Kifo cha retired major generali James Luhanga

Netanyahu

Senior Member
Oct 2, 2008
147
21
Kama mpiganaji wa porini nipo nikiwaza nchi itapata lini wapiganaji wazuri na ambao ni wazalendo kama mheshimiwa Luhanga aliyefariki jana ambaye alimfanya hadi Marehemu Raisi wa Msumbiji Samora Machel atembelee mkoa wa Iringa na atoe hotuba ndefu ya masaa matano kwenye uwanja uliopewa jina la Samora Kufuatia ziara ile.

Samora alimpenda sana Luhanga na alikuwa mshauri wake binafsi wa kivita lakini alipotaka amchukue moja kwa moja Luhanga alikataa.

Ziara yake ile ya Samora Iringa mojawapo ya agenda kuu zilizokuwa zimemleta alikuwa akitafuta uwezekano wa kumshawishi Luhanga kwa kupitia wazee Fulani wawili ahamie msumbiji.Angeshinda ajenda yake lakini kilichotibua ni kuwa Angola walikuwa na kambi yao kule Kijiji cha Mgagao Iringa na mkuu wa kule naye akatumwa kuwa Angola Akina Augustino Neto walikuwa wakimhitaji akawe mkuu wa kikosi vita cha Anga kule .Nyerere akapata Taarifa akamtuma mkuu moja wa usalama wa Taifa Mzena ambaye alikuwa ni wa Iringa amwambie Luhanga kuwa asikubali ombi la waangola na la Samora.Nyerere alichukia kitendo chao cha wao kwenda kumrubuni mtu moja kwa moja badala ya kuomba kupitia kwake.

Jeshini Tulizoea kumwita “Kamanda Ngumi.mkononi” kwani alikuwa na msemo kuwa silaha bora kuliko zote duniani ni ngumi ya mkononi.Alikuwa akipiga ngumi mtu lazima azimie haijalishi ni askari au ni raia.Alikuwa anajua kupigana ngumi kiwango ambacho sijamwona mtu wa namna hiyo maisha yangu yote.Nilifundishwa naye "one to one combat techniques "kwenye kozi moja.Alitufundisha jinsi ya kutumia pistol na ngumi akituonya tuepuke judo au karate tukiwa karibu na adui. Alitusihi tupende ngumi zaidi kwani ngumi ndiyo silaha ya uhakika ya kummaliza mtu kuliko judo au karate za wachina na wajapani kwenye mapigano ya ana kwa ana.Sikuamini kuwa yeye ni rubani wa ndege za kivita kwa jinsi alivyomudu somo lile.Kila mwanafunzi aliyefundisha naye toka wakati ule alipenda ngumi mno.Siku hizi askari wengi ngumi hawawezi sana wanajua kutumia virungu,mikanda na silaha na kidogo labda kuruka ruka vijudo na vikarate vya kubabaishia kama yule aliyerusha kamguu ka kikarate au kijudo ka kubabaishia Raisi Mwinyi alipolambwa kibao na kijana kwenye mkutano wa waislamu.

Luhanga alikuwa msomi bora wa kivita aliyependa vita kulipo pesa au mshahara au marupurupu.Jeshi lilikuwa kwenye damu si pesa si cheo.Alikuwa mzalendo hasa.Alipigana vita ya UGANDA na Tanzania na ilikuwa nusura ampige ngumi na kuua kiongozi dhaifu wa vita toka Zanzibar ambaye kutokana na ugoi goi wake aliongoza vibaya kikosi wengi wakateketezwa na adui.Baada ya wengi kuteteketea Luhanga alitoa pistol akafuata mnzazibari yule huku akiwa na ngumi mkononi tayari kwa one two one combat na mnzazibari yule aliyesababisha kushindwa kwa kikosi kile kivita mwazo kabisa wa vita ile.Nyerere nafikiri aliamuru arudishwe nyuma ya vita na akaamua ampe vyeo vya kisiasa asije akawabonda na ngumi zake makamanda wavivu wa kijeshi basi akaishia kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali huku akijinywea pombe zake akiendelea kusubiria kufariki kwake hadi alipofariki kifo kilipomkuta hapo hapo kwao Iringa.

Huko unakoenda kaendelee kupigana. Ukikuta shetani Linalotaka kukupeleka motoni kama liko litandike ngumi usisahau one to one combat.

I salute you fellow fighter major general James Luhanga. I salute you again Kamanda Ngumi Mkononi.

Kwa waliobaki hivi hawa makamanda wa majeshi wanajulikana kama kamanda nani zaidi ya majina yao? Nawakumbuka akina kamanda mti mkavu n.k kwa jinsi walivyopewa majina kufuatana na uhodari wao katika mapambano.Walikuwa sit u na majina yao binafsi lakini pia walikuwa na majina yatokanayo na uhodari wa medani za mapambano.

Kamanda Nyerere alijulikana kama Mwalimu kutokana na uhodari wake katika maeneo kibao.

Hivi Kamanda Kikwete jina lake lingine alilopewa kutokana na uhodari wake kikazi ni kamanda nani vile? Silikumbuki anayelikumbuka humu jamii forum anitajie nakumbuka la LUHANGA NA NYERERE naomba msaada mnitajie la Kikwete.
 
R.I.P. Generali Luhanga.

Mashujaa kama hawa historia ya Taifa letu daima itawakumbuka.
 
RIP maj GENERAL james LUhanga.....Taifa linatakiwa kuwaenzi watu kama nyie..na sikufurahi juzi tunasheherekea miaka 30 kumalizika vita na miaka 45 ya jeshi letu , Amiri jeshi mkuu na mkuu wake wa majeshi wameshindwa kuwaita makamanda shupavu waliobaki kama James Luhanga,Ben msuya,musuguri ,kiaro etc etc...ambao kwa kweli mimi hawa makanda nawahusudu walipenda jeshi kuliko biasara!!!
...nchi za wenzetu siku za jeshi kama hizo makamanda kama hawa huvalishwa mavazi yao ya sherehe pamoja na medali zao na kuambata na amiri jeshi na mkuu wa majeshi kupokea magwaride ya heshima pamoja na kuwakumbuka wote...

...kwa kweli itabidi mwakani kama wanaandaa sherehe ..za kijeshi au kitaifa wawavike mavazi yao na kuwaenzi,lingine ni kuwa lazima watambulike na kiongozi wa kitaifa anapotembelea mkoa lazima ajulishwe kwa maafisa wenye cheo cha brigedia general kwenda juu wanaoishi eneo hilo ili angalau wajumuike kwenye dhifa...mnakumbuka hata kuna wakati mkuu wa majeshi mstaafu ERNEST MWITA KIARO alipata kumlalamikia kikwete kitendo cha viongozi wa mikoa wanapoishi kutowatambua makamanda na hata ugeni unapotembelea mikoa hawataarifiwi......ni vema kuwatunza wapiganaji vema ..ili hata waliopo kwenye huduma wasihofia mustakabala wao pale watakapostaafu....

Ni vema kumuenzi kamanda luhanga hata sasa amekufa ...kwa kuwezesha makamanda wenzake hata waliostaafu kupata wasaa wa kupigia saluti za mwisho kaburi lake ....
 
General i salute you!

Mpiganaji wa kweli ni mpiganaji wa kweli tuu! hata huko aendako atendelea kuwa mpiganaji wa kweli tuu!

RIP General Luhang
a...
 
General i salute you!

Mpiganaji wa kweli ni mpiganaji wa kweli tuu! hata huko aendako atendelea kuwa mpiganaji wa kweli tuu!

RIP General Luhang
a...

Rest in Peace General,

One of the very few individuals who dared to fight for their country.

These kind of individuals are endangered species, with their extinct we will have no such qualities. and no one will be able to stand for his country, what a pity.

As for the family Mweyezi Mungu awajaalie roho ya uvumilivu na awajaalie neema kwenye wakati huu mgumu wa majonzi.

Poleni sana.
 
Poleni wafiwa kwa msiba mzito uliowafika.

Jakaya anaitwa kamanda VASCO DA GAMA
 
..Rest in Peace Major General James Luhanga.

..mwisho senior commanders wote wa vita ile watakwisha.

..Brig.Hemedi Kitete, Brig.Yussuf Himidi, Maj.Gen.Muhidin Kimario, Maj.General John Walden, Lt.Gen.Imran Kombe,Gen.Abdalah Twalipo, wote wamefariki.

..inasikitisha kwasababu sidhani kama makamanda wetu wametafutwa ili kuweza kupata mawazo na mitizamo yao kuhusu historia ya vita vya Kagera,Msumbiji, pamoja na jeshi letu kwa ujumla.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom