Kifo cha Magazeti Fulani..uandishi wa siasa au siasa za uandishi??

komedi

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
204
17
Angalia magazeti yetu fulani yalivyokuwa yakiandika vichwa vya habari na linganisha na stori yenyewe.

Mheshimiwa JK Amejiuzulu

Katika hali isiyokuwa ya kawaida( inaendelea ukurasa wa 4).... bwana Jumanne Kazimoto ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa kijiji cha manumba mawili wilaya ya Nsuba amejiuzulu rasmi jana mara baada ya kutuhumiwa kuiba sungura wawili wa bi Kimoto wa kijiji cha jirani.....

Dr. Slaa kuhamia CCM leo

Habari nzito tulizozipata punde tu kutoka kwa mwandishi wetu maalum aliyeshiriki katika kikao cha dharura cha kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA zinasema kwamba( Inaendelea ukurasa wa 7)......baada ya kuongoza maandamano ya Arusha Dr. Slaa anatarajiwa kuhamia CCM kirumba City yaani mji wa Mwanza baadaye leo kupokea maandamano mengine makubwa........

Lowasa kugombea Urais 2015

Imethibitika rasmi kuwa katika uchaguzi ujao wa( inaendelea ukurasa wa 2)... chama cha mpira wa mkufu wilaya ya Monduli mwaka 2015 bwana mmoja anayejulikana kwa jina la Josephath Sakatai Ngarenanyuki au kwa jina la utani ' Lowasa' atagombea urais wa chama hicho kwa kuwa atakuwa amefikisha miaka inayotakiwa kikatiba kuweza kugombea kwa..........

Yathibitika Waziri wa Serikali ya Kikwete Kabaka

Baada ya mabishano ya chini kwa chini na minong'ono ya hapa na pale sasa imethibitika bila ubishi kuwa mheshimiwa waziri wa kazi na ajira( Inaendelea Ukurasa wa 4)...... aliyechaguliwa katika Baraza jipya la mawaziri ni Bi Gaudensia Kabaka.


Jamani waandishi wa magazeti fulani mnatupasua mioyo wenzenu? Kha! mweh!

Yaani mnataka muuze leo tu? Kesho hapana?

Najua wanajamvi mna mengi upande huu.
 
Mods I stand to be corrected, bado najifunza, naomba hii iwe moved kwenda hoja mchanganyiko...nadhani niko sawa.
 
Ndiyo maana ni vema ukayajua magazeti mahiri ya siku zote ukawa unayanunua. Usivutiwe na vichwa vya habari vya siku kwa siku.
 
Ndiyo maana ni vema ukayajua magazeti mahiri ya siku zote ukawa unayanunua. Usivutiwe na vichwa vya habari vya siku kwa siku.

Huna haja ya kumung'unya maneno:-

Mahiri ya kila siku (ya kiswahili):-
1. Tanzania Daima
2. Mwananchi
3. Nipashe

Ya kila wiki:

1. Raia Mwema
2. MwanaHalisi

Sioni jingine.
 
Huna haja ya kumung'unya maneno:-

Mahiri ya kila siku (ya kiswahili):-
1. Tanzania Daima
2. Mwananchi
3. Nipashe

Ya kila wiki:

1. Raia Mwema
2. MwanaHalisi

Sioni jingine.

Naunga mkono hoja hasa pale kwenye ratiba za Bilicanas na busara za Kubanda.
 
Usilete upupu kwa great thinkers! Chakachua vitu unavyoleta hapa.

Ningekueleza maana ya Thanks 0, Thanked 44 times in 27 posts. Always far less than 6''type.........tuishie hapo.

As far as being a great thinker is concerned, you will never even dream of being in my league.

Hili si jukwaa lake, nitafute kwenye jukwaa muafaka nikuvalishe nguo ya kioo.
 
Back
Top Bottom