Kifo cha Mama Fatuma Ndolanga (R.I.P.)

Ab-Titchaz

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
14,631
4,225
Wakuu wa JF,

Nasikitika kutangaza kifo cha Mama Fatuma Ndolanga aliyekua mkewe former chairman wa FAT, Al-haj Muhidin Ndolanga, kilichotokea hospitali India.Marehemu alikua anapata matibabu ya breast cancer lakini Mungu alikua na mipango mengine.Amewaacha nyuma mume na watoto sita: Omari, Halima, Ahamad, Salum na Muhidin.

Mazishi yamefanyika leo mchana shambani kwake Picha ya Ndege, Kibaha.

The Lord Gives and the Lord takes.Blessed be his name.


Mama%20Fatuma%20Ndolanga.jpg



Rose1.gif
 
RIP Mama Ndolanga... Mwenyezi Mungu akusamehe maovu yako na akupe pumziko la amani.

Sote tuko njia moja. Muhimu ni sote kutambua kuwa "Wema hawaishi... Tupatapo fursa ya kuwa nao tuwatumie ipasavyo". Mama huyu kawasaidia wengi, namuombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema ampumzishe kwa amani.
 
Poleni nyingi sana Alhaji Ndolanga, na familia yote, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu ampe raha ya milele mama Ndolanga; Amina
 
Pole Alhaj Muhidin Ndolanga na wanafamilia wote. RIP Mama Ndolonga.
 
I happen to visit her at Apollo Hospital, New Dheli on New Year's Eve. Despite being terminally ill, Mama Fatuma Ndolanga was full of hope a vigour.
Mungu aifariji familia yake na kuiweka roho yake mahali pema peponi, apumzike kwa amani-Amen.
 
Pumzika kwa amani mama.

Saratani ya matiti inaua sana, ninawafikiria kina mama mamilioni ambao hawana uwezo wa kufika hospitali ya wilaya, achilia mbali Ocean Road.

Moja ya mikakati inayowafanya wenzetu waweze kufanikiwa katika vita dhidi ya gonjwa hili (na mengine mengi ya aina hii) ni kutazamwa mapema kama wana uvimbe na dalili nyingine, kansa hii inaweza kuzuilika kabisa kama ikigundulika mapema.

Naomba tufikirie kidogo kuhusu uwezekano wa kuongeza huduma za kupima mapema na kuliwahi gonjwa hili katika hatua ambazo linaweza kuzuiwa kuchukua maisha ya kina bibi, mama, dada na binti zetu.
 
asalamu alaykum.

poleni wafiwa nyote na tnakutakieni kila la kheri na Mola akupeni subra katika msiba huu ambayo ni wetu sote.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi
 
Napenda kuungana na wote katika jamvi hili na wengine wasiopo hapa kutoa pole kwa familia ya Mzee wetu Muhidin Ndolanga kwa kufiwa na Mke, Mama na ndugu yao mpendwa. Nawaombea wapate nguvu ya kukabiliana na msiba huu mkubwa wakijua kuwa hiyo ndio njia ambayo wote tutaipitia hatimaye ili kufika katika makazi yetu ya milele.

Mungu ailaze roho ya Mama Fatuma Ndolanga mahali pema peponi, Amen.
 
Sisi sote ni wa mwenyezi mungu na kwake lazima tutarejea. Mungu amrehemu mama Ndolanga. Na kwetu sisi tujue kuwa kifo chochote miongoni mwetu ni moja ya ukumbusho kuwa maisha ya duniani ni kama maua, hivyo hatuna budi kuandaa hatma yetu baada ya kufa kwa kutenda mema hapa duniani.
 
Matatizo ya ufisadi ambao bwanake Ndolanga ni mmoja wao. Wanafikiri watakimbiza wagonjwa nje kumbe wakati huo inakuwa too late.

Amkeni Watanzania, tutengeneze hospitali zetu ili haya magonjwa yajulikane mapema na hivyo kuongeza uwezekano wa kutibiwa.

Lakini sisi Watanzania kazi zetu ni kuiba na kutoroshea pesa nje, kupeleka wagonjwa wetu nje huku maskini wanakufa na kurundikana kwenye hospitali zisizo na huduma.

Tunajifanya werevu kumbe ni wajinga tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom