Kibonde, Jahazi, Clouds FM na maneno mbofumbofu

Al Zagawi

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
2,461
1,448
Nipo nasikiliza Jahazi kutoka Clouds FM....

Kitu sijakipenda ni namna Kibonde ametumia kipindi cha leo kusema maneno mbofumbofu dhidi ya Sugu....asili ya ugomvi ukiwa ni mradi wa Zinduka...

Mi ufahamu wangu ni kuwa Zinduka haikuwa na ukweli wowote kutoka katika nafsi za waandaaji zaidi ya kuwa ni mradi wa kutengeneza pesa kama vile tunavyofahamu kuwa waingiaji pale walitoa kiingilio....tofauti na miradi mingine mfano ya ukimwi n.k.

Naamini kuna mengi katika hili suala ambayo siyajui....naomba wajuvi wanipe info zaidi..
 
Huyo kibonde naye utadhani wale waghani mashairi kwenye rusha roho! kwani ndio dhumuni la kipindi cha jahazi?? low mind!!
 
Ngoja wapandishwe Kizimbani kwa utapeli hao akina Kibonde ndo watatia akilini.
Sa Kibonde anaanza kuongelea ishu hiyo kwenye taarabu ka vile amekuwa mtu wa mipasho?:mad:
Kesi ya pili itakayowakabili ni kumdhalilisha RAHISI WA NCHI, na kumfunguza tamasha la uwizi-mtupu!
 
Hivi huyu kibonde mbona yuko hivi ??
kama anataka kutoa single basi aingie kwenye ulingo wa kughani ...
 
Jamani tusimlaumu Kibonde yeye yupo kazi na ametumwa kufanya hivyo, ni kweli ameongea maneno mabaya sana juu ya Sugu, hii yote ni mbinu ya Kusaga ya kumsakama kijana wetu Sugu.
 
Jamani tusimlaumu Kibonde yeye yupo kazi na ametumwa kufanya hivyo, ni kweli ameongea maneno mabaya sana juu ya Sugu, hii yote ni mbinu ya Kusaga ya kumsakama kijana wetu Sugu.

hata kama ni kazi huwezi tumwa kumponda mwenzio na wewe ukakubali ...
Katumwa na nani?????????????
 
shida kubwa naiona hapo ni kuwa hakuna fairness kwa upande clouds, kama wanaona Sugu hana point katika hili jambo wasiicheze ngoma peke yao..wamuite studio wamuhoji aseme lake la moyoni...wathubutu kama hakuna mawaa yoyote kwa upande wao katika hili...
 
Sugu ameshazungumza na Msg Sent, wanatafuta namna ya Kujisafisha lakini Ujumbe umefika mpaka Magogoni
 
jamaa kibaraka tu,na chakufurahisha watanzania sio wajinga ka anavyofikiri, na sio wote wanaosikiliza li redio lao. imefika mahali sasa watanzania tunatakiwa tuwe tunasusia bidhaa za madhalimu kama wakina Kusaga na genge lake lote, wanakera saana, hawaoni aibu kuibia maskini
 
Hata kama watamfanyia vitimbi vya namna gani, SUGU ni shujaa. Ameweza kuweka wazi utapeli na ufisadi mkubwa ambao mpaka sasa hivi umeiumbua hata Ikulu kiasi cha kutoa matamko ya kujichanganya katika kujibu hoja za SUGU na kugundulika kuwa Rais naye alifanywa mradi. HEKO SUGU. KWELI WEWE NI " SUGU MOTO CHINI" Nakitafuta sana kibao chako hicho maana umeonyesha njia kwa wale chipukizi.
 
Nimekumbukia hiki kipande katika wimbo wa Ride Natty Ride wa Marley

[FONT=Trebuchet MS, Verdana, Arial][SIZE=-1]Tell you what: now the people gather on the beach
And the leader try to make a speech,
But the Dreadies understandin' that it's too late
A-fiyah is burning
Man, pull your own weight!
Fiyah is burning
Man, pull your own weight! [/SIZE][/FONT]
 
untitledk.jpg


Sikutegemea kusikia maneno ya kishenzi shenzi toka kwa mtu kama huyu ambaye nilikuwa na muheshimu sana kutokana na kazi yake ambayo kwa upande wangu naikubali, ila kwa maneno yake ya leo juu ya Sugu amejishusha hazi yake na anaonekana kama kibaraka flani hivi.
 
nipo nasikiliza jahazi kutoka clouds fm....

kitu sijakipenda ni namna Kibonde ametumia kipindi cha leo kusema maneno mbofumbofu dhidi ya Sugu....asili ya ugomvi ukiwa ni mradi wa zinduka...

mi ufahamu wangu ni kuwa zinduka haikuwa na ukweli wowote kutoka katika nafsi za waandaaji zaidi ya kuwa ni mradi wa kutengeneza pesa kama vile tunavyofahamu kuwa waingiaji pale walitoa kiingilio....tofauti na miradi mingine mfano ya ukimwi n.k.

naamini kuna mengi katika hili suala ambayo siyajui....naomba wajuvi wanipe info zaidi..

yaani unapoteza uda wako kusikiliza redio hii?
 
Taizo la wabongo yaani sasa hivi Sugu kawa adui wa Raisi!!! amini usiamini hata ile taarifa ya Ikulu ilikuwa na lengo la kushushua Sugu pia.
Watatumia mbinu nyingi mno kumshugulikia, subirini, hata kesi anaweza kubambikiwa.

Pole sugu, vumilia yanamwisho haya JK atakapotoka madarani watatuambia ujasiri huo waliutoa wapi?
 
Hivi huyu kibonde mbona yuko hivi ??
kama anataka kutoa single basi aingie kwenye ulingo wa kughani ...
Msameheni bure huyu Kibonde njaa inamsumbua,anajua asipofanya hivyo kibarua kitaota mbawa,alafu ni maskini wa ubunifu,mnafikiri atafanyanini,akheri akina Masoud kipanya wenye uwezo wa kutumia jicho la tatu na wenzake wote,much love wherever they are!!
 
Msameheni bure huyu Kibonde njaa inamsumbua,anajua asipofanya hivyo kibarua kitaota mbawa,alafu ni maskini wa ubunifu,mnafikiri atafanyanini,akheri akina Masoud kipanya wenye uwezo wa kutumia jicho la tatu na wenzake wote,much love wherever they are!!

Nakubaliana na wewe kabisa huyu jamaa ubunifu ni sifuri kabisa. Mimi sipendi sana namna ambavyo hujifanya kusoma yale magazti ya alasiri. Halfu anvyoongea kama kajaza mate mdomoni. Nadhani ni aina ya mtu ambaye unaweza kumpa bia mbili halafu ukamwambia nitukanie mtu fulani basi akaenda na kuangusha matusi bila mantiki
 
Duu,kweli hawa watu hawanafadhila,Sugu huyu huyu Ruge anayemponda na kumdhurumu hakizake ndiye aliyekuwa akimsaidia,mi nakumbuka kipindi cha nyuma kabla Ruge hajamiliki kile kivitara chake alikuwa anauzia sura mjini na ile gari aina ya Honda ya Mzee Sugu,leo hii ananyanyua mdomo na kuponda,fadhila ziende kwa mbuzi tuu,binadamu atakuudhi!!
 
Back
Top Bottom