Kifo cha mwandishi wa Channel Ten: Kauli za Polisi na mwitikio wa Wanahabari

Katiba iliyopo kwasasa inampa mamlaka makubwa sana Rais kuhusiana na uteuzi ninaamini nafasi kama hiyo isingekuwa na mamikono ya wanasiasa tusingekuwa tunashuhudia mauaji na vitendo vya kikatiri namna hii, Polisi wengi wanaumizwa na maagizo yanayotolewa na viongozi wao ambao kimsingi wanateuliwa na mwenyekiti wa CCM taifa. Kwa mfano kuna Polisi inasemekana kwenye ile Operation ya Morogoro aligomea kwenda kufanya ukatili kama alivyoagizwa mpaka huu mda inasemekana amewekwa pembeni akisubiri uhamisho wake.
 
Wakuu, ni wazi kuwa sasa ukombozi wa pili unakaribia!

Ukombozi wa kiuchumi, ambao utamuwezesha mtanzania kufaidika na rasilimali alizopewa na Mola. Magamba wamepaniki, wanatafuta kila njia kujiokoa, hata kwa kutumia njia haramu na kuua.

Kamanda aliyepoteza maisha yake, RIP. Msiba wake uwe chachu ya ukombozi na kuzidi kuunganisha nguvu.

Kwa hatua hii, hakuna tena kurudi nyuma, ni kumzika kamanda, na kuendelea na M4C.

Wakuu, tuelewe na kuzingatia kuwa ukombozi uko mikononi mwetu wenyewe. Mataifa ya nje, yanaona, lakini hakuna muda wa kupoteza kuzidi kubisha hodi kwao na kuomba omba. Wengi wanapenda kuendelea kufanya kazi na wajinga wasiojua umuhuhimu wa hazina kubwa tuliyonayo na rasilimali nyingi, waendelee kuwasainisha mikataba ya kijinga ya muda mrefu kwa kuwapatia senti kidogo na kuwafichia Uswisi.

Hawa, hawawezi kwa sasa kujitokeza kwa uwazi na kuunga mkono harakati hizi, juhudi binafsi, hizo zinawezekana. Watasubiri. Wakiona kweli sasa Watanzania wako serious, watasimama, kupaza sauti zao na kuingilia kati.

Kinachotakiwa, ni kuendeleza kutoa ujumbe wa ukombozi kupitia M4C.

Viongozi toeni matamko mapema ya kuongoza umma from time to time, na kuwaandaa wanachi wanachotakiwa kufanya wanapotendewa kinyume na haki za binadamu. Camarade Marando, nadhani unanielewa.

Utengenezwe mkakati pia wa kuwa na vyombo vyenu huru vya habari, wazo hili limetolewa muda mrefu, watu wana nia njema ya kuchangia.

Aluta Continua!
 
masikini ameambiwa kupambana na kuwazuia cdm lakini aliyeuawa ni mwandishi wa Channel Ten na na wala sio 'mwajiliwa' wa adui wao cdm.
Basi hata kama ni maelekezo kutoka juu basi watumie akili katika kuua maana hata Morogoro, Arusha waliouawa sio 'adui' yao bali ni wananchi wapenda amani!
RIP ndugu yetu Mtz
 
wanasikia kwani? lakini hata wakifa, lazima siku moja makaburi yao watachalazwa viboko tu
 
Kwahiyo anafikiri akistaafu ndio mwisho?Lisu alisema
Wawe wamevaa magwanda au wamevua hawataachwa.Anaelewa
Maana ya huo ujumbe?
 
Naombeni mnipe mfano mmoja tu ambapo mwananchi/wananchi wamefanyiwa unyama na hii serikali halafu maneno yakasaidia!! Mfano mmoja tu ambapo reasoning ili fanya kazi Tanzania!! Mimi sikumbuki kwa kweli, Hivyo wananchi wakiwa tayari kukamata mitutu ndio mnishtue.
 
Wakati umefika kwa jeshi la polisi kutafakari upya mbinu yao ya kuzuia kuenea kwa matawi ya vyama vya upinzani hapa nchini na hasa chama cha CHADEMA. Haiingii akilini kuwa matukio haya ya polisi kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kuzuia harakati za kisiasa za CHADEMA kujitanua na kusambaa kwa kufungua matawi na kuelimisha sera zake ni AKILI ZA KIPOLISI.

Katika mazingira ya kawaida inaonyesha kuwa jeshi letu la polisi ama linatumwa na serikali chini ya maelekezo ya CCM au baadhi ya viongozi wa polisi ni wanachama wa CCM na wanataka kujijengea ujiko ili watunukiwe vyeo ndani ya CCM au serikalini.

MAONI YANGU:

Wakati umefika kwa polisi kutambua mali ni kodi ya wananchi wote bila kujali itikadi ya siasa na rasilimali zote za nchi ni zetu wote kwa manufaa yetu wote. Wajibu wa polisi ni kulinda wananchi wote na mali zao kwa haki na usawa wakiwa wamelala, wanatembea, wanacheza, wanaandamana, wanaelimishana kwa njia ya mikutano, mihadhara au kwa burudani.

Polisi wangejijengea heshima kama wangehakikisha wanatoa ulinzi uliotukuka kwa CHADEMA katika harakati zake za kisiasa za kujitanua, kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha wananchi kujua haki zao, wajibu wao na kulinda rasilimali za nchi yao.

Penye red unauliza majubu, Unakumbuka Tibaigana akiwa madarakani alisema yeye si mwanachama wa Chama chochote na hashabikii chama chochote? lakini alipostaafu akataka kugombea Ubunge kwa ticket ya CCM kama mwanachama Mkongwe
 
Siku yaja atamtaja aliyempa hayo maelekezo, kama ni wasira, nape mukama, lukuvi, mkuchika, mwigulu au pinda!!!! Tutajua na tutawapunguza kuwa udongo.
 
Akihojiwa na kituo fulani cha redio kwa njia ya sim leo hasubuhi, kamanda kamuhanda amesema kuwa mwandishi huyo ameuwawa na mlipuko uliotokea kusiko julikana, na amevilaumu vyombo vya habari kuripoti habari zisizo za kweli tofautitofauti, amesema ripoti kamili ataitoa leo baadae.
nawasilisha.
 
Nimesoma habari hii kwenye gazeti la Tanzania Daima na imenishtua sana, kwamba watawala wameamua kufanya lolote lile ilimradi wawazuie Chadema, soma baadhi ya paragraph hapa chini;


"Alipofuatwa na kuombwa awazuie askari wake kumshambulia mwandishi huyo, kamanda huyo alifunga vioo vya gari lake, akapiga honi mara kadhaa, na akaondoka. Baada ya RPC kuondoka eneo hilo, ndipo bomu lilirushwa na kumfumua mwandishi utumbo."


Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Michael Kamuhanda, alisema awali kwamba anaipenda kazi yake, hivyo hawezi kuruhusu mikutano katika mkoa wake mpaka atakapopata maelezo ya ziada.

Alisema: "Ni kweli jana saa mbili tuliwapa barua ya kuruhusu shughuli zao ila hili ni agizo na mimi ninakaribia kustaafu na kazi yangu ninaipenda, hivyo siwezi kuruhusu maandamano kinyume na maagizo yaliyopo."

Alisema CHADEMA hawawezi kufanya mikutano kwa kuwa hawana jeshi wala vifaa vya kupambana na Jeshi la Polisi, hivyo wakijaribu kutotii sheria ni lazima washurutishwe.

Source; Tanzania Daima; Polisi waua tena kikatili
Mkuu ni kweli ipo siri, nadhani polisi hasa wa kada ya chini wana agenda yao dhidi ya wakuu wao na serikali pia, kwa kuua raia waio na hatia, wanataka serikali ichukiwe na jeshi la polisi lichukiwe na wananchi , kitu ambacho wameshafanikiwa sana katika agenda hiyo. Imefika wakati sasa viongozi wa pilisi na serikali kukaa kuangali hayo badala ya kuendelea kutupa sababu zisizo na mshiko. Fuatilia matukio ya polisi kujiua, kuwaua wenzao na haya yote utaona kuna kitu, kuna agenda ya kufanyia kazi. Nabaki na imani na JWTZ lakini si Polisi katika kulinda wananchi.Inanikumbusha pia enzi za Soweto, askari wa makaburu ndio waliokuwa wakisababisha fujo na mauaji na si wananchi, hii ndiyo inatokea sasa hapa kwetu. Tusiishie kusema MUNGU IBARIKI TANZANIA, tujiulize aibariki katika lipi.
 
Maundumula tume ipi ambayo imeshawahi kuundwa hata tanzania na ikaja na jibu la uhakika
Unategemea nini mwenye tume akiwa ashatoka na majibu yake ambayo anayasema hadharani
Chagonja alisema waliofanya fujo songea ni wahuni na tume iliundwa ambayo mpaka leo hata majibu hakuna.
Huwa naona ni ulaji mwingine tuu unafanyika kwa hao wanaoteuliwa kwenye hizo tume
m

tume zote zilizoundwa before hazijawahi kuja na mapendekezo ya namna nyingine ya kukabiliana na raia wasio kuwa na silaha ili kuzuia maafa kama yaliyotokea,nini mchango wa izo tume sasa?manake kila siku naona tunarudia makosa yale yale na sababu zile zile kwa malengo ya kujustify kwamba always raia ndio wanakuwa wakaidi ktk kutii sheria.
 
Last edited by a moderator:
Mi simo katika maneno ya police Mungu nisamehe kama nimeyasikia kwa bahati mbaya kwani halikuw kusudio langu kusikiliza uongo ule
 
Penye red unauliza majubu, Unakumbuka Tibaigana akiwa madarakani alisema yeye si mwanachama wa Chama chochote na hashabikii chama chochote? lakini alipostaafu akataka kugombea Ubunge kwa ticket ya CCM kama mwanachama Mkongwe

mahita nae,,,ingawa hakufanikiwa malengo,lets wait kwa KOVA
 
Kwahiyo anafikiri akistaafu ndio mwisho?Lisu alisema
Wawe wamevaa magwanda au wamevua hawataachwa.Anaelewa
Maana ya huo ujumbe?

mkuu naona siasa zimezuia uwezo wao wa kufikiri,lazima wajue na watambue kuwa one day they will be held accountable for what they have done today.
 
Akihojiwa na kituo fulani cha redio kwa njia ya sim leo hasubuhi, kamanda kamuhanda amesema kuwa mwandishi huyo ameuwawa na mlipuko uliotokea kusiko julikana, na amevilaumu vyombo vya habari kuripoti habari zisizo za kweli tofautitofauti, amesema ripoti kamili ataitoa leo baadae.
nawasilisha.

ripoti tena inatoka kwake????
 
Back
Top Bottom