Kifo hakipangwi na Mungu

Nimesikiliza watu wengi mtu akifa wanasema "Mungu amepanga". Uongo huu umepita kizazi hata kizazi ili tufarijike katiba misiba.

Ukweli ni huu, Mungu hapangi kifo cha mtu chini ya miaka 70. Mtu anayekufa akiwa na miaka zaidi ya 70 ni mapenzi ya Mungu.

Mungu hana kitabu ameandika aina ya kifo cha mtu chini ya miaka 70. Watu wanakufa kutokana na aina ya maisha wanayo ishi, mazingira wanayoishi na imani za kishetani.

nimesikia
wanasema
imeandikwa kwenye biblia si mpango wa mungu binadam afe akiwa kijana..

ila ujue kuwa toka uumbaj umri wa kuish wa binadam kila miaka inavyopita kumbuka wana israel wa kipind cha biblia waliish had miaka zaid ya miatano wengine wakioa wakiwa
na miaka zaid ya mia.. lakin kipind cha yesu hali ilikuwa tofaut watu walikua wanafika kwenye hundred and somthimg ss hv hata wa 90 wakuhesabu ..

so nadhan bado nahis ni mpango wa mungu mtu akifa isipokuwa kama kifo chake kitakuwa na walakin ambao shetan kaweka mkono wake...
 
Hata jibu lako hili linaonesha ulivyo mtu wa kukurupuka kujibu. Ikiwa unaamini kwamba kuna mambo yanayoweza kupita kimo cha ufahamu wangu, kwanini basi nisiamini hivyo kwako kwamba hata hilo la Mungu ni jambo lililokupita kimo chako cha ufahamu? .

Unaweza kuamini chochote unachotaka kuamini. Lakini kuamini hivyo hakufanyi Imani yako kuwa kweli.

Unaweza kuamini kwamba Mungu ni jambo lililonipita ufahamu.

Lakini, nimekupa nafasi kuthibitisha kama mungu yupo.

Umeshindwa.

Hivyo, unaamini habari isiyothibitishika.

Ukitaka kuamini kitu kipo kwa kusema kimepita uelewa wetu, unaweza kuamini chochote.

Unaweza kuamini mungu yupo, na kapita uelewa wetu.Na hapohapo ukaamini mungu hayupo, na kuelewa hilo kumepita uelewa wetu.

Dhana nzima ya kutafuata ukweli kwa mantiki inavunjika.

Utakubali vipi habari ya kwamba mungu yupo na kapita uelewa wangu wakati hata huwezi kumuelezea na kuthibitisha yupo?

Nikiondoa mungu na kuweka neno lingine lolote, kwa mfano, "nyani mkuu" aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyopo, yupo, na humjui kwa sababu kapita uelewa wako tu, utawezaje kukataa kama umekubali kwamba mungu yupo na kapita uelewa wangu tu?

Ukitaka nikuthibitishie na kukuonesha jinsi ulivyochanganyikiwa, nioneshe kwanza na kunithibitishia kwamba Mungu hayupo.

Inaonekana hujaelewa habari nzima niliyoiandika kuhusu falsafa ya uthibitisho.

Tena nimeandika Kiswahili usije kusema nimeandika lugha ngeni hukuelewa.

Visivyopo havithibitishiki kwamba havipo.Kwa sababu havipo.

Vinavyothibitishika ni vilivyopo, kwa sababu vipo.

Ndiyo maana hata polisi wakija kumkamata mtu kwa kosa la kuwa na madawa ya kulevya nyumbani kwake, hawamwambii "thibitisha kwamba nyumba yako haina madawa ya kulevya". Hata akiichambua nyumba hiyo kwa miaka milioni moja kutaka kuonyesha kwamba nyumba haina madawa ya kulevya, hilo halitathibitisha kwamba nyumba haina madawa ya kulevya.

Njia pekee ya uhakika kuthibitisha ni Polisi kusachi nyumba kwa taratibu na hakika mpaka wapate madawa ya kulevya.Hapo watakuwa wamethibitisha kwamba madawa ya kulevya yamo kwenye nyumba hiyo.

Sasa unachofanya wewe ni sawa na polisi anamwambia mtu "thibitisha nyumba yako haina madawa ya kulevya". Ni kutoelewa falsafa ya uthibitisho.

Unachotakiwa kufanya ni kuonyesha madawa ya kulevya yapo.

Sasa wewe unayesema mungu yupo, unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

Najaribu kukusoma kwenye michango yako, kwa mfano unasema imani ya kuwepo Mungu ilianzia zama za giza, je unaweza kutupa uthibisho wa kuwepo kwa zama hizo? .

Kabla ya kukujibu, unaelewa nini mtu akikwambia "zama za giza"?

Wewe ni atheist lakini msimamo wako huo umejengwa juu ya wengine ndio maana unapata ujasiri wa kuturejesha kifikra kwenye zama ambazo hukuwepo na hakuna anayethibitisha kwamba zilikuwepo.

Wewe unayekubali mungu wa kutungiwa na wengine na kuletewa kwenye vitabu ulikuwepo wakati huyo mungu alivyofanya hayo anayosemwa kuyafanya kwenye vitabu?
 
Ninaamini yupo kwa sababu nimemu-experience ktk maisha yangu na katika maisha ya wengine.
Umemu experience vipi?

Experience is not necessarily objective.

Mimi naweza kumuonea huruma maskini kwa utu wangu, maskini akamuomba mungu (ambaye hayupo), mimi na ubinadamu wangu nikampa maskini msaada.

Maskini badala ya kunishukuru mimi mtu anayeniona nimemsaidia, akaenda kumshukuru mungu ambaye hayupo kwa sababu katika "experience" yake, kaona kwamba mungu kamjibu maombi yake.

Umesema unakuwa mwangalifu kutopoteza uwezo wako wa kufikiri.

Usipoteze uwezo wako wa kufikiri katika hili pia.

Watu hawapendi ukiwa na uyatima. Hawapendi kuwa wenye wajibu wa mwisho.

Hivyo, wameamua kumuweka mungu - ambaye kiukweli hayupo- ili awe baba wa wote na mwenzi wa wote.Muweza wa yote, kimbilio la mwisho.

Yakikushinda kabisa, unapata jibu rahisi kwa kumuomba mungu tu. Therapy on the cheap. This might have served an evolutionary cause in the past, or maybe even served as a morality compass, but that does not mean it is true and absolutely necessary.

Mungu ameumbwa na binadamu (kama idea). Mungu hakumuumba binadamu, kwa sababu hayupo.
 
Nyie watu mtu akiwafatisha lazima apotee.
Maneno yako yana mantiki lakini kwenye swala la Mungu hutakiwi kutumia mantiki sana bali imani, ingawa wakati mwingine swala la imani ni kwenda nalo kwa makini pia.

It's complicated.
 
Afadhali umekubali kwamba umeamua kuamini tu bika kufuatisha mantiki.

Mtu akiniambia hivyo namuheshimu sana na naheshimu anavyoamini, sinabhaja hata ya kumuuliza zaidi. Kwa sababu naona ni mtu anayeelewa anafanya nini.

Tatizo ni hawa watu wengine wanafuata mkumbo wa imani, halafu wanataka kuchanganya imani na mantiki.

Wanabisha kabisa kwamba dini yao ndiyo yenye ukweli, uzuri na mantiki.

Wakati hapo hapo wanakuambia hawawezi kumjadili mungu wao kwa mantiki, kwa sababu wanaogopa kukufuru.
 
Kanuni za asili haziwezi kubadilishwa na chochote. Nafurahi kusikia watu wanaona Mungu sio muweza wa yote.Tukiondoa nadharia hii vichwani basi tutatatua matatizo mengi ila tukiendelea kungoja huruma za mungu tutahangaika maishani
Kwasababu umezingirwa na upofu wa ufahamu wa Mungu, utaendelea kufurahia maoni ya wanaojidanganya km wewe
 
Yes hakuna kifo kinachopagwa na Mungu hata uwe na miaka zaidi ya 70
Wala sijawahi kupata sababu za kuridhisha ya kwanini mtu akifa wanasema kazi ya Mungu haina makosa.
Weka vigezo vya kujiaminisha kuwa hakuna kifo kipangwacho na Mungu
 
Afadhali umekubali kwamba umeamua kuamini tu bika kufuatisha mantiki.

Mtu akiniambia hivyo namuheshimu sana na naheshimu anavyoamini, sinabhaja hata ya kumuuliza zaidi. Kwa sababu naona ni mtu anayeelewa anafanya nini.

Tatizo ni hawa watu wengine wanafuata mkumbo wa imani, halafu wanataka kuchanganya imani na mantiki.

Wanabisha kabisa kwamba dini yao ndiyo yenye ukweli, uzuri na mantiki.

Wakati hapo hapo wanakuambia hawawezi kumjadili mungu wao kwa mantiki, kwa sababu wanaogopa kukufuru.
Si kwamba naamini tu bila mantiki. Nilichomaanisha ni kwamba naamini lakini katika kuamini natumia mantiki pia.

Mantiki pekee ni hatari kwani kwa kiasi kikubwa hupingana na uwepo wa Mungu tena kwa sababu na hoja zenye uzito (kama sababu zako mfano). Lakini pia imani peke yake bila mantiki inaleteleza ujinga. Huwezi kuamini tu kiholelaholela.

Hivyo basi naamini lakini ktk mchakato wa kuamini kuna baadhi ya vitu siviamini, navikataa na navichallenge kwa kutumia mantiki.
 
Si kwamba naamini tu bila mantiki. Nilichosema ni kwamba naamini lakini katika kuamini natumia mantiki pia.

Mantiki pekee ni hatari kwani kwa kiasi kikubwa hupingana na uwepo wa Mungu tena kwa sababu zenye uzito (kama sababu zako mfano). Lakini pia imani peke yake bila mantiki inaleteleza ujinga. Huwezi kuamini tu kiholelaholela.

Hivyo basi naamini lakini ktk mchakato wa kuamini kuna baadhi ya vitu siviamini, navikataa na navichallenge kwa kutumia mantiki.
Ukitumia mantiki katika kuamini, utaona mungu hayupo.

Kwa sababu hutaki kuona mungu hayupo, ukifikia hapo, utaacha mantiki na kufuatisha kuamini kusiko na mantiki.

This is pretty much what you have said here.

Kwa nini mantiki iwe hatari kama inapingana na uwepo wa mungu ikiwa hilo (kwamba mungu hayupo) ni kweli?
 
Siwezi kuona Mungu hayupo eti kwa kutumia mantiki ktk kuamini. Mantiki inanisaidia nisiwe bendera fata upepo kwenye maswala ya imani.
Mantiki ni muhimu ktk kuamini.

Hata wewe huna uhakika kuwa Mungu hayupo. Unatumia mantiki tu ktk kudhibitisha hoja zako ambapo inafikia mahali unakwama.
 
Ninaamini yupo kwa sababu nimemu-experience ktk maisha yangu na katika maisha ya wengine.

Kiroho safi kabisa....

Kama huyo mungu tayari una tajiriba/ uzoefu naye, iweje tena uamini kwamba yupo?

Mi nilidhani labda hiyo tajiriba/ uzoefu ilikupa ufahamu/ ujuzi kwamba yupo kweli.

Sasa kama yupo kweli [kwa mujibu wa hiyo tajiriba/ uzoefu wako kwake na kwa maisha ya wengine], kwa nini unaamini, na si kujua, kwamba yupo?

Vilivyopo huwa vinaaminika au huwa vinajulikana kuwa vipo?

Au hayo maneno 'kuamini na kujua' huwa yanatumika interchangeably?
 
Siwezi kuona Mungu hayupo eti kwa kutumia mantiki ktk kuamini. Mantiki inanisaidia nisiwe bendera fata upepo kwenye maswala ya imani.
Mantiki ni muhimu ktk kuamini.

Hata wewe huna uhakika kuwa Mungu hayupo. Unatumia mantiki tu ktk kudhibitisha hoja zako ambapo inafikia mahali unakwama.
Umesema unaamini kwamba mungu yupo kwa experience, ni experience gani hiyo inayokufanya uamini kwa mantiki?

Hujaitaja.

Mimi nishaeleza kwamba mungu wenu huyu muumba vyote, mwenye ujuzi wote, uwezo wote na uoendo wote hawezi kuwepo.

Kwa sababu anajipinga yeye mwenyewe (the idea) kuwepo kabla mimi sijampinga.
 
Unaweza kuamini chochote unachotaka kuamini. Lakini kuamini hivyo hakufanyi Imani yako kuwa kweli.

Unaweza kuamini kwamba Mungu ni jambo lililonipita ufahamu.

Lakini, nimekupa nafasi kuthibitisha kama mungu yupo.

Umeshindwa.

Hivyo, unaamini habari isiyothibitishika.

Ukitaka kuamini kitu kipo kwa kusema kimepita uelewa wetu, unaweza kuamini chochote.

Unaweza kuamini mungu yupo, na kapita uelewa wetu.Na hapohapo ukaamini mungu hayupo, na kuelewa hilo kumepita uelewa wetu.

Dhana nzima ya kutafuata ukweli kwa mantiki inavunjika.

Utakubali vipi habari ya kwamba mungu yupo na kapita uelewa wangu wakati hata huwezi kumuelezea na kuthibitisha yupo?

Nikiondoa mungu na kuweka neno lingine lolote, kwa mfano, "nyani mkuu" aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyopo, yupo, na humjui kwa sababu kapita uelewa wako tu, utawezaje kukataa kama umekubali kwamba mungu yupo na kapita uelewa wangu tu?

Inaonekana hujaelewa habari nzima niliyoiandika kuhusu falsafa ya uthibitisho.

Tena nimeandika Kiswahili usije kusema nimeandika lugha ngeni hukuelewa.

Visivyopo havithibitishiki kwamba havipo.Kwa sababu havipo.

Vinavyothibitishika ni vilivyopo, kwa sababu vipo.

Ndiyo maana hata polisi wakija kumkamata mtu kwa kosa la kuwa na madawa ya kulevya nyumbani kwake, hawamwambii "thibitisha kwamba nyumba yako haina madawa ya kulevya". Hata akiichambua nyumba hiyo kwa miaka milioni moja kutaka kuonyesha kwamba nyumba haina madawa ya kulevya, hilo halitathibitisha kwamba nyumba haina madawa ya kulevya.

Njia pekee ya uhakika kuthibitisha ni Polisi kusachi nyumba kwa taratibu na hakika mpaka wapate madawa ya kulevya.Hapo watakuwa wamethibitisha kwamba madawa ya kulevya yamo kwenye nyumba hiyo.

Sasa unachofanya wewe ni sawa na polisi anamwambia mtu "thibitisha nyumba yako haina madawa ya kulevya". Ni kutoelewa falsafa ya uthibitisho.

Unachotakiwa kufanya ni kuonyesha madawa ya kulevya yapo.

Sasa wewe unayesema mungu yupo, unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

Kabla ya kukujibu, unaelewa nini mtu akikwambia "zama za giza"?

Wewe unayekubali mungu wa kutungiwa na wengine na kuletewa kwenye vitabu ulikuwepo wakati huyo mungu alivyofanya hayo anayosemwa kuyafanya kwenye vitabu?

Mkuu nimesoma post zako nyingi unataka tu watu kuthibitisha kuwa Mungu yupo, na tumekueleza kwa yupo. Wakuu mbalimbali ikiwemo na mimi tumekuliza ututhibitishie kuwa MUNGU HAYUPO OBJECTIVELY ili wote tujuwe hayupo. Mfano wako wa madawa ya kulevya ni mzuri sasa TUTHIBITISHIE KAMA MUNGU HAYUPO. Uliulizwa kuhusu "zama za giza" JIBU SWALI HILO! Haina haja ya kurumbana na wakuu hapa! wewe THIBITISHA TU MUNGU HAYUPO! its just simple!
 
Hivi ninachoandika unasoma?

Ulifuatilia mjadala kuhusu "zama za giza" au unarukia tu kwa kuungaunga habari?

Unayekubali kuwepo kwa mungu kwa imani unaweza kuongelea "objectivity"?

Unaelewa kwamba imani na objectivity havichangamani?

Unajua kusoma na kuelewa kwa kituo?

Umeelewa nini kwa habari niliyosema kwamba kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo, na kilichopo tu ndicho kinathibitushika kwamba kipo?

Umeelewa nini nilipotoa mfano wa kusema polisi hawakuambii uthibitishe kwamba nyumba yako haina madawa ya kulevya, bali hutaka uthibitisho kwamba nyumba yako ina madawa ya kulevya?

Umeelewa nini nilipoandika kwamba mungu wenu hawezekaniki kuwepo, kama pembetatu duara isivyowezekanika kuwepo katika Euclidean geometry, kwa maana idea yake inajipinga yenyewe kabla mimi sijampinga kwa kukosa logical consistency?

Umeelewa nini?

Hata una uwezo wa kuelewa?
 
Kiroho safi kabisa....

Kama huyo mungu tayari una tajiriba/ uzoefu naye, iweje tena uamini kwamba yupo?

Mi nilidhani labda hiyo tajiriba/ uzoefu ilikupa ufahamu/ ujuzi kwamba yupo kweli.

Sasa kama yupo kweli [kwa mujibu wa hiyo tajiriba/ uzoefu wako kwake na kwa maisha ya wengine], kwa nini unaamini, na si kujua, kwamba yupo?

Vilivyopo huwa vinaaminika au huwa vinajulikana kuwa vipo?

Au hayo maneno 'kuamini na kujua' huwa yanatumika interchangeably?
Kwani imani ni nini?

Mungu sio physical mpaka useme umemuona au kumgusa. Lakini kupitia imani anajidhihirisha kwetu na tunamjua.

Wewe unaamini au unajua kuwa kuna sayari inayoitwa Jupiter?
 
Mungu unayemuamini wewe ni yupi?

Kitu gani specifically - a vague answer like "experience" is insufficient I am afraid, I want to examine specifics- kinakufanya uamini kwamba yupo na si hadithi tu?
 
Back
Top Bottom