Kifaa cha kusafishia rangi ya tv

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
WanaJF mambo vp?Kuna kifaa fulani kinachotumika kusafishia rangi ya tv sikijui jina lake kinaitwaje niliwahi kukiona nchini Kenya kwa fundi mmoja kama miaka mitano iliyopita.Kifaa chenyewe ukubwa wake unalingana na lile boksi la dawa ya whitedent ile ya sh 1000.Hicho kifaa kinatumia umeme unapokiwasha kinawaka na kuunguruma kama ilivyo mashine ya kunyolea unapokielekeza kwenye uso wa tv iliyoharibika rangi kinaanza kuchanganya rangi na unapokizima tu tayari tv inakuwa imerudisha rangi yake ya asilia.Natumai kwa maelezo haya machache kama yupo anayekifahamu kifaa hiki kinapopatikana kwa huku bongo tafadhali tujulishane.Natanguliza shukrani
 
Poapoa.
Kifaa hicho binafsi sikifahamu, ila najua kwamba kioo cha TV unaweza kukisafisha kwa kupitisha sumaku mbele ya kioo kwa ku-sweep kutoka upande mmoja kwenda mwingine ukirudiarudia until you cover the whole screen.Hicho kifaa kinachotumia umeme nafikiri is the way of producing magnetism from electricity.
 
Sijui kama kifaa hicho kipo ila, kama tatizo ni tivii kuingiliana rangi
kuna njia ya kienyeji na ya BUREEEEEEEEE inaweza kukusaidia

cha kufanya:
1)tafuta sumaku(magnet kwa kidhungu) unaweza kuipata kwenye spika au kifaa chochote kinachotumia, au waombe watoto wakutafutie maana wanachezea kila siku

2) washa TV yako ambayop imeingiliana Rangi, wacha iwake kama dk 5 hivi ili tube iwe ya moto..

3)chukua magnet yako nasogeza kwenye uso wa tv(kioo) utaona rangi zinachanganyika Zaidi.

4)sasa fanya kama unafuta kioo kwa kutumia sumaku yako kuelekea pembeni ya Tv(bila kugusisha kwenye kioo hata kidogo) yaani juu juu utaona rangi zinafata muelekeo wa sumaku

5)so unavyofuta uwe unazielekezea zifate sumaku pembeni ya kioo hadi utaona rangi rangi zote zimepotelea mwisho wa kioo na kioo kitabaki safiiiiiiiiiiiii

Hope it helps!!

Cheers.
 
Hiyo ya sumaku naifahamu ila hicho kifaa ninachoulizia kinafanya kazi vizuri sana na ni kama kazi ya sekunde 15 tu.chenyewe ndio kinafanya kazi ya kukoroga rangi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom