Kifo cha gazeti la MwanaHalisi, Je wameshidwa kuliendesha?

naona hoja yako ni kulishambulia mwanahalisi, na si zaidi ya hapo.Kwa sasa limekubalika na lina soko la kutosha ukilinganisha na nakala zinazotoka kila wiki.
Fanya utafiti kati ya magazeti yanayochapishwa kwa kila wiki lipi linauza nakala nyingi zaidi.Acha biashara ya kuponda bila utafiti.
 
Hivi ni vichwa vya ukurasa wa mbele wa Mwana Halisi jumatano ya wiki hii.Chadema kufuta kinga ya Mkapa, Kanumba kanumba,Maji ya dawasco hatari, Shilingi bilioni 300 kufukia migodi chambua mwenyewe
 
Hoja yako makini ila makosa ni madogo tu. Mwanahalisi halimchafui mtu bali linawaweka hadharani wachafu, na hao wachafu hujitetea kwa kuita majungu.
 
Asante sana kaka/dada

Ukiwambia ukweli wanaJF wanakubishia wanakuporomoshea matusi
Kichekesho ukipigwa ban hapa JF unaenda kulalamika huko huko Mwanahalisi unaowaponda!!......kweli wewe ni mtu wa ajabu sana. out of topic vipi nasikia Burji agombei ubunge tena mafia? kweli fitina mnazimudu.
 
Nionavyo mimi, MWANAHALISI la miaka ya hivi karibuni ni tofauti sana na MWANAHALISI la miaka miwili iliyopita kwa ubora wa habari!
Wakuu chunguzeni mtitiriko wa waandishi wa gazeti hilo kwa sasa mtagundua kuwa mwandishi mmoja anaweza kuandika habari zaidi ya mbili au hata tatu, na kibaya zaidi maudhui ya ujumbe anaouleta unafanana kimantiki ( sana Josta Mwangulumbi), hili linapoteza ladha wakati.
Ktk gazeti hili, yupo mwandishi mmoja ambaye anaitwa Kondo Tutindaga huwa analiandikia habari yakinifu na fikirishi zisizo na ushabiki wa kisiasa.
Kadhalika tangu Kubenea aende masomoni ndo kama vile ameondoka na gazeti lake, wakurugenzi wa gazeti hili wajifunze kilichowapata RAI ambalo lilikimbiwa na wasomaji baada ya kuanza maroroso kama haya. Sisi ni wapenzi wa wa gazeti la MWANAHALISI, ushauri huu uwe changamoto kwenu kwa kuwa nafahamu kuwa nanyi ni wadau wazuri hapa JF.

Kuna kile kichwa kinaitwa Naronyo Kicheere. Ile mashine ni noma, anaandika makala fikirishi hadi msomaji unatetemeka ndani kwa ndani unaposoma
 
hayo ni mawazo yako na uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo kuwa mwanahalisi imekufa.kwani najua unakitu ulikua unakitafuta umekikoso lakini usiwe na mawazo ya mjumuisho.
 
Kumwagiana tindikali, kupelekana mahakamani, waandishi kuandika habari with their eyes toward the TISS, nk huenda zimepunguza ule ujasiri walioanza nao.
 
Ni miezi na Miezi sasa tokea nisikie na kuona gazeti hili la mwanahalisi
Hili gazeti lilileta changamoto kwa jamii na kwa wanaJF kwa ujumla katika
habari zake.

Siku hizi hili gazeti limekuwa jalala sijui ni nini kimelipata

Je Mkurugezi Mkuu Kubenea ndo kalitupilia mbali ? maana nasikia bado yuko india anatanua


Nawasilisha
Kumbe Dr. Kupeng'e bonge la kifaa?
 
naona hoja yako ni kulishambulia mwanahalisi, na si zaidi ya hapo.Kwa sasa limekubalika na lina soko la kutosha ukilinganisha na nakala zinazotoka kila wiki.
Fanya utafiti kati ya magazeti yanayochapishwa kwa kila wiki lipi linauza nakala nyingi zaidi.Acha biashara ya kuponda bila utafiti.
Peter hoja ya mleta mada ni kuwa Mwanahalisi ya sasa siyo Mwanahalisi ile tuliyo izoea na kutoa angalizo la kuelekea kaburini.

Kama hoja hiyo ni kweli, then hata kama circulation yao ni kubwa kiasi gani, down the drain it will go!.

Kwa Rai ilikuwaje?.
 
y
Naona wewe una lako jambo. Mbona gazeti bado linasomeka vizuri tu? chungulia hapa Gazeti la MwanaHalisi kwenye toleo la wiki iliyopita kisha utueleze matarajio yako ambayo hayakutimizwa. au lile lililotangulia...Gazeti la MwanaHalisi. La wiki hii bado liko mitaani lifuate.
Kitendo cha gazeti la Mwanahalisi kuweko mitaani kwenye mbao za matangazo mpaka leo siku ya Jumamosi ni dalili mbaya!. Enzi hizo Mwanahalisi lilikuwa ni hot cake, likitoka unaliwahi by saa 6 mchana limeisha!.
 
kaka kuwepo mtaani sio jambo wala sio hoja
Je watu wanalinunua?

Siku za nyuma watu walikuwa wanakuja na "qoute" za mwanahalisi lakini siku hizi kama jalala
hata halisomeki huu ndo mwisho wake
Japo sio dalili nzuri ila bado sio mwisho, inawezekana limezorota kutokana na mmiliki kuwa nje ya nchi hivyo kukosa zile hot hot za interest home!.

Akirudi anaweza ama kulirudisha kwenye chart kwa kumwaga mavitu kama zamani, au kuliacha liwe kama Rai kwa ku compromise na upande fulani!
 
Asante sana kaka/dada

Ukiwambia ukweli wanaJF wanakubishia wanakuporomoshea matusi
Hili ni tatizo la wanajf wenye upande, kwao ukweli ni ule tuu wanaoutaka wao kinyeme cha hapo utaambulia matusi!.

Nimewahi kufanya ukosoaji wa CCM kuwa imechokwa wana CCM humu wakavumilia na kujibu kistaarabu!.

Nimewahi kufanya ukosoaji wa CUF kuwa SUK inatekeleza ilani ya CCM hiyo ni safari ya kuzimu, japo walibisha ila ni kistaarabu!.

Nilipofanya ukosoaji wa CDM humu kuwa "hawajajipanga" chamoto nilikipata!, Niliambulia sio matusi tuu bali mitusi, lakini ujumbe ulifika na sasa ndio hao wanajipanga na njia ya Feri ni nyeupe kwao.

Vivyo hivyo ujumbe huu kuhusu Mwanahalisi umefika, wenye macho wameona, wenye masikio wamesikia!, only time will tell kwa wanashabikia kwa mapenzi upofu!.
 
Gazeti lipo mtaani na kweli halisoemeki kama unapenda kusoma JAMBO LEO, UHURU ,MZALENDO
 
yamkini ni wewe tu ndo umeona ubora wake umepungua na hii hutokana na mambo yasiyo pungua mawili au zaidi mfano halina habari ulizotengemea wewe kuzipata humo
 
Back
Top Bottom