Kichaa 'mhubiri'.

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,648
Daktari wa vichaa aliingia wodi ya vichaa kuangalia wagonjwa wake wanaendeleaje.
Akawakuta wagonjwa wote wametulia huku wakimsikiliza mgonjwa mwenzao ambaye alikuwa anaonekana kama anawahubiria vichaa wenziwe huku kichaa mmoja akiwa amejitenga mbali kidogo.
Yule kichaa 'mhubiri' alipomwona daktari, bila kuulizwa akapayuka kwa nguvu
"Mimi nimetumwa na Bwana toka mbinguni nije kuwaokoa hawa wanadamu"
Mara sauti ya ukali kutoka kwa yule mgonjwa aliyejitenga ikasika
"Muongo huyo sijamtuma"
 
Umenifanya nicheke baada ya hasira za dereva wa daladala kunipitiliza kituo!
 
Kichaa Mwingine alipanda juu ya gorofa akaanza kukojoa mara watu wakapita karibu akaamua kuubana mkojo, walipopita akaanza tena, mara mmoja akarudi na kumuuliza mbona tulipopita hapa ulisitisha kukojoa, kichaa akamjibu kule chini niliwaona watu wanapita na nikaogopa watavuta mkojo wangu halafu nitaanguka.
 
Teh yule kichaa kilimpitiliza mpaka akajiona yeye ni MUNGU duh teh teh
 
Ahahahaha..nimecheka sana mpaka nikasahau mgao wa umeme kwa muda..joto kali sana huku kwetu Tandale chaka
 
Ilitokea vichaa kupewa jaribio kuwapima akili zao, je yupo atakayefanikiwa?
Basi ndipo ikachorwa picha ya mlango na kusanifiwa ili kuwa kama mlango halisi kisha wakaambiwa wapite. Mmoja alibaki ila waliyobaki wote walikwenda na kujaribu kila njia ya kuufungua mlango ili wapite lakini hawakuweza. Daktari akaona huyu aliyebaki kapata afadhali kidogo lkn akaamua kumuuliza...
Dokta: mbona ww hujaenda?
Kichaa: mi nawaangalia tu wale, maana hawajuwi kama ufunguo ninao mimi.
 
Hiyo ya unabii imenikumbusha kisa cha Messi na Ronaldo kabla ya El-Classico ambayo Madrid walifungwa tano. Ronaldo alidai kuwa yeye ni nabii, ametumwa na Mungu wa soka kuja kuwafundisha WaCatalan jinsi mpira unavyotakiwa uchezwe. Kesho yake Messi alipoulizwa maoni yake kuhusu kauli ya Ronaldo, akatoa jibu fupi,"Mimi sikutamka maneno yale." Awali ile kauli haikueleweka, ila wachambuzi wakaja kugundua kuwa Messi ndiye mungu mpira ambaye anakana kumtuma Ronaldo! Iliniua mbavu ile scenario.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom