Kifo cha Rais wa Poland chamshtua sana JK!!

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete amepatwa na mshtuko mkubwa kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Poland kilichotokea Urusi hivi karibuni kutokana na kuanguka kwa ndege aliyokuwa akisafiria.
Source: Majira
My intake
Hivi wana JF mnauchukuliaje huu mshtuko mkubwa alioupata mkuu wetu wa nchi unaweza
ukasaidia kumfanya aogope kupanda ndege, na kwa hiyo
ukapelekea kuokoa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yanatumika kumsafirisha nje ya nchi
mara kwa mara pamoja na msururu wa viongozo wa serekali!
 
hahaha! Tungepewa taarifa ya pesa anayotumia katika hizi safari, nadhani tusingelala!!
 
Hivi huo mshtuko alioupata JK ni kwa sababu President wa poland amefariki
au ni kwa sababu ndege ya Rais mwenziwe imedondoka so anahofu na ya kwake itadondoka?
Mi naona hakuna cha mshtuko wowote ni 'siasa' tu kuonyesha kuwa ameguswa sana na msiba huo.
 
Mkuu Boflo, kuna ka ukweli fulani ndani ya maneno yako. Nafikiri haka ka mchezo ka Rais kusafiri na msululu wa watu wa juu wa serikali, dunia nzima imepata fundisho.

Mara ya mwisho nakumbuka fundisho lilitokea Sweden. Waziri Mkuu Palme, alikuwa akijiona kuwa yeye ni mtu wa watu na ataishi maisha ya kawaida kabisa. Walimdaka akitoka kuangalia film yeye na familia tu, bila hata mlinzi mmoja na wakamuuwa. Dunia nzima iliwalaani Waswidi kwa uzembe huo. Kutoka hapo dunia nzima zikawa zimeanza sheria za "hakuna kiongozi kutembea bila mlinzi". Ila wakazembea na kuwaacha Mawaziri bila ulinzi. Mjinga mwingine akaja akamuuwa yule Mama aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje, tena jua jeupe kwenye super market.
 
Maneno ya kisiasa tu hayo, huenda hata huyo MEMBE AMEAMBIWA atangaze tu chochote atakachoona kinafaa kwa wananchi juu ya tukio hilo...Hapo penyewe labda anaulizia wasaidizi wake kama aende kwenye huo msiba ama la!
 
Nani asiyestushwa na kifo? mwanadamu mwenzio akifariki huumii? Suala hapa siyo JK kashtuka na kwamba ataogopa kupanda ndege bali yeye ni kiongozi kama alivyo wa Poland na yeye pia ni binadamu ambaye jambo kama hilo laweza kumtokea mda wowote? Suala la safari kwa JK na misululu ya viongozi ni jambo jingine kabisa! Hata akihudhuria mazishi ni sawa.....kwani ni nani asiyependa kupewa pole wakati wa msiba?
 
Ni maneno tu hata kwenye kanga yapo. Siasa zaidi tusha zizoea. Amestushwa na nini hasa? Ajali au safari? Huyu hawezi acha kusafiri hata kama ni kwa kupanda boti atakwenda tu. Sijajua wiki ijayo atakuwenda wapi huyu mzee wa misafari!
 

Kikwete alishashtukia vile videge tunavyouziwa na kina Vithlani vitakuja kumtosa, mara nyingi huwa anapanda ndege za kawaida za abiria.



 
Ifike hatua ajali ya Mdau wa poland iwe fundisho kwa Mdau wetu maana safari zikiwa nyingi mwisho ndo ivo na ukizangatia mabadiliko ya hali ya hewa siku hizi hayatabiriki...namuomba sana Mdau apunguze safari mbona wenzie wanatuma mawaziri wao yaani anataka kutuambia Wadau hawatoi msaada hadi aende YEYE!!!??? Chonde chonde jenga nchi ukiwa ndani, mbona wenzio wakina Bashir wanafanya maisha wakiwa ndani?
 
atakuwa amejifunza,
maana na yeye huwa anasafiri na watu kibao
 
Hajastuka kitu huyu sindbad,si kasafiri jana huyu,kwenda kuombaomba majuu wakipata wanatapanya.wanang'ang'ania pesa za rada zirudi serikalini wakati walizifisadi wao wenyewe na hatua hawajawachukulia wahusika
 
Acheni masikhara jamani.............kilichotokea ni kifo............neno "mshtuko" kwa watu wali/naosikia kifo ni kawaida kutumika..........wala si ajabu...........
 
My intakeHivi wana JF mnauchukuliaje huu mshtuko mkubwa alioupata mkuu wetu wa nchi unaweza
ukasaidia kumfanya aogope kupanda ndege, na kwa hiyo
ukapelekea kuokoa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yanatumika kumsafirisha nje ya nchi
mara kwa mara pamoja na msururu wa viongozo wa serekali!

Hapana kidyana wangu.... hiso kama walifyosema wensangu ni mbwewe tu... hata hifyo nimedikuta nacheka mwenyewe....
 
Acheni masikhara jamani.............kilichotokea ni kifo............neno "mshtuko" kwa watu wali/naosikia kifo ni kawaida kutumika..........wala si ajabu...........
Kweli mkulu kuhusiana na neno "Mshtuko" swali linakuja hapo kwenye "sana"
Lazima kuna jambo lililopelekea mh Rais "kushtuliwa sana"
 
.........Rais binadamu kama mimi na wewe, hivyo JK lazima apate mshtuko wa kufiwa na rais mwenzio. Hivyo hakuna cha ajabu hapa kapata mshtuko wa kawaida tu ambao kama binadamu hana budi kuupata.
 
Ukute alipanga kwenda kuomba Poland ndo maana kashituka lol!! safiri mwaya baba weeee usiogope kifo kipo popote pale!
 
.........Rais binadamu kama mimi na wewe, hivyo JK lazima apate mshtuko wa kufiwa na rais mwenzio. Hivyo hakuna cha ajabu hapa kapata mshtuko wa kawaida tu ambao kama binadamu hana budi kuupata.

Boflo said:
Kifo cha Rais wa Poland chamshtua sana JK!!
Boflo said:
Waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete amepatwa na mshtuko mkubwa

Haya bibie nimekupata!
 
Ha haa haaa! Labda alikuwa na kasafari ka Poland, sasa kifo hiki kimemuharibia! The sun has never set in JK tour,yaani ni kigulu na njia! Keep going JK kwa raha zako mpaka Guness book of records wakutambue!! Na bado na bado...!
 
Back
Top Bottom