Kifo cha Swetu Fundikira

Jamani hii hatari inasikitisha sana ...

FL1

The whole saga inasikitisha ndiyo, lakini, hili la uana-ndoa sijajua limehusishwa vipi na kesi hii tena?

Sehemu kibao za kujirusha ni nadra saaaaaaaaaana ukakuta wana-ndoa! Ukitaka dataz njoo "Corner Baa" au "Highway" na hata hapa petu "Zero" Pub Tegeta!

Tuachie Mahakama aka sheria ichukue nafasi yake.
 
'jeshi la wananchi'....'jeshi la kuua wananchi'

hivi huwa wanajisahau na kuona wao ni 'miungu watu' na wako juu ya sheria and...aah mara nyingi they just break the law as they wish!!!! huko jeshini huwa wanafanywa nini jamani ambacho kinawapelekea kuwa ivi?? ona sasa wametupotezea nguvu kazi ya taifa...

haya acha marshal law ichukue mkondo wake!!!
 
'jeshi la wananchi'....'jeshi la kuua wananchi'

hivi huwa wanajisahau na kuona wao ni 'miungu watu' na wako juu ya sheria and...aah mara nyingi they just break the law as they wish!!!! huko jeshini huwa wanafanywa nini jamani ambacho kinawapelekea kuwa ivi?? ona sasa wametupotezea nguvu kazi ya taifa...

haya acha marshal law ichukue mkondo wake!!!

mkuu, the whole saga is around mapenzi na pombe, ukinielewa utanielwa.. wale watu walishamaindia mda na si ajabu ahata angekua muuza magazeti na demu wake muuza magazeti wangekua na misuli wangeua vilevile

tupinge mauaji si kwa sababu aliyeua ni mwanajeshi, tupinge mauaji kwa nguvu yote bila kujali aliyeua

nakwambia mauaji ya namna hii yametokea moro na moshi wakati wa krismas bila mtu kusema na ndio maana tunazidi kuumia kwani tunachagua vya kulaani, mwenye vocal ndio anasikika

haya mauaji huko village ndio usiseme... kumbuka mtoto wa kapuya kaua juzi tu sasa hivi tushakauka tunaingilia mauaji haya

INAUMA SANA JINSI TUNAVYOKOSA KULAANI MAUAJI KWA NAMNA YOYOTE HASA YA KI-DHAMBI AND WE PICK ON SCENARIOS
 

Marehemu Swetu akiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) Muhimbili muda mfupi kabla ya kukata roho kama zilizvyonaswa na shushushu wa Uwazi




RAFIKI wa marehemu Swetu Fundikira aitwae Sostenes Mbuya ambaye alikuwa naye muda mchache kabla ya kupigwa na wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ameeleza kilichomponza
Akizungumza na mwandishi wetu jana Mbuya alisema yeye ndiye alikuwa dereva na kilichomponza Fundikira ni kumtetea asipigwe.

“Mimi nilikuwa naendesha na tulipofika Kinondoni kwa Manyanya askari wale walitusimamisha na kuanza kunipiga, Fundikira aliponitetea wakamgeukia yeye na baadaye wakamshusha na kutoweka naye,” alisema Mbuya ambaye alidai aliamua kwenda kuwaarifu rafiki wengine wa marehemu akiwemo Benny Kinyaiya.

Fundikira alifariki dunia juzi Jumapili saa tatu asubuhi baada ya kile kinachodaiwa kupigwa na askari wa JWTZ kutokana na kukwaruzwa kwa gari lao lenye usajili namba T880 AVW na marehemu.


Wanajeshi wanaotuhumiwa kufanya unyama huo ni Koplo Ali Ngumbe na ndugu yake Praiveti Mohamed Ngumbe pamoja na Sajenti Rhoda Robert ambaye awali ilidaiwa kuwa ni mke wa Koplo Ali, hata hivyo taarifa zilizopatikana baadaye zimebaini kuwa si wanandoa.

Habari za kiuchunguzi zilizofanywa na waandishi wetu na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, zinasema Mohamed Ngumbe ‘ameingia mitini’ baada ya kutokea tukio hilo wakati wenzake wanashikiliwa na polisi katika Kituo cha Salender. Askari hao wote wanafanya kazi Kambi ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo, Kinyaiya, aliyezungumza na mwandishi wetu alisema mara baada ya askari hao kuanza kumpiga Fundikira , alipigiwa simu na marehemu.

“Fundikira alinipigia simu akiniarifu kuwa anapigwa. Nilichukua gari langu na kwenda eneo la tukio na kukuta akipigwa na askari hao. Niliwaambia kuwa wasimpige na kama ana kosa wamfikishe polisi lakini mama mmoja ambaye anaitwa Rhoda alikataa, akawa akisisitiza marehemu andelee kupewa mkong’oto akidai kuwa eti mimi hayanihusu,” alisema Kinyaiya.

Aliongeza kuwa aliwaomba askari hao wasiendelee kumpiga marehemu kwa kuwa wakati huo alikuwa akitokwa na damu mdomoni na askari hao wakamwambia kuwa wanampeleka Kituo cha Polisi Oysterbay, lakini alipowafuata huko hakuwakuta.

“Pale Oysterbay, polisi waniliambia kuwa hakuna tukio kama hilo lililoripotiwa hapo, hivyo mimi na wenzangu tukaamua kwenda Kituo cha Salender ambako tuliambiwa rafiki yetu amepelekwa hospitali kwa kuwa hali yake ni mbaya,” alisema Kinyaiya ambaye ni mtangazaji maarufu wa televisheni nchini na kuthibitisha kuwa ameshatoa maelezo yake katika kituo cha polisi Salender.

source; global publishers


Too BAD too SAD!!! RIP!!!
 
Hivi huyu waziri anaeshungulikia usalama wa raia si ajiuzulu tu?Mauaji yamezidi hii inonyesha kuwa maharamia yamekuwa na uhuru zaidi wa kuua Raia wasio na hatia kwa sababu hakuna mtu wa kuyazuia.
 
Really bad! Sad! Rip Swetu!.
Asante Mzee wa Global ila pia sio maadili, ni "Morbid Curiosity"!
 
Too sad kijana wa kwetu.

Hakuna la zaidi ila kusema Mungu akupe mapumzisho mema.

Mizimu ya Mirambo, Isike, Fundikira, Mkasiwa, Mwana Lwelwe na wengineo itakuwepo na kuhakikisha hawa waliofanya huu unyama wanapata haki yao hapahapa duniani.

Hawa wanajeshi wa jeshi lipi? Sidhani ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Davis Mwamunyange, funga hizi kambi zote ziliko karibu na makazi ya watu. Zibaki kuwa na Maofisa wa juu wa jeshi tu maana hawa wanajeshi wa vyeo vya chini ni Nuksi sana. Ngumi mkononi na hawana ADABU. Mara wamepiga watu, mara wamepiga Traffic, mara wameuwa watu .........

Sikonge, uko deep sana...
kuna siku niliuliza hizi kambi vipi??? nikajibiwa jibu sahihi mno... hivi yupi alianza kambi au watu???

Kama ni kambi basi ni sisi kuson=gea mbali... na kama ni sisi basi kambi zivunjwe

KAZI KWETU
 
inabidi sasa wananchi tukiwaona polis au wanajeshi tuwe tunawakimbia
another shallow grave... basi ukiona wanawake kimbi maana waheshaua waume zao; ukiona wamanaume kimbi.. wameshau wanawake zao

kimbia kwa shida zako na mapungufu yako na polisi au wanajeshi... kwani wachuna ngozi wa shinyanga ni wanajeshi?
 
..off duty army officer ni tofauti na aliyeko kazini.

..waandishi wanaotoa habari hizi wawe makini ili wasiwakwaze askari watiifu wakati wakifanya kazi zao.

..kwa mfano kuna askari wako kule Kilombero na Kilosa wanasaidia wananchi walioathirika na mafuriko.

..kuna tabia mbaya sana ya ukatili na kujichukulia sheria mkononi. suala hili nadhani linatokea hata miongoni mwetu raia.

..kuna tabia nyingine mbaya ya wananchi badala ya kusaidia waliopatwa na ajali wanaaza kuwaibia.

..pia kuna tabia isiyo nzuri ya madereva kuendesha wakati wamelewa pombe.

NB:

..inasemekana ugomvi ulianza na marehemu kuendesha gari on a wrong lane.

..kama alifanya hivyo akiwa amekunywa pombe, basi abiria aliokuwa nao wanapaswa kuadhibiwa pia.

..vilevile, mwenye baa aliyemruhusu mteja wake kuendesha gari akiwa amelewa pia anapaswa kuadhibiwa.

..askari aliyemshambulia na kusababisha kifo ana kesi kubwa zaidi, kesi ya mauaji.
 
My thoughts and prayers are with his friends and family at this most difficult time.

Rest In Peace.

My question is:
JK anasema nini kuhusu hii issue. He is the president and I believe he should make a statement regarding this.
 
My question is:
JK anasema nini kuhusu hii issue. He is the president and I believe he should make a statement regarding this.


Jamani sasa tunamdharau rais ... hii ishu inakuwa handled na KOVA na wenzake ....Watuhumiwa wapo ndani,mmoja anatafutwa..............sasa rais hapo ana sababu gani ya kutoa statement ...wakati watendaji wake wapo?
 
Mara nyingi nikiwa kwa Manyanya kununua chips chafu, huwa naona sana Nissan Patrol ya rangi ya orange, hii gari huwa kwanza ina kuja kwa fujo ,kupaki kwa fujo na kuondoka kwa fujo, speed yake ikija utadhani iko kwenye rally, Imesha taka kunigonga mara moja na siku iliyo fuata ili mgonga muuza chips na kuondoka bila kujali na si mara moja,

Niliuliza ni ya nani ,nikatajiwa jina la mtu mwenye famous last name ,ila nime sahau ni nani , sasa nilikua naomba kuuliza huyu marehemu Swetu alikua anaendesha gari gani ?
 
nitasikitika sana kama wauwaji wa swetu wataachiwa....

hii kesi ipo waZi sana ,haina utata...labda jaji awaachie kama watu wa DPP waboronge kwenye kuandika mashtaka..kama walivyokosea kwa kesi ya ditopile.........

ila magazeti ya shigongo hayana maadili....picha ya marehemu waliyotoa ni mbaya sana ..inaingilia privacy yake na kuwaachia majozi zaidi watu...sijui maadili yanasemaje.....lakini rafiki zangu waislamu ...wanasema pia maandiko yanakataza kudhalilisha mtu ambaye ameshakuwa maiti namna walivyofanya kina shigongo....
 
My thoughts and prayers are with his friends and family at this most difficult time.

Rest In Peace.

My question is:
JK anasema nini kuhusu hii issue. He is the president and I believe he should make a statement regarding this.

That will be too much to ask kwa rais wetu... unajua weekend iliyopita tu wameuwawa watu wangapi? Kwani ya ukerewe alisema nini?

Let the president be the president na mapolisi, wapelelezi, wizara husika na sisi raia tufanye kazi yetu --- kulinda amani na utulivu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom