Kibamba na jukwaa la katiba

NZURI PESA

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
5,960
2,938
Wakuu naomba mnijuze kibamba na jukwaa lake la katiba amechaguliwa na nani? na anawakilisha nani?
 
Wakuu naomba mnijuze kibamba na jukwaa lake la katiba amechaguliwa na nani? na anawakilisha nani?

Nami naomba NZURI PESA anijuze kwani D. Kibamba alitakiwa kuchagiliwa na nani? na alitakiwa kumwakilisha nani?

Halafu pia NZURI PESA anijuze, Mku wa Chuo cha DSM, Mkuu wa Chuo cha Dodoma, na wakuu wa vyuo vungine vya Umma huchaguliwa na nani? huwawakilisha watu gani?
 
Nami naomba NZURI PESA anijuze kwani D. Kibamba alitakiwa kuchagiliwa na nani? na alitakiwa kumwakilisha nani?

Halafu pia NZURI PESA anijuze, Mku wa Chuo cha DSM, Mkuu wa Chuo cha Dodoma, na wakuu wa vyuo vungine vya Umma huchaguliwa na nani? huwawakilisha watu gani?

We si ndo ULIFELI MTIHANI kwa kushindwa kufuata maelekezo.Nimesha kupata mkuu.
 
Kwa upeo wangu mdogo..Jukwaa la Katiba ni jukwaa linalojumuisha asasi mbalimbali zisizo za kiserikali zilizosajiliwa kisheria zinazofanya kazi ya kuangalia kwamba haki za binadamu zinalindwa kama ambavyo zimeainishwa na sheria mama yaani katiba...sijajua hizo asasi ziko ngapi lakini ni nyingi sana....na kwa hivyo viongozi wake wanatoka ndani ya hizo asasi kupitia uchaguzi halali na taratibu zao...kuhusu wanamuwakilisha nani ni wananchi kwa ujumla wake na serikali haipaswi kuwatenga kuwa hawawajui wakati ni asasi iliyosajiliwa..huku ni kukimbia kivuli chako mwenyewe.....
 
Hilo aliitaji jibu.Kachaguliwa na wanajamii wanaomwamini.
Kwa taarifa yako Ndg Kibamba kama akifanikiwa kwa hili nategemea siyo mwenzetu tena.
Kwa sasa anachumia juani lakini nategemee atalia kivulini.
 
Kuna umhimu, kwa maoni yangu, kujua kwamba vikundi kama hivi Jukwaa la Katiba ni vipaza sauti vya nani? Mimi nimepata kuwafuatlia kwa karibu Jukwaa la Katiba. Tamko lao walilolitoa kabla ya mjadala Bungeni juu ya Mswaada wa Tume ya Katiba haujaanza, ni kwamba kama wabunge wataafiki kwamba Mkatba usomwe mara ya pili Jukwaa litawashawishi watu wafanye maandamano Tanzania nzima. Na kabla ya maandamano wangejipa mwezi mmoja kupita Tanzania nzima kuwashawishi watu juu ya maandamano. Tofauti na walichokisema mbele ya watu, mara baada ya Mswaada kusomwa mara ya pili na kupitishwa, Jukwaa la Katiba likaja na kauli mpya kwamba maandamano ya taifa zima yanafanyika Jumamosi, siku chache baada ya mswaada kusomwa mara ya pili. Hii inatia wasiwasi na umakini wa kauli zao.

Sasa baada ya Jukwaa la Katiba kutoa matamko hayo ya kutisha (kwa maoni yangu) zimezuka tena taasisi mbalimbali nyingine zinafahamika na zingine hazifahamiki zinazotaka kufanya maandamano nchi nzima kwa sababu tofauti. Kama kila taasisi, kila mtu, kila kikundi kitakuwa na haki ya kuhamasisha wananchi kufanya maandamano nchi nzima kulishinikiza Bunge, Mahakama au Raisi kufanya wananchokitaka tutaweza kuishi kwa amani na kuheshimiana kweli? Tutaweza kuishi katika mazingira ya ustaarabu wa utawala wa sheria? Nionavyo mimi sisi kama watanzania ambao tunapaswa tutafakari kwa pamoja na kuwa makini juu ya tunayoyafanya. Siasa zikizidi sana ni matatizo. Kila mtu anayejua kusema siasa akiruhusiwa kuwahamasisha watu kuandamana kwa lengo la mashinikizo kwa vyombo vya dola kufanya anachotaka itakuwa ni mtafaruku.

Ndio maana ndugu zetu wa Chadema baada ya kutafakari kwa kina wameona busara kuunda kamati ya watu wenye busara na upeo wa juu kwenda kumuona Raisi na kumpa kwa kina maoni ya Chadema kuhusiana na Tume ya Uchaguzi. Wameenda kumuona Raisi sio kama kiongozi wa juu wa CCM bali kiongozi Mkuu wa Dola.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom