Kidumu Chama Cha Machinjachinja-Barua ya Siri

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Barua hii ni ya siri kwa WanaMapinduzi:

Ndugu wapenda mauaji ya Mapinduzi, sisi wakubwa zenu kwanza tunapenda kukupongezeni kwa msimamo wenu wa kutetea Mapinduzi ya Zanzibar na haki ya Tanzania nchini mwanu.

Barua hii mnaandikiwa kuwataka muongeze juhudi kuyatetea Mapinduzi japokuwa kuna Waziri mmoja mwehu wa SMZ ametamka moja kati ya siri nyeti ya kwamba tayari tumeshatuma Vifaru Pemba ili tuhakikishe kuwa 2010 mambo yanakuwa swafi.

Kinachoonekana sasa ni kuwa mtumie ule ufedhuli na ujeuri wanu dhidi ya Wazanzibari wenzenu ili hili suala la vifaru lipate kusahauliwa. Maana kumbuka kuwa hakuna nchi yeyote duniani inayoweza kujigamba kuwa ina demokrasia ikiwa wananchi wake wanatishwa kwa kutumia vifaru katika zoezi la Kura, seuze uandikishaji.

Tunafahamu ni juzi tu wakati tukiangalia harakati zenu tuliona jinsi mlivyofanikiwa kuitia nguvu hii hoja ya kwamba CUF ilikuwa ikiiba chaguzi zilizopita kwa kupandikiza wapiga kura wenye umri mdogo na mamluki toka Tanga na Mombasa. Hivi sasa uongo huu unaonekana haufai tena maana goma la uovu lishaburukia kwetu tuliotuma vifaru.

Tunajua ni kazi kubwa lakini tunawakukumbusha kuwa msisahau mafao tuliyokuahidini, ijapokuwa mtashutumiwa kwa kukosa uzalendo, lakini pia msisahau mangapi maovu mmeshayafanya na kumbuka lakuvunda halina ......

Mwisho, inafahamika kuwa Mwezi wenu wa Ramadhani unakuja, lakini hapa ndipo patapohitajika ule umwamba wenu katika Mapinduzi. Tafadhali ondoeni huruma dhidi ya ndugu zenu na mnachotakiwa kuweka mbele ni Mapinduzi na wala siyo Mungu.

Namalizia kwa salam za pongezi na lawama kwa kazi ya mabomu na tindikali huko Pemba. Sisi tulikuwatuma muuwe siyo mrushe acid mkimbie au mtege vibaruti mtoroke, japo masheha ni rafiki zenu hii haina maana kuokoa maisha yao,mkiwapatia sawa wamalizeni, sababu sisi tulitaka kuipakazia CUF haya masuala ingekuwa vizuri masheha wangekufa ,maana CCM isingeweza kumuua sheha wake. Sasa inaonekana wazi kuwa haya majaribio yalikuwa ya kupangwa na kila mwenye akili yake timam alitambua hivyo. Kwa hivyo mara nyengine fuata maelezo kama unavyoagizwa.


Kidumu Chama Cha Machinjachinja!!!!!!
 
Last edited:
Ubongo wangu na macho yameshindwa kuwasiliana na kuelewana katika hili.
 
Back
Top Bottom