Kifo cha mwandishi wa Channel Ten: Kauli za Polisi na mwitikio wa Wanahabari

  • mbogamtosi :baby:
MMmeshindwa kutekeleza ahadi mlizo toa kwa wananchi sasa mmeamua kuwaua walikuwako watawala wa dunia lakini waliacha madaraka kama yalivyo.
 
  • :baby:mbogamtosi

MMmeshindwa kutekeleza ahadi mlizo toa kwa wananchi sasa mmeamua kuwaua walikuwako watawala wa dunia lakini waliacha madaraka kama yalivyo.
 
Mkuu ni kweli ipo siri, nadhani polisi hasa wa kada ya chini wana agenda yao dhidi ya wakuu wao na serikali pia, kwa kuua raia waio na hatia, wanataka serikali ichukiwe na jeshi la polisi lichukiwe na wananchi , kitu ambacho wameshafanikiwa sana katika agenda hiyo. Imefika wakati sasa viongozi wa pilisi na serikali kukaa kuangali hayo badala ya kuendelea kutupa sababu zisizo na mshiko. Fuatilia matukio ya polisi kujiua, kuwaua wenzao na haya yote utaona kuna kitu, kuna agenda ya kufanyia kazi. Nabaki na imani na JWTZ lakini si Polisi katika kulinda wananchi.Inanikumbusha pia enzi za Soweto, askari wa makaburu ndio waliokuwa wakisababisha fujo na mauaji na si wananchi, hii ndiyo inatokea sasa hapa kwetu. Tusiishie kusema MUNGU IBARIKI TANZANIA, tujiulize aibariki katika lipi.

Polisi hawachomoki kwenye hii kashfa nyingine ya mauaji. Ukatili na uhuni wa JK na serikali yake ya ccm hauvumiliki tena. Wasijelaumu mbele ya safari
 
Mkuu Crashwise umeelewa swali langu? Tokana na maelezo ya Tumaini Makene kuwa marehebu alipigwa sana kabla ya kuuwawa; ningependa kujua kuwa alipokuwa anapigwa sana walimchukua kando au mbele ya macho ya wananchi? Hio picha moja wapo inaoneshwa akizungukwa na polisi sio chini ya sita, iwezekana ndio walimkamata, hivo sitaki nifanye kwa assumptions bali kwa kuhakiki kupitia walioshuhudia...
Nimekusoma lakini mkuu Neiwa ukiangalia hata azingila alipo zungukwa na polisi huku akipigwa na baaade mwili wake ukiwa umesambalatishwa unaonyesha ni maeneo hayo hayo.... bado nakubaliana na wewe kuwa ungependa kupata uthibitisho kutoka wa walio shuhudia...
 
Last edited by a moderator:
This has continue to gloom my day. I just can't get going and we're approaching halfday. CCM is a longterm problem so we need permanent solutions, not the temporary ones. That was a problem to previous strategists, no longer to us.

Heads must roll. Now it is a time whereby strong words must be replaced with strong actions. Hopeless silence must be replaced with proactive civility.

Kwa wingi na umoja wetu wananchi wa Tanzania sasa tunajua tunachotaka. Tunataka uwajibikaji na haki, HATUTAKI TUME wala "taarifa rasmi".
 
Muongoza kipindi ndachi amekuwa na hasira sana lakini kwa kusema ukweli kama kulikuwa na kufungua tawi tu kijijini kulikuwa na haja gani ya kutumia mabomu lakini kasema paul chagonja anasema hajui bomu lilitoka wapi lakini mbona picha kwenye gazeti la mwananchi inaonyesha askali akimwelekezea mtutu wa bunduki mwandishi tumboni??????
 
Police wengi wanavuta bangi, unategemea nini kuhusu usalama wa raia? Jeshi la police limejaa wavuta bangi!

Ni polisi wachache sana wanaofanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi yao, wengi utawaona walivyo na hasira na raia hata kama mtu hana kosa/hatia yeyote.

Pamoja na hayo, kulikuwa na fujo gani hadi kuamua kutumia nguvu kiasi hicho? Tufike mahali tuanze kuhoji matumizi ya siraha kama mabomu ni nani anagharamia? Tufahamu nani ni nani, amefikaje hapo alipo?

Wenzangu niliisha tahadharisha huko nyuma kuwa Tawala inapokosa uhalali wa kutawala , huwa inageukia watu wake na kuwaua . Hii si Tanzania tu angalia yaliyotokea Libya sasa Syria angalia madikteta wote duniani ,wote wanakitu kimoja wanafanana waliposhindwa kutawala wakaanza kutumia mabavu kuua watu wake. CCM na serikali yake wataendelea kuua tu. Hata hao mapolisi ni watu waliokata tamaa. wataua tu . Makamanda wao ni majambazi hiyo haina ubishi . Ukiangalia hiyo picha wanayomsurubu huyo mwanadishi unashindwa kupata picha kwa nini wanakuwa na hasira kiasi hicho. Mtu wa kawaida mwenye akili timamu anawezaje kumsurubu raia ambaye hana siraha na kumuua kama mnyama. Huyu mtu walikuwa wanamjua. Iringa ni mji mdogo sana haiingii akilini kuwa mapolisi hawamjui huyu mtu! walitaka kumuua tu !!!!!!!
 
Mimi nimeshachoka kulalamika! nimeshaandika mengi humu inatosha! ningeshauri badala ya kauli za kulaani Polisi tujadili tuchukue hatua gani! naomba mijadala hapa JF iwe ni jinsi ya kuchukua hatua na si kulalamika.
 
Kwa mauaji haya ya polisi na kusingizia kuwa wana cdm ndiyo waliofanya hivyo ni sababu tosha ya kumfikisha kikwete the hague. Kwani hao plisi wanafanya hivyo kwa maelekezo ya wakuu wao ambao waliteuliwa na kikwete.Chonde chonde polisi acheni kuua watu ili muwafurahishe mabosi wenu ambao wana kaa na kuchekelea kuona au kusikia vifo vya watu wasio na hatia vikiendelea.Kwa sababu kinachowatokea raia hao kitawatokea polisi hao,ndugu zao au uzao wao.Mungu Ibariki Tanzania,Mungu iondoe CCM
 
Maundumula tume ipi ambayo imeshawahi kuundwa hata tanzania na ikaja na jibu la uhakika
Unategemea nini mwenye tume akiwa ashatoka na majibu yake ambayo anayasema hadharani
Chagonja alisema waliofanya fujo songea ni wahuni na tume iliundwa ambayo mpaka leo hata majibu hakuna.
Huwa naona ni ulaji mwingine tuu unafanyika kwa hao wanaoteuliwa kwenye hizo tume
m

Labda tume ya akina Zombe!
 
Afisa wa polisi haruhusiwi kupiga raia maana huwa wanakula kiapo cha kulinda na kutetea haki za raia...
Hata katika katiba ya nchi, inaeleza wazi kuwa moja ya haki ya raia ni "kuishi"...
Uwepo wa mwandishi wa habari katika mkutano au maandamano ni sawasawa na uwepo wa Polisi katika eneo husika, wote wapo kazini...
Natamani sana kama kungekuwa na watu wanao document haya matukio ili yaje kuwahukumu serikali iliyopo madarakani mwaka 2015...
Haya matukio laiti kama yangekuwa yakikemewa na Rais, yasingekuwa ya kujirudia rudia...
Leo hii Polisi wanajitetea kwa kuwabambikizia Chadema mzigo wa mauaji,
vipi jinsi wanavyoshughulikia maandamano ya wanafunzi?
vipi walivyowapiga waumini wa kanisa moja Mwenge Dar es Salaam na kupelekea mtu mmoja kuuawa ingawa vyombo vya habari havikuhabarisha umma?
Vipi mauaji ya kule Songea ambayo chanzo kilikuwa ni hili Jeshi la Polisi?
Hivi Jeshi la Polisi linajiamini nini? Na sisi wananchi tukiamua kujifunga vibwebwe na kupambana nao wanadhani hii nchi itakalika?
Rais Kikwete ni muhalifu namba moja kwa kila tukio la kijeshi linalotokea, maana haya matukio yamekuwa yakijirudia na hatuoni kama yanakemewa.
Wewe Polisi uliyemuua mwandishi wa habari siku zako za kuishi duniani zinahesabika, maana uhai wako pia u mikononi mwa Mungu, damu hiyo itakusakama na wala hutafurahia siku zako za kuishi hapa ulimwenguni.
 
Hakika Mauaji haya Mungu ameamua kuwa onesha Umma mauaji yafanywayo na Polisi. Hakika Polisi wamezidi kuua na kusakizia kesi za ajabu watu ni hakika haki za watu hazipotei bure na Damu ya Ally Morogoro ukichanganya na hii Ya Mwandosi hakika hatumuuwachii Mungu kama wengine wanavyosema ni kusimama imara na kupambana na wadhurumaji wote wa haki za watu unaoendelea leo. Kila sehemu hakuna haki nenda Mahakamani, Polisi, Ardhi, hospitalini. Ni Muda wa kamua maisha gani tunapaswa kuishi sasa hili la kuweka rehani maisha yetu kwa wauwaji hawa kamwe si wa kuuwachia. Tuungane pamoja wote kupambana
 
Huu ni muendelezo wa mauaji dhidi ya raia wasio na hatia toka kwa Jeshi la Polisi.. Haya yalianza kidogo kidogo mpaka sasa yameshika hatamu.. Polisi wanaua bila ya kuogopa na wanakuja na vicingizio vya uongo mweupe kabisa..! CCM kwa manufaa yao wameliachia Jeshi la Polisi kupanga njama za kuwaua raia ambao wao CCM wanaona ni tishio kwao.. Leo wananchi wamepoteza imani na Jeshi la Polisi.. Cifa kubwa ya Polisi sasa ni kuchukua rushwa.. kuwabambikia wananchi kesi za uongo na kuwaua wananchi kwa sababu nyingi tofauti.. Inacikitisha sana sana...
 
Mimi nimeshachoka kulalamika! nimeshaandika mengi humu inatosha! ningeshauri badala ya kauli za kulaani Polisi tujadili tuchukue hatua gani! naomba mijadala hapa JF iwe ni jinsi ya kuchukua hatua na si kulalamika.
MTAZAMO Mkuu, ninaelewa uchungu wako na uchungu wa WaTZ wengine ambao kwa njia moja au nyengine ni wahanga wa serikali katika sekta zote: vifo vya ajali za barabarani, vifo vya ajali za meli, vifo vya kuuliwa na vibaka, vifo vya magonjwa yatibikayo, kifo kibaya cha kuwanyima watoto elimu...na hivi vifo vya polisi ambao wanaua live!

Hatua za kuchukua ni mbili tu, ama ndani ya masanduku ya kura au kupambana ana kwa ana. La mwanzo huwa haliwezekani kwa sababu ya uchakachuaji wa matokeo na hili la pili nisingeshauri hasa kwa kuutumia mtandao wa JF kama "nyumba ya kupangana upambanaji huo."

Nisingependa kuona JF inakuwa chanzo cha kuandaa na kuchochea uasi. Kumbuka dhima ya vyombo vya habari katika mauaji ya kimbari Rwanda na katika vurugu za baada ya uchaguzi wa Kenya. JF as Home of Great Thinkers must think greatly every move in and out of this.
 
Last edited by a moderator:
Nimekusoma lakini mkuu Neiwa ukiangalia hata azingila alipo zungukwa na polisi huku akipigwa na baaade mwili wake ukiwa umesambalatishwa unaonyesha ni maeneo hayo hayo.... bado nakubaliana na wewe kuwa ungependa kupata uthibitisho kutoka wa walio shuhudia...


Ile ni still picture mkuu, picha inaweza ikawa distorting, katika hili NATAMBUA kuwa kosa kubwa lipo kwa jeshi la polisi. Ila bado hainipi haki ya kuhitimisha kuwa ile picha ilikuwa ya kipigo. Maadamu usha ni hakikishia hilo nabaki naumia kuwa alipigwa mbele ya macho ya hadhara hadi akauwawa na bado wananchi wakawa wanatazama kwa mbali na kupiga picha? Hivi umenipata where it is coming from? Hilo la kusema kauwawa kikatili vile na bado umma haukufanya kitu... Hata hivo najua ni rahisi kuongea kama mtu hukuwepo katika tukio... Shakrani kwa udadavuzi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom