police are above the law and they can do anything against innocent civilians.

You have a point here... It is the same thing pointed by others and much emphasized by Mkandara and Bongolander. That is where we as members of this society have to come to a healing solution, the first step maybe through discussions like we are doing right now and eventually and hopefully actions will follow.
 
AshaDii

"Never get angry. Never make a Threat. Reason with People" -God Father/Mario Puzo

I no longer support state investigations by forming the so called tume. Kwanza report zake hatuzisikii na hakuna msaada wala mabadiliko yoyote tume hizo zimeshaleta so far.

Ila nakubaliana na Mario Puzo...never show anger to your enemies...treat them with respect ili siku ukiwarudi heshima iendelee kuwepo

Nakubaliana na Mario Puzo Pia, ila at the end of the day hata kama haoneshi anger ni mtu wa kuchukua 'action' mradi apata kile ambacho kapanga. Katika hili naweza tumika msemo ambao naukubali sana katika kupanbana na adui hasa katika vita (toka katika kitabu cha The Art of War), ni ya centuries ago but still applicable to any war which could ever occur.

"If your enemy is secure at all points, be prepared for him. If he is in superior strength, evade him. If your opponent is temperamental, seek to irritate him. Pretend to be weak, that he may grow arrogant. If he is taking his ease, give him no rest. If his forces are united, separate them. If sovereign and subject are in accord, put division between them. Attack him where he is unprepared, appear where you are not expected." - sun wu (Chinese Military Strategist).
 
Hoja yangu kwenu wakuu AshaDii na MAMMAMIA ni moja tu;

Ningeomba muwe specific kabisa kwamba Chadema wanatakiwa kufanya nini katika mazingira haya kandamizi ambayo kila mmoja anayaona kwa macho yake, kwamba Chadema kufanya shughuli za kisiasa Iringa tarehe 02/09/2012 ni haramu lakini ccm kufanya shughuli za kisiasa Bububu siku hiyo hiyo ni halali.


Kuna hayo ambayo MAMMAMIA kazungumzia kwa kina, yote nakubaliana nayo; Pia naomba niongeze yafuatayo:

Mie naomba niwe wazi kwa hili na nitoe maoni yangu jinsi nionavo. Naweza nikawa nakosea ila wewe kama mmoja wa wana CDM damu naamini utaniweka sawa katika hili eneo... Mie naamini kabisa kuwa wengi wa viongozi wa CHADEMA litokeapo jambo kama hili deep down wanasikitika kuwa vurugu zimetokea hadi kusababisha vifo. Lakini pia kwa upande mwingine huwa wanafurahia kwa vurugu ambazo hutokea tokana na wafuasi wa CHADEMA kushiriki katika vurugu ambazo huwa zinakuwa dhidi ya police.

Kwa njia moja ama nyingine naweza diriki kusema kuwa wanakumbatia, labda sababu ni ujumbe kwa Serkali ya CCM kuonesha kuwa wana nguvu ya Umma nyuma yao, ama labda kwa sababu ya kuonesha ujumbe kuwa wao sio wa kuchezea AMA for whatever reasons wanaweza kuwa nazo.

Kwanini nasema kwa Kiasi fulani CDM Wanakumbatia? (Najua hii kama kawa itawakwaza wana CDM wengi ambao kwa bahati mbaya sana wao huona kusifiwa tu ndio tija ila wasikosolewe hata kama hoja jengevu);


Wafuasi wa CDM wengi wao wapo 'Chademically Brain-washed'

Hawaambiwi lolote lile na wala hawatambui na wala kukuelewa utapozungumza baya kuhusu CDM. Kundi kubwa la wanaoudhuria mikutano ni wale Watanzania wa kawaida na wa chini, (achana na hii middle class ambao wengi tupo nao hapa mtandaoni). Hilo kundi limechoka na hali halisi ya maisha, na CDM imetokea kuwapa matumaini ya a better Tanzania.

Hata kama umekosoa kujenga wao hawaelewi! Ni baadhi ya watambuzi na wajuvi ambao huwa waelewa... Hio ni wazi hata hapa hapa jf hasa pale Jukwaa la Siasa. Comment nyingi ni ushabiki radher than deep genuine insights. NAAMINI Slaa aama kiongozi yeyote wa CDM akiongea mbele ya umati wake kuwa wajitahidi kuepusha shari kwa vovote vile inawezekana.

Vurugu (baadhi) zaweza epushwa kwa kuchukutumia pre-emptive measures

Nitolee mfano wa maandamano ya Morogoro ambapo ilisababisha kifo cha Marehemu Ally Zona; Lile tukio CDM pia ni wakulaumiwa. So far tokana na habari nilizosikia na jinsi ilivotangazwa, wana CHADEMA walikuwa na kibali cha kufanya Mkutano hapo Morogoro lakini hawakuchukua kibali cha kufanya Maandamano (ambayo yalianzishwa na kuleta vurugu zote zile).

Wao CDM sio wageni na matendo ya Polisi dhidi yao hasa kwenye mikutano na maandamano yao ambayo kwa sasa inakuwa maarufu kwa kusababisha vurugu. HAIPENDEZI, Kwa kutambua hilo ni jukumu lao kutambua kuwa yale maandamano ni LAZIMA yangeleta vurugu, ustaarabu ingekuwa mipango mizuri ya mobilisation ambayo haipelekei maandamano.

Kaka Maranya huo ndio mtazamo wangu, nitashukuru kama wewe ama yeyote yule atanielewesha ipasavo kuwa nipo wrong.
 
Kwa mara nyingine tena Tumepewa harufu ya kahawa wadanganyika tuamke lakini kwa hali tete naona ndio kwanza wengi wanalivuta Blanketi zito na kutokomea ktk usingizi mzito kama pono..In fact Wadanganyika tunaweza kuitwa wanadamu pekee wanaotembea wakiwa macho lakini akili zao zimelala..

Sisi sote tuna matatizo makubwa sana ya kufahamu UHURU wetu una maana gani kwetu zaidi ya kutoka mikononi mwa mkoloni mweupe. Niliwahi kusema kwamba tatizo la Mdanganyika ni kutokuwa na IMANI ya UTU wake isipokuwa imani ya dini ambayo pia hatuzifuati isipokuwa kwa kutiwa maji uya Ubatizo (kusilimu) na kuitwa jina la kiislaam au Kikristu na tukaamini kwamba sasa tumeokoka pasipo hata kufanya ibada zinazotakiwa..

Kwa fikra hizo hizo tunafikiri ukisha kuwa Mtanzania basi inatosha, serikali ndio yenye jukumu a kukuletea maendeleo nyumbani, serikali ndiyo inayotakiwa kukupa kazi, na hata kukujengea nyumba na kulea watoto wako kama tunavyoamini Mungu anatupenda wote hivyo kuwa na mafanikio ni kazi ya Mungu. Aliyekupa wewe ndiye katunyima sisi.. Hapa ndipo akili za Mdanganyika zilipogota na pengine hatuna tofauti na Mnyama, samaki au mdudu ktk hali hiyo.

Jamani AKILI pasipo ELIMU haina tofauti na Mnyama (Gods must be crazy) na hata mwenye ELIMU pasipo kuitumia ktk kupambanua zuri na baya, kujua umuhimu wa kudai uhuru, haki na usawa mbali kabisa na kutafuta riziki na maendeleo ya jamii yetu ni sawa kabisa na mtu asiyekuwa na elimu. ELIMU ndio huchochea UTU wa mwanadamu ktk kutafakari na ubunifu wa falsafa ktk kuyaongoza matendo yetu na hapa ndio UTU wetu hupata kuonekana.

Usiku wa jana nikiwasikiliza Demokratic Convention nilipata msisimko mkubwa baada ya kusikia wajumbe wake wakizungumzia falsafa ya AMERICAN DREAM kuwa msingi wa maandalizi ya Utaifa wa nchi hiyo. Wakati Republican wakiamini UWEKEZAJI mkubwa na kodi nafuu ili kuwezesha ndoto hizo kushuka kwa walalahoi..Democratic wakisema walalahoi waliisha achwa siku nyingi nyuma na ni wakati wa kuwatazama middle class ambao ndio waajiri wakubwa na mkazo zaidi ktk kuwekeza kwa kizazi kijacho ktk elimu na Afya na kwamba ELIMU ni fundamental RIGHT ya mtoto wa Kiamarika wala sii privilege kwa sababu wanataka ku invest ktk kizazi kijacho ili kuwawezesha kushindana ktk dunia hii ya Utandawazi. Ndoto hii unaiona ktk picha ya kufikirika na kukupa matumaini kwa viongozi wako wanakufikiria..

Hawa wenzetu wanatafuta kusonga mbele na hata wamefikia kuwa na NDOTO ya kila mtu anayeishi Marekani wala sii uongo hata kidogo, na wanazifanya jitihada kubwa kuhakikisha kwamba kwa kila mtu anayeweka jitihada kubwa pasipo kujali background yake anaweza kuwa chochote anachotaka kuwa. Sisi leo hii tumekwama ktk shimo la Umaskini utadhani kaa wa baharini ktk tenga la mvuvi na hatuna hata fikra za kujikomboa zaidi ya kusbiri Mungu katuwekea hatma gani.

Sasa unaweza vipi kunambia wale kaa ktk tenga la mvuvi wanaweza kuwa na ndoto gani?. Kwani sio swala la ndoto ila ni ulazima wa kutoka ktk tenga lile au sivyo?..Je sisi wadanganyika tulokwama kama wale kaa tuna mpango gani wa kujikwamua ktk umaskini acha mbali kusonga mbele wala kuwa na ndoto. Tuna mipango gani ya kuhakikisha haturudi ktk umaskini kwa kupitia mfumo ule ule ulotufikisha hapa leo..Halafu tujiulize pasipo elimu leo hii tuna tofauti gani na wale kaa ktk kau la mvuvi, maana wadudu wale hawana akili na hivyo hawana elimu, na ndio maana huishia ktk mafuta ya moto..

Na mdio maana kwa ujinga huu hatujui tutatoka vipi, kwa ujinga huu hatujui hata maan ya sensa. kwa ujinga huu leo Watanzania wako zaidi ya millioni nchi za nje lakini hawajui Uhumimu wa Diaspora, na hata Diaspora wenyewe hawajui wanaweza kufanya nini wakiwa pamoja Marekani, Canada au Uingereza zaiadi ya Udaku na kusodoana wakati mataifa mengine wanapiga hatua kubwa ktk maendeleo ya jamii zao. Je, nasema Uongo?, sasa unategemea vipi Mdanganyika asiyekuwa na elimu Tanzania atakuelewa!..

Wanaweza vipi wasiokuwa na elimu kukaa pamoja wakafikiria jinsi ya kutoka ktk tenga hili la umaskini ikiwa mijitu yenyewe haina ELIMU na elimu kwa sio kipaumbele. Ni mijinga sawa sawa na kaa alivuliwa baharini maana sisi tunasoma ili tupate riziki na maendeleo kjambo ambalo hata viumbe wasiokuwa na akili wanavifanya!. Huu ndio ukweli mtupu hata msomi mwanasiasa mahili nchini ni yule anayefikiria Kula kulala na jinsi ya sustainable economy. Jamani hata yule Mamba wa mto Mara, Simba wa Serengeti, Bear wa Canada ama Papa wa bahari kuu ya Hindi wote hawa hujiandaa kutokana na mazingira tofauti ili waishi maisha marefu zaidi.

Tofauti yetu sisi na hawa wanyama ni kwamba tumeumbwa na AKILI, akili ambayo hutuwezesha sisi kutofautisha kati ya baya na zuri.. UTU wetu utabeba jukumu kubwa zaidi ktk kutafakari thamani ya UHURU, HAKI na USAWA kuwa stahiki ya kila binadamu na viumbe vya mwenyezi Mungu. Akili inayotuwezesha sisi kufikiria nje ya maumbile na mahitaji yetu katika kumsifia hekima kubwa ya mwenyezi Mungu ktk kuiumba dunia hii na vilivyomo na ni elimu pekee ndiyo itakayo tuwezesha....

Kuna sehemu moja Michelle Obama alinigusa zaid alizungumzia historia ya maisha yake yeye na mumewe, walikotoka na hadi kufika hapo walipo ya kwamba rwasiwasi yake ilikuwa pengine Obama angekuwa mtu tofauti baada ya kutoka ktk umaskini na kukabidhiwa kiti cha IKULU..Lakini hakikuwa hivyo isipokuwa kuwepo mkwake IKULU kumemwezesha kuwatazama zaidi watu wa chini, watu wanaokutana na matatizo ya kimaisha kaa alokutana nayo marehemu bibi yake na aliweza kuelewa matatizo yao...

Lakini Tazama wadanganyika sisi, ukipewa cheo tu basi unasahau ulikotoka, tumewaona wangapi ndani ya uongozi wa CCM. Hivyo leo hii imefikia hadi Askari Polisi anayekabidhiwa kazi ya kuwalinda wananchi, yeye kwa fikra zake anaona amepewa kazi ya kulinda Utawala hivyo kuwanyanyasa wananchi maana ndivyo ilivyokuwa toka wakati wa mkoloni au utawala wa Apartheid. Askari kazi yake ilikuwa kuulinda utawala wa Mkoloni, askari kazi yake ilikuwa kumlinda mkuu wa wilaya, Mkoa na hata Kitaifa. Maswala ya wezi na kadhalika yalimalizwa na wajumbe wa nyumba kumi unless umeiibia serikali..

Huu ndio mfumo unaoendelea leo nchini na kwa bahati mbaya kila kiongozi anayeshika madaraka ya juu huchukua nafasi ya Mkoloni au Apartheid kuwa na Utawala wenye mamlaka juu ya sheria. Sheria zinatungwa kuwalinda wao na ni haki yao kutawala., hivyo ni jukumu la jeshi la ulinzi na polisi kuwalinda wao. yawezekana kabisa Kikwete anafikiria hivyo, Mukama na Nape wanafikiria hivyo, Pinda, Sitta hadi yule askari wa chini kabisa kituoni anafikiri hivyo.

Na ndio maana kwao ni lazima mkutano au maandamano yapewe kibali na sio ombi la kulindwa. Huku Ulaya ukiandamana au kufanya Mkutano waandaaji huwalipa jeshi la Polisi kwa kazi ya siku hiyo maana huomba kulindwa na sii kibali na ruksa ya kuandamana. Na nimemsikita jana tu Nchmbi akizungumza kuhusu Dr.Slaa inathibitisha kabisa kwamba Tanzania yetu leo hii haina tofauti kabisa na utawala wa Apartheid na itachukua muda mrefu sana hata hawa viongozi wetu kujitambua kama wao ni Watanzania kama sisi na sio jamii ya WaCCM ama viumbe tofauti..
 
Azimio Jipya,

Falsafa has got nothing to do with what's going on. In 70s when the country was fully of philosophical cliches, but the police force behaved the same way. Do you remember mauhaji Shinyinga? Do you remember mauhaji Kilombero?

In old days we didn't have instant communication or for that matter freedom to speak.

C'mon Zakumi,

You have refreshed my memories, great deal ... Lol! What was that threadagain!! ha hah!

We realy went down to explore everything on those lines! Even the Mkandara"DIRA thing" ... I don't even remember how we concluded !!

Anyway as you can see it wasn't me "This time" .. who brought it up... !! see how I am making them explain it? Please join and do some contributions ...!!
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na Mario Puzo Pia, ila at the end of the day hata kama haoneshi anger ni mtu wa kuchukua 'action' mradi apata kile ambacho kapanga. Katika hili naweza tumika msemo ambao naukubali sana katika kupanbana na adui hasa katika vita (toka katika kitabu cha The Art of War), ni ya centuries ago but still applicable to any war which could ever occur.

"If your enemy is secure at all points, be prepared for him. If he is in superior strength, evade him. If your opponent is temperamental, seek to irritate him. Pretend to be weak, that he may grow arrogant. If he is taking his ease, give him no rest. If his forces are united, separate them. If sovereign and subject are in accord, put division between them. Attack him where he is unprepared, appear where you are not expected." - sun wu (Chinese Military Strategist).

Is it a concidence you read the books that I read? Adui yetu wote ni mtu anayetaka kutuona tunasambaratishana kwa ajiri ya manufaa yake binafsi. Huyu tuombe Mungu amrudi na tumkate kwa nguvu zetu zote.
 
Let me ask you guys this question. Do you think if CHADEMA takes power, the police force or for that matter our security forces will behave differently?
 
Azimio Jipya,

Falsafa has got nothing to do with what's going on. In 70s when the country was fully of philosophical cliches, but the police force behaved the same way. Do you remember mauhaji Shinyinga? Do you remember mauhaji Kilombero?

In old days we didn't have instant communication or for that matter freedom to speak.

Falsafa ndiyo ingeamua nini kiwepo au kitokee nini kwa wakati gani!

Ni zaidi ya Dira ama msingi! Ni JINSI GANI TUNAPASWA KUISHI kwanini, kwa namna gani, ili iwe nini na kwa nani! Hapo ndipo Falsafa kuu inapohitaji kufanywa maisha yetu halisi, yaani kuanzia ngazi ya imani, mila, desturi, itikadi, mitazamo, mienendo, vitendo, n.k. vitakayosadifu na kufungwa na falsafa kuu. Kisha hayo yatazaa sera bora kusadifu na kufungwa na falsafa kuu, sera hizo zitazaa sheria zitakazosadifu na kufungwa na falsafa kuu, sheria hizo za kiuchumi, siasa na utamaduni zitazaa mfumo utakaosadifu na kufungwa na falsafa kuu! Hapo kila kitakachotokea, au tutakachotaka kufanya, kitapimwa kwa mizani ya falsafa yetu kuu!

TUJIULIZE LEO: Ni falsafa ipi ituongozayo, itufungayo na kututambulisha?

Sheria zinatungwa kwa jinsi watu wajisikiavyo tu, ameshawishiwa na mkewe ama rafiki yake mweupe, anasimama jukwaani "tunataka rais asishtakiwe 'katiba iseme' " wengine nao "tunataka utawala wa majimbo" hawa nao "tunataka serikali tatu/mbili/1" laiti kama tungekuwa na Falsafa yetu, kusingekuwa na malumbano yasiyokuwa na msingi kama yale yanayotokea Dodoma! Kila mtu angepima mawazo yake katika kupata mashiko kwenye falsafa yetu! Kama ameyaona anayawasilisha kwetu.

Ninaamini kabisa haya yatokeayo leo, yasingekuwepo kama tungekuwa na falsafa yetu, labda tu kama ingezaliwa kutokana na HULKA za binadamu na si MANTIKI ya mambo, naita UTU!

Taifa pasi na Falsafa bora, raia wake huongozwa na HULKA na MATAMANIO yao, na hapo UKINZANI ndipo uibukapo, ni chuki na visasi, hofu na umungu kila mtu atapigania kuwa juu ya mwenzake, mauaji kama pombe...matabaka, unyonge, n.k Haipo Falsafa ya kutufunga!

Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani, anaita sasa!
 
Let me ask you guys this question. Do you think if CHADEMA takes power, the police force or for that matter our security forces will behave differently?

Zakumi,
Let me give you an answer. Do you remember the mutiny of 1964? Nyerere used that as an opportunity to retrain our army and it became the peoples army. When we take over we will retrain the police force to become the people's police and not the fisadi police.
 
Zakumi,
Let me give you an answer. Do you remember the mutiny of 1964? Nyerere used that as an opportunity to retrain our army and it became the peoples army. When we take over we will retrain the police force to become the people's police and not the fisadi police.

You see sir. You say "When we take over". another says "CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015". What I see is EYES ON PRIZE, nothing more.

The police force has been used as hunting dogs of those in power, and I am pretty sure CHADEMA won't change it.

By the way I attended CHADEMA's meeting last Saturday. My assessment is as a country we lack brain-power.
 
Falsafa ndiyo ingeamua nini kiwepo au kitokee nini kwa wakati gani!
Ni zaidi ya Dira ama msingi! Ni JINSI GANI TUNAPASWA KUISHI kwanini, kwa namna gani, ili iwe nini na kwa nani! Hapo ndipo Falsafa kuu inapohitaji kufanywa maisha yetu halisi, yaani kuanzia ngazi ya imani, mila, desturi, itikadi, mitazamo, mienendo, vitendo, n.k. vitakayosadifu na kufungwa na falsafa kuu. Kisha hayo yatazaa sera bora kusadifu na kufungwa na falsafa kuu, sera hizo zitazaa sheria zitakazosadifu na kufungwa na falsafa kuu, sheria hizo za kiuchumi, siasa na utamaduni zitazaa mfumo utakaosadifu na kufungwa na falsafa kuu! Hapo kila kitakachotokea, au tutakachotaka kufanya, kitapimwa kwa mizani ya falsafa yetu kuu!
TUJIULIZE LEO:
Ni falsafa ipi ituongozayo, itufungayo na kututambulisha?
Sheria zinatungwa kwa jinsi watu wajisikiavyo tu, ameshawishiwa na mkewe ama rafiki yake mweupe, anasimama jukwaani "tunataka rais asishtakiwe 'katiba iseme' " wengine nao "tunataka utawala wa majimbo" hawa nao "tunataka serikali tatu/mbili/1"
laiti kama tungekuwa na Falsafa yetu, kusingekuwa na malumbano yasiyokuwa na msingi kama yale yanayotokea Dodoma! Kila mtu angepima mawazo yake katika kupata mashiko kwenye falsafa yetu! Kama ameyaona anayawasilisha kwetu.
Ninaamini kabisa haya yatokeayo leo, yasingekuwepo kama tungekuwa na falsafa yetu, labda tu kama ingezaliwa kutokana na HULKA za binadamu na si MANTIKI ya mambo, naita UTU!
Taifa pasi na Falsafa bora, raia wake huongozwa na HULKA na MATAMANIO yao, na hapo UKINZANI ndipo uibukapo, ni chuki na visasi, hofu na umungu kila mtu atapigania kuwa juu ya mwenzake, mauaji kama pombe...matabaka, unyonge, n.k Haipo Falsafa ya kutufunga!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani, anaita sasa!

Do you know that fascism is a falsafa in its own right? Do you know that fascim is a vision on its own?
 
Zakumi,

Mkuu wangu shukran sana kwa kuliweka swali hili.. nadhani swala zima linatakiwa kutazwa toka nje ya sanduku la Uchadema au UCCM kwa sababu sio CCM ama Chadema wanaowawezesha Polisi kuwa brutal isipokuwa mfumo mzima wa kiutawala..

Nadhani unakosea unaposema hakuna umuhimu wa Falsafa ya uhai wetu kama WATANZANIA na sio fikra za uhuru wa bendera unaolenga sovereignty na mipaka ya nchi husika..Falsafa ni uhai wa WATU ktk mazingira (A system of values by which one lives) na hizi values ndio huwa Principal ya Utaifa wa watu hao.. Hivyo hata hao unaosema Fascism ni Falsafa kwa watu wale.. Hivyo kuwepo kwa Fascism ndiko kunako tulazimisha sisi kuwa na Principal zinazopingana na fikra kama hizi ili tuwe na zile zinazotulenga sisi kama Watanzania - Principles of reality. Na ndio maana muda mwingi nimesema sana kuhusu sisi kurudi nyuma na kujitazama, kujitambua who we are kwanza kama Taifa, laa sivyo leo hii tusingekuwa tunabishana humu isipokuwa kutazama ethics na values zetu kujua ni wapi tunakosea..Ukiona watu wanabishana juu ya jambo basi elewa ni kwa sababu wamepoteza DIRA hivyo ethics na values..

Binafsi yangu nimekuwa na matatizo na hili neno UTU linapochukuliwa kama faslafa kwa sababu UTU ni ile quality of being human ambapo maswala muhimu ya Uhuru, haki, na Usawa vinapotafsiri fikra, maamuzi na matendo yetu ktk mazingira tuliyopo. Hivyo faslafa kwa mapana yake tunatazama falsafa ya maisha..Haya yanayofanyika Tanzania leo ni kutokana na sisi wenyewe kutothamini UTU hivyo tumepoteza ethics na values hata kwa kutumia logical reasoning tunabishana kutwa nzima. Mtu atasimama kueteta Ufisadi, mwingine atasimama kutetea Polisi kwa sababu hatuna values ktk utu wetu isipokuwa ule anaouthamini yeye..

Kila mmoja wetu humu ana values zake aidha iwe za kiasili au imani ya dini au Upagan na hakuna control tena ndio maana tunazitetea. Jambazi sugu litasifika na kuitwa Pedejee - jizi hili!, Fisadi atasifiwa kwa kuiba mabillioni na kujengea wanawake nyumba na mashangingi na wanaolalamika ndio wenye wivu ujinga na hila. Pengine niongezee kusema (mtanisamehe) hata wakristu hapa janvini hawawezi kumtazama Muislaam kama mwenzao isipokuwa ni WALE, WAO against SISI kama kundi tofauti la kijamii ktk Utanzania wetu hivyo hata kuyasikiliza machungu yao inakuwa bughudha kwao. Amini maneno yangu huwa nashindwa kuelewa kwa nini jamaa zangu wakristu tunapowaambia serikali inawakandamiza waislaam wana question waislaam na sio serikali? halafu unaambiwa tuko pamoja!.. Chadema wanailalamikia serikali kuhusu Mafisadi nchini lakini wanaCCM wanawa question Chadema uhalali wa madai yaokuwa ni uzushi, wadini, wenye wivu na wakosa..

Ni katika hali hii ya utengano wa ambao uemtokana na kutokuwa na dira ya Kitaifa ndio maana kikila mmoja wetu anaiona haki upande wake na dhulma anapokosa..Hata ukimuuliza Chenge kuhusu Ufisadi atakuona mchawi tu kwa sababu kisha jitenga na kundi la maskini, wajinga na wenye maradhi. Vile vile ukimuuliza mwana CCM atakujibu kuwa Chadema wajinga wanalalamika tu kwa kila kitu wakati ni wao wenye kuleta vurugu.

Umoja wetu umesha kwisha vunjika na sii kazi rahisi kurudisha Umoja huu pasipo ku sacrifice UBINAFSI, UMIMI, USISI kwa kutambua sisi ni taifa moja lenye watu wenye tofauti zake za kijamii. Hata Nyerere alianzia hapo kabla ya kubuni Azimio la Arusha maana inakulazimu uanze na Watu (walikotoka na walipo) ktk Mazingira (maliasili na rasilimali zake) ndio unaweza kuipata picha halisi ya unakotaka kwenda. Tukiweza kundoa ubinafsi na kila mmoja kujenga Uzalendo mkubwa utakaolazimishwa na PATRIOT ACT ya kwetu kusisitiza UZALENDO wa kila Mtanzania kufuata falsafa yetu itayolingana na WATU na MAZINGIRA yetu -Principal of reality..

Mitazamo yote hii ya Ubinafsi inatokana na kwamba kila mtu kabeba msalaba wake hivyo badsi hata Chadema wakiingia Madarakani nina hakika watafanya kile wanacho kiamini japokuwa hakitakubaliwa na wengine. Mafisadi watalaani, pengine Polisi watatumiwa kuwanyanyasa wenye nacho na pengine mauaji kutokea..It all round up to what set of ideas or beliefs developed into policies relating to particu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom