Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Mudhihir alipata ajali baada ya kulumbana na Zitto Kabwe. na chacha Wangwe amelumbana na chadema sana hivi karibuni kama mawazo amesababishiwa na mambo kadhaa wa kadhaa.

1. Hivi Mudhihir na Zitto "walilumbania" wapi? Mie nadhani aliyelumbana na Zitto ni Karamagi.

2. Kabla ya Chacha wangwe kufariki amelumbana na watu wengi, hata kwenye gesti alikolaa Dodoma, na wala hayakuwa masuala ya Chadema, bali ugomvi wa kawaida tu kama mnavyojua. lakini sidhani kama malumbano hayo ndiyo chanzo cha ajali na kifo chake.

3. Mtu yeyote aliyefuatilia michango ya Mgagagigikoko hapa, atajua anakotaka kutupeleka, anachekelea kifo hiki kwa sababu anataka kukitumia kwa maslahi anayojua....watu wanaomboleza yeye anakenua...
 
Jamani ama kweli uhai wetu wanadamu unaweza kuzimika kama mshumaa tu!!! Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na kuwapa faraja na subira wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao.
 
Mgagagigikoko, nadhani una matatizo yako unatafuta wa kumuambukiza, bahati mbaya hapa wote ni watu wazima, watoto mko wachache sana. Unayoandika na unayemwandikia (siju unamwaddress nani?) ni vitu viwili ambavyo vinaonyesha hicho ninachokisema. Pole, kama unataka kutumia msiba kuonyesha udhaifu wako. pole. Hapa si mahali pake, na sina dawa kwa ugonjwa wako. Utajadiliana na watoto wenzio...

sijamjua Wangwe leo kwenye msiba niko nae toka mlipoanza kumuwekea zengwe,soma mada zangu kwenye Chacha Wangwe na Chadema.kiasi cha kijana wako Mushi akanibatiza jina la Wangwe na kusema bora apigwe Risasi.
 
LAKINI AIRBAG SYSTEM YA MASHANGINGI NI BORA KULIKO YA MARK 11...,NDIO MAANA WATAALAMU WA USALAMA WANAPENDEKEZA MASHANGINGI KWENYE OFFROAD AU SAFARI NDEFU.......HATA UKICHUNGUZA MISAFARA YA RAIS..OR THE LIKE KAMA ANAENDA SAFARI NDEFU ZAIDI YA KM 100 AU KWENYE BARABARA MBAYA ..HUPANDA MASHANGINGI..YAPO SECURED ZAIDI...

...AIRBAG INASAIDIA SANA..UKIONA ILIVYOMSAIDIA MTU KAMA KAPUYA ..UTAAMINI ...NA UKIONA NAMNA MAMA MBATIA AMBAYE KWA BAHATI MBAYA ILE NISSAN PATROL YAKE ILIKUWA OLD MODEL KIDOGO NA HAIKUWA NA AIRBAG...INGEKUWEPO ANGEWEZA KUTOKA MZIMA.....hata mtu kama MUDHIHIR alipopata ajali na cruizer yake kama sio AIRBAG zaidi ya kuumia angeweza hata kupoteza maisha...

SIKU ZA KARIBUNI WABUNGE WAMEKUWA HAWAPEWI CHAGUO LA MAGARI AMBAYO WANATAKIWA KUYANUNUA YAKIWA MAPYA..BUT I REMEMBER KABLA ..KILA BUNGE JIPYA LINAPOANZA DEALERS WA MAGARI MAPYA...LANDROVER,TOYOTA,NISSAM,MITSUBISHI ..ets walikuwa wanakaribishwa bungeni na wabunge walitakiwa wachague magari miongoni mwa make zinazoaminiwa na serikali.....baadaye naona huu utaratibu umeachwa na hii imesababisha wabunge wengi kuingizwa mkenge na wauzaji wa USED.....najua wabunge wengi tu ambao sasa hivi magari yao yanawasumbua sana...na hayakidhi mahitaji ya wanakotokea ..kutokana na kuchakaa haraka....

PM,

Aliyekuambia hivyo kakudanganya. Faida ya hizo 4WD ni kwamba ni comfortable, kwahiyo kama unaenda safari ndefu basi zinakufanya usichoke sana. Pia zinaweza kupita kwenye matope na mashimo lakini sio kwenye suala la safety.

Soma mail niliyomjibu invisible, wameongelea mambo hayo hayo. Kwenye barabara nzuri kama Dar mpaka Dodoma, una nafasi kubwa ya kupona kwenye gari dogo kuliko shangingi, kama yote yana ubora sawa.
 
Mudhihir alipata ajali baada ya kulumbana na Zitto Kabwe. na chacha Wangwe amelumbana na chadema sana hivi karibuni kama mawazo amesababishiwa na mambo kadhaa wa kadhaa.

Acha fikra potofu!! Basi wangekuwa wameshakufa watu wengi sana katika kipindi ambacho Zitto amekuwa hapa duniani. Maana kuanzia utoto wake hadi utu uzima atakuwa amelumbana na wengi tu na hatujasikia lolote kuhusiana na hizo dhana zako potofu. Mbona wale walioamua kumfungia Bungeni pamoja na kuwa alikuwa hana kosa lolote hawajafa hata mmoja!!!? Au wale waiodai alikuwa anatembea na marehemu Amina Chifupa!!!? Mwe! Kuna watu wana fikra potofu!!!!
 
Poleni sana Wazalendo wenzangu, Watu wa Tarime na Watanzania kwa ujumla.

Wangwe alikuwa ni mpenda maendeleo.

Asubuhi hii nilikuwa Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine nilihudhuria bunge la asubuhi na baadaye kuonana na baadhi ya wadau kuhusu TPN akiwemo Mzalendo Slaa na wengineo kabla ya jioni hii kuondoka na kurudi DSM.

Sina uhakika chanzo cha Ajali ya Mh. Wangwe ni nini, lakini traffic ya magari wakati mwingine ni kubwa. Malori mengi husafiri usiku na barabara ya Dodoma ni nyembamba japo ni nzuri. Baadhi ya madereva si waangalifu. Sina uhakika kama vitu hivi vilichangia, lakini ni vyema kwa miaka ya mbeleni kuangalia ni namna gani ya kuboresha mapungufu haya.

Mungu awafariji wafiwa wote.
 
1. Hivi Mudhihir na Zitto "walilumbania" wapi? Mie nadhani aliyelumbana na Zitto ni Karamagi.

2. Kabla ya Chacha wangwe kufariki amelumbana na watu wengi, hata kwenye gesti alikolaa Dodoma, na wala hayakuwa masuala ya Chadema, bali ugomvi wa kawaida tu kama mnavyojua. lakini sidhani kama malumbano hayo ndiyo chanzo cha ajali na kifo chake.

3. Mtu yeyote aliyefuatilia michango ya Mgagagigikoko hapa, atajua anakotaka kutupeleka, anachekelea kifo hiki kwa sababu anataka kukitumia kwa maslahi anayojua....watu wanaomboleza yeye anakenua...

wewe mnafiki Wangwe hajagombana na watu wengi,huo ni uzushi na ulikuwa unafuatilia nyendo zake hadi guest ya Dodoma? huo nao uzushi, amekwisha kufa bado unamzulia? nadhani furaha unayo wewe kuona kuwa mambo yako sasa yako tambarare, nakutakia uchaguzi mwema kwani unagombea na kivuli.
 
This world is not my home I'm just a passing through
My treasures are laid up somewhere beyond the blue
The angels beckon me from heaven's open door
And I can't feel at home in this world anymore

Oh Lord you know I have no friend like you
If heaven's not my home then Lord what will I do
The angels beckon me from heaven's open door
And I can't feel at home in this world anymore

I have a loving mother just up in Gloryland
And I don't expect to stop until I shake her hand
She's waiting now for me in heaven's open door
And I can't feel at home in this world anymore

Oh Lord you know I have no friend like you
If heaven's not my home then Lord what will I do
The angels beckon me from heaven's open door
And I can't feel at home in this world anymore

Just over in Gloryland we'll live eternaly the saints on every hand are shouting victory
Their songs of sweetest praise drift back from heaven's shore
And I can't feel at home in this world anymore

Oh Lord you know I have no friend like you
If heaven's not my home then Lord what will I do
The angels beckon me from heaven's open door
And I can't feel at home in this world anymore
 
Game Theory ,

Acha mambo ya kitoto kwani unarush kwenye Judgement ? atujajua hiyo ajali ilitokea vipi , kosa lilikuwa la nani ..kwa hiyo nadhani ni muhimu watu tusubiri mpaka tupate habari kamili . Ila kikubwa ninachoomba ni kwamba ikiwezekana wamfanyie marehemu blood analysis pia...
 
..definatelly ..wabunge wana umuhimu wa kuwa na madereva....QUOTE]

Hata Mudhihir, Kapuya, Salome Mbatia na wengine walikuwa na madereva. Jamani ndio maana zikaitwa ajali (kitu kitokeacho muda, mahali, siku, na kwa mtu yeyote bila kutarajiwa).

Kikubwa ni kuchunguza nini chanzo la ongezeko la ajali nchini. Vitu vinavyoweza kuchangia ajali ni pamoja ni Mwendo wa kasi, kupasuka kwa gurudumu, ubovu na uchakavu gari ama barabara, ulevi, uzembe wa watumiaji wa barabara(waendesha baiskel, watembea kwa miguu, wanyama, n.k), dangerous Drivers, e.t.c

So Kuwepo na chombo maalum kinachofuatilia na kuchunguza vyanzo mbali mbali vya ajali na kutoa maoni kwa wasimamia sheria ili kudhibiti wimbi la ongezeko la ajali.
 
wewe mnafiki Wangwe hajagombana na watu wengi,huo ni uzushi na ulikuwa unafuatilia nyendo zake hadi guest ya Dodoma? huo nao uzushi, amekwisha kufa bado unamzulia? nadhani furaha unayo wewe kuona kuwa mambo yako sasa yako tambarare, nakutakia uchaguzi mwema kwani unagombea na kivuli.

Haya ndiyo baadhi ya mambo yanayo-put off watu wengi serious katika mijadala ya maana. Sasa mimi nimeingiaje katika kugombea na kivuli? Haya yananihusu vipi mimi? Mimi ni nani na wa wapi hadi niingizwe huko unakosema wewe? Na kabla ya hapa, hapo juu kwenye mcango wako mmoja, umemuita mtu "kijana wangu".

Sasa naanza kupata mwanga wa mwelekeo wako wa mawazo, lakini katika uptofu huu, haya mambo ya kigagaggigikoko ndo yanathibitisha kwamba baadhi ya watu hapa wanavamia na kuchanganya hoja na watu. Kama kuna kupotea, ndiko huku, na hii inapunguza credibility ya forum maana inatumiwa na baadhi ya wahuni kwa ajili ya kutimiza malengo yao machafu. Mfano wa haraka haraka hapa ni huyu Mgagagigikoko na kauli zake hizi....!Aibu!
 
Baada ya siku kama kumi nashauri watu someni tena hii thread halafu nenda kasome ile ya ajali ya mama Mbatia au Mudhihir, hapo utagundua jinsi tulivyo. Consistency ni kitu haba sana kwa watu walio wengi hapa JF.

Ajali ni ajali tu tu lazima tukubali hivyo. Kutumia ajali ku score points ni makosa makubwa.

Wangwe amekufa kwa ajali wala hatakuwa wa mwisho, kuna wengine wengi tutaendelea kuangamia kwa njia hiyo hiyo.

Kwasababu tunakwepa kutambua sababu kamili za ajali na kukimbilia kwenye mikono ya watu, tunaishia kwenye kuyaacha matatizo pale pale na hivyo watu wengi zaidi kuendelea kuchinjwa.

Hivi serikali itasubiri mpaka watu wangapi wafe kwa ajali ndio ianze kuchukua baadhi ya hatua kupambana na sababu kuu zinazosababisha ajali?

Hizi ajali zinashutua sana na kusikitisha sana wakati huo huo.
 
Wafiwa poleni.

Moja ya nguzo muhimu katika juhudi za kujenga Taifa ametutoka.

Mungu amlaze pema peponi.

Tatizo la ajali za barabarani pia tunahitaji kulikazia macho kama lile la ufisadi.

Apumzike kwa amani.
 
Mbunge wa Tarime Mhe. Chacha Wangwe (Chadema) amefariki dunia majira ya saa tatu za usiku (saa za Tanzania) katika ajali ya gari akitokea Dodoma kuelekea Jijini Dar-es-Salaam. Habari za kifo hicho zimethibitishwa na Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma Bw. Omar Mganga na uongozi wa Chadema.

Kwa mujibu wa habari zinazoendelea kuingia KLH News ajali hiyo imetokea saa tatu za usiku mahali panapoitwa Pandambili ingawa chanzo cha ajali yenyewe bado hadi hivi sasa hakijafahamika. Uongozi wa Chadema saa hii unakutana mjini Dodoma nyumbani kwa Mwenyekiti wake Bw. Freeman Mbowe na taarifa nyingine zozote zitapatikana baadaye.

Habari zaidi zinasema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa ajali hiyo haikutokana na kugongana na gari jingine isipokuwa kupasuka kwa mataria/tairi (kupata pancha) na gari imeharibika vibaya. Ajali hiyo imetokea wilayani Kongwa eneo la Pandambili. Muda mfupi uliopita mwili wa Marehemu umefikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambako ulipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. William Lukuvi pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi.

Mlolongo wa taarifsa za msiba zinaonesha kuwa zilianzia kwa Polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa Spika na hatimaye uongozi wa Chadema ambao ulituma ujumbe ulioongozwa na Dr. Slaa kuelekea eneo la tukio. Hata hivyo kabla ya kufika eneo la tukio walikutana na gari la kubebea wagonjwa la wilaya ya Kongwa lililokuwa likiuleta mwili Dodoma. Msafara wa Dr. Slaa ukaungana na gari hilo ili kulindikiza. Taarifa nyingine zinasema kuwa watangazaji wa TVT wameelekea eneo la tukio na bila ya shaka watatoa taarifa yao mapema asubuhi saa ya za Tanzania kuhusu eneo la tukio.

Majaribio yote ya kupata kujua ni nani aliyekuwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kumtambua Mhe. Wangwe bado hazijafanikiwa; tunatarajia Polisi kutoa taarifa yao kesho pia.

Vyanzo vya Bunge vinasema kuwa mapema kesho Spika wa Bunge ataongoza dua ya asubuhi na pia kuahirisha kikao cha Bunge ili kutoa nafasi kwa wabunge kuomboleza. Mapema asubuhi pia kikao cha kamati ya uongozi kitakaa na kujadiliana na familia ili kuandaa mipango ya mazishi na taratibu nyingine za maombolezo.

Mhe. Wangwe alizaliwa tarehe 15 Julai 1956 na kupata elimu yake ya msingi kwenye shule za Rosana na Magoto huko Tarime na baadaye kuendelea na elimu ya sekondari kwenye shula za Nyaroha na Kinondoni Muslim. Kabla ya kujiunga na Chadema Mhe. Wangwe aliwaku kuwa Katibu wa Mkoa wa chama cha NCCR Mageuzi na baadaye kujiunga na Chadema ambacho kilimsimamisha kugombea Ubunge wa Tarime.

Mwishoni mwa mwaka jana Bw. Wangwe alichaguliwa kukaimu nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa chama hicho kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa makamu Dr. Walid Kaborou. Hata hivyo Bw. Wangwe alisimamisha nafasi hiyo na Chama chake baada ya kudaiwa kuwa alikuwa akiuka maadili ya uongozi na kufanya mambo ambayo yalikuwa hayana maslahi ya chama.

Hata hivyo Bw. Wangwe aliendelea kusimamia msimamo wake wa kutaka mabadiliko ndani ya Chadema na alikusudia kuyaongoza mabadiliko hayo kwa kutangaza nia yake ya kugombea nafasi ya Uenyekiti katika uchaguzi mkuu wa chama hicho baadaye mwaka huu. Unaweza kusikiliza mahojiano ya KLHN na Mhe. Chacha Wangwe kwenye eneo la "listen shows".
 
Mwanakijiji, this is one the most thorough and even-handed news report I have ever seen from a Tanzanian journalist.

(Samahani kutoka nje ya subject ya Msiba, lakini juzi walifariki watoto wa Mbunge mwingine, lakini Bunge likatoa kitaarifa cha kiholela holela na crummy media ya Bongo haiku pick up the slack. Mpaka leo sijui yule aliyefiwa alikuwa ni Mbunge wa wapi)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom