Kifo cha Mama Fatuma Ndolanga (R.I.P.)

Poleni wafiwa na Mola awape nguvu na imani katika kipindi hichi cha majonzi. "Kila nafsi itaonja mauti", kwa kuwa hiyo ni njia nasi tutapita.
 
Pole sana Mzee Ndolanga na familia yako kwa msiba wa mpendwa wenu Mama Fatuma.

Ukarimu wenu kwa yatima hautaweza kusahaulika.

Mwenye Mungu ailaze roho ya marehemu mama Fatuma mali peme peponi, Amina.
 
Pole sana Mzee Ndolanga na Ndugu na jamaa wote.....RIP Mama Ndolanga
 
Wana JF wanafiki sana au tuseme mna ubaguzi wa hali ya juu, kule kwa Chadiel mmerusha pole nyingi na madongo lakini kwa mke wa Ndolanga mnashindwa hata kumwambia alale pema na kumwombea Ndolaga kwa mungu asirudi tena kufanya kazi Wanyamapori au TFF?
 
Matatizo ya ufisadi ambao bwanake Ndolanga ni mmoja wao. Wanafikiri watakimbiza wagonjwa nje kumbe wakati huo inakuwa too late.

Amkeni Watanzania, tutengeneze hospitali zetu ili haya magonjwa yajulikane mapema na hivyo kuongeza uwezekano wa kutibiwa.

Lakini sisi Watanzania kazi zetu ni kuiba na kutoroshea pesa nje, kupeleka wagonjwa wetu nje huku maskini wanakufa na kurundikana kwenye hospitali zisizo na huduma.

Tunajifanya werevu kumbe ni wajinga tu.

Mkuu Engineer,
Hapa kidogo umekiuka maadili. Hapa tunaomboleza kifo cha mama yetu. Kama mumewe ni fisadi msimtuhumu huyu mama kuwa naye alikuwa fisadi. Source nyingi za fedha za wanaume haziwi disclosed kwa wake zao hasa zile ambazo hazina account katika sources za income kwa family. Akina mama wengi wamekuwa hivyo.

Kuhusu kutibia nje ni kwa uwezo wa mtu (individual). Sidhani kama ni serikali iligharimia matibabu yake. Hata leo mimi nikiugua nikapelekwa kutibia nje utasemaje. Itategemea uwezo wangu financially na wa ndugu pia, hata marafiki kwa kuwa wanapenda bado niishi. Kuna mwanangu nilimpeleka India 2005 kwa matibabu ya moyo na amepona kabisa, ni kwa sababu nilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Fedha hizo sikuzipata kwa ufisadi bali ni juhudu zangu halali. Please, si vema kufanya hivi hasa pale ambapo ni kifo kama hiki. Thanks.
 
Mkuu Maane,

Sina tatizo na Watanzania wanaopeleka watoto au ndugu kutibiwa nje maana kwa mtu yeyote, utatumia kila ulicho nacho ili kuokoa familia yako.

Ila kwa mafisadi kufikiri wataokoa maisha ya ndugu zao kwa kuwapeleka nje huku wanaiba na kuua hospitali zetu ni ujinga mkubwa sana.

Nyie mnaongelea msiba wa mtu mmoja wakati leo hii kuna maelfu ya Watanzania wanakufa kwa kukosa Aspirin shauri ya watu kama Ndolanga ambao ni ufisadi tu kila sehemu kuanzia kwenye maliasili mpaka kwenye michezo.

Hili tatizo ni kama ajali, tunajifanya kulia, kesho tunaenda kusababisha ajali zingine. Sitaki niwe mnafiki, sina jonzi hata dogo kwa mafisadi.

Tutengeneze hospitali zetu ili kila mtu afaidike, hili la watu waliotuibia kukimbiza ndugu zao nje wakiumwa wanajisumbua tu. Hii ni fire fighting wala haitawasaidia kabisa, tunataka fire prevention.

Ndolanga leo analia kilio ambacho Watanzania wengine wanalia kila siku. Ina maana kifo cha mtu mmoja kina thamani kuliko maelfu ya Watanzania wanaokufa shauri ya wezi na majambazi kama Ndolanga?

Niko radhi kwenda kwa mungu na msimamo huu na kuhukumiwa naye. Acheni upuuzi na unafiki wenu hapa.

Pole mkuu maane kwa huyo mtoto wako na mungu akubariki ili aendelee kuwa na afya njema.
 
Pumzika kwa amani mama.

Saratani ya matiti inaua sana, ninawafikiria kina mama mamilioni ambao hawana uwezo wa kufika hospitali ya wilaya, achilia mbali Ocean Road.

Moja ya mikakati inayowafanya wenzetu waweze kufanikiwa katika vita dhidi ya gonjwa hili (na mengine mengi ya aina hii) ni kutazamwa mapema kama wana uvimbe na dalili nyingine, kansa hii inaweza kuzuilika kabisa kama ikigundulika mapema.

Naomba tufikirie kidogo kuhusu uwezekano wa kuongeza huduma za kupima mapema na kuliwahi gonjwa hili katika hatua ambazo linaweza kuzuiwa kuchukua maisha ya kina bibi, mama, dada na binti zetu.

Mkuu, vifo hivi vinasikitisha sana, ni mambo ambayo yakijulikana mapema vifo vinaweza kupunguzwa kwa asilimia kubwa.

Kuna kundi la madaktari wazalendo nawafahamu, wapo wanaandaa system au tuseme NGO specifically kwa ajili ya B. Cancer na Cervical Cancer, hii siyo MEWATA iliyozoeleka, nadhani hawa jamaa wana mambo mengi mapya watakayokuja nayo in terms of eary diagnosis of these killers. Nitawahabarisha mambo yakiiva kwani mkakati utaanzia huko vijijini
 
Mwenyezi Mungu Muumba ailaze roho ya marehema mahali pema peponi na awajaalie wafiwa nguvu na imani ya kuhimili machungu ya msiba huu. Amiin.
 
Pumzika kwa amani mama.

Saratani ya matiti inaua sana, ninawafikiria kina mama mamilioni ambao hawana uwezo wa kufika hospitali ya wilaya, achilia mbali Ocean Road.

Moja ya mikakati inayowafanya wenzetu waweze kufanikiwa katika vita dhidi ya gonjwa hili (na mengine mengi ya aina hii) ni kutazamwa mapema kama wana uvimbe na dalili nyingine, kansa hii inaweza kuzuilika kabisa kama ikigundulika mapema.

Naomba tufikirie kidogo kuhusu uwezekano wa kuongeza huduma za kupima mapema na kuliwahi gonjwa hili katika hatua ambazo linaweza kuzuiwa kuchukua maisha ya kina bibi, mama, dada na binti zetu.

Kiranga,

Saratani za aina ambazo zinaweza kutibiwa kama zikigundulika mapema zinaua wote, wake kwa waume. Prostate cancer, kwa mfano, inaongoza kwa kuua baada ya lung cancer (ambayo nayo haichagui), halafu kuna colon cancer, brain tumors, na saratani nyingine nyingi ambazo hazina jinsia wala kabila. Sio tatizo la "kina bibi, mama, dada na binti zetu."

Habari zikiwa hazijanyooka kama hivyo zinaweza kupotosha, halafu wanaume, yani nusu ya wananchi, watasema, aaah, saratani ni za wanawake tu, na juhudi za kupambana hazitafikia potential yake.

Wafiwa poleni sana.
 
Habari inahusu saratani ya matiti, bandiko langu limelenga katika saratani ya matiti kwa sababu ndiyo ninayoielewa kuwa inagundulika mapema kirahisi na kuzuilika kirahisi.Sijawahi kusikia mwanamme mwenye saratani ya matiti ndiyo maana nikawataja watu wake tu.

Kama wewe una utaalamu mwingine wa kuweza kuainisha saratani nyingine ambazo zinaweza kutambulika mapema na kuzuilika kirahisi si vibaya kama ukizibainisha. Kwa uelewa wangu mdogo saratani ya ubongo kutambulika na kuzuilika kwake kiurahisi kamwe hakuwezi kulingana na saratani ya matiti. Ukiigundua mapema saratani ya matiti mabingwa wanafanya operesheni, au hata kukata titi, saratani ya ubongo kutokana na unyeti wa eneo inapokuwa operesheni yake si rahisi na huwezi kusema utakata kichwa. kwa hiyo upande wako wa kuzilundika saratani hizi zote pamoja umeonyesha ukosefu wa kufikiri.

Hongera kwa kujaribu, lakini katika kutaka niseme nisichokijua kuwa kweli, hususan kwa sababu hakina mantiki wewe mwenyewe ndiye unajionyesha kukosa umakini.
 
Mkuu Engineer,
Hapa kidogo umekiuka maadili. Hapa tunaomboleza kifo cha mama yetu. Kama mumewe ni fisadi msimtuhumu huyu mama kuwa naye alikuwa fisadi. Source nyingi za fedha za wanaume haziwi disclosed kwa wake zao hasa zile ambazo hazina account katika sources za income kwa family. Akina mama wengi wamekuwa hivyo.

Kuhusu kutibia nje ni kwa uwezo wa mtu (individual). Sidhani kama ni serikali iligharimia matibabu yake. Hata leo mimi nikiugua nikapelekwa kutibia nje utasemaje. Itategemea uwezo wangu financially na wa ndugu pia, hata marafiki kwa kuwa wanapenda bado niishi. Kuna mwanangu nilimpeleka India 2005 kwa matibabu ya moyo na amepona kabisa, ni kwa sababu nilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Fedha hizo sikuzipata kwa ufisadi bali ni juhudu zangu halali. Please, si vema kufanya hivi hasa pale ambapo ni kifo kama hiki. Thanks.

Si rahisi kutenganisha mke na mume mkuu, angalia wa Vijisenti alifanya 75% ya kampuni mali yake na 25% ilikuwa ya mkewe kule Jersse!
 
Mkuu Engineer,
Hapa kidogo umekiuka maadili. Hapa tunaomboleza kifo cha mama yetu. Kama mumewe ni fisadi msimtuhumu huyu mama kuwa naye alikuwa fisadi. Source nyingi za fedha za wanaume haziwi disclosed kwa wake zao hasa zile ambazo hazina account katika sources za income kwa family. Akina mama wengi wamekuwa hivyo.

Kuhusu kutibia nje ni kwa uwezo wa mtu (individual). Sidhani kama ni serikali iligharimia matibabu yake. Hata leo mimi nikiugua nikapelekwa kutibia nje utasemaje. Itategemea uwezo wangu financially na wa ndugu pia, hata marafiki kwa kuwa wanapenda bado niishi. Kuna mwanangu nilimpeleka India 2005 kwa matibabu ya moyo na amepona kabisa, ni kwa sababu nilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Fedha hizo sikuzipata kwa ufisadi bali ni juhudu zangu halali. Please, si vema kufanya hivi hasa pale ambapo ni kifo kama hiki. Thanks.

Ukweli utabaki kuwa ni ukweli na wala hakuna haja ya kuwa wanafiki. Kama tungepunguza ufisadi matibabu yangepatikana kirahisi sana Tanzania.
 
Habari inahusu saratani ya matiti, bandiko langu limelenga katika saratani ya matiti kwa sababu ndiyo ninayoielewa kuwa inagundulika mapema kirahisi na kuzuilika kirahisi.Sijawahi kusikia mwanamme mwenye saratani ya matiti ndiyo maana nikawataja watu wake tu.

Kama wewe una utaalamu mwingine wa kuweza kuainisha saratani nyingine ambazo zinaweza kutambulika mapema na kuzuilika kirahisi si vibaya kama ukizibainisha. Kwa uelewa wangu mdogo saratani ya ubongo kutambulika na kuzuilika kwake kiurahisi kamwe hakuwezi kulingana na saratani ya matiti. Ukiigundua mapema saratani ya matiti mabingwa wanafanya operesheni, au hata kukata titi, saratani ya ubongo kutokana na unyeti wa eneo inapokuwa operesheni yake si rahisi na huwezi kusema utakata kichwa. kwa hiyo upande wako wa kuzilundika saratani hizi zote pamoja umeonyesha ukosefu wa kufikiri.

Hongera kwa kujaribu, lakini katika kutaka niseme nisichokijua kuwa kweli, hususan kwa sababu hakina mantiki wewe mwenyewe ndiye unajionyesha kukosa umakini.

Actually there are cases of men who have suffered breast cancer, however, in small %s

Male breast cancer
http://www.mayoclinic.com/health/male-breast-cancer/DS00661

Breast cancer isn't just a woman's disease. Men also have breast tissue that can undergo cancerous changes. While women are about 100 times more likely to get breast cancer, any man can develop breast cancer. Male breast cancer is most common between the ages of 60 and 70.

The prognosis for male breast cancer is the same as for breast cancer in women. In the past, male breast cancer was often diagnosed at a more advanced stage, which may have led people to believe it had a worse prognosis. Although male breast cancer and breast cancer in women are similar, important distinctions such as breast size and awareness affect early diagnosis and survival in cases of male breast cancer.
 
Last edited:
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, sote ndio njia. R.I.P Mama yetu, will always remember your cheerfulness
 
Ukweli utabaki kuwa ni ukweli na wala hakuna haja ya kuwa wanafiki. Kama tungepunguza ufisadi matibabu yangepatikana kirahisi sana Tanzania.

Muzee you have nailed it!

Sisi akina yakhe tukiugua, hii fursa ya kwenda angalau Muhimbili fasttrack haipo, hivyo KATU HATUTOACHA kusema tugawane haq bin haq KEKI YA TAIFA.

Hivi tumeshafanya tathmini kuwa huko India kunani cha ziada ambacho hapa tunashindwa kuwa nacho tukiamua?
 
RIP Mrs Ndolanga.......Poleni sana familia ya marehemu Mungu awatie nguvu ktk kipindi hichi kigumu.Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe..Amen.
 
Muzee you have nailed it!

Sisi akina yakhe tukiugua, hii fursa ya kwenda angalau Muhimbili fasttrack haipo, hivyo KATU HATUTOACHA kusema tugawane haq bin haq KEKI YA TAIFA.

Hivi tumeshafanya tathmini kuwa huko India kunani cha ziada ambacho hapa tunashindwa kuwa nacho tukiamua?

Mkuu Mtindio, Kwanza nitangulize Rambirambi zangu kwa wafiwa nilimjua marehemu nikiwa Arusha mwishoni mwa miaka ya sabini, nilikutana nae tena mwanzoni mwa miaka ya tisini akiwa mgeni katika Hoteli niliyokuwa nikifanya kazi huko ughaibuni napenda kuungana na wana JF wenzagu kuomboleza msiba huu. Cha pili mkuu ni tathmini ya kujilinganisha na India!! hata tukiamua kama ulivyosema its going to take long long time kwani jamaa wametangulia mno katika safari ya maendeleo ya teknologia. pamoja na ufukara uliokithiri kwa wengi wa watu wao, wadosi wako juu katika sekta nyingi, hiyo ya Tiba ndio zaidi hata hao wanaojiita dunia ya kwanza hupeleka wagonjwa wao India. Kwa sasa si Ligi yetu.Tupunguze ufisadi, tuweke sera nzuri , tuwe watekelezaji na tuanze kwa kukimbia.(angalau ..........)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom