Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee?

Lipumba anatumiwa na CHADEMA Kwa taarifa yenu.

Anaiua CUF CHADEMA inabaki kuwa Chama kikuu

Watu wanahisi ni CCM inaivuruga CUF wakati sio ni changa la Macho mnachezewa

Siasa za Mbowe kuweni makini nazo

Wenu

Ethos
Ungekuwa na ushahidi ingekuwa poa sana.
 
Hata wakati wa sakata la Zitto na Chadema mlikuja na story hizi za ubabaishaji. Haikifa.
Leo mnaleta ubabaishaji ule ule hamuoni aibu?
Yaani cuf ife sababu ya Lipumba v u kwani yeye nani?
 
Lipumba anatumiwa na CHADEMA Kwa taarifa yenu.

Anaiua CUF CHADEMA inabaki kuwa Chama kikuu

Watu wanahisi ni CCM inaivuruga CUF wakati sio ni changa la Macho mnachezewa

Siasa za Mbowe kuweni makini nazo

Wenu

Ethos
Bado,kwenye siasa we ni mchanga mno.

Chadema ndio walio wapandisha CUF kwenye chati 2015,haiwezekani wawe wa kwanza kukiua.

Uongonzi wa CUF katika halmashauri,una pewa nguvu na Chadema,hawezi kuwa wa kwanza kukiua.

Chadema hawana maslai na cuf kwa sasa zaidi ya kuongeza nguvu kupitia UKAWA kukitisha chama cha mapinduzi.

SOMA,ELEWA,BISHA.
 
Hehe.. ToKwa Povu Tu

Umdhaniae ndiye kumbe siye. CHADEMA kumsimamisha mgombea Kwa kivuli cha UKAWA 2020 Ni ngumu na italeta mvurugano katika umoja huo.

Njia pekee iliyobaki ni kuiua CUF indirectly ili wasipoteze credibility yao

Kigezo cha kuiongezea wabunge sio rafiki lengo ni kuifumba Macho CUF

CHADEMA inachangia kuia CUF sio CCM hata kidogo na Ushahidi ninao

Nitauweka soon hapa!!
 
Mkuu,kuna post hapo juu imetolewa na mtu anaitwa,GHIBUU isome utapata majibu.
 
Hehe.. ToKwa Povu Tu

Umdhaniae ndiye kumbe siye. CHADEMA kumsimamisha mgombea Kwa kivuli cha UKAWA 2020 Ni ngumu na italeta mvurugano katika umoja huo.

Njia pekee iliyobaki ni kuiua CUF indirectly ili wasipoteze credibility yao

Kigezo cha kuiongezea wabunge sio rafiki lengo ni kuifumba Macho CUF

CHADEMA inachangia kuia CUF sio CCM hata kidogo na Ushahidi ninao

Nitauweka soon hapa!!
Weka ushahidi si tupo maana leo weekend.
 
Bado,kwenye siasa we ni mchanga mno.

Chadema ndio walio wapandisha CUF kwenye chati 2015,haiwezekani wawe wa kwanza kukiua.

Uongonzi wa CUF katika halmashauri,una pewa nguvu na Chadema,hawezi kuwa wa kwanza kukiua.

Chadema hawana maslai na cuf kwa sasa zaidi ya kuongeza nguvu kupitia UKAWA kukitisha chama cha mapinduzi.

SOMA,ELEWA,BISHA.
Bavich bhana, unajua ulichokiandika hapo kwenye red juu??
Haina maslahi ila kupngeza nguvu, labda chadema na cuf kila mmoja ana wabunge wangapi??
 
Ungekuwa na ushahidi ingekuwa poa sana.
Kwani wale wanaosema Lipumba kapewa Fedha na CCM Kuna ushahidi.. Umewekwa..

Ushahidi ni pale Seifu alipoweka kikao na Lowassa Bila Lipumba kuwepo.. Wakamshawishi Duni Haji ajiondoe CUF.. Je ulimuona Lipumba katika hiko kikao
 
Hata hao unaowasema niliomba ushahidi kwao.Nataka ushahidi kwako ili tumeze vizuri haya maneno yako.
 
Hata hao unaowasema niliomba ushahidi kwao.Nataka ushahidi kwako ili tumeze vizuri haya maneno yako.
Tafuta picha, mbona zipo katika mitandao.. Kile kikao walikua watatu.. Seifu, Lowasa, Duni... Cha kwanza Duni hakuwepo
 
Kwani wale wanaosema Lipumba kapewa Fedha na CCM Kuna ushahidi.. Umewekwa..

Ushahidi ni pale Seifu alipoweka kikao na Lowassa Bila Lipumba kuwepo.. Wakamshawishi Duni Haji ajiondoe CUF.. Je ulimuona Lipumba katika hiko kikao
Kwani Lipumba na Dk Slaa walipomfuata Lowassa Seif alikuwepo?
 
Lipumba anatumiwa na CHADEMA Kwa taarifa yenu.

Anaiua CUF CHADEMA inabaki kuwa Chama kikuu

Watu wanahisi ni CCM inaivuruga CUF wakati sio ni changa la Macho mnachezewa

Siasa za Mbowe kuweni makini nazo

Wenu

Ethos
Tumezisoma propaganda zako mfu, ila tumezipuuza....
 
Tumezisoma propaganda zako mfu, ila tumezipuuza....
Mnapuuza ukweli ndio maana CCM itatawala Daima Milele... Mtakuwa wazelendo tu pale mtakapokubali kuuwa vyama vyote na kuunda Chama kimoja

Anayofanya Le Profeseri sasahivi ni moja ya Agenda ya Kamati Kuu Iliyokaa mara ya mwisho
 
Jumanne, 10 Januari 2017.
Tunapenda kuwajulisha kuwa chama chetu kimeibiwa fedha za Ruzuku kiasi cha Shilingi za Tanzania 369,378,502.64 (Milioni 369).
MPANGO ULIVYOSUKWA...
Fedha hizo zilitoroshwa kutoka Hazina ya Serikali Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Alhamisi, tarehe 05 Januari 2017 na kuingizwa kwenye Akaunti ya NMB Tawi la Temeke yenye jina la The Civic United Front ikiwa na akaunti namba 2072300456. Utoroshaji huo umefanyika bila idhini ya Bodi ya Wadhamini ya The Civic United Front ambayo ndiye msimamizi wa jumla wa masuala ya akaunti za fedha na mali za The Civic United Front haiitambui akaunti hiyo na haikuwahi kuiidhinisha ipokee ruzuku ya CUF kutoka Serikali Kuu. Katibu Mkuu wa The Civic United Front ambaye ndiye muwajibikaji mkuu wa masuala ya fedha na mali za chama haitambui akaunti hiyo na hajawahi kumuandikia Msajili wa Vyama vya Siasa kumpa akaunti hiyo ili iwekewe fedha za Ruzuku ya CUF. Vikao vya kitaifa vya The Civic United Front kwa maana ya Kamati ya Utendaji ya Taifa (ambayo ilikutana hivi karibuni kumpitisha mgombea wa Ubunge jimbo la Dimani) na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa havikuwahi kupitisha maamuzi yoyote kwamba fedha za CUF ziwekwe katika akaunti hiyo ya wilaya iliyoko NMB Temeke.
Siku mbili kabla ya utoroshaji wa fedha hizo ulisukwa mpango wa kuwaondoa baadhi ya Viongozi wa CUF wa Wilaya ya Temeke kwenye utiaji saini unaoihusu akaunti tajwa. Uondoaji wa Viongozi hao ulikwenda sambamba na kuwageuza baadhi ya Wateule wa Lipumba wanaofanya kazi za kukihujumu chama kutokea Buguruni, kuwa watia saini wa akaunti ya Wilaya. Watia saini wapya walioshiriki kwenye ughushaji huo ni Bi. Magdalena Sakaya (MB), ndugu Thomas Malima na Bi. Zainab.
FEDHA ZILIVYOWEKWA...
Siku moja baada ya NMB na wala njama hawa kukamilisha mchakato wa kubadilisha watia saini wa Akaunti ya CUF inayomilikiwa na wilaya ya Temeke (Yaani tarehe 05 Januari 2017) ndipo hazina ikaweka mzigo huo wa pesa bila kuchelewa. Siku hiyo hiyo ambapo hazina walitorosha fedha hizo, watia saini wapya wa Akaunti ya NMB ya Wilaya ya Temeke waliulizia kiasi cha fedha kilichomo kwenye akaunti hiyo na walifanya hivyo katika tawi la NMB Mandela Road.
FEDHA ZILIVYOCHUKULIWA...
Kesho yake, siku ya Ijumaa, tarehe 06 Januari 2016, Watia saini hao wakiongozwa na Thomas Malima walikwenda katika Benki ya NMB Tawi la Temeke na kufanya mambo mawili. Kwanza wakatoa kiasi cha Shilingi 69,000,000 (Milioni 69) kama pesa Taslimu, kisha wakahamisha Shilingi 300,000,000 (Milioni 300) kwenda kwenye akaunti ya mtu binafsi. Mchezo wote huu umefanyika Chapchap kama zilivyochotwa pesa za ESCROW!
AKAUNTI BINAFSI ILIYOWEKEWA PESA...
Akaunti ya Mtu Binafsi iliyotumika kutoroshea fedha hizo kutoka kwenye akaunti ya Wilaya ya Temeke ni akaunti ya NMB yenye namba 41401600207 ikimilikiwa na mtu aitwaye MHINA MASUOD OMARY ambaye ni Diwani wa CUF wilayani Handeni, mtu wa karibu wa Lipumba.
Yaani ni kama vile leo hii, Ruzuku ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itoroshwe na kuwekwa kwenye akaunti ya NMB ya Chama Cha Mapinduzi ngazi ya wilaya huko Kahama. Kisha Fedha hizo ziondolewe kwenye akaunti hiyo ya wilaya na kuingia kwenye akaunti ya mwana CCM aliyesimamishwa uanachama na halafu mwana CCM huyo azitoe fedha hizo na kuzipeleka kusikojulikana. Haya yote yafanyike bila Katibu Mkuu wa CCM kujua, Kamati Kuu ya CCM ikiwa haijui, Halmashauri Kuu ya CCM ikiwa haijui na Bodi ya Wadhamini ya CCM ikiwa haijui chochote.
AKAUNTI BINAFSI ILIVYOTAKATISHA FEDHA...
Jana Jumatatu tarehe 09 Januari 2017 MHINA MASUOD OMARY alianza kazi ya kuondoa fedha hizo majira ya asubuhi ya jana, kwanza kwa kuondoa Shilingi 100,000,000 (Milioni 100) kutokea Benki ya NMB tawi la Magomeni, kisha akiwa hapo hapo Magomeni akatoa Shilingi 50,000,000 (Milioni 50) halafu akaelekea tawi la Kariakoo na kutoa Shilingi 100,000,000 (Milioni 100) na mwisho akiwa hapo hapo Kariakoo NMB akatoa tena Shilingi 49,500,000 (Milioni 49.5). Wakati MHINA MASUOD OMARY anazunguka kwenye matawi haya kutoa fedha hizi jana alipewa ulinzi wa POLISI waliokuwa wamevalia kiraia wakiwa kwenye Magari ya CUF na aliambatana na Thomas Malima wakiwa chini ya usimamizi wa watu wengine wawili, Magdalena Sakaya na Abdul Kambaya.
Baada ya kutorosha fedha hizo zote, Akaunti ya Masoud Mhina imebakia na Shilingi 207,907 (Laki Mbili Elfu Saba Mia Tisa na Saba).
FEDHA ZA CUF ZAGAWANWA KAMA NJUGU...
Msafara wa magari yenye fedha hizo uliekea nyumbani kwa LIPUMBA (a.k.a BWANA YULE) huko Kilongawima, Kunduchi na baadaye majira ya jana usiku Lipumba na wenzake walianza kugawana fedha hizo.
A. Walipoanza kikao ikajengwa hoja kuwa Lipumba amesimamia harakati nyingi za chama na eti anadai Milioni 500, wakaazimia kuwa alipwe TZS 120,000,000 (Milioni 120) za awali, akalipwa fedha Taslimu TZS 120 Milioni jana usiku.
B. Kikao cha Lipumba na watakatishaji Fedha wake wakakubaliana kuwa Mhe. Sakaya afidiwe TZS 30,000,000(Milioni 30), Mhe. Maftaha (MB) afidiwe TZS 20,000,000 (Milioni 20), Ndugu Thomas Malima akagawiwa TZS Milioni 5, Ndugu. MHINA MASOUD OMAR akagawiwa TZS Milioni 5, Bi. Zainab akagawiwa TZS Milioni 5 na viongozi wengine watatu wa Wilaya ya Temeke wakiwemo Mwenyekiti na Katibu wa Wilaya hiyo wamegawiwa TZS Milioni 2 @(Kila mmoja).
C. Kikao hicho kimeshagawana TZS 171,000,000 (Milioni 171) na jana hiyohiyo kukawa na maazimio kuwa TZS 128,000,000 Taslimu zilizobakia zitumiwe kama ifuatavyo; Tzs 20,000,000 (Mil 20) apewe Lipumba kwa ajili ya kujiandaa na Ziara ya Mwanza, Mara na TANGA.
D. Ikaamuriwa kuwa TZS 108,000,000 (Mil 108) zitunzwe na Bi. Magdalena Sakaya na zitumike kwa ajili ya kufanya mambo mbalimbali ikiwemo; TZS 50,000,000 (Mil 50) kusaidia Wagombea wa CUF kwenye kata mbalimbali za Tanzania Bara na TZS 58,000,000 zitumike kwa ajili ya kuendesha Ofisi ya Chama Buguruni ikiwa ni pamoja kulipa posho za walinzi na watu wanaomsaidia Lipumba kulinda ofisi za Buguruni.
# Note ; Tumezungumza na Vyombo vya Habari na kutoa taarifa na nyaraka zote ikiwemo Barua ya Msajili wa vyama ya tarehe tarehe 10 Oktoba 2016 ikieleza kuwa amesitisha Ruzuku ya CUF kwa sababu haridhishwi ikiwa vyombo vya usimamizi wa fedha za CUF uko salama.
# Note2 ; Bodi ya Wadhamini ya chama, Wanasheria wa chama na Vikao vya chama vinakutana kupanga hatua za kuchukua haraka. Hatua za kiutawala zimeanza kuchukuliwa na Katibu Mkuu.
# Note3 ; Hili ni shambulio lingine kubwa dhidi ya CUF, UKAWA na Demokrasia. Lakini hili ni shambulio kubwa dhidi ya Utawala Bora, Utashi wa serikali katika kudhibiti vitendo vya jinai katika fedha na ni pigo dhidi ya vita ya utakatishaji fedha.
Julius Mtatiro,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi,
The Civic United Front,
Jumanne 10, Januari 2017,
Dar Es Salaam.
Taratibu za kifo ndio hizi zimeanza.

Paskali
 
Back
Top Bottom