Kifo cha mwandishi wa Channel Ten: Kauli za Polisi na mwitikio wa Wanahabari

Police wengi wanavuta bangi, unategemea nini kuhusu usalama wa raia? Jeshi la police limejaa wavuta bangi!

Ni polisi wachache sana wanaofanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi yao, wengi utawaona walivyo na hasira na raia hata kama mtu hana kosa/hatia yeyote.

Pamoja na hayo, kulikuwa na fujo gani hadi kuamua kutumia nguvu kiasi hicho? Tufike mahali tuanze kuhoji matumizi ya siraha kama mabomu ni nani anagharamia? Tufahamu nani ni nani, amefikaje hapo alipo?
Nimeipenda hii. Na ningependa sasa wananchi waelewe hawana polisi wa usalama. wanapolisi majambazi wauaji. Ninakumbuka CUF miaka ya nyuma walilielewa hili na wakaanza kuwafundisha vijana mafunzo ya judo na kareti kukabiliana na haya majambazi yanayojiita polisi. Sasa ninaelewa ile mantiki ya kujifunza kujilinda wenyewe na kulinda wananchi dhidi ya haya majambazi wanaojiita polisi. MABWEPANDE wao kuanzia akina zombe hadi huyu wa Salenda bridge aliyemulimboka steven. Je tunahitaji nini tena kuthibitishiwa hakuna polisi??? Tujiandae kujihami wenyewe tuko peke yetu na polisi wa CC MABWEPANDE!!
 
Mzee Mwanakijiji sijui hawa wachumia tumbo wanaoteuliwa kwenye hizo tume wana kazi gani
Tume tume tume kila kitu wakati hakuna hata moja iliyotoa report yake au maamuzi yake yakatekelezwa au kufanyiwa kazi
Zote zinaishia kwenye makabati au kuwasafisha wahusika
Ni ulaji tuu wa pesa
Angalia hata ile ya mauaji ya songea ambayo kiongozi wa tume alikwishatoa hukumu hata kabla ya kufanya uchunguzi wake

Well said, point blank. Salaam mkuu...
 
Mungu yupo na hakika wauaji wanafahamika tunmeona picha zao wanajidai eti bomu bomu gani liue m tu mmoja tu na wakati watu walikumbatiana
 
Mi simo katika maneno ya police Mungu nisamehe kama nimeyasikia kwa bahati mbaya kwani halikuw kusudio langu kusikiliza uongo ule

Mkuu umeona huo usanii sio,yani wamesahau kuwa wanaongea na watu wazima tena wenye akili timamu.
 
hawa polic wamefika pabaya watakufa tu kwan wananch wataanza vita ya mmoja baada ya mmoja!
 
Lawama za kuuwawa kwa mwandishi huyo wa habari zisitupwe kwa CHADEMA kabisaaaaaa ila ni asikari polisi wasio kuwa na uvumilivu na kutumia bunduki na risasi kama karanga..hawajui matumizi ya silaha ni wakati gani na sababu zipi! Jeshi la polisi ni hoivyooo sn.
 
Naombeni mnipe mfano mmoja tu ambapo mwananchi/wananchi wamefanyiwa unyama na hii serikali halafu maneno yakasaidia!! Mfano mmoja tu ambapo reasoning ili fanya kazi Tanzania!! Mimi sikumbuki kwa kweli, Hivyo wananchi wakiwa tayari kukamata mitutu ndio mnishtue.


Great Thinking..
Naunga mkono Hoja..
 
Mi nadhani wamefanya hivi kwa makusudi kabisa ili kuwaogopesha wanahabari wasihudhurie mikutano ya chadema, we hujui akili ya POLISI? nampenda sana mwana philosophia aitwae plato, watu kama polisi, na wanajeshi hawafai katika utoaji wa maamuzi, lakini hapa nchini eti ndo chombo kinacho aminika! HII NI LAANA!
 
Kifo cha mwanahabari mahiri wa chanel ten, kimekuja wakati mbaya sana na kimesikitisha kila mpenda haki. Hivi tunavyoongea kama ilivyokawaida ya polisi wa Tanzania, wanajipanga kuleta uongo wao kuwa mwanahabari labda alichomwa na kitu chanye ncha kali, oh alianguka... alipigwa kitu chenye uzito nk. Halafu wanahabari wataibeba habari hiyo na kuutangazia umma wakati waandishi walikuwepo na kuona kilichotokea.

Jana mwandishi wa Star TV katika taarifa ya habari alisema CDM ilikuwa inafungau tawi, waandishi walikuwa kama mita 100 kutoka eneo la tukio wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea. Viongozi walikuwa wanaingia ofisini kusaini kitabu cha wageni ili kufungua tawi, Ghafla wakashangaa kuona mwenzao amepigwa bomu na utumbo kusambalatika. na hapo hapo akafariki.

Hapo utasikia story za polisi....


Tuwagomee kutoa habari zao kama wiki moja, wataomba radhi baada ya muda huo....

nawasilisha
:redface:
 
Polisi wa ccm wanajanja yao ya kuthofisha nguvu ya umma hasa ktk M4C, kamwe hawata weza hasa wanatupandisha hasira ili siku moja nasi tuwarudi..
 
“Sisi hatuna bunduki, hatuna mabomu
wala majeshi, lakini Serikali ya CCM na
polisi wanapaswa kutambua haya
tunayoyafanya ni sawa na gharika.
Kuyazuia ni vigumu, hata kama
watatuua viongozi wote, watambue mioyo ya Watanzania itaendelea kulilia
mabadiliko haya,”
 
kwa picha tu za kutoka katika tukio inaonyesha hayakuwa maandamano bali ufunguzi wa Tawi la chadema. wao waseme tu walidhamiria kumuua mpendwa wetu Daud Mwangosi.tuona wenye Picha waliochukua kwa simu zao za mkononi waziweke hapa Jf kama ushahidi zaidi.RIP DAUDI MWANGOSI
 
WanaJF, kuna polisi mmoja Iringa amesema upinzani mkubwa wa polisi Iringa dhidi ya M4C yana mkono wa Lukuvi (Mnadhimu mkuu wa serikali bungeni). Je kuna uwezekano amri ya kumuua mwandishi wa chanel ten ni ya kupangwa kutokana na umahiri wake mwangosi katika kuripoti habari za kisiasa?
 
Tumaini Makene amekiri kuwepo katika eneo la tukio. Kazungumzia kwa kirefu sana jinsi hali ilivokuwa hapo jana wakati wa vurugu. Na pia imezungumziwa kuwa marehemu kabla ya kusambazwa kwa mwili wake kwa silaha iliomfumua utumbo wote kuwa nje alipigwa sana.

Kuna mahala hadi kataja Maremu David aliomba msaada kwa jeshi la polisi huku akilalama kuwa anauwawa. Hii imenifanya nijiulize na kutaka kujua, hicho kipigo alichopata marehemu ilikuwa imesababishwa na Polisi mbele ya macho ya wanachi ama alichukuliwa kando?
Ina maana hujaona picha mkuu swali gani unauliza au sijakuelewa..marehemu alipigwa vibaya sana kabla hajapigwa bomu...
 
Ina maana hujaona picha mkuu swali gani unauliza au sijakuelewa..marehemu alipigwa vibaya sana kabla hajapigwa bomu...


Mkuu Crashwise umeelewa swali langu? Tokana na maelezo ya Tumaini Makene kuwa marehebu alipigwa sana kabla ya kuuwawa; ningependa kujua kuwa alipokuwa anapigwa sana walimchukua kando au mbele ya macho ya wananchi? Hio picha moja wapo inaoneshwa akizungukwa na polisi sio chini ya sita, iwezekana ndio walimkamata, hivo sitaki nifanye kwa assumptions bali kwa kuhakiki kupitia walioshuhudia...
 
  • :baby:


MMmeshindwa kutekeleza ahadi mlizo toa kwa wananchi sasa mmeamua kuwaua walikuwako watawala wa dunia lakini waliacha madaraka kama yalivyo.
 
Back
Top Bottom