Kifo cha CCM Ifakara; JK, Makinda wameshuhudia

MABARAZA YA CHADEMA ITUNZENI HESHMA YA MHE REGIA KWA KUKAMATA MAJIMBO YOTE MIKOA YA DAR ES SALAAM NA MOROGORO BILA AJIZI!!!

Mi-Baraza yetu ya BAVICHA na AWACHA mkoani Morogoro, hakikisheni kwamba kiuhakika hatumuaibishi Mhe Regia na azma yake yo kuwakomboa wanyonge vijijini wasiokua na pa kusemea.

Shambulieni Mkoa huu wa Morogoro kwa mtindo wa kijiji kwa kijiji, kata kwa kata, na kigango kwa kigango mpaka elimu ya uraia usambae kila mahala na majimbo yote kuwekwa chini ya vijana machachari na wenye moyo kama Mhe Regia ndani ya CHADEMA kunakowadia 2015.

Kumbukeni yale maneno mazito na yenye busara kubwa kutoka kwa Mzee Mtema (Baba ya Regia) kwamba CHADEMA japo mmepoteza kamanda kwa maana ya huyu mwanangu lakini naamini kwamba Mungu atawaibua Regia wengine wengi zaidi ndani ya chama siku si nyingi.

BAVICHA na BAWACHA kazi kwenu kwa kuhakikisha mkoa mzima wa Morogoro na Tabata Dar es Salam aliko Mhe Regia mambo shwaaaari mapema iwezekanavyo bila kuendelea kuwakilishwa kwa siku zaidi na Magamba maeneo hayo. Kazi iendeleeee sasa huku uongozi wetu wa Taifa wakiendelea kuwa karibu sana na juhudi zenu katika hili.
 
MABARAZA YA CHADEMA ITUNZENI HESHMA YA MHE REGIA KWA KUKAMATA MAJIMBO YOTE MIKOA YA DAR ES SALAAM NA MOROGORO BILA AJIZI!!!

Mi-Baraza yetu ya BAVICHA na AWACHA mkoani Morogoro, hakikisheni kwamba kiuhakika hatumuaibishi Mhe Regia na azma yake yo kuwakomboa wanyonge vijijini wasiokua na pa kusemea.

Shambulieni Mkoa huu wa Morogoro kwa mtindo wa kijiji kwa kijiji, kata kwa kata, na kigango kwa kigango mpaka elimu ya uraia usambae kila mahala na majimbo yote kuwekwa chini ya vijana machachari na wenye moyo kama Mhe Regia ndani ya CHADEMA kunakowadia 2015.

Kumbukeni yale maneno mazito na yenye busara kubwa kutoka kwa Mzee Mtema (Baba ya Regia) kwamba CHADEMA japo mmepoteza kamanda kwa maana ya huyu mwanangu lakini naamini kwamba Mungu atawaibua Regia wengine wengi zaidi ndani ya chama siku si nyingi.

BAVICHA na BAWACHA kazi kwenu kwa kuhakikisha mkoa mzima wa Morogoro na Tabata Dar es Salam aliko Mhe Regia mambo shwaaaari mapema iwezekanavyo bila kuendelea kuwakilishwa kwa siku zaidi na Magamba maeneo hayo. Kazi iendeleeee sasa huku uongozi wetu wa Taifa wakiendelea kuwa karibu sana na juhudi zenu katika hili.

Well said mkuu!
 
Mwisho wa siku NEC ndo msema kweli baada ya kura kupigwa..

Siku zote mimi si muumini sana wa umati wa watu. Hili la Ifakara kupokelewa na alama ya CDM, linanikumbusha wakati fulani miaka ya nyuma(simba na Yanga) nilijikuta nimekaa upande wa timu pinzani kwa sababu kaka yangu alikuwa mshabiki wa timu ile, bahati mbaya timu yangu ilifunga goli, kabla sijanyenyuka kushangilia kaka yangu aliniminyia chini. haraka nikaelewa hatari iliyokuwepo, nikaendelea kufurahia kimyakimya kwa kujumuika pamoja nao.

Sitaki kuamini kwamba umati uliojitokeza kwenye msiba wa Regia ndiyo kipimo cha kifo cha CCM Ifakara, No. bado CDM inatakiwa kufanya kazi ya ziada ikiwa ni pamoja na kumpata mtu wa aina ya Regia. Tukumbuke kwamba wapo waliomuunga au kumpenda Regia si kwa sababu ya chama chake, hawa pia ni wazi walikuwepo barabarani kumpokea.

Sijajua ni kigezo gani huwa kinatumika kuhalalisha umati wa watu unaojitokeza kwenye hii mikutano ya vyama vyetu kwamba umati huo ni zaidi ya wakazi wa eneo husika, Je, wale wanaobaki majumbani tunazo hesabu zao?

Na ndiyo maana mtu kama Mh. Mnyika na hata Regia walitambua hilo, badala ya kutegemea mikutano, walifanya pia kampeni za nyumba kwa nyumba.
 
Baada ya kuulizwa kuhusu mgogoro huo mkubwa,Dr Slaa alikiri kupewa taarifa hizo na kusema kuwa alikuwa anategemea kuanza kuushughulikia lakini kwa sasa kwa kuwa tupo kwenye msiba hatuwezi kuzungumzia hilo.kifo cha rejia kina siri nyingi na susan kiwanga ana mengi ya kutueleza kuhusu mgogoro wake na marehemu na jinsi ulivyokiathiri chama hadi inafikia walitaka kupigana na marehemu.
Tangu lini marehemu akawa na uwezo wa kupigana?
 
Ilikwisha kufa zamani kwani wako hapo kwa uchakachuaji wa Tume ya Uchaguzi ya CCM! Walishindwa vibaya!
 
Jamani wana ccm ubishi wa nini? Kwa kawaida dalili ya mvua ni ...? Nadhani ni busara kwenu ukweli kuwa hamna mvuto Ifakara na kupanga mbinu za kuwarudishia watu imani na chama chenu! Vinginevyo mnaonekana wapuuzi tu! Kwa nidhamu ya hapa nchini Tanzania, ukisikia kwenye tukio linalohudhuriwa na JK, rais wa nchi na bado watu wakaimba jina la Slaa kama rais ni lazima ubaki na maswali kichwani.Na hii ni ishara iliyo wazi wazi kuwa ccm kwishney Ifakara. Mtanataka kuona dadili gani zaidi za mvua?
 
mimi sidhani kama hicho ni kipimo tosha cha kufa kwa ccm."kushinda uchaguzi ni mbinu tu" jk.
 
RAIS Kikwete hivi karibuni alishuhudia Live kifo cha CCM yake kule Ifakara katika mazishi ya mbunge wa viti maalum chadema Rejia Mtema.

ni ukweli ulio wazi kuwa kutokan na picha ile jamani CCM bye bye.

kazi ilianza pale msafara uliobeba mwili wa Rejia Mtema, kufika Kilombero mkoa wa Morogoro, msafara huo uliokuwa ukiongozwa na spika wa Bunge ana makinda na baadhi ya mawaziri wengine wa serikali ya Jk akiwemo Stephan Wasira, njia nzima ilikuwa ji salamu za chadema , ilikuwa bomba la mtihani kwa wanaccm kuitikia salamu ile ama Laah, nadhani ndio maana hata wakati wa kuaga mwili wa mbunge wa CCM Solomon Sumari makinda alidai kuwa tusichanganye siasa wakati wa misiba, its True aliliona hilo lakini wale ni wananchi wapenda chadema,ki ujumla kilombero , ifakara ni ngome ya chadema,

Kipigo kingine kwa CCM ni pale makaburini ambapo baada ya mazishi Rais na msafara wake waliondoka , na alipoanza kuondoka DK Slaa wananchi walianza kuimba Rais Rais, na kuwaancha vinywa wazi CCM,
watanzania wa sasa hawana woga tena kama zamani, hivi sasa ukikosea unapewa Kubwa tu

pia Tukio Lingine ni pale mbunge wa wa CCM Abdul Mteketa alipozomewa Live mbele ya viongozi wa kitaifa wa CCM, jamani picha Hii yote imemdhihirishia wazi Jk kuwa kifo cha CCM kimefika.

