Kifo cha kamanda barlow na hadithi ya nchi ya kusadikika

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,681
1,109
Niliwahi kusoma sifa za viongozi na ulevi wa madaraka katika nchi ya kusadikika,hadithi iliyotungwa na mwandishi maarufu bwana Rwegasira kama sitakosea jina lake wa gazeti la Rai akijaribu kuzungumzia ulevi wa madaraka na ukikwaji wa maadili wa viongozi wa nchi hiyo.Mwandishi huyo ambaye kwa sasa ni marehemu na Mungu amlaze mahali pema peponi kwa kuweza kutufumbua macho kwa kile alicho kitabiri.

Pia Watanzania hususani viongozi wetu ambao tumewapa dhamana ya kutuongoza ifike mahali wajue kuwa cheo ni dhamana.Kusema hivi namaanisha kutokana na tabia ya viongozi wetu kujisahau pale wanapopata madaraka na kujiona wana right ya kufanya chochote kila na zaidi ya hayo wanajiona kuwa wapo juu ya sheria.

Jamii imechoshwa na umangimeza na utovu wa nidhamu unaofanywa na baadhi ya viongozi kwa kuvunja sheria makusudi na kusahau kauli mbiu yao ya utii wa sheria bila shuruti.Ni mara ngapi tumeshuhudia ndoa za walalahoi zikivunjwa kwa kuwa tu mkubwa fulani ana mtaka mke wa mlalahoi.

Kuhukumu si jambo jema lakini mazingira ndiyo yanayo sababisha watu kuhukumu na kuhoji.Ni kikao gani cha harusi kilichowahi kufikisha muda wa usiku mkubwa wa saa nane,ikiwa kikao ni mpaka saa nane basi harusi itakesha.

Ifike mahali Watanzania tuwe wakweli na kutofumbia macho matukio yanayo sababisha utata ndani ya jamii yetu.Mwandishi wetu wa hadithi ya kusadikika alifika mbali na kusema "mheshimiwa mkuu wa nchi hiyo kwa kuwa ilikuwa desturi yake kuandaliwa mwanamke yeyote bila kujali kama ni mke wa mtu wakati wa ziara yake alipotembelea mikoa yake,ilifika mahali siku mmoja alijisahau na kutoa chupi ya mwanamke na kujifutia jasho akidhani ni leso".

Maono ya mwandishi yule ndiyo ambayo leo yameikumba jamii yetu,lakini pamoja na matukio kama hayo bado viongozi wa serikali wana jaribu kusimama kidete na kusema ni tukio ya ujambazi inapothibitka kiongozi fulani amevunja kanuni na taratibu za haki ya kuishi bila kuwabugudhi wengine.

Maadili ya jamii yetu yatazingatiwa vipi ikiwa tutashindwa kuweka ukweli hadharani na kutokuficha matukio ambayo yana dhalilisha utu wa mtu.

Kutokana na hali hii na uchafuzi wa hali ya amani kwa nchi yetu,suala la ajali hii lisiachwe likapita hivi hivi kiasi cha kusababisha minong'ono ikachukuliwa kuwa ukweli.Tunataka uchunguzi wa kina ufanyike na kubainisha ukweli kuliko kuishia kumweka mwalimu wa watu ndani kwa sababu dhaifu ya kuisaidia polisi.
 
tusipende kufanywa mbuzi wa shughuli kwa kutolewa kafara na kunufaisha wenye matakwa yao.Haki lazima ionekane ikitendeka na wajibu ukitimizwa hapo ndipo tutakapo kubali kuwa huu ni utawala wa sheria.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom