andate
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 2,651
- 1,006
Waziri wa maliasili na utalii lazima afuatilie kwa sababu aliyeuawa ni mtalii. Kwa sheria za kimataifa mtu anapouliwa kwenye nchi isiyo yake lazima nchi husika itoe taarifa za kueleweka kwa nchi ya aliyeuliwa. Waziri wa mambo ya ndani lazima atoe ushirikiano kwa waziri wa utalii kwa sababu yeye ndio anahusika na usalama wa mtu yeyote(m-tz/mgeni) aliyeko nchini. Ukizingatia kila KLM inapotua KIA, inashusha watallii zaidi ya mia na kupakiza wengine zaidi ya mia(wengi wao waholanzi) serikali inaingiza pesa nyingi sana kutoka kwao(ingawa wanazila, na hawakarabati uwanja) wakiogopa kuja revenue itapungua. Majirani zetu wametupaka matope sana, huku napoishi wazungu wengi wanaamini wakija Tz watauawa, unaweza ukaamini Tz kuko hivyo?katika taarifa ya habari ya leo nimeshuhudia mawaziri wawili(yule wa mambo ya ndani na yule wa maliasili na utalii) wa JMT wakifika katika eneo la tukio.
sio muda mrefu tuliwahi kusikia mauaji ya kutisha mfano kiongozi wa chadema kuchinjwa na chainsaw,vijana wanne kunyongwa,zeru zeru kuuliwa kikatili na viungo vyake kunyofolewa.
swali;je mawaziri wanathamini wazungu kuliko watanzania?
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Kuhusu kutofuatilia mauaji ya watanzania Wizara ya mambo ya ndani ndio wahusika isipokuwa hawawajali wananchi, wanapaswa kulaumiwa kwa hilo.