Hivi unawaelewa vyema WATZ? kelekele nyingi sana mdomoni lakini vitendo sasa hakuna

tena ktk maeneo ambayo wala usipigie chapuo ya CDM ni Mkoa wote wa morogoro,wao wanatabia hiyo kama ilivyo humu Jf ya kuwa na maneno mengi lakini si wapiga kura

na kuhakikishia kuwa morogoro inahitajika elimu ya hali ya juu,sio tu kuja hapa na kuandika na watu kutoa maneno ukanadhani basi,ushindi unahesabiwa kwa kura na wala sio maneno mengi mdomoni

kama hamtafanya kazi ya ziada na mkakalia kuchukua kelekele za kushangiliwa ndio ushindi basi hapo mmepoteza mkuu,siasa haipo hivyo
 
We kijana hojatete zinduka kwenye usingizi mzito huu si wakati wa porojo za hovyo hovyo. Shauri zako watoto na kizazi chako watakuja kuaibika pale historia yako itakavyosomeka kuwa wakati vijana wenzio wanapobadilika na kupigania nchi yao wewe ulikuwa unaleta maneno ya hovyo hovyo na kukatisha tamaa.
 
lugha unayotumia cio ya wana jf,unachotakiwa kufanya ni kujenga hoja inayokidhi,na si matusi wala kejeri bali ni Logic.kama ww ni mpenda matusi nenda kasajiri Facebook huko ndiko saiz yako wewe. Hujakua!!
 
nilikuwepo ifakala acha kampeni za uongo kama kuna mtu kakusimulia pengine anaka kujua kama wewe ni mmoja wa mazuzu
 
kama chadema hamkuhitaji ccm kwenye msiba wenu mungesema badala ya kutengeneza matukio ambayo hayakuwepo ifakala
 
Sahihi kabisa mkuu!elimu ya uraia inahitajika sana,mimi wewe na yule popote pale tulipo itolewe!cdm nao waache kujikita sana mijini,pembezoni nako kuna kura,matawi zaidi na yawe rahisi kufikika,kadi,scuff nk zikosekane matawini!hv vitu upatikanaji wake mgumu sana hata mijini,sijuhi kwa nini!vimahamsha hamasa hv!Moro yetu ina kila kitu ila imestuck kutokana na viongozi hovyo hovyo wenye mipango hovyo hovyo,tunahitaji waje kina Regia(R.I.P) zaidi ya 20 kuiamsha na kuikomboa Moro yetu na Tz kwa jumla,naamini ikiwa hivyo Regia nae atafarijika huko alipo
mkuu twanga kote kote sasa hivi vijijini wanajua kuwa mjini wamehamia Chadema nao watahamia huko maana mijini kuna maendeleo kuliko vijijini nani hapendi maendeleo

kumbuka kuwa vijijni wakigeuka wanageuka jumla labda hawa jamaa waboreshe maisha ya watu wa vijijini hapo labda wataweza
 
CCM haitishiwi Nyau wana mbinu zaidi ya mia mbili wana ifakara kuweni makini msijeletewa Mvua ya Njaa... Siasa ni Mchezo Mchafu! wanaofaidika ni Wachache..
 
Kauli ya Makinda ni ya busara zaidi, tukiendekeza siasa mpaka misibani uko mbeleni tutashindwa kuzikana. CCM na viongozi wa serikali kwa ujumla wameonyesha mfano mzuri kwa kujumuika kwenye mazishi ya Regia(RIP) bila kujali itikadi zao. Je wasingefika si watu wangesema CCM/serikali haiwajali wananchi wake waliopo kwenye vyama vyingine? Siifagilii serikali ya chama tawala lakini kwa ili nawaunga mkono.
 
CCM haitishiwi Nyau wana mbinu zaidi ya mia mbili wana ifakara kuweni makini msijeletewa Mvua ya Njaa... Siasa ni Mchezo Mchafu! wanaofaidika ni Wachache..

Hoja isiyo na mashiko hata kidogo,ilistahili kuwepo kwy mazungumzo ya vijiwe vya kahawa
 
Back
Top Bottom