Kichaa hana afadhali

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Madaktari wa vichaa katika Hospitali moja ya vichaa katika jiji la London, walikutana siku moja kujadili kifo cha mwendawazimu mmoja… baada ya kugundua kuwa amejinyoka masaa machache baada ya madaktari na manesi kufanyakazi ya ziada kumuokoa asizame kwenye moja ya mabwawa ya kuogelea yaliopo pale hospitali… mmoja wa kati ya waliosaidia kumuokoa mwendawazimu yule aliyejinyonga ni mwendawazimu aliyekuwa anaonekana kuwa ana afadhali kuliko wengine…

Baada ya madaktari kukutana mahojiano ya yule kichaa mwenye afadhali yalikuwa kama ifuatavyo…

Daktari: Mr xxx… tunasikitika kukwambia kuwa, yule rafiki yako uliyemsaidia asizame kwenye swimming, amekutwa amejinyonga muda mchache baada ya kumuokoa na ameaga dunia…

Yule Kichaa akamkatiza daktari na kumjibu daktari kama ifuatavyo…

Hapana bwana daktari rafiki yangu NIMEMTUNDIKA MWENYEWE KWENYE KAMBA ILI AKAUKE MAANA ALIKUWA AMELOWA SANA….
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom