Kifaa cha kisasa kinachorusha internet kwa njia ya wireless kwa kutumia line za simu

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
Habari njema kwa watanzania wote. Sasa tumaweletea kifaa kipya na cha kisasa kiitwacho MiFi kutoka Marekani, ambacho kinatumia line za mitandao ya simu za mikononi na kurusha internet kwa njia ya wireless. Kifaa hichi kama kinavyoonekana hapo chini kwenye picha kina uwezo wa kuunganisha hadi computer tano kwa njia ya wireless na kukupa internet yenye kasi ya ajabu tofauti na modem za mitandao ya simu za mikononi.

MiFi_2372_front_V2.png
579085_360291057355171_100001228408321_1094464_1613862918_n.jpg

Sifa za kifaa hiki:

  • Kifaa hiki kina uwezo wa kuconnect hadi device 5 zenye uwezo wa WiFi kwa wakati mmoja kama vile Computers, PDA's, cameras, music players, personal game players n.k huku ikiendelea kukupa internet yenye speed na kasi ya ajabu.
  • Kifaa hiki kinatumia Rechargeable battery aina ya Lithium Ion yenye uwezo wa kukaa na chaji hadi masaa manne hivyo huna haja ya kuwa na wasi wasi wa kukosa mtandao endapo ukiwa katika eneo ambalo halina umeme.
  • Pia kifaa hiki kinamrahisishia mtumiaji kuweza kuconnect internet kwa njia ya wireless mahali popote na wakati wowote bila ya kuwa na haja ya kuinstall software yoyote.
  • Pia kifaa hiki kinatumia line za mitandao yote ya simu ya mkononi hivyo kukurahisishia wewe mtumiaji kuweza kubadilisha line endapo mtandao mmoja utasumbua badala ya kuwa na modem za mitandao yote ya simu ambazo pia zinaweza kusababisha error katika computer yako endapo utainstall software nyingi za modem katika computer yako.
  • Kifaa hiki pia kina muonekano mzuri, kidogo mfano wa simu aina google IDEOS na ni chepesi ambacho kinakuwezesha wewe kuweza kutembea nacho kwa urahisi mahali popote upendapo.
  • Kifaa hiki pia kina uwezo wa NovaSpeed ambayo inakupa internet yenye kasi ya ajabu tofauti na modem za mitandao ya simu za mikononi.
  • Kifaa hiki kina uwezo wa kusafirisha signals za wireless kwa zaidi ya mita 10 (30ft).

Kwa sasa kifaa hiki kinapatikana Arusha ila kwa wale ambao wako nje ya Arusha na wangependa kupata kifaa hiki wawasiliane nasi na tutawapa maelekezo ya jinsi ya kuvipata vifaa hivyo.

BEI: Bei ya kifaa hiki ni sh. 140,000/=

Kwa wale wangependa kununua kifaa hiki tafadhali naomba mtoe order zenu kupitia sales@youngmaster.co.tz

Pia kama kuna mtu yoyote mwenye maswali au maoni kuhusiana na hiki kifaa asisite kuwasiliana nasi kupitia support@youngmaster.co.tz
 
Umechelewa best. Simu zote za Android zinaweza kugawa net kwa wifi kwa kompyuta hadi tano na simu zingine.
na bei hiyo ya mifi unapata simu nzuri tu.
Hiyo kitu hata ulaya ime fail ni sawa na Vodacom web box.
Na simu ninayotumia mimi kama wifi hotspot inakaa na chaji masaa 12 ukijumuisha na phone calls, messaging na media play!
 
unafanyaje mkuu.
 
But makampuni yanatofautiana mkuu so bei haziwezi kuwa the same na hii iko full unlocked.
Hii technogy yaweza kuwa nzuri ila bei yake si ya kitanzania. Kama ni faida nadhani mmeweka juu sana kwani siku hizi kuna options nyingi sana za wireless internet. Kazima mfikirie sana iwapo mmeamua kweli kufanya biashara kwani siku hizi Dubai si mbali na USA watu wanaenda kila siku. Hata hivyo tunashukuru kwa kutujulisha jambo hilo
 
Ni kama WiFi router lakini hii ni tofauti kidogo kwa sababu hii inatumia SIM card tofauti na router zingine ambazo zinatumiaR Ethernet au DSL.
Bado ni sawa na modem naona bora modem unajua moja inamaana kinafaa katika cafe,and small office kwa binafsi ni usumbufu mkuu!!
 
Hii technogy yaweza kuwa nzuri ila bei yake si ya kitanzania. Kama ni faida nadhani mmeweka juu sana kwani siku hizi kuna options nyingi sana za wireless internet. Kazima mfikirie sana iwapo mmeamua kweli kufanya biashara kwani siku hizi Dubai si mbali na USA watu wanaenda kila siku. Hata hivyo tunashukuru kwa kutujulisha jambo hilo

Bei yake kwa nje inakaribia dola 70 sasa piga mahesabu gharama za kusafirisha, ushuru n.k Unadhani tumepanga bei kubwa hapo?
 
Back
Top Bottom