Kidato cha sita kujiunga na jkt mwaka huu

Luraja

Member
Oct 15, 2012
27
4
Hizi ni shule ambazo kidato cha sita watachaguliwa kwenda JKT mwaka huu kuanzia machi
Kibondo, Musoma, Kibaha, Ilboru, Bagamoyo, Jitegemee, Tabora Wavulana na Nganza. Shule nyingine ni Mtwara Wasichana, Ihungo, Kilakala, Benjamin Mkapa, Maswa Wasichana, Dodoma, Tumain-Singida na Galanos.Nyingine ni Ashira, Nangwa-Manyara, Iyunga, Mpanda, Lindi, Iringa Wasichana, Kawawa-Iringa na Ruhuwiko-Songea.
 
Mbona hizi taarifa zako hazionekani kuwa na ukweli wowote ulee??? inakuwaje watenge shule nyingi sana za privates?? source ya taarifa plz!!
 
kama serikali imekosa hela kwa ajili ya hayo mafunzo ni bora waache maana haiwezekani kuchagua shule ,hii inatakiwa kuwa kabya ya kujiunga chuo wote wanapitia jeshini na huwa ilikuwa inafanyika wakati wa kusubiri matokeo ya form six
 
mshahara tu wa mwezi wa kumi na mbili ofisi zingine hawajapata, iwe pesa ya jkt itakuwepo kweli? pamoja na kwamba, kama wangepata hela hawa watoto waende jkt ingekuwa safi sana.
 
Mbona hizi taarifa zako hazionekani kuwa na ukweli wowote ulee??? inakuwaje watenge shule nyingi sana za privates?? source ya taarifa plz!!
Mbona shule nyingi ni za serikali.Source kasome gazeti la mwananchi la leo ( 7/1/2013)
 
Labda mimi sijaelewa kitu kimoja, mwaka 2014 vijana watahitimu kidato cha sita mwezi mei. Ina maana kama watajiunga na mafunzo ya jkt kwa miezi 6, chuo haitawezekana kwa mwaka huo itabidi wasubiri mpaka 2015 septemba huko. Swali linakuja, je kwa wanafunzi ambao shule zao zitakuwa bado hazijachaguliwa kujiunga na mafunzo ya jkt watawasubiri wenzao hadi mwaka unaofuata au wataendelea na chuo?. Na kama wataendelea na chuo si watawaacha wenzao walio mafunzoni kwa mwaka 1?. Kwa yeyote anayefahamu atufahamishe.
 
Back
Top Bottom