Kichekesho cha Wanyambo kujiengua kabila la wahaya!

msichoelewa si kila mwana kagera ni muhaya wapo wanyayangilo, waziba, wanyambo, wahamba, wakara,wahaya,wasubi n.k sasa mimi sioni hoja iko wapi kuwabeza wanyambo na umoja wao. ni mtazamo tu nipo tiyari kusahihishwa kwa hoja
 
Kakakiiza, ulitakiwa uhudhurie pale Makumbusho ili uone mambo mbalimbali yanayohusu utamaduni wao badala ya kuuliza hapa, maana si mahala pake. Vilevile Padre Kalugendo aliiandika sana hoja hii kwenye gazeti la Raia Mwema kwa wiki mbili mfululizo. Tafuta usome
 
Nashindwa kuelewa kwa wanajamii wa kagera kujitenga,juzi kulianzishwa siku ya wanyambo pale makumbusho,Kwa misingi hiyo wanyambo wanasema siyo wahaya!!Je ni wanyarwanda??walioko Tanzania??ila wote hao ni mbwenu ila hizo ni mbwembwe zao tu !!

Kwanza nikuweke sawa, si kweli kwamba walianzisha siku ya Wanyambo ila ni utaratibu wa kawaida kwa nchi hii kuwa na Siku ya Utamaduni wa makabila yetu. Makabila mbalimbali yamekwisha onyesha utamaduni wao pale makumbusho wakiwema Wahangaza kutoka Ngara waliofanya hivyo Mwaka jana. Ukisoma kwenye link niliyokupatia utajua makabila yote ambayo yamesha adhimisha utamaduni wao pale Kijiji cha Makumbusho. Lakini kwa kukusaidia pia ili uweze kupata majibu ya maswali unayo jiuliza basi soma hapa Karagwe ni ya Wanyambo na Wanyambo ni wa Karagwe
Wanyambo ni Wanyambo tu, kigezo ulichotumia cha wao kutoka Kagera hakiwafanyi kuwa Wahaya na hata Lugha yao kuendana kidogo kimaneno na Wahaya hakuwafanyi kuwa Wahaya. Kwa mfano mdogo, Wapare hawawezi kusema wao ni Wachaga kwa kisingizio cha kutoka Kilimanjaro. Lakini pia ukitaka kujua historia ya wanyambo waweza kusoma hapa Wanyambo kuwa na Siku ya Utamaduni wao

icon1.png
Re: Kichekesho cha wahaya!! nziriye

"Wanambwembwe za kizamaani ,mbna mie nasikia hawa jamaa ni kabila kadogo kenye watu wasiosoma na kapo ndani ya wahaya ni kweli au?|

Nziriye labda ungejiuliza kama kweli hawajasoma na {kiukweli hakuna kabila ambalo wamesoma wote} mbona walikuwepo kwenye baraza la kwanza la mawaziri wa nchi hii. Huyo aliyekuwemo ilikuwaje akawemo wakati huko kwao Unyamboni hawakusoma.

My take
Lakini suala la makabila na ukabila halitusaidii kujenga nchi yetu. Mimi si Mnyambo na wala sihitaji kujua kabila lako. Lakini nahitaji kuona input yako kwenye kujenga nchi yetu. Tanzania kwanza. Mbona kabila langu si maarufu na wala halizungumziwi mahali popote lakini hilo halijawahi kuondoa utanzania wangu.
 
Asante Chona kwa kumjibu maana nilikuwa nataka kumuwekea link uliyomuwekea aliyoiandika Fr. Kalugendo.
Labda kwa ufafanuzi kidogo watu kutoka Karagwe Si- Wahaya kama ilivyoelezwa hapo juu. Karagwe Kwa asili ni wilaya ya kabila la Wanyambo(Ab'hanyambo) na lugha yao ni Orunyambo. Kuwaita Wahaya ni kuwakosea heshima na kuwanyima haki yao ya msingi ya kuwa kabila kubwa na huru linalojitegemea. Upo ushaidi wa kutosha wa maandishi unaoelezea kabila la Wanyambo na jinsi mwingiliano wao na makabila mengine ulivyokuwa. Kwa maelezo zaidi soma kitabu cha Profesa Israel Katoke "The Karagwe kingdom" . Ndani ya kitabu hicho pia maswali ya mwanzilishi wa habari hii atapata majibu mengi.

Thanks.
 
Wanambwembwe za kizamaani ,mbna mie nasikia hawa jamaa ni kabila kadogo kenye watu wasiosoma na kapo ndani ya wahaya ni kweli au?

Mwenzetu, issue ya kusoma ya mtu mmoja mmoja kwa ajili ya kupambana na maisha. Sasa we twambie we elimu yako ni ipi na sidhani kama ungekuwa na elimu ya kutosha ungeweza andika aibu tupu kama hii. Mi ni mnyambo halisi na shule nimeenda yawezekana elimu niliyonayo huoni ndani, sasa kutaja kabila fulani halikusoma, umeonesha kwamba we shallow minded person na kama una kadigrii kamoja kwa hivi sasa ni kitu cha kawaida, watu wanacheza na PhD wana deal na issue za kuboresha maisha. Sijui mwenzetu unaelimu gani unayoweza kusimama na ku-generalize society kwamba haikwenda shule! nakuonea huruma nziriye!!!!!!!!!!
 
  • Thanks
Reactions: MJJ
Kuwaita Wahaya ni kuwakosea heshima na kuwanyima haki yao ya msingi ya kuwa kabila kubwa na huru linalojitegemea.

Hapa baba umechemsha. Ukweli ni kuwa mkiwa Bukoba nyinyi mnajiita WAHAYA na mkiwa nje basi mwasema siyo wahaya. Lkn hapo juu mimi mmeniacha hoi eti kuwakosesa heshima nafikiri ungesema amekosea tu.. Vile vile hata kusema ni kabila kubwa nayo imeniacha hoi. Mwanafunzi wa darasa la pili ukimuliza makabila makubwa atalitaja la wahaya, sijui kama hilo lingine litatajwa
 
Mwenzetu, issue ya kusoma ya mtu mmoja mmoja kwa ajili ya kupambana na maisha. Sasa we twambie we elimu yako ni ipi na sidhani kama ungekuwa na elimu ya kutosha ungeweza andika aibu tupu kama hii. Mi ni mnyambo halisi na shule nimeenda yawezekana elimu niliyonayo huoni ndani, sasa kutaja kabila fulani halikusoma, umeonesha kwamba we shallow minded person na kama una kadigrii kamoja kwa hivi sasa ni kitu cha kawaida, watu wanacheza na PhD wana deal na issue za kuboresha maisha. Sijui mwenzetu unaelimu gani unayoweza kusimama na ku-generalize society kwamba haikwenda shule! nakuonea huruma nziriye!!!!!!!!!!
Aiseeeee!!!!!!!
 
msichoelewa si kila mwana kagera ni muhaya wapo wanyayangilo, waziba, wanyambo, wahamba, wakara,wahaya,wasubi n.k sasa mimi sioni hoja iko wapi kuwabeza wanyambo na umoja wao. ni mtazamo tu nipo tiyari kusahihishwa kwa hoja

sikuwa na sababu ya kufanya ivi kama usingeomba ivi: ni kwamba wahaya ni group name,humu kuna vipande vingi mfano wanya'iangilo si wanyayangilo;wa kihanja/wahamba; waziba;wanyarutenge;wasubi na wanyamulenge na wanyambo si wahaya!nk. Mkuu uhaya ni kabila na wana lugha moja Luhaya au kihaya. Ukisema Luamba,runyahiangilo nk ni lugha katika Luhaya! Mi ni mtunzi wa adithi na Majina ya miaka kwa Luhaya bukoba Diosisi na naelewa fika ninayosema. Mfano kwenye mwaka wa Sha'abuka 2004 nilieleza vizuri. Nakaribisha swali!
 
Nashindwa kuelewa kwa wanajamii wa kagera kujitenga,juzi kulianzishwa siku ya wanyambo pale makumbusho,Kwa misingi hiyo wanyambo wanasema siyo wahaya!!Je ni wanyarwanda??walioko Tanzania??ila wote hao ni mbwenu ila hizo ni mbwembwe zao tu !!

asante mkuu,nafikisi lengo la tamasha hili sasa linaonekana kutimia,tulifanya tamasha ili kuuelimisha umma tofauti kati ya wahaya na wanyambo.tofauti ni kubwa km baadhi ya wajumbe walivyochangia.ili kuelimika na kuweza kueneza ujumbe jitahidi usome makala ulizopewa hapa juu.Elimu haina mwisho.
 
mleta hoja/mada "unapashwa"........kufanya utafiti kidogo aisee........
 
Bukoba(Vijijini), Bukoba (Mjini), Misenye, = Wa-Haya
Biharamulo, Chato = Wa-Subi
Ngara = Wa-Hangaza
Karagwe = Wa-Nyambo

Tatizo liko wapi? Wote wanatoka mkoa wa Kagera na wanajulikana kwa umoja wao kama "Wahaya"
 
Wahaya sio mkusanyiko wa makabila, ni kabila mojawapo kati ya yaliyopo kagera/bukoba, hebu somasoma, tena na kwingine sio JF tu, halafu, hawa ndugu zetu wameanza kuandika siku nyingi, unaweza hata kukuta mambo mengi tu online.
halafu pia kugomaa kuhusishwa na jambo au kundi sio mbwembwe, ni kukataa
 
Back
Top Bottom