Kibano cha Ngeleja Bungeni: Hotuba ya Madini na Nishati 2011

Status
Not open for further replies.
Dah,sasa sijui wanataka tufanyeje,tuandamane au wabunge watoke nje ya bunge?
 
mimimndo maana napendekeza NATO wakimaloza kwa gadafi waje pia kutuondolea jk na ccm yake....... hatuwataki!!

Hahaha can't help but kucheka sana.

Lakini jamani hivi hawa watu vipi? Yaani weshaona waTz ni vikaragosi wa kuchezewa the way watakavyo wao? Naunga mkono post ya mkuu mmoja aliyesema cdm waandae hoja na ziletwe uraiani kama hazitapewa fursa ya kusikika humo bungeni
 
Mama Kilango unauaaaa... Ngeleja una roho ya paka.... Naibu speaker mpaka anakuokoa...
Huyu maza kammaliza sana Ngeleja! Amedai kwamba Ngeleja amepeleka umeme kwenye vijiji 9 Jimboni Sengerema, vijiji kadhaa Same Magharibi, vijiji kadhaa Siha, nk lakini ameacha kupeleka umeme Same Mashariki na kwa maana hiyo ana upendeleo wa Jimbo lake (Ngeleja), pamoja na majimbo ya mawaziri wenzake! Huwa anakunywa chai na Ngeleja lakini anao uwezo wa kununua chai, anachotaka ni umeme, haungi mkono hoja!
 
wakati naibu speaker akimkaribisha waziri wa nishati na madini, ametahadharisha kuwa wabunge walioomba kuchangia ni wengi sana hivyo watakaopewa kipaumbele ni wale ambao hawajawahi kuongea kabisa na wale waliowahi kuchangia mara moja tu. Maana yake ni kwamba watu makini kama tundu, mbowe, zitto, mdee n.k hatutawasikia. Labda wangoje kwenye kamatihuu ndio ule utatu usiokuwa mtakatifu niliokuwa naulaani (kiti cha speaker, wabunge wa ccm na serikali). Watasema sana mwisho utasikia naunga mkono hoja asilimia 100
uongo!
 
Hapa nilipo nimepiga magoti wabunge hawa wapewe nafasi ya kuchangia see below:
  1. Mh. Aikaeli Mbowe
  2. Tundu Lisu
  3. Halima Mdee
  4. John Myika
  5. Msigwa (Mchungaji)
  6. Godbless Lema
  7. Zuberi Zito Kabwe.
Kama na wewe uko kwenye maombi kama mimi hembu na wewe muweke unayemjua ili Ngeleja leo aone wapinzani wako pale bungeni sio kwakulala bali ni kwa maslahi ya wananchi!
hapa tupo pamoja
 
wakati naibu speaker akimkaribisha waziri wa nishati na madini, ametahadharisha kuwa wabunge walioomba kuchangia ni wengi sana hivyo watakaopewa kipaumbele ni wale ambao hawajawahi kuongea kabisa na wale waliowahi kuchangia mara moja tu. Maana yake ni kwamba watu makini kama tundu, mbowe, zitto, mdee n.k hatutawasikia. Labda wangoje kwenye kamati

huu ndio ule utatu usiokuwa mtakatifu niliokuwa naulaani (kiti cha speaker, wabunge wa ccm na serikali). Watasema sana mwisho utasikia naunga mkono hoja asilimia 100


napinga huu mkakati ....hawa sisiem na supika wao wasituletee udaku tutaanza kuwapopoa mawe kama mwenzao wa tarime!!! Wadau pingeni hili swala kwa hali na mali .....hizi ni dalili za mkakati wa sisiem kunyamazisha wapinzani makini....shenzi zao!
 
Anna Kilango kamchana Ngeleja kuwa kajipelekea umeme kwake na kwa rafiki zake mawaziri akadanganya wananchi wa Same Mashariki hivyo awaombe radhi
 
Binafsi huyu mama kanifurahsha kaongea pointi za kumtosha ngeleja,na kweli madini hayaozi kwa nn tusisubr tukuwe kiteknolojia kwani hao wanaoenda kuchekecha mchanga nje tumezaliwa tumbo moja akamaliza akisema siungi mkono hoja,very lovely
 
Wana JF ya leo bungeni kali. Anne Kilango Malecela MB amedadabua jinsi Ngeleja alivyo mwepesi kupenyeza rupia pale palipo na udhia. Hii inatuthibitishia ilie ishu ya Kafulila jinsi alivyowakamata Mawaziri na Wabunge wa CCM wakiomba rushwa ( lakini ishu ilizimwa kiaina) leo tena limeibuka lingine ni uthibitisho tosha kuwa baadhi ya viongozi waandamizi kutoka Tannesco walitembeza bahasha zilizo jaa fedha ili kuwahonga wajumbe huko Mjengoni ( Hii nayo imezimwa kiaina) tunamwomba Ngeleja akanushe hili la kuhonga chai na vitafunio kwa Anne Kilango ili kumfichia UFISADI unaofanywa na Wizara ya Nishati na Madini. HAKIKA NI WIZI MTUPU. RUSHWA KWA KWENDA MBELE.
 
Watanzania tuendelee kuwa makini ipo siku tutaweza kufanya tukio la kuustaajabisha ulimwengu na utakuwa mwanzo mzuri wa maendeleo yetu
 
Alishasema hatajiuzulu na mkubwa wake wa kazi akamtetea...........kwamba tatizo sio ngeleja tatizo ni ukame....

Kwa hali ilivyo jamani Nakuambia atachia madaraka kama ana nawa,

Je Anna Kilango anasema haungi mkono hoja na patachimbika hapo bungeni na Job ndugai nae akaongezea hilo hilo kwa ngereja kuwa patachimbika tiyari vitabu vyake vya budget ya Nishati na madini imeanza kumfunga najua ngeleja atakuja na visingizio vingi tu.

Je wabunge wengine wa CCM watakuwa pamoja na Anna kilango na Job Ndugai kuhakikisha hoja ya Ngeleja kutokupita hapa ni uzalendo zaidi unahitajika maaana wakati Anna Kilango akitoa yake yaliko moyoni na yale toka kwa wananchi wa Jimbo lake baadhi ya wabunge wa CCM na upinzani walikuwa wakitoa ishara ya kuunga mkono sasa sielewi je itawabidi nao wafanye hivyoooo hao wana CCM?????
 
Nafikiri hilo suala la kunyima nafasi ya kuchangi katika bajeti ya wizara ya nishati, wabunge waliozoea kutoa michango ni sawa na kutayarisha bomu kwa ajili ya kulipuka! - hakuna mtanzania YEYOTE asiyekerwa na tatizo la umeme katika nchi hii, sembuse wawekezaji kutoka nje ya tanzania. sasa unapoanza kunyima wabunge tena wale ambao wananchi wanawategemea kuwa ndio sauti yao (irrespective of constituency), itawapandishia wananchi hasira na kuamua kuingia barabarani!!!! - labda niseme kuwa nahisi kumbe upande wa serikali kunahitajika "psychologists" wanaoweza kusoma hali tete ya nchi na si polisi...kazi ipo mbele yetu tena kubwa sana.
 
Watanzania tuendelee kuwa makini ipo siku tutaweza kufanya tukio la kuustaajabisha ulimwengu na utakuwa mwanzo mzuri wa maendeleo yetu

Duuuuh ama kweli macho wanayo lakini wamevaa miwani ya mbao, masikio wanayo lakini wameyaziba na karatasi za posho, pua wanazo lakini hazinusi sijui watu hawa wamekula ugolo wa wapi? Mi nafikiri safari yetu inazidi kukaribia...lakini hapohapo wanatusukuma ili tufike haraka
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom