Kifo cha mwandishi wa Channel Ten: Kauli za Polisi na mwitikio wa Wanahabari

Anasema mwangosi alitoka kusiko julikana na kumkumbatia ocd ndipo hicho kitu kizito kikamwangukia ma kumlipua.

Source: chagonja mwenyewe habari chanel10
 
Hawa jamaa wana vituko, wanatuona sisi ni wajinga. Wamekaa usiku kucha kutengeneza stori... let me try to guess..

Mwandishi huyo alivalishwa kitu kinachosadikika kuwa ni bomu na wafuasi wa CHADEMA. Katika kujiokoa akakimbilia kwa maaskari. Alipofika akamkumbatia OCD na mara hilo bomu likaripuka....

It dosent make sense, inawezekana vipi mtu yuko katikati ya watu 5 na amemkumbatia askari mmoja then yeye akavurugika kiasi kile na kufa peke yake??? Ni bomu la aina gani hilo?? Radial effect yake ni kiasi gani mpaka limuuwe mtu mmoja tu wakati walikuwa in close contact na askari??? It doesnt make sense, not to me.
 
Mzee Mwanakijiji sijui hawa wachumia tumbo wanaoteuliwa kwenye hizo tume wana kazi gani
Tume tume tume kila kitu wakati hakuna hata moja iliyotoa report yake au maamuzi yake yakatekelezwa au kufanyiwa kazi
Zote zinaishia kwenye makabati au kuwasafisha wahusika
Ni ulaji tuu wa pesa
Angalia hata ile ya mauaji ya songea ambayo kiongozi wa tume alikwishatoa hukumu hata kabla ya kufanya uchunguzi wake
 
Last edited by a moderator:
Anasema mwangosi alitoka kusiko julikana na kumkumbatia ocd ndipo hicho kitu kizito kikamwangukia ma kumlipua.

Source: chagonja mwenyewe habari chanel10

Hv kumbe changonja nae ni mwepesi namna hii! Ina maana hajui kama watu wanapicha za kitu halisi kilichotokea kwenye field?
They say a picture tells 1,000
words but when I see these all
I see is 3 words: 'THEY KILLED HIM'. Rip DM
 
Kwa hiyo anataka kutuaminisha kuwa hao wafuasi wa CDM walikuwa wamebeba mabomu
Anataka kutuambia kuwa walishapanga kumuua huyo mwandishi ndo maana wakamvalisha bomu
Duh hii story mbona ngumu kumeza
Na licha ya kwenda kumkumbatia OCD bomu likamlipukia mwenyewe na kuumuua yeye mwenyewe ila aliyekumbatiwa hata jeraha hakupata
Na kwa nini anajitetea yeye tuu upande mmoja kwani hakukuwa na wafuasi wa CDM kutoa na yao kwa upande wao
Kwa nini wanatoa conclussion wao kabla ya kusikia na upande wa pili
Na kama hakukuwa na fujo yoyote ya nini walivamia wakiwa wamejihimili kabisa na mabomu na silaha na nguo za kuzuia risasi
 
Tume ni muhimu maana kila mtu anasema lake. Na picha inaweza kuku deceive wakati mwengine ingawa huongea maneno 1000
 
Hivi ni wapi Polisi wanakopata Uhalali wa kumuua mtu kwenye Uzinduzi wa Tawi la chama cha siasa? Fiesta na uzinduzi huo ni mkusanyiko upi wenye watu wengi?.. Serikali ijiangalie. Inachopika hakifai kuliwa
 
Inabidi nitafute dili la tume na mie sasa. Hivi nahitaji kwalifikesheni gani?

King'asti inabidi uwe kwenye system upate deal aise sio bure bure na ujue kuandika uwongo na kutoa report ya uongo hata kama umeambiwa ukweli wote
 
Last edited by a moderator:
Uue mwenyewe, uunde tume ya kujichunguza wewe mwenyewe, na taarifa ya kifo uiandae mwenyewe. *^@#} yenu!
Halafu kamishna wa polisi anasema CDM walifanya mkutano kinyume cha sheria. Sheria ipi hiyo inayokataza chama cha siasa kufanya mkutano? Hakuna sheria inayowapa mamlaka polisi ya kutoa kibali kwa chama cha siasa ili kifanye mkutano wake kokote kwenye Jamhuri hii. Hapa polisi wamechemka, wasitafute huruma ya wananchi.
 
Sasa ndio Muda wa kila mpenda amani Kushikamana!! Polisi wanajichukulia sheria mikononi Kuua? Watu wasiokuwa na silaha!! Hata wana Habari??
 
Hv kumbe changonja nae ni mwepesi namna hii! Ina maana hajui kama watu wanapicha za kitu halisi kilichotokea kwenye field?

Chagonja ni tatizo kubwa ndani ya jeshi la Polisi Tanzania. Huyu ndiye mkuu wa mafunzo na operesheni,amekua mkuu wa tume za kipolisi zinazoundwa kuchunguza mauaji ya Polisi kuanzia Arusha, Tarime, Mbarali, Mbeya na Songea,lakini hakuna mabadiliko yoyote. Kamuhanda aliua Songea,hakuchukuliwa hatua yeyote ya nidhamu,jana ameua tena Iringa. Sijui baada ya Iringa atatumwa kutekeleza mauaji mkoa gani! Chagonja anatakiwa kuwa ameisha timuliwa kazi siku nyingi kama siyo utawala dhaifu unaoongoza nchi hii.
 
Hv kumbe changonja nae ni mwepesi namna hii! Ina maana hajui kama watu wanapicha za kitu halisi kilichotokea kwenye field?
They say a picture tells 1,000
words but when I see these all
I see is 3 words: 'THEY KILLED HIM'. Rip DM

Hakuna polisi mjinga nchi hii kama Chagonja Mkuu!! Lile tumbo na mashavu yamejaa rushwa na Upepo Mkuu!!
 
Tume ni muhimu maana kila mtu anasema lake. Na picha inaweza kuku deceive wakati mwengine ingawa huongea maneno 1000

Maundumula tume ipi ambayo imeshawahi kuundwa hata tanzania na ikaja na jibu la uhakika
Unategemea nini mwenye tume akiwa ashatoka na majibu yake ambayo anayasema hadharani
Chagonja alisema waliofanya fujo songea ni wahuni na tume iliundwa ambayo mpaka leo hata majibu hakuna.
Huwa naona ni ulaji mwingine tuu unafanyika kwa hao wanaoteuliwa kwenye hizo tume
m
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma habari hii kwenye gazeti la Tanzania Daima na imenishtua sana, kwamba watawala wameamua kufanya lolote lile ilimradi wawazuie Chadema, soma baadhi ya paragraph hapa chini;


"Alipofuatwa na kuombwa awazuie askari wake kumshambulia mwandishi huyo, kamanda huyo alifunga vioo vya gari lake, akapiga honi mara kadhaa, na akaondoka. Baada ya RPC kuondoka eneo hilo, ndipo bomu lilirushwa na kumfumua mwandishi utumbo."


Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Michael Kamuhanda, alisema awali kwamba anaipenda kazi yake, hivyo hawezi kuruhusu mikutano katika mkoa wake mpaka atakapopata maelezo ya ziada.

Alisema: "Ni kweli jana saa mbili tuliwapa barua ya kuruhusu shughuli zao ila hili ni agizo na mimi ninakaribia kustaafu na kazi yangu ninaipenda, hivyo siwezi kuruhusu maandamano kinyume na maagizo yaliyopo."

Alisema CHADEMA hawawezi kufanya mikutano kwa kuwa hawana jeshi wala vifaa vya kupambana na Jeshi la Polisi, hivyo wakijaribu kutotii sheria ni lazima washurutishwe.

Source; Tanzania Daima; Polisi waua tena kikatili
 
Wakati umefika kwa jeshi la polisi kutafakari upya mbinu yao ya kuzuia kuenea kwa matawi ya vyama vya upinzani hapa nchini na hasa chama cha CHADEMA. Haiingii akilini kuwa matukio haya ya polisi kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kuzuia harakati za kisiasa za CHADEMA kujitanua na kusambaa kwa kufungua matawi na kuelimisha sera zake ni AKILI ZA KIPOLISI.

Katika mazingira ya kawaida inaonyesha kuwa jeshi letu la polisi ama linatumwa na serikali chini ya maelekezo ya CCM au baadhi ya viongozi wa polisi ni wanachama wa CCM na wanataka kujijengea ujiko ili watunukiwe vyeo ndani ya CCM au serikalini.

MAONI YANGU:

Wakati umefika kwa polisi kutambua mali ni kodi ya wananchi wote bila kujali itikadi ya siasa na rasilimali zote za nchi ni zetu wote kwa manufaa yetu wote. Wajibu wa polisi ni kulinda wananchi wote na mali zao kwa haki na usawa wakiwa wamelala, wanatembea, wanacheza, wanaandamana, wanaelimishana kwa njia ya mikutano, mihadhara au kwa burudani.

Polisi wangejijengea heshima kama wangehakikisha wanatoa ulinzi uliotukuka kwa CHADEMA katika harakati zake za kisiasa za kujitanua, kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha wananchi kujua haki zao, wajibu wao na kulinda rasilimali za nchi yao.
 
Back
Top Bottom