Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
..Mtanzania hunitendei haki ..kwani thread ya chacha ..sikuwa active ..revise your notice ...its seems you have just presumed ....that i was a severe critic..sidhani...huu mgogoro nilikuwa naona kama unakuzwa..thats why sikuchangia namna hiyo unayofikiria..ahsante!!

PM,

Sawa tuendelee kuomboleza, kuna siku ukitaka nitakuwekea maandisho yako juu ya Wangwe na kulinganisha na hicho ulichoandika hapo juu.

Kule kwetu wanasema mwanaume aliyepitia jando haogopi kukabiliana na ukweli hata kama ni mchungu. Is better to stand up and be counted kuliko kuwa mnafiki.
 
Watu wasijehusisha hiyo accident na mgogoro wa kiuongozi aliokuwa nao ndani ya CHADEMA.

Mungu aiweke roho ya marehemu pema peponi. Sote ndiyo njia yetu hiyo.

Watu wengine wana fikra za kichawichawi vile! Sasa haya yametokea wapi? Kichuguu, tanguliza ubinadamu kwanza...hata kama hujiheshimu na unadhani hufahamiki! Hata kama huheshimu wengine, na marehemu akiwamo, basi jiheshimu nafsi yako inayokusukuma hapa.

Poleni wanafamilia na wapambananaji wote. Mungu alitoa, Mungu ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe!
 
Alikuwa anaendesha gari ndogo aina ya Toyota Corolla nje kidogo ya mji wa Dodoma na ndilo alilopata ajali nalo.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma anasema chanzo cha ajali hakijajulikana na gari limeharibika sana na tairi mbili za upande wa kulia zimepasuka.

Pamoja na Wangwe ni kuwa na rafiki yake Deus Francis Mallya alipona lakini amekimbizwa hospitali.

Eneo hilo ni maarufu kwa ajali maeneo ya Dodoma

Inawezekana kweli hakuna hata watu walioshuhudia?

Na ni kwanini aulizwe kamanda wa polisi badala ya watu walishuhudia ajali.

Hii inatia shaka.

Natamani technology ikue haraka na pawe na "breaking and live news".
 
Warudishe Bunge Dar safari kila siku na barabara zetu hizi za mashimo tutakwisha
 
najua wabunge wanachoka sana ....kukaa bungeni,na mara nyingine wakitoka wapate nyama na moja mbili...wanashauriwa kuwa na madereva,huyu muhashimiwa huwa anaendesha mwenyewe gari??,,,..its time now parliamentary service commission ..wahakikishe madereva wote ni compulsory kuwa na madereva waliohakikiwa na ofisi ya bunge.na pia kuhakikisha kuwa hata kama magari wanajinunulia..wapewe minimum features za gari la mbunge....gari ya nuhashimiwa ingekuwa at least ina AIRBAG nzuri..kama za fourwheels ingesaidia sana..juzi tumeshuhudia ilivyomuokoa mke wa dr shein...na prof kapuya....
Ukweli ni kuwa vigari hivi vidogo huwa control yake ovyo kabisa. Tena mbaya watu wanaviongezea 'bushes' kitu ambacho huaribu kabisa hata design yake. Na Chacha naona hakuwa na dereva na kumbuka kamtindo ketu ka kuendesha hata kwenye kona ukapokea simu... Halafu alikuwa na safari ya kurudi Tarime (nadhani katika msiba hivi) hivyo mawazo yalikuwa mengi tu, ninachoweza kusema ni kuwa katika hali kama hii Japhet alitakiwa kumsoma mbunge huyu na kumsisitiza kuwa na dereva wakati wote kwakuwa alishamhabarisha juu ya matatizo yake nyumbani.

RIP Chacha! Nenda murra, nasi tunakuja
 
Tragedy! kumbe huko Chadema nako kuna Ku-Kolimbana. Pole mjane na ndugu wote

Mtu mzima, akili za mtoto wa miaka 6! Ama kweli, kumbe na wewe uko hivi, huu ndio uwezo wako wa kufikiri? Unajua haya mambo huwa tunayajadili na uwapuuza watu wanaohusisha ajali kama hizi na siasa, kumbe na wewe uko kundi hili? Bora nisingekuwa na kujua, maana imeniuma saaaaaana kwamba nawe uko hivi.

Anyway, turudi kwenye msiba. RIP Wangwe!
 
Imeniuma zaidi mimi niliefiwa na Mbunge wangu. Bora nami nisingekujua maana "imeniuma" SANA
 
Watu wengine wana fikra za kichawichawi vile! Sasa haya yametokea wapi? Kichuguu, tanguliza ubinadamu kwanza...hata kama hujiheshimu na unadhani hufahamiki! Hata kama huheshimu wengine, na marehemu akiwamo, basi jiheshimu nafsi yako inayokusukuma hapa.

Poleni wanafamilia na wapambananaji wote. Mungu alitoa, Mungu ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe!

Kichwamaji,

Wewe umenikurupukia bila kutafakari maneno yangu; tafadhali soma kwa makini maneno yangu. Ninaijua nchi yetu ambako watu tunatabia ya kutoa majibu rahisi kwa jambo lolote, mojawapo likiwa ni hili; ndiyo maana nikatoa tahadhari hiyo kuwa tusitafute majibu rahisi. Hata hivyo kama umesoma posts zilizofuata unaona kabisa kuwa hapa hapa JF watu wameshaanza kuelekea huko huko kwenye majibu rahisi kama nilikokuwa naonya.

Huu ni msiba wetu sote. Kama umeniona sina ubinadamu kwa kuonya hivyo basi na yaishie hapo tusichafue thread hii zaidi.
 
Was Chacha Wangwe a lesser human..? Lets try to respect the dearly Departed.

Do you actually believe that "dearly departed" thing or you just flip around depending on who "dearly departed"? Remember that Ballali fella? You didn't show him much respect when he "dearly Departed," did you?

Hiyo pesa ya EPA................. Ndio hivyo sasa wanasema amekufa...yameisha!!! Hakuhojiwa na Tume ya uchunguzi na yeye akiwa ndio FUNGUO ya hii kashfa nzima. Tutamuomboleza na kama kawaida, ukifa ni kwamba mazuri yooote duniani ni wewe!

JF itafundisha watu kitu kimoja ambacho Wabongo wengi sana hawakijui: ukisema kitu basi iwe ni principle yako, sio kugeuka geuka tu kutokana na upepo wa siku hiyo. Invisible na website yako hii you have no idea what it's doing to the country, yani ni shule ya public discourse Tanzania. Sijui tutakulipa vipi.
 
...duh! ama kweli! ...haya, tulitoka kwa udongo tutarudi kwa udongo, ama ajali haina kinga na kazi ya mungu haina makosa!

mkono wa rambirambi kwa wafiwa.
 
Poleni na msiba na Mwenyezi mungu amrehemu marehemu. RIP.
 
PM,

Sawa tuendelee kuomboleza, kuna siku ukitaka nitakuwekea maandisho yako juu ya Wangwe na kulinganisha na hicho ulichoandika hapo juu.

Kule kwetu wanasema mwanaume aliyepitia jando haogopi kukabiliana na ukweli hata kama ni mchungu. Is better to stand up and be counted kuliko kuwa mnafiki.

..mimi ni mmoja wa wale waliopita jando bila ganzi...weka tu hiyo qoute..yangu sasa hivi ..[yenye ref number].......najua haina content za KIHAINI....kwa sababu si imani yangu......nadhani umekosea tu..kwa kuwa waliotoa comment za aina hiyo wapo..
 
Kichwamaji,

Wewe umenikurupukia bila kutafakari maneno yangu; tafadhali soma kwa makini maneno yangu. Ninaijua nchi yetu ambako watu tunatabia ya kutoa majibu rahisi kwa jambo lolote, mojawapo likiwa ni hili; ndiyo maana nikatoa tahadhari hiyo kuwa tusitafute majibu rahisi. Hata hivyo kama umesoma posts zilizofuata unaona kabisa kuwa hapa hapa JF watu wameshaanza kuelekea huko huko kwenye majibu rahisi kama nilikokuwa naonya.

Huu ni msiba wetu sote. Kama umeniona sina ubinadamu kwa kuonya hivyo basi na yaishie hapo tusichafue thread hii zaidi.

Basi, kama nimekuoena nomba radhi! Ila ninavyoona, na kama unavyothibitisha mwenyewe, wewe umetoa onyo kwa KUCHONGA njia ya kelekeza watu HUKO HUKO ulikotaka kuwaonya wasiende, kana kwamba kifo cha Wangwe hakikukugusa, ukaona uwaelekeze watu huko ambako wamekufuata. Kwa maelezo yako hapo juu, inaonekana haikuwa nia yako kufanya hivyo, lakini umedondosha yai njiani ukidhani halitapasuka? Pole kwa yote, turudi kwenye msiba. Labda umejifunza kitu hapa namna ya kuongoza na kupotosha mijadala.
 
PM,

Sawa tuendelee kuomboleza, kuna siku ukitaka nitakuwekea maandisho yako juu ya Wangwe na kulinganisha na hicho ulichoandika hapo juu.

Kule kwetu wanasema mwanaume aliyepitia jando haogopi kukabiliana na ukweli hata kama ni mchungu. Is better to stand up and be counted kuliko kuwa mnafiki.
Design ya hao wako wengi hapa JF ukiweka maandishi yao utaandika kitabu cha maneno mabaya aliyoandikwa kwa kuwa mkweli, pale alipoweza kusema hili ni jembe si kijiko.
 
Watanzania wenye uchungu na nchi tuna utamaduni wa pamoja kinapokuja kifo. Wote husikitika na kuhuzunika anapofariki mtanzania mwenzetu bila kujali uadui. Utamaduni ambao MAFISADI Hawana, kwani wao huchukulia kifo kuwa ni ushindi kwao. Kwa sasa watanzania tupo kwenye maombolezo tuache siasa za KIFISADI za kushabikia kifo. Tumuombee Chacha mungu ampe makazi mema ya milele

RIP WANGWE, JF Will miss you too.
 
..mimi Ni Mmoja Wa Wale Waliopita Jando Bila Ganzi...weka Tu Hiyo Qoute..yangu Sasa Hivi ..[yenye Ref Number].......najua Haina Content Za Kihaini....kwa Sababu Si Imani Yangu......nadhani Umekosea Tu..kwa Kuwa Waliotoa Comment Za Aina Hiyo Wapo..

Nlifikiri Mmesahu Bora Ya Ndugu Yangu Mushi Kaja Kuomba Radhi Kwa Uchuro Aliyomfanyia Marehemu. Wengine Hata Kusema R.i.p Wangwe Wanaona Aibu Hadi Sasa,

Nilitegemea Kuona Timu Nzima Ya Chadema Inakuja Kutoa Pole Hapa Kuanzia Hadi Kieleweke,dr.slaa.zitto,mnyika,kitila Mkumbo Kwani Wote Ni Active Members Hapa, Na Mpaka Kieleweke Alikuwa Wa Kwanza Kusema Jinsi Alivyonyang'anywa Umakamu,timu Yote Ya Kina Kitila Walijaa Kujaza Fitina Zao, Kuwa Si Siri Alikuwa Zigo Kubwa Ndani Ya Chadema, Labda Sasa Wamefurahi Kuona Zigo Limeondoka Ila Wajue Kuwa Mawazo Yake Na Ukweli Wake Katupatia.
 
Inawezekana kweli hakuna hata watu walioshuhudia?

Na ni kwanini aulizwe kamanda wa polisi badala ya watu walishuhudia ajali.

Hii inatia shaka.

Natamani technology ikue haraka na pawe na "breaking and live news".

Hapana Richard, kitaalauma mtu mwenye authority ya kuthibitisha tukio la ajali ndiye huyo ambaye waandishi wamemnukuu. Eye witnesses wanaweza kucomment, lakini bila kauli ya kamanda taarifa inachukuliwa kama uzushi! Haipendezi, lakini ndo hivyo. Ndo maana siku zote tunasoma habari za vifo Muhimbili kutoka kwa "Tibaigana" na madaktari, badala ya ndugu wa marehemu n.k. Ndugu wanaweza kusimulia kilichotokea lakini wao si source ya taarifa rasmi za kifo au ajali...na kwa kuwa hiii ndo taarifa ya kwanza ya kifo hicho, tunatarajia kwamba taarifa lazima itoke huko ilikotoka. Sasa baada ya hapo tutajua mengi kwa walioshuhudia tukio hilo.
 
Ukweli ni kuwa vigari hivi vidogo huwa control yake ovyo kabisa. Tena mbaya watu wanaviongezea 'bushes' kitu ambacho huaribu kabisa hata design yake. Na Chacha naona hakuwa na dereva na kumbuka kamtindo ketu ka kuendesha hata kwenye kona ukapokea simu... Halafu alikuwa na safari ya kurudi Tarime (nadhani katika msiba hivi) hivyo mawazo yalikuwa mengi tu, ninachoweza kusema ni kuwa katika hali kama hii Japhet alitakiwa kumsoma mbunge huyu na kumsisitiza kuwa na dereva wakati wote kwakuwa alishamhabarisha juu ya matatizo yake nyumbani.

RIP Chacha! Nenda murra, nasi tunakuja

Invisible,

Labda ongelea ubovu wa gari lakini kama unaongelea gari ambazo ni safi basi gari ndogo nyingi tu ni bora zaidi kuliko hizo shangingi inapokuja kwenye ajali.

Bahati nzuri wenzetu kila mara huwa wanapima ubora wa gari kwenye ajali na safari zote gari ndogo ni bora zaidi. Una nafasi ya kutoka salama kwenye gari ndogo kuliko hizo shangingi.

Tunadanganywa na hayo mashangingi, yanafaa kwenye kutanua lakini sio ubora kwenye ajali.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom