ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 605
- 1,536
Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ndg. Hussein Ruhava ametangaza rasmi kwamba Elimu ya Kidato cha Tano na cha Sita katika Manispaa itakuwa bila malipo. Manispaa itafidia mapato ya ada hizo kwenye mashule kupitia makusanyo yake ya ndani yanayotokana na tozo za minara ya simu
Ikumbukwe Manispaa ya Kigoma Ujiji inaongozwa na ACT Wazalendo, na chama kiliwaahidi wakazi wa manispaa na watanzania kwa ujumla kuwa Manispaa hii itakuwa ya mfano, na kwamba ACT Wazalendo inataka kufungua ukurasa mpya katika siasa za Tanzania, tunafanya siasa za masuala kwa maslahi ya watanzania wote.
Tunaomba watanzania muendelee kutuunga mkono.