Kifo cha Mh Regia, Kilombero walia na Mteketa!

Imekwishatokea na kumhukumu mtu kwa sisi binadamu si jambo jema bali tumwachie Mungu ndiye atakaemhukumu kama kuna mtu kahusika na hicho kifo chake na kumuumbua kwani siku zote haki itasimama na damu ya mtu haipotei bure
 
na wananchi wanachomaanisha hapa ni ushirikina unaominika kufanywa na Mh Mteketa! Imani yao kubwa ilikuwa kwamba mbunge wa jimbo ni marehemu regia! Inashangaza kwa kweli,ila kwa ujumla msafara mzima umefika salama salmini kwa mengine ni kwamba huku pia naona chadema wanakubalika sana
Mkuu mimi Regia niliwahi kukutana nae ana kwa ana na aliniambia hiki ninachokisema, Mungu amemwepusha na mengi ila nitakuwa wa mwisho KUTOAMINI kuwa hii ajali Mteketa hajahusika
 
Mteketa huyo akiwa na kanumba
ab6.gif
 
Siamini kwamba hicho kifo kuna mkono wa mtu kutokana na mazingira ya ajali ilivyotokea. Mimi nadhani ni uzoefu ktk kuendesha na hali ya ulemavu wa marehemu imesababisha ajali.
 
Yaaaani nilikuwa nime reserve hii umeniwahi..huyo ndo mpango mzima maana walikuwa na bifu WEWE UNAANDIKA UKIWA HAUKO FIELD! Mimi niko hapa ndani ya dk 5 zilizopita imebidi mh nyerere mb atumie busara za kiuongozi na kumwambia lwakatare kiongozi wa CDM ajaribu kuwanyamazisha vijana waliokuwa wakiimba kwenye viwanja hivi kuwa Mteketa mteketa... Mwanga wetu wajaribu kutulia ili wabunge wa ccm wasifedheheke wewe na kiwanga hiyo ni yako hapa haipo
 
Hata mimi nilishangaa kwani eneo la ruvu darajani halina kona yoyote iweje asione mbele kama kuna gari wakati ana overtake?pili, kama gari lilipinduka mara saba na kugalagazwa vile why only Regia??ndio kuna mipango ya Mungu lakini hapa napata mashaka kwamba huenda ni mapenzi ya Mungu yaliyotimia kupitia kwa mtu flani kama ambavyo Yesu alikufa lakini kwa kupitia usaliti wa Yuda,
 
Bado nasubiri detail zaidi wakuu kabla cjasema lolote baya,eti yeye suzan kafanyaje na bf lilianzaje?
 
MSAFARA UMEHITIMISHWA MAJIRA YA SAA TANO ILA WALIANZA KUINGI SAA KUMI NA MOJA JIONI LEO. WAJUA MTEKETA USHINDI WAKE ULIPINGWA MAHAKAMANI NA REGIAH NA PIA DC NDIKILO & TEAM WALICHELEWESHA SANA KUTANGAZA MATOKEO YA KILOMBERO HIVYO BIFU HII HAIJAWATOKA WANANCHI NA KWA VILE ABDUL HAJAACHIWA MAHAKAMANI BASI MANENO HAYATAISHA MPAKA SIASA 2015 ZIKAMILIKE......VIFO HAVIKOSI SABABU TULIAMBIWA KAWAWA KAMUUA SOKOINE LICHA YA KUWA HAIKUWA KWELI..... MIMI NAAMINI DADA REGIAH MUNGU AMEMCHUKUA KWA MAPENZI YAKE, NA SISI TUNALIA KWA MAPENZI YETU KWAKE. ISSUE YA KUONYA HAPO NI KITENDO CHA MTEKETA KUONEKANA TANGU MSIBA UMETOKEA AMEKUWA AKIRANDARANDA MITAANI NA HUMMER YAKE SASA HII IMEAMSHA CHUKI ZAIDI JUU YAKE; SOMETIMES MAISHA RAHISI YANASAIDIA KUONDOA CHUKI NA HUSUDA, BRO MTEKETA ANADHANI YUKO LUMUMBA AKIDALALIA MAGARI KUMBE KWA WALIMA MPUNGA KAMA AKINA FDR.Jr HAPA. ALL IN ALL REST IN PEACE BIG SIS REGIAH MTEMA
 
MUNGU WANGU!

Naamuru kuvuruga anga la kwanza na hata la saba!
Mungu nitakutaja maana hakika unaweza!
Naenda kinyume kbs na pepo wachafu wote wanaoranda ktk anga lako kuwatafuta watu wako.

MUNGU wangu nitakutaja daima na hata siku zote ya maisha yangu!
Hakika una uwezo wa yote juu ya Mbingu na Nchi
Naenda kinyume kbs na pepo wachafu,wachawi,mapepo,na hawa washirikina nawafunga vinywa kwa jina la YESU KIRSTO aliye hai na hata leo.

Nawaamuru kwa jila hilo lenye mamlaka Mbinguni na Duniani,hamna mamlaka yeyote ktk Mji wa walio HAI nitakuja Mungu pale ninapomwamuru shetani atoke arudi kuzimu akachomwe moto, ninakuita JEHOVA kwa hakika upo.
Naenda kinyume kbs nao,nikiwaamuru watoke kwa Jina la YESU KIRSTO BWANA aliyetufia msalabani. Shetani toka toka toka hauna mamlaka yeyote hapa Nchi toka toka rudi kuzimu ukachomwe moto wa jehanam.
MUNGU WANGU MWENYE UWEZO NINAIMANI TOSHA YA KWAMBA WATU WAKO WATAKOMBOLEWA SIKU MOJA NA WAKAWA HURU KWA KUWA WOTE WANAOKUTEGEMEA NI KAMA MLIMA WA SAYUNI,na hawatatikisika kamwe!
Mungu ninapoondoka hapa jukwaani naomba ukawalinde watu wako wote ktk Jina lake YESU KIRSTO anayeishi na kumiliki na mwenye uwezo wa kusema mwisho kabla ya mwanzo.

Na nikiomba hayo naimani ya kwamba YESU watu wako hawataangamia maana upo!
Ni katika Jina lenye ushindi YESU KIRSTO!

Ameni!
 
sijawahi kukibaliana na MS hata siku moja lakini katika hili Ustaadh acha niungane na MS. Umepotea njia mkuu.

Ustaadh amewasikia watu wakilia na Mteketa na kuna post moja inasomeka kuwa ilimbidi Lwakatare awanyamazishe. Sasa Ustaadh amepotea njia kivipi? Kwa mimi mwandishi nampongeza kutujuza kuwa Ifakara wanaamini kuwa kuna njama za kishirikina; ziwepo au zisiwepo. Msimsakame mtoa habari. Jibuni kulingana na habari.
 
Baada ya umati kuimba nyimbo za kulaani na kupiza kulipa kisasi kwa njia wanazojua wao ilibidi Mh Zitto kabwe kuwaomba watulie huku Mh Vincent Nyerere kupita katika Makundi yao na kuwaasa vijana wapunguze Munkari na kuwaambia ni msiba wa Bunge na si Msiba wa Chama tuna wabunge wa vyama vyote waliofiwa na ni Msiba wa Taifa,Hakuna muuaji ila mapenzi ya Mungu,japo ilikuwa ngumu kumuelewea hatimaye vijana walimpa heshma na Kunyamaza, ila hali sio shwari sana.
 
Taarifa nilizozipata usiku huu kutoka Kilombero zinasema kumeibuka mvutano nyumbani kwa Marehemu Regia Jana usiku ambapo kambi mbuili zinazopingana ndani ya CHADEMA wilayani humo zimefikia hatua ya kupigana msibani. Kambi hizo moja ilikuwa ikimuunga mkono Regia na nyingine inamuunga mkono Suzan Kiwanga. Kwenye tukio hilo mwenyekiti wa chadema wilaya alifikia hatua ya kutimuliwa msibani. Nitawapeni taarifa zaidi baadae
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom