Kibanda ana ndoto zake za mchana Dr Slaa, akiwa rais atakuwa msemaji wa Ikulu!
vazi halibuniwi, vazi linatokana na watu wenyewe wanavyovaa tofauti na mataifa mengine.
Hivyo eeh?
Mkuu tatizo letu hatuna vipao mbele katika maamuzi na mipango yetu ya kila siku kama nchi. Tumejaa ubinafsi mno. Hapa watu wametengeza ulaji na kama ulivyosema tutaingia mkataba na Pakistan watushonee vazi la Kitaifa. Siku unapata Kitambulisho chako cha uraia unatakiwa ununue na vazi la Kitaifa. Ni ujanja ujanja tu.Inachekesha kuona serikali iko mstari wa mbele sana kuhimiza tume za vazi la taifa wakati haina mpango wowote wa kuokoa viwanda vya nguo.
Hata ukisema uondoe philosophical differences, useme unakubali vazi la taifa linaweza kubuniwa na viongozi, utoe hili ndio vazi la taifa, vazi litashoneshwa wapi wakati nchi haina viwanda vya nguo?
Au ndo tunataka tuwape tender wa Pakistan watushoneshee vazi la taifa?
Hivi kibanda amejua serikali inanyanyasa waandishi baada ya yeye kunyanyaswa?
Asante Kibanda kwa kauli yako, watu wamehoji kwa nini leo wamesahau hii vita si yakushinda siku moja zinatakiwa mbinu mbalimbali kama hizi, tukawaambia kila mtu na mipango yake na kila jambo na wakati wake, safi Kibanda, wakasema umejitoa kwa sababu ya kukamatwa na polisi ofcourse nayo ni sababu tosha kwa sababu mvaa kiatu ndiye anajua kinapomchoma zaidi. Ingawa umesema sababu kubwa zinakugusa wewe lakini hata kujitoa kwako kumesaidia kuwaonyesha watawala kuwa hilo vazi halina umuhimu mkubwa sana kama wanavyofikiria.Mwanakijiji sitaki kuamini kwamba umesahau haraka hivi. Nimetambua unyanyasaji wa waandishi wa habari miaka mingi na ushahidi upo. Kwanza niliongoza maandamano ya kulaani kumwagiwa tindikali kwa Saed Kubenea nikiwa Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania tena baada ya baadhi ya wahariri 'kuingia mitini'. Mimi ndiye niliyetoa tamko la kulaani kitendo hicho. Nilishiriki kikamilifu kuanzisha Jukwaa la Wahariri mwaka 2008 kama moja ya njia ya kutetea uhuru wa uhariri na wa kutoa maoni. Nimeshiriki katika mikutano na shughuli mbalimbali za kudai Sheria Mpya ya Habari nchini sambamba na kufutwa kwa sheria kandamizi kupitia makala zangu na kupitia mikutano ya wadau wa habari. Mwaka jana wakati waandishi waliponyanyaswa katika safari za kampeni za wagombea wa vyama vya siasa, niliitisha mkutano wa dharura wa wahariri na kulaani vitendo hivyo na tamko langu likaripotiwa katika vyombo mbalimbali nchini...
Mwisho sababu za kujitoa katika kamati ziko bayana. Zinanigusa mimi mwenyewe na ni zaidi ya kupinga unyanyasaji wa waandishi wa habari.
Nampongeza kwa dhati ndugu Kibanda kwa uamuzi wake wa kuachana na hili zoezi la kipuuzi. Tanzania tuna matatizo lukuki lakini Nchimbi anaona jambo la muhimu ni mavazi?
Vazi la taifa kamati husika ilikuwa ni kujitolea kwa mujibu wa barua walizoandikiwa sasa unaposema kuna ulaji sijajua watu wanamaanisha nini hapa.....kazi kubwa.kuhusu vipaumbele mbalimbali ni kuwa kila wizara ina kipaumbele chake....utamaduni wana vazi,habari wanaandaa sheria mpya bora zaidi.....michezo wanaandaa mpango mkakati wa michezo utakaoainisha wajibu wa kila mwanamichezo na mwananchi chini ya baraza la michezo na vijana sijajua bado.sasa wewe ukisema waongelee umeme au maji hayo yana wizara zake....
Kibanda ana ndoto zake za mchana Dr Slaa, akiwa rais atakuwa msemaji wa Ikulu!
asilimia 35 ndo mlompa kikwete na vile vile katangazwa na tume yake kuwa rais kama kabila zaire
Alipochaguliwa alikubali na kufurahi sana na kesho yake kulikuwa na column kubwa kwenye gazeti analoliongoza lenye heading ya " Kibanda aula kamati ya Vazi la Taifa" na mbaya zaidi aliye mteua ni waziri wa habari...hizi habari za leo kujitoa kwa ajili ya unyanyasaji ni ubinafsi wa hali ya juu, na ikumbukwe kuwa huyu jamaa ni mwenyekiti wa wahariri bongo.